Wednesday, November 30, 2011

JERRY MURO MARA BAADA YA KUFUTWA KWA KESI YAKE

Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Jerry Muro na mke wake wakitoka mahakamani.
Mmoja kati ya watuhumiwa waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya shilingi milioni kumi, Edmund Kapama akitoka katika chumba cha Mahakama huku akina na furaha kwa kuwa huru.
Nipo huru sasa.
Pascal Kamara wakili wa Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya kisutu.
Pokea Mvinyo Baba.

Waandishi wa habari wakiwa Mahakamani hapo 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewaachia huru kwa mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jarry Muro na wenzake wawili.

Hakimu Frank Moshi, alisema anawaachia washitakiwa hao kwasababu upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi shaka.

Muro, Edmond Kapama pamoja na deogratius Mgasa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba na kutaka kupokea rushwa ya Sh milioni 10 toka kwa aliyekuwa Muhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage.

Mashitaka yao yalikuwa ni ya kula njama, kuomba rushwa na kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU shitaka linalowakabili Mgasa na kapama.

Muro baada ya kutoka mahakamani alitangaza kwa wanahabari kuwasamehe wabaya wake wote ambao ni viongozi wa serikali baadhi na baadhi ya maafisa wa polisi na kuwataka waandishi wa habari kushikamana kuendelea kuibua uozo unaoendelea bila woga.

Katika hukumu, hakimu Moshi alisema baada ya kuangalia ushahidi mahakama ilikuwa na maswali ya kujiuliza kama upande wa jamuhuri uliweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa ambapo shitaka la kula njama kwa nia ya kuomba rushwa ambalo linawahusu washitakiwa wote, ushahidi ulikuwa wa Wage.

Shahidi huyo wa tatu wa jamuhuri lisema alikutana na Muro kwenye mgahawa wa Califonia ambapo mawasiliano kati yao yaliendelea kwa njia ya simu ya mkononi. 

Ushahidi huo ulikuwa hafifu kwasababu upande wa mashitaka haukuweza kuwasilisha karatasi ya mawasiliano kati yao kutoka kwenye kampuni ya mtandao wa simu (printout).

Vile vile alisema picha za CCTV iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa ni kivuli kisichoonyesha sura za watu badala yake wangeleta CD kuonyesha kwenye video ili watu waweze kutambulika kwa urahisi. 

Mawasiliano ni jambo la msingi kwasababu ili kula njama ni lazima mawasiliano yafanyike hivyo kuna mapungufu makubwa katika shitaka hilo.

Dereva aliyemwendesha wa Wage alidaiwa kuwa na Wage pale mgahawa wa Califonia walipokutana na Muro, alitakiwa kuletwa athibitishe kama Wage na Muro walikutana upande wa mashitaka hawakumwita shahidi huyo.

Katika shitaka la kuomba rushwa lilowakabili wote katika ushahidi wake Wage, alieleza Muro na wenzake walimtaka awapatie Sh milioni 10 watamsaidia kwenye tuhuma zinazomkabili lakini hakuwa nazo akawapa sh milioni moja mbali na ushahidi huo hakuna ushahidi mwingine wa serikali unaoonyesha kuwa walipokea fedha hiyo.

“Mahakama ilitegemea kuwe na ushahidi wa mawasiliano kama haupo wa kuona lakini hayo yote hayakufanyika,” alisema hakimu Moshi.

Muro alikamatwa ndani ya gari, mahakama haielewi ni kwanini kulikuwa na haraka hiyo kwanini asingeachwa wakakutana na Wage. Kwa upande wa hotel ya Sea Cliff ni sehemu ya watu yoyote anaweza kwenda.

Washitakiwa Mgasa na Kapama hakimu Moshi alisema hawakukamatwa eneo la tukio walikamatwa na kuunganishwa na halikufanyika gwaride la kuwatambua na cheti kuletwa mahakamani.

Shitaka la linalowakabili Mgasa na Kapama la kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU mahakama ilisema halikuthibitishwa lina mashaka. Alisema washitakiwa walijitambulisha kwa moja anaitwa Dr na mwingine Musa.

Upande wa mashitaka ulitakiwa kufatilia mtaani kama majina hayo washitakiwa walikuwa wakiyatumia lakini hilo halikufanyika.

“Wage kama msomi ngazi ya uhasibu aliwezaje kukubali mtu ajitambulishe kwa mdomo kama afisa wa TAKUKURU bila kuonyeshwa vitambulisho na akakubali mahakama inapata mashaka”. 

Aliongeza hakimu huyo hakuna vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha bila kuacha shaka hivyo wanaachiwa huru kwa mashitaka yote.

Alisema Moshi risiti, pingu na miwani havikuwa na mgogoro katika kesi na kwavile vilipatikana kwa risiti basi arudishiwe muhusika na upande unataka kukata rufaa wana ruhusiwa. Wakili kiongozi wa kesi hiyo Boniface Stanslaus alisema taafifa atampelekea Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ataamua kama watakata rufaa.

Washitakiwa walifikishwa mahakamani Februari 5 mwaka jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu mkazi, Gabriel Mirumbe.

Monday, November 28, 2011

Rais Kikwete ashiriki MAHAFALI YA 11 YA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Jaji Mkuu Mh Mohamed Chande Othman mara baada ya kuwasili katika sherehe za mahafali ya 11 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, mkoani Tanga
 Rais Jakaya Kikwete akipokewa na Jaji Mkuu Mh Mohamed Chande Othman kwenye sherehe hizo
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Sheria mstaafu Mh Bakari Mwapachu
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Jaji Bwana
 Rais Kikwete akisalimiana na mwakilishi toka PPF
 Waalikwa wakimsubiri kumlaki mgeni rasmi
 Rais Kikwete akisalimiana na mke wa Jaji Mkuu, Mama Saada Othman
 Wapiganaji wa habari wa mkoani Tanga walikuwepo kurekodi sherehe hii
 Rais Kikwete  akifunua kitambaa kuashiria kuwekwa kwa jiwe la msingi kwa jengo la hosteli ya wanaume chuoni hapo. Nyuma yake ni hosteli ya wanawake ambayo imekamilika
 Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya ujenzi wa hosteli ya wanaume toka kwa Msajili wa Mahakama ya Rufani Mh Francis Mutungi
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifunua kitambaa kufungua hosteli ya wanawake iliyopewa jina lake
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kufungua hosteli ya wanawake iliyopewa jina lake
 Mama Salma Kikwete akikagua moja ya vyumba katika hosteli ya wanawake chuoni hapo. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Celina Kombani na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mama Chiku Gallawa
 Rais Kikwete akiongozana na uongozi wa chuo kuelekea kwenye mahafali
 Baadhi ya wafanyakazi katika chuo hicho wakiwa katika mahafali
 Waziri wa Sheria na Katiba Mh Celina Kombani (shoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Chiku Gallawa na mkuu wa Wilaya ya Lushoto na viongozi wastaafu wa chuo hicho pamoja na wake wa Jaji Mkuu na mke wa mkuu wa Chuo
 Wimbo wa Taifa
 Mama Salma kikwete akiwa na Waziri wa Sheria na katiba Mh Celina Kombani (kulia) na Mke wa Jaji Mkuu, Mama Saada Othman (shoto)
 Mke wa Jaji Mkuu Mama Saada Othman akimpongeza Mkuu wa Chuo wa kwanza baada ya kupewa tuzo na Rais Kikwete
 Rais kikwete na Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo wa sasa na uliopita pamoja na uongozi wa mkoa wa Tanga na wilaya ya Lushoto
 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo na Jaji Mkuu Mh Mohamed Chande Othman akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mahafali
  Mama Salma Kikwete akipanda mti
 Juu na Chini Rais Kikwete, Jaji Mkuu Mh Chande Othman na Mkuu wa Chuo wakipozi na wahitimu wa Cheti cha Sheria 

 Rais Kikwete, Jaji Mkuu Mh Chande Othman na Mkuu wa Chuo wakipozi na wahitimu wa Cheti cha Sheria 
 Rais Kikwete akimtunuku tuzo Balozi Paul Rupia aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo kilipoanzishwa mwaka 2000
 Rais Kikwete akihutubia
 Rais Kikwete akihutubia kwenye mahafali hayo
Rais Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo na Jaji Mkuu Mh Mohamed Chande Othman kwenye mahafali hayo
Rais Kikwete akipanda mti

Sunday, November 27, 2011

MKUTANO WA KIHISTORIA KATI YA RAIS KIKWETE NA UONGOZI WA CHADEMA IKULU DAR ES SALAAM LEO NOVEMBA 27, 2011

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo toka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe baada ya kupokea  mapendekezo ya chama hicho juu ya kuundwa katiba mpya yatayozungumzwa kwenye mkutano huo wa kihistoria uliofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa CHADEMA katika mkutano huo wa kihistoria
 Mkutano ukiendelea 
 Rais Jakaya Kikwete akiongea na uongozi wa CHADEMA (kushoto) pamoja na ujumbe wa Serikali (kulia)
 Mh. Tundu Lissu akikoroga chai baada ya mkutano huku Profesa Baregu naye akijiandaa kujisevia
 Rais Jakaya Kikwete akimpa juisi Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe baada ya mkutano
 Rais Jakaya Kikwete akiongea na wageni wake kwa bashasha baada ya mkutano
 Rais Kikwete na wageni wake wakilegeza makoo baada ya masaa mawili na nusu ya mkutano
 Rais Jakaya Kikwete akiongea na wageni wake
 Furaha ilitawala baada ya kumalizika kwa mkutano na wageni kuinuka na kuaga
 "....Asante sana Mh Rais kwa kukubali mwaliko wetu..." anasema Mh Freeman Mbowe wakati akiaga
 Mh Arfi akiaga
 Kaimu Katibu Mkuu Mh John Mnyika akiaga. Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa alitoa udhuru kuwa unauguliwa hivyo hakuweza kufika
 Mh Mrema akiaga
 Kwaheri Mheshimiwa na asante kwa kutukaribisha Ikulu...
 Profesa Mwesiga Baregu akiaga
 Profesa Abdallah Safari akiaga
 Mh Tundu Lissu akiaga
Mh Tundu Lissu akiondola Ikulu taratibu baada ya mkutano huku gari iliyombeba mwenyekiti wa CHADEMA ikiondoka pia...