Monday, August 31, 2015

SIMU TV: HABARI ZA USIKU WA LEO

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewatia mbaroni majambazi sugu 38 wakiwa na silaha za kivita kwa tuhuma mbalimbali. http://youtu.be/Iw4G2yTtLXc

Mgombea mwenza wa uraisi wa CCM ahaidi kujenga na kuboresha skimu za umwagiliaji pamoja na kuondoa tatizo la maji wilayani Bayi.http://youtu.be/cmErc5QXrWY

Mgombea uraisi Kupitia Chadema Edward Lowassa aendelea kunadi sera zake wilayani Makambako huku akihaidi kuresha afya, na tatizo la maji. http://youtu.be/lksrCjT18jk

Wizara ya  sayansi na teknolojia yatangaza rasmi kuanza kutumika kwa sheria ya makosa ya mtandao hapo kesho huku ikitoa tahadhari. http://youtu.be/psoGHFueeuw

Polisi Mkoani Morogoro imewapandisha kizimbani watu 10 kwa tuhuma za kuchoma kituo cha polisi pamoja na kula njama za kutenda kosa. http://youtu.be/LWfOIuMdtTs

Ukosefu wa mafunzo ya udereva wa kujihami miongoni mwa madereva wengi hapa nchini waelezwa kuwa sababu kubwa ya ajali za barabarani.http://youtu.be/oDSm8sR-Rr8

Mgombea uraisi wa CCM DR.Magufuli ahaidi kuondoa kero za wakulima mkoani Ruvuma huku akihaidi kuwapatia umemehttp://youtu.be/SDEMXpHmt-s

Chama cha ADC chazindua kampeni zake za uraisi kitaifa katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga. http://youtu.be/q9vLs7UpDjQ

Mgombea uraisi Kupitia Chadema Edward Lowassa aendelea kunadi sera zake Mkoani Njombe huku akihaidi kutatua migogoro ya ardhi. http://youtu.be/P5MUnVhmExw

Mgombea mwenza wa CCM afanya mikutano ya makundi mbalimbali ya wanawake wa mkoa wa Dodoma huku akihaidi neema kwa walemavu na wanawake wajasiriamali.http://youtu.be/Z1Wk4TgEEHI

Mgombea wa CCM ahaidi kupambana na Mafisadi pamoja na watendaji wazembe kazini endapo atachaguliwa kuwa raia wa Tanzania. http://youtu.be/1-6B3UUbNME

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr. Willbroad Slaa avunja ukimya apanga kuongea na watanzania kupitia vyombo vya habari hapo kesho. http://youtu.be/rVxs43Ais68

Umoja wa vyama vya katiba vya wananchi UKAWA wazindua kampeni zake katika jimbo la Babati huku akihaidi maendeleo katika jimbo hilo.http://youtu.be/wgabm6dJj8w

Shirika la umeme nchini Tanesco lakanusha kutumika kisiasa kuhujumu baadhi ya vyama huku liki bainisha matengenezo yanayoendelea. http://youtu.be/urYUtHuOkZc

Mvutano waripotiwa kuendelea katika umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kuhusiana na kusimamisha Mgombea mmoja jimbo la Mtwara mjini.http://youtu.be/2AGN1uWo4mQ

Katika hali ya kusikitisha mtu mmoja akutwa amekatwa viungo mbalimbali vya mwili wake ikiwemo nyeti katika chumba cha Hoteli mkoani Arusha.http://youtu.be/6irzDc7sKGQ

Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Dar es salaam  chazindua kampeni zake za ubunge na udiwani katika majimbo ya mkoa huo. Chama cha Mapinduzi Mkoani Morogoro chazindua kampeni zake za ubunge na udiwani
katika kata za jimbo la Morogoro mjini. http://youtu.be/vrEU3QjlStw

Chama cha ACT jimbo la Bukoba mjini chazindua kampeni za ubunge jimboni humo huku kikiwataka wananchi kutochagua viongozi wenye migogoro.http://youtu.be/6Z4mYbPkKzs

Mgombea uraisi Kupitia Chadema Edward Lowassa aendelea kunadi sera zake Mkoani Njombe huku akihaidi kuondoa matabaka kati ya masikini na matajiri.http://youtu.be/cVVj2r1mI-M

DC PAUL MAKONDA AZINDUZI WA VITABU VYA MWL.LILIAN NDEGI

MKUU wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda siku ya jana katika kanisa la Living Water Center chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi alikuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa vitabu vitatu  "MJUE MWANAMKE,USIIPE HOFU NAFASI na RAFIKI ANAYEKUFAA vilivyoandikwa na Mwl Lilian Ndegi wa Kanisa la Living Water Center Kawe.Ibada hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama Living Waters wenyeji Upendo Nkone,GUG Dancers na More Than Enough Band.
Mkuu huyo wa wilaya ndiye aliyezindua vitabu hivyo na kuendesha zoezi zima la uuzaji wa vitabu hvyo,kwa kuanza alinunua vitabu hivyo vitatu kwa shiling Milioni 5 ikiwa ni kuchangia na kusapoti huduma hiyo ya uandishi wa vitabu vya Mwl Lilian Ndegi ambaye ni Mama yake kwa malezi ya kiroho kanisani hapo Living Water Center Kawe.
Katika uzinduzi huo uliambatana na kukata keki ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kazi ya uandishi wa Mwl Lilian Ndegi na ugawaji wa zawadi katika tukio hilo ulifanyika kwa watu ambao wamekuwa wakihusika katika ufanikishaji kwa namna moja au nyingine au kumuwezesha Mwl Lilian kufanikisha uandishi wake wa vitabu.
Mh Paul Makonda aliwasihi washirika wa Kanisa la Living Water Center Kawe kusapoti kazi ya Mwl Lilian ikiwa ni kwa kununua na kuvisambaza vitabu vyake ili viwafikie wasomaji wengi ikiwa vitaleta matokeo mazuri katika maisha yao kutokana na ujumbe ulio ndani ya vitabu hivyo.
Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na mme wa mwandishi wa vitabu Mwl Lilian Ndegi katika kuzungumza kwake alikuwa akijivunia Mkuu huyo wa Wilaya na kusema ni kijana wake anamfahamu vizuri siku nyingi tangu bado anasoma na kusema amelelewa hapo na kusema kuwa alikuwa msikivu,na mpaka Mh Rais kumteua kwa nafasi hiyo ya kuwa Kiongozi wa Wilaya hakukosea.

Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda alipokuwa akizungumza baada ya kuzindua vitabu. 
Mh.Paul Makonda akizindua vitabu 
 Mh.Paul Makonda alipokuwa akionesha vitabu baada ya kuzindua
Apostle Ndegi akimlisha keki Mwl Lilian Ndegi ambaye ni mke wake ikiwa ni ishara ya kupongezana
Mh.Paul Makonda akilishwa keki Mwl Lilian Ndegi mwandishi wa vitabu vilivyozinduliwa
Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wa vitabu wa kwanza kush Mchungaji Deborah Ntepa,Mama Mchungaji Tumwidike koka Mbeya na Mwl. Lilian ndegi mwenyeji
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Mzee wa Kanisa vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Kiongozi wa mabinti Kanisani hapo Magreth vitabu baada ya kuvizindua

Mama Mchungaji Tumwidike kutoka mbeya alikuwepo katika uzinduzi huo
Mchungaji Deborah Ntepa kutoka Oasis Healing Ministry alikuwepo katika uzinduzi huo
Upendo Nkone alipokuwa akihudumu katika ibada ya uzinduzi wa vitabu iliyoongozwa na Mh. Makonda

Mwl Lilian Ndegi na Upendo Nkone wakicheza mbele za Bwana ilikuwa full shangwe
Mh.Paul Makonda wa kwanza kushoto,katikati ni Apostle Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na wa mwisho ni Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi 
Mh.Paul Makonda na Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya mabinti  wa kanisani hapo.
Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya wakina mama wa  kanisani hapo.

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOITIKISA RUVUMA LEO,MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA


 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini  humo mkoani Ruvuma,Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya. 

 Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani Ruvuma.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi,ambapo pia alimkabidhi Ilani ya chama hicho.

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini.
 Dk Magufuli akishuka kwenye Kivuko cha Mto Ruhuhu akitokea Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kwenda Mbinga  mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni za urais ubunge na udiwani. Dk Magufuli ameahidi kujenga daraja la mto huo.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkazi wa mji wa Peramiho ambaye ni mlemavu wa ngozi,jioni ya leo mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga.


 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25,kwa sababu ni Muaminifu,muadilifu na ni mchapa kazi.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji jioni ya leo.
 Maelfu ya Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa maji maji mjini Songea jioi ya leo kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,mkoani Ruvuma jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe aliwahutubia wananchi hao.
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbinga.
 Waanchi wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha-Peramiho mkoani Ruvuma jioni ya leo.
 Wananchi wakishangilia 
 Umati wa wakazi wa Peramiho wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tamasha ndani ya jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma. 
 Baadhi ya Wananchi wa Peramiho wakifurahia jamo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Mbinga.
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za ccm leo jioni ndani ya uwanja wa Maji Maji mjini Songea.

 Wananchi wa Songea mjini wakishangilia jambo wakati mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Maji maji mjini humo.

WASANII WAMUUNGA MKONO SAID FELLA

 Mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Kilungule Said Fella (kushoto) akiteta jambo  na mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mbagala Issa Mangungu, wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani ambazo zimezinduliwa jana.
Msanii Richard  Maviko, (katikati) akiwa na wasanii wenzake  wakitoa salamu maalum ya kumuunga mkono mgombea wa udiwani katika Kata ya Kilungule Said Fella, ambaye  amezindua rasmi kampeni katika kata hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lameck Ditto akiongea kwa niaba ya wasanii wenzake  ambao walikuwepo katika uzinduzi wa mgombea wa udiwani kata ya Kilungule iliyopo.

Asha Kigundula
WASANII mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya juzi walimuunga mkono Mkurugenzi wa  Kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yamoto Band na meneja wa Wanaume Family Said Fella, katika uzinduzi wa kampeni za kuwania Udiwani katika kata ya Kilungule, iliyopo  Mbagala Dar es Salaam.

Katika mkutano huo ambao ulifurika vilivyo kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) na wakazi wa kata hioyo kujitokeza kwa wiki kumsikiliza mgombea huyo, ambaye  alifanyika uzinduzi wake kwenye uwanja wa njia panda ya Chasimba Majimatitu B.

Baadhi wasanii hao ni Siti Almas, Amin Mwinyimkuu, Lameck Ditto, Rich Mavoko,  Queen  Darleen na meneja wa msanii Nassib Abdul Hamis Taletale  'Babu Tale'.

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake   Ditto aliwataka wakazi wa Maji matitu  kutofanya makosa kwa kumpa mpinzani, wampe Said Fella ili awe diwani wao.

Alisema kila mtu atambue kuwa ukimchagua mtu wa CCM utakuwa umefanya jambo la  muhimu kwa sababu ndiyo anayeweza kutelekeza ilani ya chama hicho.

Ditto alisema atamfahamu Fella ni mchapakazi hivyo kumpa kwake kata hiyo lazima iwe  na mafanikio makubwa.

Alisema sehemu yoyote anayokuwepo Fella lazima iwe na mafanikio hivyo hata kama hiyo  itakuwa moja ya kata zenye mafanikio makubwa.

"Naomba msifanye makosa kuchagua upinzani mchagueni Fella kuwa diwani wenu na  mchagueni Issa Makungu kuwa mbunge wenu wa Mbagala na John Magufuli kuwa Rais wa  Tanzania"alisema Ditto.

Akizungumza kwa upande wake Fella alisema anaitambua Kata hiyo ina matatizo mengi,  hivyo akipata nafasi atahakikisha anaziofanyia kazi.

Fella alisema yeye ni mkazi wa eneo hilo ana amini kupata kwake nafasi kutatua mambo  mengi kwa kuwa yupo karibu na viongozi wakubwa ambao atakuwa akikutana nao.

"Nitaweza kukutana na viongozi wakubwa na kutatua matatizo yetu ya huku Kilungule  ambayo ninayofahamu vizuri kwa sababu nami ndiyo mkazi wa eneo hilo"alisema Fella.

WATANZANIA WAHIMIZWA KUTUMIA HUDUMA ZA BIMA.

Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora.

Jovina Bujulu-MAELEZO
WATANZANIA theluthi mbili hawana ufahamu wa kutosha kuhusu namna Bima inavyofanya kazi nchini hasa Bima ya Maisha na Mali.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora alipokuwa akifunga mafunzo ya wiki ya huduma kifedha na uwekezaji mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

Kamuzora aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kueneza ujuzi na ufahamu waliopata ili wananchi walio wengi waweze kunufaika na huduma za bima nchini.

“Ninawaomba muwe mabalozi wazuri wa kueneza ufahamu juu ya faida za Bima kwa ndugu, jamaa na marafiki ambayo ni mojawapo ya mbinu za kujilinda kimaisha na kujikwamua katika umasikini”. Alisema Kamuzora.

Kamuzora alisema kuwa kwa upande wao kama waratibu wa huduma za Bima nchini wanao wajibu wa kuendelea kujenga mazingira ambayo ni rafiki na wezeshi kwa watoa huduma  ya Bima ili waendelee kuwa wabunifu katika kufikisha huduma hiyo kwa Watanzania wenye uwezo mkubwa na mdogo.

Aidha, Bw. Kamuzora alisema kuwa mpango wa Taifa wa huduma Jumuishi za kifedha nchini unalenga kuwafikia watu wazima asilimia 50 wanaotumia huduma rasmi za kifedha ifikapo mwaka 2016.

Ili kufanikisha mpango huo, Bw. Kamuzora alitoa wito kwa taasisi za kifedha na za utafiti wa sayansi kuendelea kushirikiana na mamlaka ya Bima kuona namna ya kuendeleaza matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya kuwapatia wananchi fursa ya kupata huduma za Bima ili kulinda mali na maisha ya Watanzania waliowengi.

Hadi sasa nchini, takwimu zinaonyesha kuwa karibu asilimia 90 ya wenye simu za mkononi nchini wanatumia huduma za fedha za simu ziliongeza ndugu Kamuzora.

Mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yalipambwa kwa kauli mbiu inayosema “Maisha ni Duni Bila Bima” yaliwahusisha wajariamali, benki, na kampuni za Bima yalidhaminiwa na kampuni ya NUEBRAND na Shirika la PESCODE.

WATUMIAJI WA MITANDAO VIBAYA SHERIA KUWADHIBITI KUANZA LEO SAA 6:00 USIKU.

 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini jijini Dar es Salaam leo.

Na Magreth Kinabo 
SHERIA mpya   ya Makosa ya Mtandao ya mwaka   2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 zitaanza kutumika rasmi kesho Septemba Mosi mwaka huu, hivyo watumiaji   na watoa huduma waaswa kuzingatia sheria hizi ili kuepuka mkondo wa sheria.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

“Sheria hizi ni nzuri zitaanza kutumika Septemba Mosi mwaka huu,kuanzia saa 6.00 usiku . zina maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya Taifa letu,” alisema Profesa Mbarawa.

 Aliongeza kuwa sheria hiyo ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 hazihitaji utungaji wa kanuni kwa kuwa iko wazi.

 Alisema tayari wizara imeanza kuelimisha watu kuhusu sheria hiyo na itendelea kuwajengea uwezo wadau mbalimbali.

Profesa Mbarawa alisema sheria ya makosa ya mtando ya mwaka 2015 na Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa nayo, bali nchi mbalimbali zina sheria kama hiyo ,ambapo alitolea mfano Uingereza,India,Malaysia, Uganda na Korea ya Kusini.

 Akizungumzia kuhusu  madai sheria hiyo kuhusika na suala la Uchaguzi Mkuu, alisema si kweli, bali imekamilika katika kipindi hicho ndio maana baadhi ya watu wanadai hivyo.Aliongeza kwamba sheria hiyo imetunga ili kudhibiti matumizi ambayo  si mazuri. 

“ Mtu akitumiwa ujumbe akiupokea hapaswi kuisambaza  kwani atakapousambaza atakuwa na amefanya kosa,”alisisitiza.

Aliyataja baadhi ya makosa kuwa ni usiri, usalama wa upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo  kama vilekuingilia mawasiliano ya kompyuta au mifumo ya kompyuta kinyume cha sheria na wizi wa taarifa kimtandao.

Makosa  dhidi ya kompyuta ikiwa ni pamoja na,udanganyifu kwa kutumia kompyuta,kugushi kwa kutumia kompyuta wizi wa utambulisho wa mtu binafsi  mtandaoni, matumizi ya vifaa kinyume cha sheria.

Makosa yanayohusiana kimaudhui kama vile usambazaji wa ponografia, ponografia za watoto makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki, michezo ya kmari mtanadaoni kiunyume cha sheria, kashfa na habari za uongo na makosa dhidi ya haki na hati miliki.

Pia inatambua muungano wa makosa inajumuisha kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa kutumia mtandao.

Kwa upande wa sheria ya miamala ya kieletroniki ya mwaka 2015, baadhi ya makosa likiwemo la wajibu wa watoa huduma kwa walaji, bidhaa ,huduma au mawasiliano ambayo hayajaombwa na uhalali wa Muamala wa elektroniki.

Aliongeza kuwa kanuni za sheria hiyo zinatayarishwa zikiwa tayari zitangazwa  na zitaanza kutumika wakati wowote.

STARS YAMALIZA KAMBI UTURUKI

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro chini ya Kocha wake Mkuu Charles Boniface Mkwasa imefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe – Kocaeli nchini Uturuki.
Taifa Stars ambayo imeweka kambi nchini Uturuki kwa takribani wiki moja, inajiwinda na mchezo wake dhidi ya Nigeria siku ya Jumamosi Septemba 5, 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017.
Kocha Mkuu wa Stars Charles Mkwasa akiongea na tovuti rasmi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) www.tff.or.tz amesema anashukuru kambi imekua na mafanikio makubwa kwani vijana wanaonyesha mabadiliko makubwa sana.
“Ukiondoa mchezaji moja tu ambaye ni majeruhi Abdi Banda, Mkwasa amesema wachezaji wengine wote wapo fit na kila mmoja atakayepata nafasi katika mchezo wa sikuya jumamosi atafanya vizuri” amesema Mkwasa.
Mkwasa amesema mazingira ya kambi yamekua mazuri, na katika mechi ya maozezi dhidi ya Libya iliyochezwa siku ya ijumaa, vijana wake walicheza vizuri kwa nguvu na kufuata maelekezo yake, makosa machache yaliyojitokeza katika mchezo huo wameyafanyia kazi na sasa anaamini wako tayari kuwakabili Nigeria.
Mwisho Mkwasa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa siku ya jumamosi  kuishangilia timu ya Taifa, kwani uwepo wa washabiki wengi uwanjani utawaongeza morali zaidi wachezaji na kujiona wapo nyumbani wanapambana kwa ajili ya Taifa lao.
Naye nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub “Cannavaro” amesema maandalizi waliyopata ni mazuri na yamewajenga vilivyo kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Nigeria siku ya jumamosi na kuwaomba watanzania kuja kwa wingi kuwasapoti.
Nadir amesema wao kama wachezaji kila mmoja yupo fit na anahitaji  kucheza mechi hiyo, hivyo yeyote atakayepata nafasi ya kucheza ana imani atafanya vizuri katika kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Stars ambayo iliweka kambi ya takribani siku nane katika milima ya Katrepe - Kocaeli, inatarajiwa kuodoka kesho jumanne saa 1 jioni nchini Uturuki kurejea nyumbani kwa usafiri wa shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) na kuwasili uwanja wa JK Nyerere majira ya saa 9 kasoro usiku.
Mara baada ya kuwasili Dar es salaam timu itaendelea na kambi kwa kufanya mazoezi mepesi siku ya jumatano pamoja wa wachezaji wa kimataifa Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya Nigeria.

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA QATAR NA BURUNDI LEO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mhe. Abdulla Jassim Al Maadadi wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mhe. Abdulla Jassim Al Maadadi wakati Mabalozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015 .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu    Dar es salaam leo Agosti 31,2015 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015, kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka wakati Mabalozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015, kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. (Picha na OMR)