Saturday, February 28, 2015

WAVAMIZI NA WAMILIKI WA ARDHI KINYUME CHA SHERIA JIJINI DAR KUKIONA, KUKUMBWA NA BOMOA BOMOA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Alphayo Kidata (kulia) bakitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa awamu ya tatu linaloendelea katika Manispaa ya Kinondoni jana jijini la Dar es salaam.Kulia ni Muhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Baraka Mkuya.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bw. Alphayo Kidata (hayupo pichani) alipokuwa akitoa tathmini ya zoezi la bomoa bomoa kwa wananchi waliovamia maeneo yanayomilikiwa kisheria na watu wengine katika manispaa ya Kinondoni jana jijini Dar es salaam.
Moja ya ukuta uliojengwa kinyume cha sheria katika eneo lisiloruhusiwa eneo la Tegeta ukibomolewa jana.
Baadhi ya wananchi katika manispaa ya Kinondoni wakiondoa bidhaa zo katika maduka eneo la Tegeta Machakani kupisha zoezi la bomoa bomoa kufuatia maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.
Fundi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) akiendelea na zoezi la kukata umeme eneo la Mikocheni B kufuatia zoezi la bomoa bomoa lililokuwa likiendeshwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Manispaa ya Kinondoni, jana jijini Dar es salaam.
Tingatinga likiendelea kubomoa maduka eneo la Tegeta Machakani kufuatia maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jana jijini Dar es salaam.
Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi wakati wa zoezi la bomoa bomoa maeneo ya wazi na yale yaliyochukuliwa kinyume cha sheria kutoka kwa wananchi wanaoyamiliki kihalali eneo la Mikocheni na Tegeta jijini Dar es salaam.

Waziri Fenella akutana na wasanii nchini

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimueleza jambo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Francis Michael wakati wa mkutano na wasanii uliofanyika katika ukumbi wa uwanja mpya wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko akiongea na wasanii nchini na kuwaeleza kuhusu umuhimu wa sekta hiyo kushiriki kikamilifu katika masuala ya kitaifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea upatikanaji wa Katiba Mpya, Kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fisoo.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na wasanii nchini na kuwaasa wasanii kuielimisha na kuhamasisha Jamii kuhusu Katiba Inayopendekezwa kupitia kazi mbalimbali za sanaa, wakati wa mkutano na wasanii nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Francis Michael akiongea na wasanii nchini na kuwaeleza namna gani makundi mbalimbali yalivyoainishwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ikiwemo haki za wasanii tofauti na Katiba ya Mwaka 1977.
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na baadhi ya wasanii mara baada ya kuisha kwa mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara wakati wa mkutano huo.

TASWIRA MBALI MBALI ZA ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYANI RUNGWEWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Misingi la ujenzi wa nyumba za watunmishi wa Halmashauri ya Busokeleo wilayani Tukutu unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika kijiji cha Rungwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Beya Februari 27, 2015. Wapili kushoto ni mkewe Tunu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akigua nyumba zinazojengwa na Shirikal la Nyumba la Taifa (NHC) karika kijiji cha Rungwa kwa ajili ya watumishi wa Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 27, 2015. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mark Mwandosy na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa NHC, Haikaman Mlekio.Mke wa Waziri Mkuu, Mamam Tunu Pinda akivalishwa kitenge na bibi Hilda Mwasikili katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mjini Tukuyu Februari 27, 2015.
Mh. Al Shaimar kwa ushirikiano na Bayport wa wazitembelea familia za watoto Albino waliopoteza maisha Jijini Mwanza

Meneja Mauzo wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugaano Kasambala, akimpa pole Ester Jonas, mama wa Yohana Bahati, mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino, aliuawa mkoani Mwanza, hivi karibuni. Mama huyo anatibiwa katika Hospitali ya Bugando baada ya kupata mareraha katika tukio la kuvamiwa na kuporwa mtoto wake. Kulia kwa Kasambala ni Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani waliyeambatana katika safari hiyo kwa ajili ya kuwapa pole na kuwafariji.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MBUNGE wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir kwa ushirikiano na Taasisi ya Kifedha, inayojihusisha na mikopo ya Bayport Financial Services yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, Tanzania, walifanya ziara ya siku mbili jijini Mwanza kwa ajili ya kutembelea familia mbili zilizopoteza watoto wao wawili ambao ni walemavu wa ngozi.

Familia hizo ni ya Ester Jonas, mama wa marehemu Yohana Bahati na ile ya Sofia Juma mama wa mtoto Pendo Emmanuel, wote wakiwa ni watu wenye ulemavu wa ngozi, huku familia zote mbili zikipewa Sh Milioni 2 kila moja.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir mwenye miwani akimfariji mama wa Yohana Bahati (Ester Jonas) aliyelazwa Hospitali ya Bugando, Mwanza, pamoja na kumpaa mafuta ya kupaka kwa ajili ya watoto wake wawili ambao nao ni albino,. Kushoto kwa Mh Shaimar ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala na wafanyakazi wengine wa Bayport waliombatana pamoja kwenye msafara huo wa kutoa pole.

Akizungumza katika safari hiyo, Mbunge Shaimar alisema ameendelea kusikitishwa na mauaji hayo ya albino yanayotoa haki ya kuishi ya watu wote wenye ulemavu wa ngozi, huku akiitaka jamii kuacha kufavya vitendo hivyo visivyokuwa vya kiungwana kutokana na kudhulumu haki za kuishi za binadamu wenzao.
“Naumia juu ya vitendo hivi kwasababu na mimi nipo kwenye kundi hili lawatu wenye ulemavu wa ngozi wanaoendelea kupukutika siku hadi siku, hivyo tupambane na majangili haya, maana najua Mheshimiwa Rais, Dr Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wamekuwa wakiguswaa mno na matukio haya yanayoichafua nchi yetu,' alisema Shaimar, ambapo pia aliishukuru Bayport Financial Services kuingia katika harakati za kupambana na mauaji ya albino nchini Tanzania.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyri (katikati), akizungumza na binti aliyekutwa nyumbani kwa Ester Jonas, mama wa albino Pendo Bahati aliyeporwa na haijulikani alipokuwa. Kulia kwake ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services, Lugano Kasambala, aliyeambatana na mbunge huyo.

Naye Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, alisema taasisi yao imeguswa na mauaji hayo na kuitaka jamii kushirikiana na viongozi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama katika kupambana vikali na watu wanaoendeleza kufanya unyama wa kuteka watu wenye ulemavu wa ngozi kwa sababu wanazojua wenyewe.

Alisema hali hiyo waliamua kufanya safari moja na mbunge Shaimar ambaye kiuhalisia ni balozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi, huku akiamini kwa ushirikiano huo unaweza kupunguza au kuondosha kabisa vitendo hivyo vya mauaji ya albino yanayoendelea kushika kasi katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara.
Wengine waliombatana kwenye ziara hiyo ni pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii Mwanza, Leah Linti, Katibu Tawala Msaidizi Crecencia Joseph, Mweka Hazina wa Chama cha Albino Taifa (TAS), Abdullah Omari, Jeshi la Polisi wilayani Misungwi, huku safari zote zikiwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanzaa, Magesa Mulongo.

TUZO ZA WASANII BORA WA MUZIKI WA ZANZIBAR MWAKA 2015

Mkurugenzi wa Biashara Zanzibar Nd. Mohamed Baucha wa kulia akimkabidhi Tunzo ya Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya Nassir Hassan (Vanila) mara baada ya kuibuka mshindi, tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation LTD katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Hall  Bwawani Mjini Zanzibar.
 Mwanamitindo marufu wa Zanzibar Farouk Abdillahi akimkabidhi Tunzo ya Video bora mwaka ya Taraab Bi. Saada Nassor
 Mwanamuziki bora wa mwaka wa Afro poo Saidi Kitwana (Mabawa) kushoto akipokea tunzo kwa Katibu Mtendaji Bodi ya Sensa Zanzibar Nd. Suleiman Mbarouk.
 Meneja wa Zenji Entertainment Seif Moh'd (kushoto) akimkabidhi tunzo Mwanamuziki Bora wa kiume wa tarabu asili Cholo Ganun.
 Mwakilishi kutoka Baraza la Sanaa Zanzibar Maulid Madam akimkabidhi tunzo ya Mwanamuziki bora wa kike wa Tarab asili Bi. Rukia Ramadhan katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar.
 Meneja wa Fedha Z.M.C.L Bi. Saide Moh'd akimkabidhi tunzo Mwanamuziki bora wa mwaka wa kizazi kipya Riko Singo katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar.
 Mwanamuziki bora wa mwaka wa kike wa kizazi kipya Baby J akipokea tunzo kwa Meneja wa Z.M.C.L Tawi la Dar es Salam mara baada ya kuipuka kidedea tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Midia Corporation LTD iliopo Zanzibar.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wadau mbali mbali wakishuhudia wasanii wa Zanzibar wakipewa tunzo katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar.
 Wasanii wa kikundi cha Smart Comed Zanzibar wakitoa Burudani.
 Msani Mr Blue akitumbuiza katika Tamasha la Wasanii wa Zanzibar.
 Mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikiulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akimkabidhi tunzo ya muandaaji bora wa Tamasha Zanzibar Music Award mwaka 2015 Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa Redio ya Zenji FM Mohamed Seif Khatib katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar. 
 Mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikiulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Zanzibar Midia Corporation LTD. Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

Friday, February 27, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti (Mammograph) kwa akinamama katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kwenye kitengo cha Uzazi na mtoto kilichopo eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhmu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupima saratani ya matiti kwa akina mama katika Hospitali ya Lugalo tarehe 27.5.2015.

Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Ulinzi na wananchi waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto cha hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akimpongeza Mama Salma Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwenye hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo tarehe 27.2.2015.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe 27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama tarehe 27.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles,28, baba mzazi wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni kupunguza baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya joto. Mama Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake kwenda kliniki. PICHA NA JOHN LUKUWI