Sunday, June 30, 2013

MAMA SALMA KIKWETE NA WAKE WA MARAIS WALIOKUWA KWENYE MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP WATEMBELEA MAONESHO

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya kumaliza ziara yake na ugeni aliouongoza kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho tarehe 30.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na ,mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Inkhosikati Lambikiza (kushoto) na Waziri wa Jinsia, watoto na familia wa DR Congo ambaye amemwakilisha mke wa Rais Joseph Kabila Mheshimiwa Inagosi Bulo na mke wa Makamu wa Rais wa Zambia Mama Charlotte Scott wakianza kutembelea mabanda kwenye uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere, kwenye barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tarehe 30.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandamana na Mheshimiwa Inagosi Bulo kutoka DRC (kushoto) na Inkhosikati Lambikiza wa Swaziland na Mama Charlotte Scott wa Zambia wakiwa nje ya banda la Zanzibar mara baada ya kutembelea banda hilo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Maendeleo Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali za aina ya shanga zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda la SIDO wakati walipotembelea maonesho hayo tarehe 30.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na wageni wake wakiangalia mashine ya kutengeneza nguo aina ya vikoi kwenye banda la SIDO wakati walipotembelea banda hilo tarehe 30.6.2013.
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia Mama Charlotte Scott ambaye aliondoka uwanjani hapo kwenda uwanja wa ndege kuungana na mume wake kwa ajili ya safari bya kurudi nchini Zambia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Waziri Inagosi Bulo kutoka DRC (kushoto) na Inkhosikati Lambikiza wa Swaziland (kulia) wakiangalia bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kutoka kwenye mnazi kama zilivyokuwa zikionyeshwa na akina mama kwenye banda la WIPE.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na wageni wake wakitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho wakiongozwa na Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Gregory Teu tarehe 30.6.2013.

Kaskazini Unguja yaongoza kwa ajali barabarani

Na Salum Vuai, Maelezo

WATU 52 wamepoteza maisha na wengine 332 wamejeruhiwa kutokana na ajali 175 za barabarani zilizotokea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kati ya Januari mwaka 2011 hadi katikati ya mwaka 2013.

Takwimu hizo zimetolewa leo na Mkuu wa Usalama Barabarani wa jeshi la Polisi mkoani humo Ali Muhsin, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya ‘Safiri Salama’, yaliyofanyika katika viwanja vya Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B.

Mkuu huyo alisema, ajali za barabarani ni tishio kubwa kwa watumiaji wote wa barabara, wakiwemo madereva, abiria na watembeao kwa miguu, na kwamba tahadhari kubwa inahitaji kuchukuliwa kuziepuka.

Alieleza kuwa, endapo watumiaji wa barabara hawatakuwa waangalifu, majanga ya maafa, ulemavu wa kudumu, majeraha, hasara kwa mali na uharibifu wa miundombinu, vitaendelea kuliandama taifa.

Alitaja sababu mbalimbali zinazochangia ajali hizo, kuwa ni uhaba wa miundombinu imara, ubovu wa vyombo vya moto, mabadiliko ya hali ya hewa, utendaji mbaya wa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani na kasoro za kibinadamu.

Ili kumaliza au kupunguza ajali za barabarani, Muhsin alisema hatua kadhaa zinapaswa kuchukuliwa, ikiwemo kutoruhusu magari na vyombo vyengine visiingizwe barabarani hadi vithibitishe kuwa na sifa kwa mujibu wa sheria.

Aidha alishauri vyombo vyenye majukumu ya kutoa huduma kwa umma na kusimamia sheria kama vile polisi, mahakama, Idara ya Usafiri na Leseni, Bodi ya Mapato Zanzibar na vyengine, vitekeleze majukumu yao kwa uadilifu na uaminifu.

Kwa upande wake, mgeni rasmi katika sherehe hizo Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa, alisema ajali za barabarani ndizo zinazoongoza kwa kuua watu wengi, kuliko vifo vitokanavyo na sababu nyengine.

Alieleza, takwimu zinaonesha kuwa, takriban watu milioni moja na laki mbili hufariki kwa ajali hizo kila mwaka duniani kote.

Kwa Zanzibar, alisema ajali 3869, zimeripotiwa kutokea kati ya mwaka 2009 hadi 2012, ambapo kati ya hizo, watu 450 walipoteza maisha, na 3855 walipata majeraha mbalimbali.

Kamishna huyo aliongeza kuwa, kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka 2013, jumla ya ajali 196 zimeripotiwa, ambazo zimesababisha vifo vya watu 24 na majeruhi 258.

Aidha alisema, ukiondoa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini Unguja ndio unaoongoza kwa ajali nyingi za barabarani, kulinganisha na mikoa mingine minne Unguja na Pemba.

Alifahamisha kuwa, kwa kutambua uzito wa jambo hilo, Jeshi la Polisi kamisheni ya Zanzibar, limekuwa likifanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wote wa matumizi ya barabara ili kuimarisha usalama wa watumiaji.

Aliwataja wadau hao kuwa, ni jamii yote ya Zanzibar, taasisi za serikali na binafsi, ikiwemo Bodi ya Mapato Zanzibar na Wizara ya Afya, ambayo imeshirikiana kikamilifu na jeshi hilo kufanikisha wiki hiyo ya ‘Safiri Salama’.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa, jukumu la kuhakikisha usalama wa barabarani la jeshi la polisi pekee, bali ni la kila mmoja kwa nafasi yake, huku akisisitiza matumizi mazuri ya barabara ikiweemo kuzitunza badala ya kuziharibu kwa visingizio mbalimbali, pamoja na kung’oa vyuma vya alama za barabarani.

Naye Meneja wa kitengo cha maradhi yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Omar Mwalimu, alisema hospitali kuu ya Mnazimmoja, imekuwa ikipokea majeruhi na maiti wengi kutokana na athari za ajali za barabarani, na kusema zinailazimu serikali kutumia fedha nyingi nje ya bajeti yake, kuwatibu watu wanaopatwa na ajali.

Wiki ya ‘Safiri Salama’ ilianza tarehe 24 Juni mwaka huu, kwa mikutano ya kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, kama vile madereva na makondakta, wanafunzi, mabagwani na wananchi wengine wa Mkoa wa Kaskazini.

Sherehe hizo zilizopambwa kwa burudani mbalimbali zilizobeba ujumbe wa usalama barabarani kutoka kwa kikundi cha Black Roots chini ya msanii Makombora na utenzi, zilihudhuriwa pia na Wakuu wa Wilaya za Kaskazini B, Khamis Jabir Makame na Riziki Juma Simai wa Kaskazini A, pamoja na makamada wa Polisi wa mikoa mitatu ya Unguja.

Kili Music Tour 2013 ilivyofana ndani ya jijini Tanga

 Msanii wa Muziki wa Hip Hop,Roma Mkatoliki akipanga na kupangua vina vyake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.
 Roma Mkatoliki akiwapagawisha wakazi wa mji wa Tanga waliojitokeza kwa Wingi kwenye Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.
 Mkali wa Hip Hop,Prof. Jay a.k.a a.ka The Heavy Weight  MC akikamua vilivyo mbele ya Wakazi lukuki waliofika kwenye viwanja vya Mkwakwani kuona Onyesho la Muziki linaloongozwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Kilimanjaro maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
Prof. Jay akiendelea kukamua kwenye Onyesho hilo Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.
Prof. Jay akiwashukuru wakazi wa Tanga.
Mwana FA a.k.a Binamu akiimba wimbo wake wa Yalaiti na Mwanadada aliepanda jukwaani kuimba badala ya Msanii alieimba nae wimbo huo.

Binamu akikamua huku shangwe zikitawala.
Msanii wa Muziki wa Taratibu,Maarufu kwa jina la Recho akiimba nyimbo zake mbali mbali wakati wa Onyesho la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.
Mamaa wa Majanga aitwae Snura akiwapagawisha wakazi wa Tanga na goma lake lililoshika hatamu sana hapa nchini (MAJANGA).
Ali Kiba na madansa wake wakitoa Burudani kwenye Onyesho hilo.
Ali Kiba akikamua..........
Mkali wa Hip Hop hapa nchini kwa Mwaka 2012/13,Kala Jeremier akifanya mambo yake mbele ya Mashabiki wake Lukuki waliofika ndani ya Uwanja wa Mkwakwani,Jijini Tanga usiku wa kuamkia leo.
Tanga ilizizima kwa shangwe wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
DJ Mackay akisimamia vyema show hiyo.

Mzee Yusuph akitoa burudani kwa Mashabiki wake wa Jiji la Tanga.
Mambo ya Mwambao....

Meneja wa Bia la Kilimanjaro,George Kavishe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa EATV wanaosimamia zoezi zila la Onyesho hilo.

Wadau Scooby na Baltazary.
Mapacha wa Snura katika Pozz.
Wadau wa EATV.
Toka kulia ni DJ Choka,Kiboya na Dada Ester wakiwakilisha ndani ya Mkwakwani,Tanga.
Wakazi wa Tanga wakikongwa nyoyo zao.

SPERANSIA MHONDELE NI BINTI WA MIAKA 18 MWENYE NDOTO LA KULITANGAZA TAIFA KISOKA

Mwanadada  mkali  wa soka  Iringa na mikoa ya nyanda za juu  kusini Speransia Mhondele  akionyesha uwezo wake  kisoka
Hapa  aklionyesha jinsi ya  kutuliza mpira  kwa gamba
Akionyesha mbinu ya  kumkabili  adui  kwa mpira  wa angani
Hapa  akijiandaa kuondoka na mpira  baada ya  kuutuliza  kutoka hewani


Timu ya  watuma  salam mkoa wa Iringa ambayo  binti Speransia ( wa pili  kushoto waliosimama) alipata  kuonyesha soka la uhakika  jana wakati wa mchezo wa kirafikin kati ya  watangazaji wa radio  Furaha Fm na  watuma  salam mchezo uliomalizika kwa  watangazaji  kushinda  baada ya kuigagadua timu ya  watuma  salam mabao 2-0
.......................................................................................

Spransia  Evaristo Mhondele ni  binti  wa miaka 18  mkazi  wa Kihesa katika manispaa ya Iringa mwenye  kipaji  cha hali ya  juu katika mchezo  wa mpira  wa  miguu mwenye ndoto  za kuj kulipa heshima  kubwa Taifa la Tanzania  katika soka la  wanawake .

“mimi nilihitimu masomo yangu ya  sekondari mwaka 2012 katika  shule ya  sekondari Mlamke katika Manispaa ya  Iringa na  nimepata  kuchaguliwa kujiunga na timu  za UMISETA katika mchezo wa  soka wanawake “

Nilianza  kucheza mpira  mwaka mwaka 2010 nikiwa katika mashindano ya UMISETA  yaliyofanyika katika Ifunda kwa wilaya ya  Iringa  ambako nilikwenda  kushiriki mchezo  wa Basketi  .

Baada ya  kufika  huku nilikuta kuna ushindani mkubwa katika mchezo huo ambao  nilichaguliwa na  hivyo baada ya   kuchujwa  wengi nikiwemo mimi katika mchezo huo  ndipo  nillipoamua  kubadili mchezo na  kuanza kucheza mchezo wa mpira wa  miguu kwa  kufanya mazoezi .

Nilifanya mazoezi  usiku na mchana na baada ya mashindano mengine ya  UMISETA ndipo nilipoamua  kuelekeza  nguvu  huko na kujiunga kabisa katika timu ya mpira wa miguu ya  wanawake .

Kujiunga kwangu na  timu ya  mpira  wa  miguu wanawake  kuniliwezesha  kupita hatua kwa  kuchaguliwa  kuwakilisha  mkoa  wa Iringa katika mashindano ya kanda ya  kusini  kwa  kuelekea  mkoani Ruvuma kwa mara  ya kwanza kufika katika mkoa  huo na baada ya kufanya vizuri huko  nilichaguliwa  kuwakilisha kanda  ya kusini katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani .

“ Jitihada  binafsi nilizoonyesha  na  wachezaji wenzangu  tuliiwezesha  timu  yetu  kutoka  kanda ya nyanda za juu kusini  kushika nafasi ya  tatu kitaifa “

Mchezaji  huyo anadai kuwa  ndoto yake  kubwa katika soka  kuja kuchezea timu  kubwa  za  kitaifa ili   kuweza  kuonyesha uwezo  wake  zaidi .

“Kwa  sasa  nasuburi  ruhusa ya  mzazi  wangu  ili  kuweza  kuniruhusu   kujikita  zaidi katika michezo  ili  kuweza  kutafuta  fursa ya  kulitumikia  Taifa  langu  Tanzania katika michezo …..nilishindwa  kujiunga na  timu  za  wanawake  nje ya mkoa  kutokana na  wazazi  kunizuia kutokana na  wakati huo  nilikuwa masomoni “

Spransia  anasema  kuwa  katika maisha  yake wakati akiwa  shule  kwa sehemu  kubwa alikuwa akiwaza  michezo zaidi  na  hasa  kuwa na ndoto ya  kuja  kuchezea timu kubwa za  mpira  wa miguu kwa  wanawake na yawezekana  hata kufeli kwake  kulitokana na mawazo ya  michezo .

Hata  hivyo anasema  kuwa kati ya mambo ambayo katika maisha  anaona  bado  kufanikiwa na hana ndoto ya  kukimbilia  kuolewa  wala katika  mahusiano na  wanaume kwa sasa ni kutokana na  kutotimiza  azma yake ya  kuchezea  timu  kubwa ya  soka  wanawake  nje ya  mkoa  wa Iringa .

Kwani amesema katika mashindano ya  UMISETA kwa jitihada  zake binafsi amepata  kuifungia  timu yake magoli matatu na  kuwa kwa  sasa baada ya  kuhitimu  elimu ya  sekondari amepata kuchezea  timu mbali mbali kama  Kwa kilosa FC , Sengo FC na  timu  ya  watuma  salam mkoa  wa Iringa  wanaume ambapo kwa upande upande wa  Sengo Fc nimepata  kufunga magoli mawili .

Pia  amesema  kuwa anaomba  chama  cha mpira  wa miguu  wanawake  Taifa  iwapo  kuna  nafasi ya  kusajili  wachezaji  wapya  kuweza  kumtazama hata  kumpa nafasi ya majaribio  ili aweze  kuonyesha kipaji chake .

Mwandishi  wa makala  haya  alipata  kushuhudia kandanda safi iliyoonyeshwa na mchezaji  huyo  Speransia wakati  wa mchezo wa kirafiki kati ya  timu ya  watuma  salam mkoa  wa Iringa na  timu ya  watangazaji  wa kituo cha  radio Furaha  Fm ambapo mchezaji Speransia  alipata  kuchezea timu ya  watuma salam na  kuwa binti  pekee katika  timu  hiyo  ya  wanaume  ila aliweza  kuwahenyesha  watangazaji wa radio  Furaha Fm japo  ndio  iliyoweza  kushinda kwa magoli 2-0 dhidi ya  watumasalam

Mwandishi  wa makala  haya ni milimiki wa mtandao  wa www.matukiodaima.com