Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Sunday, December 23, 2018

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UJENZI



Karibu Tuelimishane Mambo Muhimu Kadhaa Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanza Ujenzi

Unaweza Ku-Share Na Watu Zaidi Ujumbe Huu, Unaweza Ukawasaidia Sasa Au Hata Wakati Mwingine Kwa Namna Moja Au Nyingine


NOTE: Kufuata taratibu za kitaalamu katika UJENZI kunaweza kukusaidia kupunguza gharama za ujenzi mpaka 15% pamoja na kukuepushia hasara inayoweza kutokea mbeleni, sambamba na kukupatia kitu bora, kizuri na chenye thamani

1. Baada Ya Kuwa Umetayarisha Kiwanja Chako Kizuri Katika Eneo Ulilochagua, Anza Kujiridhisha Na Unachotaka Kujenga, kwa mfano

(i) Matumizi, jengo lako ni kwa ajili ya matumizi gani, makazi, biashara, ofisi, taasisi, starehe, godown/kiwanda n.k.

(ii) Jengo la aina gani, ghorofa au nyumba ya chini ya kawaida?

(iii) Unahitaji kuwe na vyumba vya matumizi gani(functional requirements) kama vile vyumba vingapi vya kulala pamoja na nini cha ziada kama vile movie theatre, maktaba n.k, kwa jengo la nyumba ya kuishi, au kama ni matumizi mengine ujue mahitaji yake

2. Tafuta mtaalamu wa majengo, msanifu au mbunifu majengo(architect), huyu ana utaalamu juu ya jengo, kazi zake na mipangilio yake yote ya kitaalamu. Atakushauri na kukuongezea uelewa wa sayansi ya majengo kwa ujumla

-Baada ya kumpeleka kuona eneo lako(site visit) mkajadiliana mkaelewana mwambie akafanye michoro ya mwanzo arudi mjadiliane na kujiridhisha kama kilichofanyika kimeendana na mahitaji yako, kisha mkishapitisha akafanye michoro ya 3D's(picha) za muonekano wa jengo husika uzione na ujiridhishe kama umeridhika na muonekano huo kisha ndio umruhusu amalizie michoro ya mwisho kwa ajili ya kufuatilia kibali cha ujenzi halmashauri husika
 
NB; Ni muhimu sana kujiridhisha na jengo lako usije kujuta baadaye au kujikuta unabomoa na kubadilisha baada ya kuona makosa, kwa sababu unakwenda kuweka pesa zako nyingi sana usije ukaingia gharama zaidi baadaye ambazo ungeweza kuziepuka mapema kwa kujiridhisha wakati wa michoro
Likifanyika vile unavyotaka utalifurahia na hutaona umepoteza

3. Kama jengo lako ni la ghorofa hutaishia hapo, unalazimika kumtafuta mtaalamu mwingine wa kutengeneza muundo wa mihimili ya jengo(structural engineer au mhandisi mihimili). Huyu hataongeza au kupunguza chochote ila atatumia michoro iliyofanywa na architect kutengeneza michoro ya muundo wa mihimili inayoshikilia jengo, kisha atakukabidhi michoro hiyo iliyopigwa mhuri kabisa kwa ajili ya kufuatilia kibali cha ujenzi halmashauri

4. Umeshakabidhiwa michoro yote ya msanifu/mbunifu majengo(architect) ambayo ni (architectural drawings) na ya mhandisi mihimili(structural engineer) ambayo ni (structural engineering drawings) yote ikiwa imepigwa mhuri utaenda nayo katika halmashauri yako kuomba kibali cha ujenzi ukiwa pamoja na hati yako ya kiwanja

5. Baada ya kupata kibali cha ujenzi halmashauri unaweza kuanza ujenzi lakini kama jengo lako ni la ghorofa utatakiwa kufuatilia vibali vingine kutoka kwenye bodi mbalimbali za ujenzi kutegemeana na ukubwa na matumizi ya jengo lako.

Bodi za ujenzi utakazopaswa kuchukua vibali kabla ya kuanza ujenzi wa jengo la ghorofa ni hizi zifuatazo;-

(i) AQRB(Architects Quantity Surveyors Registration Board)
(Hii ni bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi)

(ii) ERB(Engineers Registration Board)
Hii ni bodi ya Wahandisi

(iii) CRB(Contractors Registration Board)
Hii ni bodi ya Wakandarasi

Utapatiwa vibali vya bodi hizi(kwa mfumo wa stikers) ambazo utaweka kwenye kibao chako cha ujenzi kwa ridhaa za kampuni zilizokupatia huduma za ushauri wa kitaalamu na michoro husika

6. Baada ya hapo unaweza kuanza ujenzi sasa. Kitu cha kuzingatia ni kwamba siku hizi kuna usumbufu mwingi na ni vigumu kujenga bila kuwa na kibali hasa kibali cha halmashauri na hasa katika eneo lililopimwa, ni rahisi kukutana na usumbufu mkubwa.

 Faida nyingine za kupata kibali cha ujenzi ni kwamba utaingiza katika kumbukumbu zako na utaingia pia katika kumbukumbu za halmashauri husika hivyo inaweza kukusaidia muda wowote utakaohitajika kuwasilisha taarifa hizo sehemu yoyote kuhusiana na jengo lako katika kuonyesha uhalali wa umiliki na uhalali wa jengo lenyewe ili kukusaidia katika mambo mbalimbali

7. Mwisho napenda nigusie kidogo swala la matumizi ya eneo maana ni swala ambalo limekuwa changamoto kwa wengi katika kupata kibali
Kiuhalisia maeneo mengi yamepimwa kwa matumizi ya makazi japo kuna watu pia wengi wanaonunua maeneo kwa ajili ya kujenga majengo ya biashara au makazi biashara(residential apartments) Utakapotengeneza michoro kwa ajili ya jengo la biashara au makazi biashara wakati eneo lako hati inaonyesha matumizi yake ni makazi pekee hutapewa kibali na wakati huo pengine umeshafanya michoro yote na kuwalipa watu pesa halafu halmashauri wanakukwamisha na kukutaka uanze mchakato wa kuomba kubadili matumizi.

 Huu ni mchakato mrefu na utakaoweza kukuchukua tena muda mwingi na gharama wakati huo pengine ulishachukua mkopo ambao unatakiwa uwe umeanza kuulipa japo bado hujapata hata hicho kibali. Endapo umejikuta kwenye jambo kama hili unaweza kumtafuta mtaalamu mkashauriana nini cha kufanya kwa haraka wakati mchakato wa kubadili matumizi unaendelea

Karibu kwa swali au ufafanuzi wowote maana mengi nimeeleza kwa kifupi ili nisikuchoshe msomaji

Ahsanteni
Arch. Sebastian Moshi
+255717452790

Wednesday, December 19, 2018

BancABC yadhamini mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce – TWCC)



Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya BancABC Tanzania Upendo Nkini akizungumza na wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano wa chama hicho ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akiwazilisha mada wakati wa mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.

Wafanyakazi wa benki ya BancABC wakimsikiliza kwa makini mmoja wa mwanachama wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) Anna Simbeye wakati wa mkutano wa chama hicho ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akiwazilisha mada wakati wa mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akiongea kwa umakini wakati akiwazilisha mada wakati wa mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.

BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, mwishoni mwa wiki ilidhamini mkutano wa kila mwezi wa chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce TWCC) mkutano ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia maendeleo yao na changamoto ambazo wanakubana nazo.

Akiongea wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi alisema kuwa benki ya BancABC inatambua ni umuhimu wa wanawake kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na ndio sababu benki yake imeweka mikakati ya kuendelea kuwawezesha na kufikia hatua ya leo ya kuungana na Chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwenye mkutano wake huu wa kila mwezi.

Matoi alisema kuwa kwenye mkutano huo BancABC imeweza kutambua kuwa wanachama wa TWCC huwa wanashiriki maonyesho mengi nchini China akitolea mfano kuwa kwa mwezi wa Oktoba na Aprili mwaka huu, wanachama 150 walishiriki baadhi ya maonyesho ya biashara nchini China. Hata hivyo, Malai alisema kuwa wakati wa safari zao nchi China wananchama hao wamekuwa wakikubana na changamoto kadhaa na hasa linapokuja suala ya kubadilisha fedha na hasa inapotokea dharura.

Ninayo furaha kuwafahamisha ya kuwa BancABC Tanzania inayo suluhiso ya jinsi ya kupata fedha za kigeni mnapokuwa safarani China. Tunayo kadi ya malipo ya kabla – YUAN pre-paid Visa card, ambayo itawawezesha kufanya malipo kwa kwa fedha za China. Kadi ya YUAN ni kadi maalum ambayo inawafanya watumiaji waweze kupata fedha za Uchina kwa thamani ile ile ambayo imewekwa kwenye kadi yake na hivyo itapunguza sana changamoto za kubadilisha fedha ambazo nyinyi wafanyabiashara huwa mnazipata pale wanapohitaji fedha za Uchina mkiwa China au popote pale duniani, alisema Matoi.

Matoi aliongeza kuwa BancABC Tanzania kwa kushirikiana na TWCC itaweza kufaidika kwa kuwa moja ya taasisi duniani ambayo imejidhatiti kutatua changamoto za wanawake na hasa kwenye masuala ya kiuchumi, kuongeza upatikanaji wa huduma na bidhaa zake, kuongeza ushirikiano pamoja na kukuza na kuongeza idadai ya wateja wake.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TWCC Mwanjuma Hamza alisema kuwa TWCC ni chama kinachounganisha wanawake kwenye sekta zote na mikoa yote, Tanzania Bara na Zanzibar.

Lengo letu ni kufanya wanawake wakue kiuchumi ikiwa ni pamoja na kukuza na kuendeleza biashara zao kwa kushiriki maonyesho kadhaa ya kibiashara ndani nan je ya nchi, alisema Hamza akiongeza kuwa kutoka Januari mpaka Disemba mwaka huu, wanawake wanachama wa TWCC walishiriki kwenye maonyesho kuanzia ngazi ya mkoa, taifa na kimataifa na hivyo kuwajengea uwezo wa kukuza biashara zao kutoka na ujuzi wanaoupata.

Akifafanua zaidi, Hamza alisema wanawake wananchama wa TWCC 150 walishiriki maonyesho nchini China, 100 Ujerumani na kwa sasa kuna wanawake wapatao 30 ambao wanaendelea na maonyesho Eldoret, Kenya. 

Saturday, December 15, 2018

Biteko afungua Ofisi ya Madini Mahenge mkoani Morogoro

Wachimbaji madini Mahenge mkoani Morogoro watakiwa kulipa madeni yao


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi Mahenge-Ulanga mkoani Morogoro, jana Disemba 14, 2018. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali wa Serikali, Tume ya Madini pamoja na wachimbaji madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni baada ya kufungua ofisi ya Afisa Migodi Mkazi Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro. Aliyesimama ni mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga.
Mkuu wa Wilaya Ulanga, Ngolo Malenya akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi wilayani humo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu), Mkuu wa Wilaya Ulanga, Ngolo Malenya (wa pili kulia),  Kamishna wa Madini kutoka Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeke (wa kwanza kushoto), Mbunge Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Migodi Mkazi Wilaya ya Ulanga, Tandu Jilabi (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa ofisi hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali, Tume ya Madini pamoja na wachimbaji madini wilayani Ulanga.
Jengo la Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi Mahenge-Ulanga mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji madini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mahenge wilayani Ulanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Serikali.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa CCM pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ulanga.
Wananchi na wachimbaji madini Mahenge wilayani Ulanga wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Friday, December 14, 2018

Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana

Majid Abdulkarim
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu na Maafisa Mipango wote wa Halmashauri nchini kutumia taaluma zao katika kukuza uchimi wanchi ili kuleta matokeo bora kwa watanzania wanao watumikia.

Hayo yamebainishwa leo wakati  wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 yatakayo fanyika leo na kesho hapa jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli. Dk. Chaula amesema mafunzo hayo ni fursa kwa maafisa hao  kuhakikisha wanapata ujuzi wa kuweza kupata matokeo bora katika kukuza uchumi wanchi hii.
“Ili kufikia matokeo bora ya kukuza uchumi wa nchi hii mnatakiwa kuwa wabunifu kwa kuchukua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa ili kuinua uchumi nchi hii” Alisema Dk. Chaula.

Dk. Chaula ameongeza kuwa kila mtumishi wa Umma anadhamana kubwa kwa taifa hili , na dhamana yenyewe ni kuhakikisha tunawatumikia vyema watanzania wenzetu ili kuleta matokeo bora kwa nchi yetu kama Muhasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyo fanya mpaka leo kupitia matokeo yake tunamkumbuka. Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango OR-TAMISEMI, amesema kuwa kupitia mafunzo hayo maafisa hao watanufaika kwa kupata  uelewa wa kuandaa bajeti iliyobora na kuwa walimu wazuri kwa maafisa wengine katika maeneo yao ya kazi.

Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3), Dk. Emanuel Malangalila amesema kuwa maafisa hao wakatumie hujuzi huo watakao upata katika mafunzo haya ili kuleta matokeo bora katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kukuza uchumi katika halmashauri na mikoa yao. Akihitimisha kwa neno la shukurani kwa niaba ya washiriki wenzake Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Ruvuma Edmundi Godwell Siame amesema yote aloyaelekeza Dk.Chaula watayafanyia kazi ili kuhakikisha taaluma yao inakuza uchumi wanchi hii na kuhakikisha mafunzo hayo yanaleta matokeo bora katika kukuza uchumi wa nchi.
 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli. 
Baadhi ya  Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu na Maafisa Mipango  wa Halmashauri nchini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula (hayupo pichani) leo katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020, leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli.
 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) Dk. Emanuel Malangalila leo wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020, leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli.

CHAMA CHA WASANII WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR KUZINDUA TAMASHA LA WAZI

CHAMA Cha wasanii wa Kizazi kipya Zanzibar (ZFU) , kimeandaa tamasha la Muziki Safari ya Mapinduzi ambalo linatarajiwa kufanyika  Desemba 15 mwaka huu  kwa lengo la kuenzi fikra za Mapinduzi na kutangaza kazi mbali mbali zinazofanywa na Wasanii wa kizazi kipya nchini.

Akizungumza mapema leo mjini Unguja na waandishi wa habari Rais wa Chama hicho,Mohamed Abdallah 'Laki wa Promise' amesema Chama hicho kimeamua kufanya tamasha hilo ambalo litafanyika katika jimbo la Mpendae Uwanja wa Zantex  litasaidia kukumbusha jamii umuhimu wa fikra za mapinduzi.

Rais huyo amesema katika tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Unguja, Abdulrahman Khatib ambapo kabla ya kuanza kwa tamasha hilo kutatanguliwa na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, uvutaji kamba na kukimbiza kuku. "Lengo kubwa ni kuchochea fikra za mapinduzi zilizofanywa na wanamapinduzi ambao wamepoteza maisha yao kwa ajili yetu ambapo kwa sasa tunaona mafanikio yake ikiwemo kuwepo kwa amani mpaka sasa hivyo ni jambo la kuwakumbusha Wanzanzibari.

kwa hiyo tutatumia vipaji vyetu vya kuimba kuwaambia jamii,"amesema Laki kuwa ni  jukumu la Chama hicho kupitia sanaa kuwahabarisha jamii umuhimu wa mapinduzi ya Januari 12, mwaka 1964 na kwamba lazima yalindwe kwa njia yeyote ile na kwamba kupitia tamasha hilo litasaidia kuipa jamii hisia kali za Mapinduzi hayo.  "Tamasha hili litaanza kuanzia saa 6 mchana hadi saa 12 jioni hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kwamba wasanii wengi watatoka Unguja na Pemba katika kutuimbuiza tamasha hilo na katika michezo itakayochezwa washindi watapewa zawadi mbalimbali,"ameeleza Rais huyo.

Akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja za Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo  Salum Said, amewasihi wananchi wa maeneo mbali mbali ya Mjini wa Zanzibar kuunga mkono juhudi za wasanii hao walioamua kwenda kwa jamii moja kwa moja kuonyesha vipaji vyao kupitia sanaa ya muziki. Amesema sanaa ya muziki ni moja ya kichocheo cha maendeleo ya nchi kwani inatoa ajira mbali mbali kwa vijana na makundi mengine ya kijamii, hivyo jamii inatakiwa kuacha dhana za kuamini kuwa usanii ni uhuni jambo ambalo sio kweli.

Amesema maandalizi yote ya tamasha hilo yamekamilika na kuanzia kesho wasanii wataanza kutikisa majukwaa ya burudani. Kwa upande wake Msemaji wa Chama hicho, Rashid Mustaafa 'Spaider'amesema matamasha kama hayo yanasaidia kukuza wasanii hivyo ni muhimu kuyaendeleza visiwani humu.

Amesema tamasha ya aina hiyo yanasaidia kukuza soko la muziki la hapa Zanzibar katika kufanya vizuri hivyo kwa upande mwingine yatasaidia kuibua vipaji vipya ambavyo vitakuwa ni azina kwa siku za baadae. "Tunaweza kufanya vizuri Chama kama pamoja na wasanii kwa upande mwingine hivyo tamasha ya aina haya yanasaidia sana katika ukuzaji wa vipaji,"ameeleza  Msemaji wa Chama Cha Wasanii.  

Tamasha hilo linaloanza kesho Desemba 15,mwaka huu litafikia tamati disemba 29,mwaka huu ambapo michezo mbali mbali itafanyika ikiwemo kuvuta kamba, mechi za mpira wa miguu,kufukuza kuku pamoja na Wasanii mbali mbali kutumbwiza mamia ya wananchi katika sehemu husika. Zawadi mbali mbali zitatolewa kwa washindi wa michezo hiyo na kwa mashabiki wa burudani watakaoonyesha uwezo wa kuimba na kucheza.
 RAIS wa Chama Cha Wasanii Zanzibar  Mohamed Abdalla 'Laki wa Promise' (wa pili kushoto), Msemaji wa Chama hicho Rashid Mustaafa 'Spaider'(wa kwanza kushoto),Mwenyekiti wa Tamasha Salum Said(wa kwanza kulia) wakizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa tamasha hilo.
BAADHI ya Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Habari mbali mbali visiwani Zanzibar wakisikiliza maelezo ya Rais wa Chama Cha Wasanii Zanzibar Mohamed Abdallah 'Laki wa Promise' juu ya uzinduzi wa Tamasha la muziki Safari ya Mapinduzi.

TANZANIA YAFUNGUA OFISI NDOGO YA UBALOZI HONGKONG CHINA

Na Grace Semfuko-MAELEZO
Tanzania imefungua ofisi ndogo ya kibalozi Hongkong nchini China ambayo itahudumia masuala ya kidiplomasia na kuongozwa na Balozi wa Heshima wa Tanzania Dkt Annie Wu alieteuliwa Septemba 2 mwaka huu na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga wakati alipohudhuria mkutano wa wa mahusiano ya China na Afrika,  FOCAC huko Beijing nchini China.

Ofisi hiyo mpya  katika jiji la  Hongkong,  nchini China itasimamia masuala ya kibalozi na kuwasogezea karibu huduma hizo, tofauti na hapo awali ambapo huduma za kibalozi zilikuwa zikipatikana Beijing.

Akizungumza Jijini Hongkong nchini China jana, Balozi wa Tanzania nchini humo, Mbelwa Kairuki, alisema ni fursa kwa watanzania na wachina kutumia ofisi ya Hongkong kupata huduma mbalimbali katika ofisi hiyo kwa urahisi.

Kwa upande wake Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini China, Dkt. Annie Wu ameonyesha kufurahishwa kuaminiwa na Serikali ya Tanzania kwa majukumu hayo ya heshima aliyopewa na kuihakikishia  serikali kuwa pamoja na mambo ya kidiplomasia, ataitangaza Tanzania kwa wawekezaji ili kuvutia uwekezaji zaidi.

Aidha amewakaribisha wadau wote watembelee ofisi mpya ya Tanzania ili kupata taarifa husika kuhusu utalii, biashara na uwekezaji  kwa manufaa ya  Tanzania na China.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania, Bw Geoffrey Mwambe amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo kutasaidia kuongeza uwekezaji zaidi, Kwani wafanyabiashara wa China watatumia Ubalozi huo katika kufuatilia masuala ya uwekezaji.

Balozi Dkt. Annie Wu, ambaye ni mtu mashuhuri nchini China na Hongkong anasifika kwa kuitangaza Tanzania kwenye masuala mbalimbali yakiwepo ya kibiashara na uwekezaji, pia aliwahi kuandaa makongamano ya kibiashara, yaliyojenga mahusiano ya uwekezaji  baina ya China na Tanzania, ambapo atahudumu kwenye nafasi hiyo ya Ubalozi wa Heshima-Hongkong kwa miaka mitano.

Kwa mujibu wa kituo cha uwekezaji Tanzania, TIC-China, China inaendelea kuongoza duniani kwa kuweka mitaji mikubwa nchini Tanzania; kwa zaidi ya dola Bilioni 5.8,  kuanzia mwaka 1990 mpaka 2017, ambapo kuna jumla ya miradi 723, huku ikitoa ajira 87,126 kwa thamani ya dola Milioni 5 962.74, ikifuatiwa na Uingereza, yenye miradi 936 ya thamani ya dola Milioni 5,540.07, iliyozaa ajira 274,401, na Marekani ikiwa na miradi 244 ya thamani ya dola 4,721.15, iliyozalisha ajira 51,880.

Tawimu hizo za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zimebainisha kuwa China inaendelea kuwa nchi yenye lengo la kuwekeza zaidi katika maeneo mbalimbali hapa nchini, yakiwemo  kilimo, viwanda, utalii, Ujenzi, Teknolojia ya Mawasiliano na maeneo mengineyo .

SERIKALI, MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO

 Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hasani Musa Kabeke akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa kuchangia damu kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya BAKWATA  yaliyofanyika kimkoa jijini Mwanza.
 Mgeni rasmi wa zoezi la kuchangia damu kwa waumini wa dini ya kiislamu jijini Mwanza, Mratibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Kanda ya Ziwa Abel Ntahorutoba akizungumza kwenye zoezi hilo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya BAKWATA.
 Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza na Mratibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Abel Ntahorutoba (kushoto) wakichangia damu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure.
 Katibu Muhtasi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza aliyehamika kwa jina moja la Sikitu akichangia damu siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya BAKWATA mkoani hapa. Wa kwanza kulia ni Katibu wa JUWAKITA Dotto Mangu.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Mkoa wa Mwanza Nurdin Mbaji akisiriki kuchagia damu kwenye maaadhimish ya miaka 50 ya baraza hilo.
Waumini wanawake wa dini hakuwa nyuma katika kuchangia damu kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya BAKWATA kimkoa yaliyofanyika jijini Mwanza. 
Afisa Eimu wa Dini ya Kiislamu Abdi Musa pamoja na waumini wa dini hiyo wakichangia damu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure. Picha na Baltazar Mashaka

SERIKALI,  MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

SERIKALI itaendeleza ushirikiano na madhehebu yote ya dini kwa kuwa ndiyo msingi wa amani na utulivu uliopo nchini na kuwataka viongozi  wa dini waisaidie kufichua ubadhirifu wa mapato ya serikali na kuiwezesha kuleta maendeleo ya nchi kwa maslahi ya wananchi. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dk. Severin Mathias Lalika kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela,kwenye kongamano la maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza Kuu la WaislamuTanzania (BAKWATA) yaliyofanyika kimkoa jijini humu.

“Tunaamini madhehebu ya dini ni msingi wa amani na utulivu wa nchi yetu, hivyo tutaendelea kushirikiana  kwa sababu viongozi wa kiroho mmeshikilia roho zetu hata mkitangulia kusema jambo letu la serikali linakubalika kwa haraka kwenye jamii,”alisema Mongela. Alisema Yesu na Mtume Muhhamad hakuna mahali hawakuhubiri upendo kwa matendo, amani na utulivu ambavyo kuwepo kwake ndio maendeleo na kutoa wito kwa viongozi wa dini waendelee kuisaidia serikali kuhubiri amani kwenye nyumba za ibada kwani hata katiba na sheria zilizotungwa msingi wake ni vitabu vya dini.

Alieleza kuwa taasisi mbalimbali za dini kushirikiana kuadhimisha miaka 50 ya BAKWATA mkoani Mwanza iwe chachu ya kupiga vita ya kiimani kati ya madhehebu ya Kiislamu na Kikrito ikizingatiwa ni watoto wa baba mmoja (Ibrahim), hivyo wakielewa hilo hakuna sababu ya kukosana. Mongela alisema serikali haijawahi kuwa na nia mbaya na wananchi wake lakini zipo changamoto zinazokwamisha maendeleo nazo ni dawa za kulevya, mimba za utotoni na VVU, hivyo viongozi wa dini shughuli zao za kiroho wanazofanya wayahubiri hayo.

“Sheria zinazotungwa na bunge na halmashauri zinatungwa wananchi wapate maendeleo ya pamoja.Penye changamoto na pasipoeleweka tuiteni tuje kufafanua.Pia nafahamu mnapenda sana Rais John Magufuli,mpendeni zaidi tupate maendeleo zaidi ya haya ya miaka mitatu maana hatukuwa na ndoto ya kujenga reli ya umeme,”alisema mkuu huyo wa mkoa. Alihimiza kuwajenga na kuwaimarisha vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kwa kushirikiana na serikali na kutoruhusu maadui wa nje wanaokwamisha maendeleo.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke alisema BAKWATA imedhamiria kuleta mabadiliko kwa kudai na kukusanya mali za waislamu pamoja na kuwaunganisha bila kujali taasisi zao. Alisema katika uongozi wake mkoani humu ataunda baraza la wazee litakalokuwa chini ya BAKWATA, pia uhakiki wa vyeti vya ndoa utafanyika sambamba na kuwasajili wafungishaji wa ndoa wawe na leseni badala ya kutumia watu holela.

Aidha, Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Mwanza Askofu Charles Sekelwa pamoja na Katibu Mwenza wa kamati hiyo Askofu Zenobius Isaya walisema ni fahari kuona waislamu na wakristo wakishirikiana pamoja. “Mwanzo tulikuwa maadui hata kutembeleana ilikuwa taabu sana,kumbe ulikuwa ujinga.Niwapongeze BAKWATA kwa kutimiza miaka 50 na kutembea kwa taasisi si jmbo rahisi na kuna changamoto nyingi.Hadi kufikia hapa viongozi walivumilia, kuna kudharauliana hivyo lazima tumshukuru Mungu,” alisema na kuongeza kuwa;

“Jambo la busara kwa binadamu ni kutazama mbele na si kurudi nyuma na kiongozi hapaswi kuangalia cangamoto za pembeni yake, hivyo tumwombee Mufti Abubakar Zuberi alipeleke jahazi la BAKWATA kule Mwenyezi Mungu alikokusudia.” Askofu Isaya yeye alisema akili na upeo wa kusimama kwa BAKWATA kumetokana uongozi wa mtu mwenye na maono ya baraza hilo kuhakikisha linakuwa kwa kiwango pamoja na taasisi zake.