Monday, November 30, 2015

MKUU WA WILAYA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA VYOO MANISPAA YA SHINYANGA..AKUTANA NA VYOO VYA AJABU...KIMO CHA KULENGA KWENYE BOMBAHiki choo cha ajabu kiko Shinyanga maelezo yapo chini.Leo Jumatatu Novemba 30,2015 ambapo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameanza kufanya ziara kutembelea kata za manispaa hiyo ili kuangalia hali ya usafi wa mazingira kubwa zaidi ni kukagua vyoo vya wananchi ilimkukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga alikuwa ameambatana na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna,mwanasheria wa manispaa hiyo Simon Jilanga,afisa afya wa manispaa hiyo Heri Nakuzelwa,waandishi wa habari na askari wa jeshi la polisi.Mkuu huyo wa wilaya ametembelea kata ya Chibe na Kambarage na kubaini kuwa kaya nyingi hazina vyoo na kuagiza wajenge vyoo haraka huku akifunga maduka matano kutokana na kukosa vyoo.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye msafara huo ametusogezea picha 37 kilichojiri....

RAIS MAGUFULI AONANA NA MABALOZI WA CHINA NA KOREA KUSINI, PROFESA LIPUMBA IKULU LEO


 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
PICHA NA IKULU

TASWIRA MBALIMBALI JIJINI DAR LEO

 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yanasa muendesha Bajaji akivunja sheria kwa kupita pasipo ruhusiwa kupita, hii ni pamoja na kuharibu miondo mbinu ya Barabara ya  mabasi yaendayo haraka ya Morogoro jijini Dar es Salaam.
Madereva wa magari haya mambayo yameshindwa kupishana kwa usahihi  wakielewana mara baada ya kugongana leo katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kama walivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa.
 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yanasa madereva wasiopenda kuvaa kofia ngumu(Herement) pamoja na Serikari Jeshi la Polisi kutoa agizo la kuvaa kofia hizo lakini wamekuwa wakiakipuuza sheria hiyo. wakingoja ningejua ninge.......
Mchana huo marekebisho ya hali ya tumbo yakiendelea katika sehemu ya chakula kama ilivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa.

(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).

RC KILIMANJARO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA

Na Mwandishi Wetu, Moshi
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika masoko manne ya Manispaa ya Moshi pamoja na dampo za kukusanyia uchafu, ili kujionea hali ya usafi na utendaji kazi katika mkoa huo. Katika ziara hiyo, RC Makalla alitumia muda huo kuwaagiza watendaji wake, hususan katika mchakato mzima wa kuifanya Moshi iwe kwenye usafi.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla mwenye miwani, akikagua soko lililopo kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumzia ziara yake hiyo, Makalla alitoa siku tatu kwa watendaji wa Manispaa ya Moshi kuhakikisha kwamba lundo la takataka katika soko la Kwasadala linaondoshwa haraka iwezekanavyo. Alisema hawezi kukubali kuona Manispaa hiyo inashuka kiwango chake cha kuifanya Moshi inaendelea kuheshimika katika suala zima la usafi.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla aliyesimama mlangoni, akiendelea na ziara yake ya kushtukiza kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

“Pamoja na kuagiza kuondoshwa kwa uchafu huo, pia nataka kuona Mkoa wetu wote unakuwa kwenye hali ya usafi, magari ya usafi yazoe taka kwa wakati, uongozi wa masoko uthamini usafi bila kusahau uongozi wa Hospitali ya Hai unakamilisha haraka ukarabati wa vyoo,” alisema Makalla. Kwa mujibu wa RC Makalla, kitendo cha kuiweka Moshi katika mazingira ya uchafu si tu inaondosha kwa kasi ile heshima yake, bali pia itazalisha ugonjwa wa mripuko, ukiwamo ule wa Kipindupindu unaosikika kuweka katika kambi katika baadhi ya wilaya nchini Tanzania. 

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla akipata maelekezo kutoka kwa watendaji na watumishi katika Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika sehemu mbalimbali kwenye manispaa hiyo. Bashir Nkoromo 15:27 (40 minutes ago) to Kambi, Josephat, pamojapure, othmanmichuzi, me, muhidinuk, josephat.lukaza, cathbert39, zainul.mzige21, fadhiliathuman., amichuzi, assengaoscar, dande15us Mbwana, kwa nini kwenye captions unaandika "Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla"? RC si ndiyo mkuu wa mkoa kwa Kiingereza? Kumradhi, imebidi nikuambie kwa sababu umeirudia sana. Zaidi ya hapo nakutakia kazi.

MKUU WA MKOA WA TANGA ATEMBELEA MIRADI YA MAJI KATIKA JIMBO LA MLALO

 Mbunge wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi akizungumza na wananchi wa jimbo la mlalo wakati wa sherehe ya kumpongeza, katika hafla fupi ilifanyika maeneo ya Mlalo Mkongoloni mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza atembelea wilaya ya Lushoto na kuangalia miradi ya maendeleo ya Serikali ikiwepo maabara na mradi wa maji wilayani Lushoto Mkoani Tanga  baada ya kabla ya hafla fupi ya Mbunge wa jimbo la Mlalo iliyofanyika maeneo ya Mlalo mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akisalimiana na wananchi wa jimbo laMlalo.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika jombo la Mlalo kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mariam Juma, Mbunge wa jimbo la Mlalo ndugu Rashid Shangazi na diwani wa jimbo la Kwemshasha Anuari Kiwe.
Baadhi ya wananchi na madiwani wa jimbo la Mlalo waliokusanyika kwaajili ya kukubali wito wa Mbunge wa Mlalo,Rashid Shangazi mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Tanga kukagua mradi wa maji katika jimbo la Mlalo, na Mbunge wa jimbo hilo kufanyiwa sherehe ya kumpongeza hafla hiyo iliyofanyika katika jimbo hilo wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Azma ya kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI, muda wa vitendo ni sasa

Na Mark B. Childress, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mwaka mmoja uliopita wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, niliandika makala kuhusu jitihada za kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI nchini Tanzania.  Toka wakati huo, kwa pamoja tumepiga hatua muhimu kuelekea katika kufikia azma hiyo, tukielekeza rasilimali na shughuli zetu kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi nchini kote. Hata hivyo, bado tunahitajika kuongeza nguvu na kufanya zaidi. Bila ya kuongeza kasi yetu katika mwelekeo huu, maambukizi mapya yataongezeka, jambo litakaloongeza idadi ya Watanzania watakaokuwa wakiishi na VVU hivyo kuathiri maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Kipindi cha miaka mitano ijayo ni kipindi muhimu sana katika kufikia lengo la kutokomeza kabisa UKIMWI duniani ifikapo mwaka 2030. Rais Obama ameweka malengo makubwa kwa Mpango wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR), akitangaza kuwa hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, PEPFAR itakuwa inawasaidia watu milioni 12.9 kupata matibabu yanayookoa maisha ya  kufubaza VVU na kuwawezesha wanaume milioni 13 duniani kote kupata tohara.  Aidha, kwa kushirikiana na wadau wa kiserikali, asasi za kiraia na sekta binafsi, PEPFAR itajielekeza katika kupunguza maambukizi ya VVU kwa asilimia 40 miongoni mwa wanawake vijana na wasichana katika nchi zilizoathiriwa zaidi  zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

SOMA ZAIDI HAPA

WANASOKA WANAWAKE ZAIDI YA 400 WASHIRIKI TAMASHA LA LIVE YOUR GOALS

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akifuatilia kabumbu ya wanawake iliyokua ikiendelea wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume. Kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Bw. Leonard Thadeo, na kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
 Baadhi ya wanasoka wanawake kutoka katika vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu wakisakata kabumbu jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA.
  Mabalozi walioteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini wakijitambulisha kwa mgeni rasmi wakati wa tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume kwa mara ya pili baada ya kufanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza Mkoani Geita mnamo mwezi Julai 2015.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akimwangalia mtoto Zaynab Dotto mwenye umri wa miaka 10 anavyocheza na mpira kwa umahiri jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kulia ni Mratibu wa Michezo ya Vijana wadogo Bw. Raymond Gweba na kushoto ni mama mzazi wa mtoto Zaynabu Bibi. Pili Said.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akipokea zawadi ya vifaa vya michezo kutoka FIFA vilivyokabidhiwa kwake na balozi alieteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini Bibi. Ester Chabuluma jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kushoto) akitoa zawadi ya mpira kwa mwanasoka wakike kutoka shule ya msingi Kingugi walioshiriki katika tamasha la Live Your Goals linalo hamasisha mpira wa miguu wa wanawake jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na wanasoka wanawake kutoka katika shule 5 za msingi na vilabu 6 vya mpira wa miguu wa wanawake baada ya kuhitimisha tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kushoto) akisisitiza jambo jana alipokutana na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 kuikabidhi bendera ya taifa kabla ya kwenda nchi mbalimbali za afrika kwa ajili ya mazoezi ya kujihimarisha kushiriki mashindano ya kufuzu mataifa ya Afrika under 17 mnamo mwaka 2017 nchini Madagasca.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akikabidhi bendera ya taifa kwa naodha wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 Bw. Issa Abdi jana katika Viwanja vya Karume kwa ajili ya kwenda nchini Rwanda, Uganda na Kenya kupata ujuzi na mazoezi kabla ya kushiriki mashindano ya kufuzu mataifa ya Afrika under 17 mnamo mwaka 2017 nchini Madagasca.

Picha na: Genofeva Matemu.

MWINYI LEADS THE “WALK FOR A DESK”

“The former president of Tanzania, Ally H Mwinyi leading the walkers during the charity walk “walk for a desk” organized by Hassan Maajar Trust in partnership with Bank M recenly at the police officers mess. The walk was aimed at raising funds for provision of desks for Majimatitu primary school in Mbagala, Dsm. With him are Bank M’s deputy CEO Jacqueline Woiso (fourth left)The HMT chair Ambassador Mwanaidi Maajar (fifth left), Mrs. Zhakia Bilal wife of the former vice president (third right) and Mrs Saada Othman Chande, wife of the chief justice of Tanzania.”
Bank M’s Deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso addressing the walkers during the “Walk for a Desk” took place over the weekend organized by the Hassan Maajar Trust in association with Bank M.
The former president of the united republic of Tanzania Hon. Ally H. Mwinyi who was the guest of honour addressing the walkers during the “Walk for a Desk” took place over the weekend organized by the Hassan Maajar Trust in association with Bank M.
The Chairman of the Hassan Maajar Trust Ambassador Mwanaidi Maajar addressing the walkers during the “Walk for a Desk” took place over the weekend organized by the Hassan Maajar Trust in association with Bank M.

THE former president of Tanzania hon. Ally H. Mwinyi led a number of Dar es salaam citizens in the charity walk held over the weekend, the walk which started and ended at the Police Officers Mess, Oysterbay, attracted hundreds of participants from across the city. 

The event, themed ‘“Walk for a Desk” was organized by the Hassan Maajar Trust in association with Bank M, and was aimed at raising funds for providing 1, 764 desks to students for Majimatitu Primary school in Mbagala, which has 5,000 students with only 550 desks.

Speaking during the event, retired president of Tanzania His Excellency Ali Hassan Mwinyi – who was the chief guest, said that the efforts shown by the Hassan Maajar Trust and its partners in serving the community deserves recognition. He congratulated Bank M which has been the main sponsor of HMT since inception in the year 2011 and encouraged them to continue with their corporate social responsibility strategy in supporting the key sectors of national development.

Speaking at the end of walk, the HMT Chairperson, Ambassador Mwanaidi Maajar said the support extended by its corporate partners has continuously contributed to the success of the project. “Since its launch, HMT in partnership with the public and corporate Tanzania has succeeded to provide over 8,100 desks lifting over 25,000 boys and girls off the floor onto desks in eleven regions of Tanzania, thanks to all our sponsors” said Ambassador Maajar.

Bank M’s Deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso said that the bank is proud to be partnering with the Hassan Maajar Trust in such a noble cause and commended the Trust for an ongoing job well done in the previous years. “Having over 25,000 children lifted off the floor and seated on desks is an achievement we can all be proud of, We have jointly made sitting on the floor a history for thousands of Tanzanian school children. It is our policy to work together with other reputable organization in making a difference to the needy communities of this land” said Ms. Woiso

HMT is dedicated towards improving the learning environment in schools by addressing and tackling the national school desk deficit across Tanzania.

Apart from the main partner Bank M, other sponsors of the walk include Azam, OGS, Uhuru one, China Tanzania security, Hindu Mandal hospital, NHC and Tigo.

WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WASHEREHEKEA 'FAMILY DAY'

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na wafanyakazi wa NMB pamoja na familia zao kabla ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Familia (family day) kwa wafanyakazi wa benki hiyo yaliofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Tusherehekee pamoja mafanikio ya Miaka 10 ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa NMB pamoja na familia zao kabla ya kuzinduwa rasmi maadhimisho ya Siku ya Familia (family day) kwa wafanyakazi wa benki hiyo yaliofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Tusherehekee pamoja mafanikio ya Miaka 10 ya NMB. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiingia katika maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) iliofanyika jana Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakitambuliwa kabla ya kuingia katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika jana Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi wa Benki ya NMB, na wanafamilia zao wakipata maelekezo kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa maadhimisho ya Siku ya Familia (family day) kwa wafanyakazi wa benki hiyo yaliofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Tusherehekee pamoja mafanikio ya Miaka 10 ya NMB. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipewa utaratibu kabla ya kuingia kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia yenye kauli mbiu ya tusherehekee Miaka 10 ya mafanikio ya benki ya NMB yaliofanyika jana Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi kikombe mmoja wa washindi katika mchezo wa kuogelea kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) akimkabidhi kikombe mmoja wa washindi katika mchezo wa kuogelea kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya washindi wa mchezo wa kuogelea wakipata picha ya kumbukumbu na viongozi waandamizi wa NMB baada ya kukabidhiwa zawadi zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia yaliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika michezo mbalimbali na familia zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) na iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika michezo mbalimbali na familia zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipata huduma mbalimbali ndani ya Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Malaika Bandi wakiwaburudisha wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya huduma za kibenki za Benki hiyo pia zilipatikana. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakifuatilia burudani anuai katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipata huduma mbalimbali ndani ya Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park katika maadhimisho ya Siku ya Familia na kusherehekea Miaka 10 ya benki hiyo iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizunguka kubadilishana mawazo na baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki hiyo kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia na kusherehekea Miaka 10 ya benki hiyo iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwasili eneo la Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park katika maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Mmoja wa viongozi wa NMB (kulia) akizungumza na wanafamilia na wafanyakazi wa Benki hiyo kabla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Familia iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika michezo mbalimbali na familia zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) iliyofanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanafamilia na wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika michezo mbalimbali na familia zao kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia (Family Day) hafla hiyo ilifanyika Kunduchi Wet 'n' Wild Water Park ya Jijini Dar es Salaam jana.