Wednesday, October 31, 2018

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YAPEWA SIKU 14 ZAIDI KUWASILISHA TAARIFA ZA MIRADI NA MATUMIZI YA FEDHA ZA MWAKA 2016 NA 2017


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto( Idara kuu ya Maendeleo ya jamii) Dkt. John Jingu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu nyongeza ya siku 14 zaidi zilizotolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha za mwaka 2016 na 2017 kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya jamii) wakifuatilia tamko la Katibu Mkuu Dkt. John Jingu la kuongeza siku 14 zaidi kwa Mashirika ya Yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2016 na 2017 kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
Katibu Mkuu wa Braza la NGOs nchini Bw. Ismail A. Suleiman akieleza kuridhishwa kwake na kanuni mpya za NGOs (2018) ambazo zimezingatia matakwa ya kanuni za maadili katika kuboresha utendaji wa NGOs wakati wa kikao cha Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii kilichoeleza kuongeza siku 14 zaidi kwa Mashirika hayo kuwasilisha taarifa za miradi na fedha kwa Msajili wa NGOs. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.


Na Mwandishi Wetu Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa siku kumi nne zaidi (14) kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha za mwaka 2016 na 2017 zilizokaguliwa kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao.

Tamko hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Ufafanuzi ulitolewa kuwa, “Siku ya tarehe 28 Septemba, 2018, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alikutana na wawakilishi wa vyombo vya habari na kutoa maagizo yakuyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwasilisha taalifa zao kwa Mashirika hayo ikiwa ni pamoja na taarifa za miradi na taarifa za fedha zilizo kaguliwa kwa mwaka 2017 na 2018”, alibainisha DKT. Jingu.

Dkt Jingu amefafanua kuwa, maagizo hayo yalipaswa kutekelezwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe 28.9.2018 ya agizo lilipotolewa na Serikali. Hata hivyo imeelezwa kuwa mwitikio wa utekelezaji umekuwa wa kuridhisha kutokana na ukweli kuwa Mashirika mengi yamezingatia maelekezo ya Serikali.

Aidha, Wizara imepokea maombi kutoka Ofisi ya Baraza la Taifa la NGOs na baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakiomba kuongezwa muda kidogo ili waweze kukamilisha maandalizi ya taarifa zao na kuziwasilisha haraka. Kutokana na kutambua nafasi ya NGOs katika maendeleo ya Taifa, Serikali imeridhia kuongeza siku kumi na nne (14) kuanzia leo (31/10/2018) ili kuwapa fursa wale ambao walikuwa bado hawajatimiza maelekezo hayo kutokana na sababu mbalimbali kufanya hivyo. “Nasisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza kwa wale ambao hawatakuwa wamewasilisha taarifa hizo ndani ya muda wa nyongeza. Shirika ambalo litakuwa halijawasilisha taarifa Wizara itachukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria”. alisisitiza Dkt. Jingu.

Katibu Mkuu huyo amerudia kuhakikishia umma kuwa, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa NGOs kwa maendeleo ya nchi. Msisitizo wa Serikali wa uwazi na uwajibikaji unalenga kuwezesha Serikali, wananchi na wadau wa maendeleo kutambua vizuri zaidi mchango wa NGOs katika shughuli za maendeleo. Pia kama ilivyo kwenye sekta nyingine, uwazi na uwajibikaji utasaidia kuzuia matumizi mabaya ya rasilimali zinazotolewa na wadau wa maendeleo kupitia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuwa kichocheo katika kufikia azma ya maendeleo jumuishi.

Akizungumza katika Mkutano huo, katibu Mkuu wa Braza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Ismail A. Suleiman ameishukuru Serikali kwa kuridhia ombi nyenyekevu la kuongeza muda wa kuwasilisha taarifa za fedha na miradi ili kuwezesha NGOs kutimiza takwa la agizo hio. Bw. Ismail amebainisha kuwa kanuni mpya za NGOs (2018) zilizotangazwa tarehe 19/10/2018 kwa kiasi kikubwa zimezingatia utekelezaji wa kanunni za maadili; hivyo Braza la NGOs litaunda kikosi kazi kuzipitia na kutoa maoni kwa lengo la kuboresha utendaji wa NGOs kwa mujibu wa matakwa ya kisheria, kanuni na taratibu.

Baraza la NGOs limewataka wanachama wake wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha kuwa wanatekeleza kazi zao kwa mujibu wa katiba za mashirka yao ili kushirikiana na Serikali katika kuchochea ustawi na maendeleo ya watu hususan kunufaisha makundi yote ya kijamii.

Maagizo haya kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanakuja mwezi mmoja baada ya AGIZO LA Serikali kutolewa likizitaka NGOs zote nchini pamoja na mambo mengine kuwasilisha taarifa zao za kazi na matumizi ya fedha ya miradi wanayoitekeleza. Imeelezwa kuwa hadi taarifa hii inatolewa zaidi ya Mashirika 2000 yamewasilisha taarifa zao na wengi wanaendelea kuitiki maelekezo hayo.

SERIKALI YAANDAA MPANGO MKAKATI KUWANOA WASAIDIZI WA KISHERIA NCHINI

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo Maalum ya Wawezeshaji watakaotoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria ili waweze kupata usajiri rasmi na wa kisheria wa kutoa huduma za kisheria kwa wananchi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Law School of Tanzania (LST) na kufadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF) yaliofanyika Dodoma jana.


SERIKALI imeandaa mpango mkakati wa kutoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za msaada wa kisheria kwa watanzania maskini wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya kisheria nchini.

Mpango wa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria nchini unatarajiwa kuanza mapema Novemba mwaka huu na walengwa wakuu ni wasaidizi wote wa kisheria ambao wanaotoa huduma za msaada wa
kisheria katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Katika sehemu ya maandalizi ya mafunzo hayo, Serikali kupitia ofisi ya Msajili wa Watoa Huduma za Kisheria –Wizara ya Katika na Sheria, imeendesha mafunzo yaliyolenga kupika wataalum (wawezeshaji) wapatao 40 kutoka mashirika mbalimbali ya huduma za kisheria) watakaoendesha mafunzo hayo maalamu kwa wasaidizi wa kisheria.

Mafunzo ya kupika wawezeshaji yamefanyika Dodoma na yaliandaliwa na Law School of Tanzania (LST) kwa kushirikiana na Tanzania Law Society (TLS) na kufadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF)—taasisi inayofadhiliwa miradi/shughuli mbalimbali ya wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumzia mafunzo hayo Mratibu wa Mafunzo ya Wawezeshaji Suleiman Pingoni amesema mafunzo hayo yanalenga kupika wataalam mahiri wakaoendesha mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria, yanayotajiriwa kuanza rasmi mapema Mwezi Novemba, na kumalizika kabla ya Disemba 31, Mwaka huu.

Mafunzo kwa wawezeshaji, kwa mujibu wa Bw.Pingoni, yalilenga kuwawezesha kupata ufahamu wa kutosha kuhusu maswala ya msingi kuhusu sheria ya Msaada wa Sheria (Legal Aid Act ) ya Mwaka 2017 na Kanuni zake, matakwa ya sheria kuhusu usajiri na usaili wa wasaidizi wa kisheria. Sheria ya Msaada wa Kisheria inawataka wasaidizi wa kisheria kupata mafunzo maalum ili waweze kusajiliwa na kupewa leseni za kutoa huduma za kisheria kwa wahitaji.

“Kimsingi, sheria ya Msaada wa Kisheria imewatambua wasaidizi wa kisheria na kazi wanazofanya hivi sasa. Hata hiyo, sheria hiyo hiyo, inawataka wasaidizi hawa wa kisheria kupata mafunzo maalum ili waweze  kupatiwa liseni/vitambulisho ili waruhusiwa kutoa huduma za kisheria,” amesisitiza Bw. Pingoni.Kwa mantiki hiyo, Ofisi ya Msajili wa Watoa Huduma za Kisheria ameandaa mafunzo kwa wawezeshaji

watakaotoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria, ili waweze kukidhi matakwa ya sheria.Ameeleza wasaidizi wa kisheria watakapata mafunzo hayo maalum watapatiwa vyeti, ambavyo vinawazesha kutuma maomba ya kusajiliwa na kutambuliwa kama wasaidizi wa kisheria kwa mujibu wa Sheria, na baada kupatiwa vitambulisho maalum.

“Lengo kuu la michakato hii yote ni kupata wasaidizi wa kisheria mahiri na wenye uwezo, ambao wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, wakaoweza kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wananchi, amesema Bw.Pingoni.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi-LSF Scholastica Jullu ameelezea mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria kama “hatua kubwa katika jitiada za serikali na wadau wa huduma za kisheria zinazolenga kupanua wigo wa huduma za msaada wa kisheria na kuwezesha watu maskini, wanaodhulimiwa na kunyanyaswa kupigania na kupata haki zao.”



BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO KUHAMASISHA UZALISHAJI WA MAZIWA

Katika kuhakikisha tasnia ya maziwa inawanufaisha wazalishaji wadogo wadogo wa maziwa nchini Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) ipo kwenye mikakati ya kuanzisha Jukwaa la Ushirikiano wa Tasnia ya Maziwa.

Akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alisema Benki ya Maendeleo ya Kilimo imejipanga kuhakikisha uzalishaji wa maziwa unaongezeka nchini ili kutoa fursa kwa wazalishaji wadogo kuweza kuchangia ukuaji wa tasnia hiyo.

Bw. Justine alisema kuwa shughuli za usindikaji wa maziwa zipo chini ya kiwango kwa viwanda vyote vinavyosindika maziwa nchini kutokana na uzalishaji duni wa maziwa hali inayorudisha nyuma ukuaji wa tasnia hiyo. “Fursa za kimasoko na uendelezaji wa tasnia ya maziwa ni kubwa hivyo tumejipanga kuhakikisha tunachagiza tasnia hii ili kuongeza uzalishaji na kuwaongezea kipato wazalishaji hasa wale wadogo wadogo,” alisema.

Aliongeza kuwa TADB imejipanga kuwakutanisha wadau wa tasnia ya maziwa ili kujadili kwa kina mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu ili kuja na mpango mkakati wa kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini. Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARCO, Prof. Philemon Wambura alisema NARCO imejipanga kuwezesha wazalishaji wa wadogo kote nchini kwa kuwapatia huduma za ugani ili waweze kuongeza uzalishaji wa maziwa.

Prof. Wambura aliongeza kuwa mchango wa Benki ya Kilimo katika kuhakikisha tasnia ya maziwa inachangia shughuli za uzalishaji ni jambo la kuungwa mkono. “Mchango huu wa TADB utasaidia kuongeza uzalishaji hali itakayowaongezea kipato wazalishaji wadogo nchini na hivyo kutasaidia kuwaongezea kipato wafugaji wetu,” alisema.

Kwa mujibu wa twakwimu za Bodi ya Maziwa Tanzania, tasnia ya maziwa inachangia asilimia 3.9 ya GDP huku ikikadiriwa kuwa na ng’ombe wa maziwa zaidi ya milioni 1.1 kati ya jumla ya ng’ombe milioni 30.5.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akimkaribisha Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Philemon Wambura (kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Philemon Wambura (hayupo pichani) wakati walipokutana kuzungumzia nafasi ya TADB na NARCO katika kusaidia tasnia ya maziwa nchini. 
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Philemon Wambura akizungumza wakati wa kikao hicho. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Philemon Wambura (kushoto) wakihimiza jambo wakati wa kikao cha kujadili nafasi ya taasisi zao katika kuchagiza uzalishaji wa tasnia ya maziwa nchini. 

MSAFARA WA WAZIRI LUGOLA WANUSURIKA KUGONGWA NA BASI LILILOKUA MWENDOKASI LIKIOVATEKI KATIKA KONA GAIRO, DEREVA AKAMATWA



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Dereva wa Basi la Hekima za Mungu, Isaac Vian, alipomkimbilia Waziri huyo huku akimuomba msamaha mara baada ya kusimamishwa kutokana na kuendesha kwa mwendo kasi pamoja na kuovateki katika kona katika eneo nje kidogo na mji wa Gairo Mkoani Morogoro. Dereva wa Basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ lililokua linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama Mkoani Shinyanga alielekezwa akaripoti kituo cha polisi mkoani Dodoma ili aweze kufunguliwa mashtaka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiangalia namba za usajili T140 AZZ la Basi la abiria la Hekima za Mungu lililokua linatoka Jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama ambalo Waziri alilisimamisha kutokana na kosa la mwendokasi pamoja na kuovateki katika kona nje kidogo wa Mji wa Gairo Mkoani Morogoro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na abiria wa basi la Hekima za Mungu baada ya Dereva wa Basi hilo, Issac Vian kuendesha kwa mwendokasi na kuovateki katika kona kali ambapo angeweza kusababisha ajali kwa kugongana na gari la Waziri Lugola, uso kwa uso Kijijini, nje kidogo na Mji wa Gairo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akishuka katika Basi la Hekima za Mungu mara baada ya kuzungumza na abiria na kuwataka kukemea mwendokasi pamoja na kuovateki katika kona alivyofanya dereva wa basi hilo, Isaac Vian (kushoto), nje kidogo ya mji wa Gairo, mkoani Morogoro, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimuonya Dereva wa Basi la Hekima za Mungu, Isaac Vian (kushoto), kwa kosa la kuendesha basi hilo kwa mwendokasi pamoja na kuovateki katika kona nje kidogo ya mji wa Gairo, mkoani Morogoro, leo. Hata hivyo Dereva huyo Waziri huyo alielekeza akamatwe kutokana na kosa hilo ambalo lingesababisha ajali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Felix Mwagara, MOHA-Gairo.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amenusirika kupata ajali wilayani Gairo, Mkoani Morogoro baada ya basi la Hekima za Mungu kuovateki katika kona wakati gari la waziri huyo likiwa eneo sahihi.

Tukio hilo lilitokea saa 6:04 mchana wakati Waziri huyo alipokua anatokea Mjini Dodoma kuelekea Jijini Dar es Salaam, katika eneo la nje kidogo ya Mji wa Gairo, basi hilo likiwa mwendokasi likiovateki katika kona, ndipo dereva wa gari la Waziri Lugola alipunguza spidi ili kuiepuka ajali hiyo.

Hata hivyo Basi hilo lilipopita, Waziri huyo aliekeza gari hilo lifuate kwa nyuma mpaka walikamate, hata hivyo Basi hilo lilikamatwa na dereva wa basi hilo kukaguliwa kama alikua na sifa ya kua dereva. Bara baada ya kumkagua dereva huyo, Waziri Lugola alizungumza na abiria wa basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ ambalo lilikua linatoka Dar es Salaam kuelekea Mjini Kahama mkoani Shinyanga.

“Kwanini mnashindwa kukemea hii tabia ya huyu dereva, mnataka awaue?, alitaka kusababisha ajali mbaya sana hapa, nanyi mmekaa kimya, mnafanya makosa kutokuripoti hii tabia mbaya kabisa,” alisema Lugola. Aliongeza kua, yeye ni Waziri ambaye anakemea mwendokasi na kiuwataka madereva nchini waendeshe kwa umakini, lakini dereva huyo anashindwa kufuata sheria za usalama barabarani, hivyo anapaswa kuchukuliwa hatua na iwe fundisho kwa madereva wenye tabia kama hiyo.

Licha ya Dereva wa Basi hilo, Isaac Vian alikiri kosa hilo na kuomba msamaha lakini Waziri Lugola aliekeza akamatwe lakini atakapofika mwisho wa safari.

MHANDISI NDIKILO APONGEZA JITIHADA ZA TIC KATIKA KUKUZA,KUVUTIA UWEKEZAJI NCHINI

Na Ripota Wetu,Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ametembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) katika Maonesho ya wiki ya

Viwanda Mkoa wa Pwani ambapo ameipongeza TIC kwa jitihada zake katika kukuza na kuvutia uwekezaji nchini na namna inavyowahudumia wawekezaji kupitia huduma za mahala pamoja zinazotolewa na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya ofis za kituo hicho.

Akizungumza leo akiwa kwenye banda la TIC, Mhandisi Ndikilo amesisitiza ni ukweli kwamba Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa inayopokea wawekezaji wengi na hivyo nguvu ya

kuwahudumia lazima iimarishwe. Aidha ameshauri TIC kuhakikisha inapata taarifa zote muhimu zinazohusiana na uwekezaji ndani ya mkoa wa Pwani kwa kuwasilian na ofisi za Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kwani kwa kufanya hivyo kutarahisisha uratibu na

huduma kwa wawekezaji nchini.

Baadhi ya tarifa alizosisitiza TIC iwe nazo ni pamoja na maeneo ya uwekezaji yaliyotyengwa, takwimu za miradi ya uwekezaji. Katika kuhakikisha kwamba Mkoa wa Pwani unaendelea kuvutia uwekezaji Mkuu wa Mkoa atawasilisha TIC maeneo ambayo tayari yametengwa kwa ajili ya uwekezaji ili yaweze kutafutiwa wawekezaji.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika banda la TIC kwenye maonesho ya Wiki ya Viwanda Mkoa wa Pwani yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Picha ya Ndege wilayani Kibaha mkoani Pwani, Meneja wa Kanda ya Mashariki Venance Mashiba .Amesema kuwa katika kuharakisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili wawekezaji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kimeunda Kamati Maalum ya kiaifa inayojumuisha Wakuu wa Taasisi za Serikali ambazo ni wadau katika kuhudumia uwekezaji.

"Kamati hii hukutana chini ya Mwenyekiti wa muda ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIC na kujadili changamoto mbalimbali za uwekezaji na kuzitafutia ufumbuzi. Kamati hii inakaa kila baada ya miezi mitatu inajadili changamoto mbalimbali ikiwa ni sehemu yake ya mpango kazi wa kuhakikisha huduma za wawekezaji zinaboreshwa,"amesema.

Ameongeza kuwa kamati hiyo ilianza kufanya kazi mwishoni mwa mwaka jana ikiwa na wajumbe wanaounda kituo cha huduma za mahala pamoja inayoundwa na taasisi 11 zikijumuisha Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA, Uhamiaji, Shirika la Viwango Tanzania TBS, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA, Wizara ya Ardhi, Kazi na Ajira, Wakala wa Usalama mahala pa Kazi OSHA, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO na NEMC.


“TIC tunataka kuhakikisha wawekezaji wanapata urahisi wa kuendesha miradi yao hapa nchini ndio maana tunahakikisha kila mara tunaboresha mazingira ya uwekezaji, hatutaki Mwekezaji akija hapa ahangaike kutafuta vibali au leseni zinazohitajika, au achelewe kutatua changamoto zinazomkabili, kwa hiyo kamati hii lengo lake ni kuhakikisha tunaondoa changamoto zote kwa wakati,"amesema Mashiba.

Aidha Kituo kinawakaribisha watu wote, jumuia ya wafanyabiashara na wawekezaji wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho haya ili wajionee bidhaa zinazozalishwa mko wa Pwani na huduma nyingine zinazotolewa na taasisi mbalimbali zinazoshiriki

maonesho haya. Maonesho hayo yaliyoanza Otoba 29 yanatarajia kumalizika Novemba 4, 2018.
 Baadhi ya wadau wa masuala ya viwanda wakiwa kwenye banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wakipata maelezo leo baada ya kutembelea maonesho ya viwanda mkoani Pwani
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisaini kitabu cha wageni leo baada ya kufika kwenye banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC). Anayeshuhudia ni Meneja wa TIC Kanda ya Mashariki Venance Mashiba
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Kanda ya Pwani Venance Mashiba leo kwenye Maonesho ya viwanda mkoani humo

WAFANYAKAZI WATANO WA NEMC WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI SAINI YA WAZIRI JANUARI MAKAMBA

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

WAFANYAKAZI watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa mazingira.

Wakili wa Serikali Faraja Nguka amewasomea washtakiwa makosa yao leo Oktoba 31, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando.Wakili Nguka amedai washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, mawili ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 160 milioni.

Aidha Mahakama imetoa hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa Magori Wambura (38) mkazi wa Bombambili kwa sababu wakati washtakiwa hao wakisomewa mashtaka hayo yanayowakabili mshtakiwa huyo ambae ni Ofisa mazingira wa Nemc, hakuwepo mahakani.Wakili Nguka amewataja washtakiwa hao kuwa ni Ofisa wa Mazingira NEMC Deusdith Katwale, Msewe, Luciana Lawi, Edna Lutanjuka, Ofisia Mwaruka na Lilian Laizer.Imedaiwa kati ya Septemba 27, 2016 na April I mwaka huu wa 2018 washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.

Katika shtaka la pili washtakiwa hao wanadaiwa, Oktoba 17,2017 kwa udanganyifu walighushi cheti cha tathmini ya uharibifu wa mazingira chenye namba ya usajili EC/EIA/3366 wakijaribu kuonesha kuwa cheti hicho ni halali na kwamba kimetolewa na NEMC wakati wakijua si kweli.Pia washtakiwa hao wanadaiwa kughushi saini ya Januari Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira katika cheti cha tathmini ya uharibifu wa Mazingira chenye usajili namba EC/ EIA/3366 wakijaribu kuonesha kuwa cheti hicho ni halali na kwamba kimetolewa na NEMC wakati wakati wakijua si kweli.

Mshtakiwa Edna anadaiwa kuwa Oktoba 2017 katika ofisi za NEMC Makao Makuu Dar es Salaam kwa kujua alitoa cheti cha kughushi cha tathmini ya uharibifu wa mazingira chenye namba ya usajili EC/EIA/3366 cha oktoba 17,2017 kwa Deogratius Chacha, akijaribu kuonyesha kuwa cheti hicho ni halali na kwamba kimetolewa na NEMC wakati akijua si kweli.

Pia washtakiwa walijipatia kwa njia ya udangnyifu Sh.milioni 160 toka kwa PMM Estate (2001) Ltd kwa madai kuwa wangefanya tathimini ya uharibifu wa mazingira na kumpatia cheti ambacho kinatolewa na NEMC kitendo ambacho si kweli.Aidha washtakiwa wanadaiwa kati ya Septemba 27, 2016 na Aprili 6,2018 Dar es Salaam waliisababishia NEMC hasara ya Sh.milioni 160.

Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu,.Washtakiwa wamepelekwa rumande kesi imeahirishwa hadi Novemba 14, mwaka huu na upelelezi wake bado haujakamilika.

WAFANYAKAZI watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  wakiwa wamefishwa katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais -Muungano na Mazingira Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa mazingira.

Advocating for nationwide connectivity/Connecting the unconnected Tanzanians – One region at a time.

No matter what part of the world you live in, communication is a vital aspect of everyday life facilitating connection between people. The use of phones has evolved from interactions with friends and family to tools that enable commercial transactions for businesses. In Tanzania, the highest rate of mobile phone penetration is in urban areas however 67.6% of the population resides in rural areas where connectivity remains a challenge.

A Deloitte study of 40 African economies reveals that the introduction of mobile networks has the potential to influence socio-economic development for individuals and villages in remote areas.  Additionally, the study shows that 1% increase in market penetration leads to an increase of 0.28 percentage points in GDP and 1% increase in internet penetration increases the GDP growth rate by 0.077 percentage points in the economy.

We live in a world where a person in the southern highlands of Tanzania needs to be able to access breaking news as it happens from his mobile phone and also have the ability to use the same phone to source commercial opportunities in other parts of Tanzania. Without enabling rural access it would take a long time for information to reach people in rural areas thus hindering their progress. 

According to FinScope Tanzania 2017, 78% of Tanzanian adults in rural areas have a financial access point within a 5km radius. Due to the limited footprint of traditional bank branches, the majority of financial service providers found within a 5km radius are mobile money agents whose presence facilitate transactions that allow for residents to participate in economic activities that improve their livelihoods.  Rural connectivity empowers the lives of those that reside great distances from urban centers.

Vodacom Tanzania PLC, the leading telecommunications company in the country, has been at the forefront of advancing rural connectivity and has demonstrated its commitment by supporting the government in its objectives to bridge the digital divide by progressing connectivity to over 60% of the population that resides in the rural areas in order to unlock the economic potential that lies in the rural areas. The Telco has been at the forefront ensuring that all Tanzanians have access to communication. The company currently covers over 75 % of the connected population with a bouquet of technologies ranging from GSM 900/1800, 3G and WiMAX 803.16d.

The future is promising for rural connectivity in Tanzania - Vodacom recently entered into a long term contract with The National ICT Broadband Backbone (NICTBB) that allows the former to use government-owned fiber optic cable infrastructure to enhance connectivity in rural Tanzania.  With increasing demand for information services, Vodacom will use the government infrastructure to meet customer needs as fiber optics cables can carry larger amounts of information over a longer distance helping bridge the technological disparities of rural areas.

Additionally, through an agreement with Universal Communication Service Access Fund (UCSAF), Vodacom has set out to improve basic telecom services to the most rural villages and underserved urban areas in Tanzania. Under this agreement, 194 new sites have been added reaching 187 wards in Tanzania providing access to communication and internet services to improve the socio-economic standing of 654 new villages in Tanzania.  

Schools in those remote villages can now connect to the internet and share ideas with others far away, farmers can quickly check prices of produce and make informed decisions on trading.  Mwanahamisi, a woman trader in Mtwara remarks, ‘it is now so easy for me to talk to the company in Mozambique that buys my rosella products. I don’t have to keep crossing the border.’  

Connectivity also enables the transfer of critical health data and life-saving information by text messages to clinics to support rapid diagnoses for patients in remote villages.Although the socio-economic benefits are vast, the deployment of rural access services remains a challenge due to the required investment to ensure that broadband services are not only deployed but also remain sustainable.

In order for rural connectivity to be realized, key conditions have to be met: partnerships between the private and public sector, roll out of projects that provide high-speed network access, and the provision of friendly regulatory frameworks. These strategies lie at the heart of providing an enhanced and holistic service to potential customers in the rural areas of Tanzania.


DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO.

 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akizundua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo akishuhudia 
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akizundua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kuzindua Rea awamu ya tatu
  WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kuzindua Rea awamu ya tatu
 MKUU wa wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro James Ihuny'o akizungumza katika uzinduzi huo
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Tanesco Mhandisi Theodory Bayona ambaye pia ni Meneja Mwandamizi wa Usambazaji na huduma kwa wateja akizungumza katika uzinduzi huo
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Kanda ya Kati akizungumza wakati wa ziara hiyo
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akimsikiliza kwa umakini Meneja wa Shirika la Tanesco mkoani Morogoro Mhandisi Hassan Saidi wakati wa ziara yake 
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katikati akielekea kufanya uzinduzi huo
 Sehemu ya wananchi wakifurahia hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt Kalemani 
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt Kalemani




WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza Mameneja wa shirika la Umeme (Tanesco) kote nchini kuhakikisha wanakata huduma ya umeme kwa wadaiwa sugu ikiwemo sekta binafasi na serikalini. 

Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Morogoro iliyokuwa na lengo la kutembelea maeneo yanayozalisha umeme ikiwemo Kidatu ambako uzalishaji wa umeme ni 204 mw. 

Licha ya kutembelea eneo hilo lakini pia alizindua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Alisema kwamba hatua hiyo inaweza kuwa mwarobaini wa kuweza kusaidia kukusanya madeni hayo ambayo yamekuwa kwa muda mrefu na hivyo kupelekea kukwamisha malengo yao waliojiwekea. 

Aidha alisema kwamba haiwezekani shirika hilo likawa linawadai watu fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwenye kutekeleza shughuli za kimaendeleo na kuweza kuwafikia wananchi wengi huku wakiacha kuwachukulia hatua ambazo zinaweza kusaidia kupata ufumbuzi wake. 

“Ndugu zangu mameneja wa mikoa hakikisheni mnawakatia umeme wadaiwa wote sugu kwenye maeneo yenu wakiwemo wale wa sekta binafasi na serikali kwani hii ndio njia inayoweza kuwasaidia kukusanya madeni hayo “Alisema Dkt Kalemani. Akizungumzia kitengo cha huduma kwa wateja ndani ya shirika hilo Dkt Kalemani alisema ni muhimu watumishi wa kada hiyo wakabadilikana kitabia kwa sababu imedodira sana na kwenye maeneo mengi hazifanyi kazi zao ipasavyo. 

“Ukatakuta wateja wanapiga simu haipokelewi wakati watu wanaohusika nacho wapo hivyo kuanza sasa sipendi kusikia simu ikipigwa haipokelewi mameneja hakikisheni watu wa namna hiyo mnawachukuliwa hatua”Alisema. 

“Lakini pia ikibidi mtoeni yupo ndani ya uwezo wenu lakini kama anamajibu mabaya wachukulieni hatua…. Haiwezekani mtu anapiga simu unamwambia huu sio masaa ya kazi juzi manyara nilipiga simu nikaambiwa kwamba haya sio masaa ya kazi huyu mtu bado namtafuta kwani huwezi kuwa na biashara nzuri kama mtu anayekutana na wateja wao hatekelezi wajibu wake”Alisema Waziri Dkt Kalemani 

Awali akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa Shirika la Tanesco Kanda ya Kati Mhandisi Atanausus Nangali alisema mradi huo wa gharama nafuu ni mradi wa ubunifu wa miundombinu ya gharama nafuu wa majaribio uliojengwa kupitia Rea na kugharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. 

Alisema kwa Tanzania mradi huo umefanyika kwa wilaya mbili ambazo ni wilaya ya Mbozi wilayani Mbeya na Kilombero mkoani Morogoro kwa mkoa wa Morogoro mradi wa LCD ambao ulitekelezwa na mkandarasi NAMIS Corparate Limited chini ya usimamizi wa Tanesco uliandaliwa kujenga njia za umeme zenye urefu wa kilomita 137.7 na msongo wa kati. 

Alisema pia kilomita 55.4 za umeme mdogo na kuweka mashine umba 320 na kuunganisha wateja 5731 kati ya hao wateja 5637 wa njia moja na wateja 94 wa njia tatu katika kutekeleza mradi huu mkandarasi alipewa jukumu la kujenga mifumo ya kusambaza umeme kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 2.4 huku zifaa vyote vikiletwa na kampuni ya Rea.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 31,2018














Tuesday, October 30, 2018

ROCK CITY MARATHON 2018 ILIVYONOGA: Watanzania, Wakenya wang’ara Rock City Marathon

 Mwanariadha Mourice Masima Kutoka Kenya  akimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza mwishoni  mwa wiki baada ya kutumia  muda wa saa 2:19:14. Kivutio katika mbio hizo ilikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella ambae licha ya kuzindua mbio hizo, alikimbia kikamilifu mbio za km 42 akiambatana na baadhi ya viongozi  waandamizi  wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Magu  Dk. Philemon Sengati .
 Mwanariadha Emmanuel Giniki  kutoka Tanzania akimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 21 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza leo baada ya kutumia  muda wa 1:04:09 akifuatiwa na Mkenya Daniel Kayioki alietumia muda wa saa 1:04:47.
 Mshindi wa kwanza  mbio za km 42 kwa upande wa wanawake Naomi Jepngetich kutoka Kenya  aliyetumia muda wa saa 02:44:19 kukamilisha mbio hizo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella  (katikati) akishiriki katika mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella  (katikati) akishiriki katika mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
 Baadhi ya washiriki wa mbio za Rock City Marathon wakiwa kazini!
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella  akimaliza mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella  (katikati) akikabidhi zawadi ya cheti,medali na pesa taslimu kiasi cha sh mil. 4 kwa mwanariadha Mourice Masima Kutoka Kenya  aliemaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza mwishoni  mwa wiki baada ya kutumia  muda wa saa 2:19:14.
 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi akikabidhi  zawadi ya cheti,medali na pesa taslimu kiasi cha sh mil. 4 kwa mshindi wa kwanza mbio za km 42 kwa wanawake mwanariadha Naomi Jepngetich kutoka Kenya  aliyetumia muda wa saa 02:44:19 kukamilisha mbio hizo. Kulia  ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella. TIPER ni moja ya wadhamini wakubwa wa mbio hizo.
 Mwakilishi kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bi. Flora Ndutta akikabidhi  zawadi ya cheti,medali na pesa taslimu kiasi cha sh mil. 3 kwa mshindi wa kwanza mbio za km 21 mwanariadha Failuna Matanga kutoka Tanzania.
 Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA) Bw Silas Lucas (kulia) akikabidhi zawadi  kwa mshindi wa kwanza mbio za KM 21 Emmanuel Giniki kutoka Tanzania alietumia saa 1:04:09 akifuatiwa na Mkenya Daniel Kayioki alietumia muda wa saa 1:04:47.
 Baadhi ya washiriki wa mbio za km 5 wakimalizia mbio hizo zilizohitimishwa kwenye viunga vya jengo la Rock City Marathon.
 Mmoja wa washiriki wa mbio za KM 3 mahususi kwa ajili ya wazee akiwa kazini
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mbio za km 42 Rock City Marathon kwa upande wa wanawake. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa mbio hizo Bw Zenno Ngowi  (wa tatu kulia), Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi (Kulia kwa Mkuu wa Mkoa) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA) Bw Silas Lucas.
Mkuu wa Wilaya ya Magu  Dk. Philemon Sengati (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mbio za km 5 kwa upande wa watu wenye ualibino.

Katika mashindano hayo ilishuhudiwa washiriki ambao pia ni wadhamini wa mbio hizo kutoka  makampuni ya Puma Energy Tanzania, Tiper,Rock City Mall,  NSSF, Gold Crest, New Mwanza Hotel,  CF Hospital, Coca Cola, Metro Fm, EF Outdoor,  KK Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Education Link wakishiriki kikamilifu katika mbio za KM 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.