Friday, March 31, 2017

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS MHE.DKT. MAGUFULI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.
Shamra shamra zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

DAKIKA 360 ZA REKODI AZAM FC VS YANGA LIGI KUU


MACHO ya wapenzi wengi wa soka nchini wikiendi hii yatakuwa kwenye viwanja viwili nchini, lakini asilimia kubwa wanausubiria kwa hamu mtanange wa aina yake kati ya wapinzani Azam FC na Yanga, utakaofanyika kesho Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Jumapili vita nyingine itahamia mkoani Kagera, pale wenyeji Kagera Sugar watakapokuwa wakiikaribisha Simba katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mechi zote hizo zikitarajiwa kuamua hatima ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). 

Wakati Azam FC iliyo nafasi ya tatu kwa pointi 44 ikiwa kwenye vita kali ya kusogelea nafasi mbili za juu kileleni, inapambana na Yanga (53) ambayo ipo kwenye mchuano mkali na Simba (55) wa kuwania taji la ligi hiyo. 

Ushindi wowote wa Azam FC na Kagera Sugar, ambazo nazo zinafukuzana kuwania nafasi ya tatu, utakuwa unaziweka kwenye nafasi nzuri timu hizo kuzisogelea zaidi timu za juu na kuzitibulia mipango ya ubingwa Simba na Yanga. 

Kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Mromania Aristica Cioaba, tayari kipo kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo huo na kimejidhatiti kuibuka na ushindi na kuendeleza vita yake ya kukusanya pointi nyingi kadiri inavyowezekana ili kutimiza lengo lake la kufukuzia nafasi mbili za juu. 

Dakika 630 za Azam FC: Huku ikiwa imecheza mechi saba mfululizo (sawa na dakika 630) za ligi tokea mwaka huu uanze bila kuruhusu wavu wake kuguswa, pia Azam FC imecheza na Yanga katika mechi saba mfululizo za ligi bila kupoteza, kati ya hizo ikiwa imeshinda mara mbili na michezo mitano wakienda sare. 

Mara ya mwisho Azam FC kupoteza dhidi ya Yanga kwenye ligi, ilikuwa ni miaka minne iliyopita Februari 23, 2013, ikipoteza kwa kuchapwa bao 1-0, tokea hapo imekuwa ikifanya vema zaidi mbele ya Wanajangwani hao kwa mujibu wa takwimu hizo. 

Upinzani wa timu hizo kwa miaka ya hivi karibuni pia umefanikiwa kudhihirishwa na matokeo ya uwanjani tokea zianze kukutana kwenye ligi kwa mara ya kwanza msimu wa 2008/2009, Azam FC ilipocheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu, mtanange huo ulifanyika Oktoba 15, 2008 na Yanga kushinda kwa mabao 3-1. 


Hadi sasa ukiwa ni msimu wa tisa kukutana, timu hizo zimeshakutana mara 17 kwenye ligi, huku wakilingana kila kitu kitakwimu, Azam FC ikishinda mara tano kama Yanga, huku zikienda sare mara katika mechi saba, na pia zikiwa zimefungana mabao 25. 


Kombe la Kagame (mara mbili): Azam FC kabla ya kutwaa taji hilo mwaka juzi, iliweza kuandika rekodi ya aina yake ya kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2012 na kufika fainali iliyokutana na Yanga kabla ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0. 

Lakini wakati ikitwaa taji hilo la kwanza, ilirekebisha makosa na kuichapa Yanga kwa mikwaju ya penalti 5-3 kwenye mchezo wa robo fainali kufuatia suluhu kabla ya kwenda kubeba kombe hilo kwa rekodi inayosimama ya bila kufungwa bao lolote wala kupoteza mchezo. 

Kombe la FA (ASFC): Timu hizo zimekutana mara moja tu kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), ambayo ni mwaka jana na Yanga kushinda kwa mabao 3-1. 

Wakati Didier Kavumbagu, akiifungia Azam FC bao pekee, Yanga ilijipatia mabao yake kupitia kwa Amissi Tambwe, aliyefunga mawili huku Deus Kaseke akifunga jingine. 

Ngao ya Jamii (mara nne): Azam FC imekutana na Yanga mara nne mfululizo kwenye mechi za Ngao ya Jamii zinazoashiria kufungua pazia la ligi, ambapo imeweza kutwaa taji hilo mara moja msimu huu kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya 2-2. 

Wakati Yanga ikiwa imetangulia kufunga mabao mawili kupitia kwa mshambuliaji wake Donald Ngoma, Azam FC ilisawazisha yote kwa mabao ya beki Shomari Kapombe na nahodha Bocco aliyefunga kwa mkwaju wa penalti. 

Katika fainali tatu za mwanzo Yanga ilishinda 1-0 (2013), 3-0 (2014) na kwa mikwaju ya penalti 8-7 kufuatia sare ndani ya dakika 90 mwaka juzi. 

Mapinduzi Cup (mara tatu): Mara zote tatu walizokutana kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, Azam FC imefanikiwa kuifunga Yanga mara mbili na kutoka sare mchezo mmoja, mechi zote zikiwa ni za hatua ya makundi na mara zote ilizoibuka kidedea mabingwa hao waliweza kulitwaa taji hilo. 

Kwa mara ya kwanza zilikutana mwaka 2012, Azam FC ikaibugiza mabao 3-0, shukrani kwa Kipre Tchetche, aliyefunga mabao mawili huku nahodha John Bocco 'Adebayor', akipigilia bao lingine. 

Mwaka jana timu hizo zilikutana tena, safari hii zikatoka sare ya bao 1-1, Azam FC ikitangulia kufunga bao safi kupitia kwa Tchetche, aliyefunga bao lake la tatu katika michuano hiyo dhidi ya Yanga huku Vicent Bossou, akiisawazishia Yanga kwa bao. 

Azam FC iliendeleza mauaji dhidi ya Yanga kwenye michuano hiyo mwaka huu baada ya kuipa kipigo cha 4-0, kwa mabao ya kiufundi yaliyowekwa nyavuni na Bocco, Yahaya Mohammed, Joseph Mahundi aliyepiga shuti la umbali wa takribani mita 35 huku Enock Atta akipigilia msumari wa mwisho.

DC MUHEZA: AHIMIZA WANAFUNZI KUSOMA MASOMO YA SAYANSI KWA BIDII WILAYANI MUHEZA

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akitubia wananchi wa wilaya ya Muheza na wadau wa elimu katika maadhimisho ya ya Juma la Elimu wilayani Muheza kushoto ni Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa.
Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akimsikiliza kwa umakini Kaimu Afisa Elimu Msingi wilaya ya Muheza,Stuart Kuziwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Dkt Paul Kisaka.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Dkt Paul Kisaka akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza.
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Kidato cha nne Shule ya Sekondari Chief Mang'enya,Janet Justice wakati wa maadhimisho ya Juma la wiki ya Elimu.
Wanafunzi wa Shule za Msingi kutoka Maeneo mbalimbali wilayani Muheza wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye uwanja wa Jitegemee ambako kumefanyika maadhimisho ya Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlingano wenye mahitaji maalumu ya ulemavu wa kutokusikia na wale wenye ulemavu wa macho wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.

Umati wa wanafunzi na wananchi wilayani Muheza wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho hayo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muheza wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mkurumuzi wakicheza ngoma kwenye maadhimisho hayo.
Walimu wakishriki kwenye mchezo wa kukimbiza kuku kwenye maadhimisho hayo.
Walimu wakishinda kwenye mchezo wa kuvuta kamba kwenye kilele cha maadhimisho ya Juma la Wiki ya Elimu wilayani Muheza Mkoani Tanga.

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI BI. SARAH COOK AMTEMBELEA KAMISHNA JENERALI WA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA BW. ROGERS WILLIAM SIYANGA.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cook Leo amemtembelea ofisini kwake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya  Bw. Rodgers William Siyanga na kufanya mazungumzo ya  namna serikali za  Uingereza  na Tanzania zitakakavyoweza kushirikiana katika kudhibiti tatizo la dawa za kulevya . Katika ziara hiyo Balozi Cook aliambatana na maafisa kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania  Bw. Christopher Kiddle na Bw. Andrew Stephens.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cook (wapili kutoka kushoto) alipomtembelea  Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya  Bw. Rodgers William Siyanga (wa kwanza kulia) ofisini kwake leo asubui Jijini Dar es salaam. Balozi Cook aliambatana na maafisa kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw. Christopher Kiddle (wa kwanza kushoto) na Bw. Andrew Stephens (wa tatu kushoto), kutoka kulia (wapili) Makamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya

KAMATI YA KUKABILIANA NA KIPINDUPINDU YAKUTANA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA MWAKA MMOJA


Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afaya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akieleza mipango iliyoandaliwa ya kukabiliana na maradhi ya kipindupindu iwapo yatatokezea katika kikao kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Mazingira Rukaiya Mohamed Said akiwasilisha taarifa ya kikao kilichopita cha Kamati hiyo kilichofanyika mwezi uliopita.
Afisa kutoka Jumuia ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Zanzibar Jokha Masoud Salim akitoa mchango wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Kamati ya kukabiliana na kipindupindu wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu.
Afisa uperesheni na huduma za kibinadamu, Kamisheni ya kukabiliana na maafa Makame Khatibu Makame akitoa mada juu ya mpango wa kukabiliana na maafa Zanzibar katika cha Kamati hiyo kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.Na Khadija Khamis –Maelezo

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt Fadhil Moh’d Abdalla ameitaka jamii kubadili tabia kwa kuweka mazingira yaliyowazunguka safi na kuhakikisha wanatumia maji safi na salama ili kujiepusha na maradhi ya mribuko .

hayo ameyasema wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa ya kuandaa mpango mkakati wa kudhibiti maradhi ya kipindupindu hasa kipindi hichi ambacho mvua za masika zimeanza kunyesha.

Alisema lengo kuu la kamati hiyo ni kufanya tadhmini ya muendelezo wa mpango kazi wa kudhibiti maambukizi ikiwemo kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa jamii na kupambana na mazingira hatarishi katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Zanzibar.

Ameishauri Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha maji yanayotumiwa na wananchi yapo katika hali ya safi na salama kwa kutia dawa vianzio vyote vya maji na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kufanya uharibifu kwenye njia za maji kwa kutoboa mabomba yanayosamba maji .

Alieleza changamoto zinazowakabili kwa sasa ni kuwepo kwa wafanyabiashara wasiofuata taratibu za usafi wa chakula na mazingira katika utendaji mzima wa biashara zao.

Alisema uzoefu unaonyesha maradhi ya kipindupindu mara nyingi hutokea wakati wa kipindi cha mvua hivyo tahadhari zinahitajika katika kuweka mazingira katika hali ya usafi

“Wananchi wahakikishe wanakunywa maji ya kuchemsha au kuyatia watergard ili kuweka tahadhari wakati huu wa kipindi cha mvua za masika kwani kunauwezekano mkubwa wa kuchafuka vyanzio vya maji kwa kuingia maji machafu,” Alisema Mkurugenzi kinga .

Aliwashauri wananchi wanaoishi sehemu za mabondeni kuchukue juhudi za makusudi kuhama katika maeneo hayo ili kuepuka majanga katika kipindi hichi cha mvua za masika

TAARIFA KUTOKA UMOJA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM)

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM,Shaka Hamdu Shaka .


Tunawashukurukwa kupokea wito wetu na kuja, karibuni sana tunawaahidi kwamba tutaendelea kushirikiana nanyi katika kila hatua.

Aidha Umoja wa Vijana wa CCM unavipongeza sana vyombo vyote vya habari nchini kwa juhudi zenu za kuhabarisha, kuelimisha, kuwaasa, kuwaelekeza na kuihabarisha jamiii katika masuala kadhaa yanayohusiana na mipango ya maendeleo, mikakati, sera na malengo ya Serikali na mipango ya vyama vya siasa.

Ndugu Waandishi wa habari.

Tumewaita leo kuzungumzia mambo 2 makubwa, na suala zima la mtikisiko wa demokrasia katika mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulivyoendeshwa ndani ya vyama vya upinzani nchini.

Bunge la Afrika Mashariki kama mjuavyo ni chombo kikubwa na chenye heshima ya pekee katika kanda yetu. Kuwepo kwake kunaashiria muendelezo wa kufufua dhana, dhamira, mikakati, fikra na malengo ambayo yaliasisiwa na waasisi wa Mataifa yote yaliyomo katika Kanda yetu ili hatimaye siku moja ishuhudiwe Kanda hii na Bara zima la Afrika likiunda dola moja.

Ni jambo la heri na faraja kuona EAC ya sasa ikiwa ni yenye kufikia
malengo ya utengamano na mafanikio hususan katika nyanja za kiuchumi na kiusalama kama vile kuwa na Pasi moja ya kusafria, miingiliano ya
wananchi wake katika ufanyaji wa biashara pia mkakati kuelekea kupata
viwango sawia vya ushuru wa Forodha.

Masuala mengine ni kuona maeneo ya mipaka yetu kukiendelea kuwa na ustawi wa hali ya utulivu na usalama, wakati huo EAC ikifanya kila linalowezekana kumaliza migogoro yake ya kisiasa ambapo mazungumzo ya upatanishi huko Burundi yamekuwa yakiendelea chini ya mpatanishi mkuu Rais mstaafu Benjamin Mkapa sambamba na wananchi wa pande zote za nchi wanachama tukishuhudia wakiishi kwa maelewano, umoja, udugu na mafahamiano.

Ni katika jumla ya mambo yanayofurahisha na pengine yakiwasuta na
kuwaaibisha maadui na vibaraka ambao aghalab hutumiwa kwa malipo yenye ujira wa dhambi toka kwa mabeberu katika kuhakikisha mipango batili ya kutaka kudhoofisha, kuigawa na kukwamisha juhudi za EAC isiimarike..

Aidha kuibuliwa na kupokewa kwa mpango uitwao ” One Stop Boarder” yaani (OSB) sasa umefanikiwa huko mipakani baina ya nchi wanachama. Pia kuanzishwa miradi mikubwa ya kiuchumi mfano bomba la mafuta toka
Kampala (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) ujenzi wa reli toka kigali hadi
Uganda huku EAC ikielekea kuwa na sarafu moja kabla ya kufikiwa azimio
la uundwaji wa Shirikisho moja.

Umoja wa Vijana wa CCM tumelazimika kuyataja na kuyaainisha maeneo hayo yaliopata mafanikio kwa uchache lengo likiwa ni kuonyesha uwepo na
ustawi wa EAC pamoja na umuhimu wa bunge lake kama ni jambo nyeti na
wala si suala dogo au la mchezo mchezo kama ambavyo baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeonyesha udhaifu.

Ndugu Waandishi wa Habari,

Baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeshindwa hata kuteua wagombea ubunge wengi ili kuwania nafasi katika bunge hilo la Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa sababu zinazotokana aidha na ubinafsi, umimi na udikteta.

Tunachukua fursa hii kwanza kukipongeza Chama Cha Mapinduzi na wanachama wake wote 450 ambao kwa ujasiri, uwezo na kujiamini kwao wamethubutu kujitokeza na kuchukua fomu za kuwania nafasi za ubunge wa EAC.

Kitendo cha wanachama hao wa CCM kujitokeza kwa wingi kimsingi
kimeidhihirishia dunia kwamba chama chetu bado ni cha kidemokrasia
kinachoungwa mkono na kuaminiwa na wananchi wengi wakiwemo Vijana,
wanawake na wana taaluma mbali mbali wakitambua ndicho chama pekee imara chenye kujali, kuthamini na kufuata misingi ya usawa na demokrasia ya kweli.

Wanachama 450 wa CCM walichukua fomu kwa kufuata taratibu baada ya mchujo wa kidemokrasia kufanyika ndani ya CCM, wanachama 12 wamebahatika kuteuliwa na vikao vya kikatiba ambapo sasa wagombea hao watasimama mbele ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusaka ridhaa kwa kujieleza na kuomba kura.

Ndugu Waandishi wa habari,

Umoja wa Vijana CCM kwa tunasikitishwa sana na mwenendo wa demokrasia ndani ya vyama vya upinzani katika uteuzi wa kuwapata wagombea wa ubunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) Chadema, CUF na NCCR Mageuzi kwa jinsi walivyowasilisha uwakilishi haba na finyu lakini pia kujitokeza kwa wagombea wachache hali inayoonyesha uminyaji wa demokrasia ndani ya vyama vyao.

Chadema na washirika wao mara kadhaa hujigamba vichochoroni na kujionyesha kuwa wao ni watetezi wa demokrasia lakini unapofikia wakati wa utekelezaji wa jambo hilo kwa vitendo, ndani ya chama hicho humea ukandamizaji wa haki na kujitokeza upendeleo, ukanda, kubebana aidha kwa asili, ujamaa na urafiki au kulipana fadhila.

Katu huu si mwenendo mwema ulioonyeshwa na vyama vya upinzani. Vimejipaka matope ya fedheha kwa kushindwa kuonyesha kama ni waumini wa kweli wa demokrasia badala yake havikujali wala kuheshimu dhana ya demokrasia na kujikuta vimejianika na kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa vyama hivyo ni vya watu maalum vya kibwanyenye na vya kiimla .

Kufanya uteuzi wa wanachama wanaogombea nafasi za kidemokrasia kwa kumtazama asili yake, anatoka kanda ipi, kabila, imani yake au nasaba licha ya kwenda kinyume na misingi ya Taifa letu lakini pia ni kinyume na
matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM kwa kauli moja tunawaamsha na kuwatumia ujumbe watanzania wenzetu hususan Vijana mahali popote walipo wavikatae na kuvikwepa vyama vya aina hiyo, wasikubali kugawanywa kwa asili zao, imani au rangi na nasaba.

Taifa letu ni alama pana ya kuenzi na kudumisha demokrasia si tu barani Afrika lakini vile vile duniani kote, hivyo kwa umoja wetu, kwa nguvu zetu, akili na maarifa tulionayo, abadan tusijaribu kuichezea amani yetu, umoja na mshikamano wetu uliojengwa na waasisi wa Taifa letu na kukubali
kuvishabikia vyama na viongozi wasaka madaraka kwa hila ambao ni
wafujaji na wakandamizaji wa misingi ya demokrasia ndani ya vyama kama
ilivyojionyesha kwa vyama vya upinzani vya Tanzania katika uteuzi wa
wabunge EAC.

Mchakato wa Uchaguzi ndani ya UVCCM.

Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2017, unafanyika wakati ambapo CCM inatimiza miaka 40 tokea kuasisiwa kwake tarehe 5 Februari, 1977 na ni wakati ambapo nchi yetu inatimiza miaka 25 ya Mfumo wa Vyama Vingi ulioridhiwa na Mkutano Mkuu wa CCM kutokana na busara za Viongozi wake.

Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Chama na Jumuiya zake inaonesha mchakato wa Uchaguzi wa Jumuiya za CCM kuwa unaanza kabla ya ule wa CCM. Utaratibu huu unalenga kuwawezesha wanachama wa Jumuiya za CCM ambao watakuwa ni wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika CCM, au wale waliochaguliwa kuwakilisha Jumuiya zao katika Vikao vya CCM ili waweze kuhudhuria mikutano ya Chama inayowahusu.

Umoja wa Vijana wa CCM umekamilisha maandalizi yote ya msingi ya awali kwa ajili ya Uchaguzi unaotarajia kuanza tarehe 1 April, 2017 ikiwemo
kusambaza vifaa katika Mikoa na Wilaya zote nchini wa ajili ya
kufanikisha uchaguzi kwa wakati.

Aidha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
imekamilisha mapitio na uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika
Jumuiya ambao watakuwa ndio wakurugenzi wa Uchaguzi katika maeneo yao.

Tunaendelea kuwakumbusha Watendaji wetu muda wote kusimamia haki, ukweli na usawa lazima vijana wa CCM muda wote tuishi katika maneno na maagizo ya Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.

Hatutamvumilia mtendaji yeyote atakayekiuka Kanuni, Taratibu na miongozo kwa makusudi ili kufurahisha kikundi au watu fulani. Uchaguzi huu 2017 UVCCM tunataka kuidhihirishia dunia na Vyama vya Upinzani kuwa CCM ni Chuo Cha Demokrasia ulimwenguni.

Mwisho niendelee kuwahamasisha vyema wote nchini yenye sifa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali za uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya, Mikoa na Taifa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)

KAIMU KATIBU MKUU

Watumishi Wa OSHA Wapewa Changamoto

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kikao chao cha baraza. Kulia ni Kaimu  Mtendaji Mkuu wa Wakala Bi. Khadija Mwenda na viongozi wa baraza hilo. 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) mara baada ya kufungua kikao chao cha baraza.) 
Wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi (hayupo pichani) alipofungua kikao cha baraza lao mjini Dodoma jana.


Mabadiliko ya mazingira ya ufanyaji biashara yanayoletwa na maendeleo ya uchumi wa viwanda pamoja na mnyororo wa thamani, yameelezwa kuwa changamoto kubwa katika jitihada za kuimarisha hali ya usalama na afya za wafanyakazi katika sehemu za kazi hapa nchini.

Changamoto hiyo imetolewa na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Bw, Eric Shitindi, wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) mjini Dodoma leo.

Amesema mabadiliko hayo yanahusisha matumizi ya teknolojia za kisasa na ongezeko kubwa la idadi ya wafanyakazi katika sekta zote za umma na za binafsi jambo ambalo linahitaji utaalamu mkubwa katika kuweka na kusimamia mifumo ya kulinda afya na kuwahakikishia usalama wafanyakazi wote wanapokuwa katika sehemu zao za kazi.

“Hivyo mkiwa kama wataalamu katika masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi mnatakiwa kuwa na mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto hizo. Hii itakuwa ni pamoja na kubadilika kifikra na kimtazamo katika utendaji kazi,” alisema Katibu mkuu Shitindi.

Katibu mkuu huyo amesisitiza muhimu wa kutafuta mbinu mbadala ya kuweza kupanua wigo wa kufanya kazi hasa kwa kuzingatia ukubwa wa kazi zilizopo.

Aidha Bw. Shitindi ameupongeza OSHA kwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa mpango kazi wake katika kipindi cha robo tatu za mwaka huu wa fedha (2016/2017) ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa katika baraza hilo, taasisi imevuka malengo katika kaguzi, utoaji wa mafunzo ya usalama na afya kazini pamoja na huduma mbali mbali zitolewazo mahali pa kazi.

Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliahidi kuendelea kuisaidia OSHA kutatua changamoto zilizopo zikiwemo za kiutendaji na kuwaasa watumishi wa Wakala kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ikiwemo kuepuka kujihusisha na vitendo vya upokeaji rushwa wanapotekeleza majukumu yao.

“Wizara imekuwa ikipokea malalamiko mengi ya namna mnavyohudumia wateja na kushuka kwa maadili ya kiutendaji miongoni mwa watumishi, mfano masuala ya rushwa, hivyo wakati tunaendelea kushughulikia matatizo hayo ni vyema sasa mkaanza kubadilika kwa kufuata sheria, taratibu, kanuni na miongozo mbalimbali ya utendaji kazi katika taasisi,” amesisitiza Bw, Shitindi.

Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi wa OSHA ambacho kimeanza leo kitamalizika kesho ambapo pamoja na mambo mengine kitapitia na kujadili makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha wa (2017/2018) ili kujiridhisha kama itawawezesha kufanikisha utekelezaji wa malengo ya wakala yaliyowekwa

DKT. KALEMANI ATAJA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA 2016/17


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Dkt. Medard Kalemani akiongea jambo wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2016/17.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dotto Biteko, akichangia Hoja baada ya Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2016/17 kuwasilishwa kwa Kamati.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Susan Kiwango akichangia Hoja baada ya kuwasilishwa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2016/17.
Mjumbe Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Mhe. Oscar Mkasa akichangia jambo wakati wakati wa kikao baina ya Kamati na Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake, ambapo Wizara na Taasisi ziliwasilisha Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2016/17.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gisima Nyamo- Hanga, akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya REA kwa mwaka 2016/17 kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2016/17 ya shirika hilo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Haji Janabi, akiwasilisha Taarifa ya Utekelzaji wa Wizara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Baadhi ya Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakifuatilia kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

…………………………………………………………………..

Wizara ya Nishati na Madini imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuanzia tarehe 27 Machi, 2017, ambapo Wizara na Taasisi zilizo chini yake zimewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2016/17.

Akielezea baadhi ya mafanikio ya Wizara kwa Kamati ya Bunge, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, ametaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na;
 
Kukamilika kwa asilimia 100 kwa Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga wenye msongo wa kilovoti (kV), 400.

Kukamilika kwa asilimia 98.5 ya Awamu ya Pili ya Mradi Kambambe wa Kupeleka umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini- REA.
Kuzinduliwa rasmi kwa Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kupeleka umeme Vijijjini unaolenga kusambaza umeme katika vijiji vyote visivyofikiwa na huduma hiyo.
 
Kukamilika kwa Kanuni za:
The Petroleum (Retail Operations in Townships and Villages) Rules,2016
The Petroleum (Natural Gas Pricing) Rules,2016
The Electricity (Supply Services) Rules, 2016

The Electricity (Market re- organization and competition) Rules,2016 na
The Mining (Minimum shareholding and Public Offering) Regulations 2016. Kanuni hizi zinasimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu Sekta za Nishati na Madini.

Kuanza kwa maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.

Kuendeleza shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini ambapo hadi sasa jumla ya Futi za Ujazo Trilioni 57.25 za gesi asilia zimegunduliwa.
Kukamilisha utafiti wa jio-sayansi (jiolojia, jiokemia na jiofikizia katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuchora ramani za kuanisha kuwepo kwa madini mbalimbali ili kuhamasiaha uwekezaji kwenye maeneo ya Nachingwea, Ruangwa na Masasi.

Wizara kutenga maeneo 11 kwa ajili ya wachimbaji madini wadogo yaliyopo Msasa na Matabe Mkoani Geita, Biharamulo na Kyerwa yaliyopo Mkoani Kagera, Itigi, Mkoani Singida, D- Reef, Ibindi na Kapanda Mkoani Katavi, Ngapa Mkoani Songea, Nzega Mkoani Tabora na Kitowelo Mkoani Lindi. Maeneo hayo yana ukubwa wa takriban hekta 38.567
 

Kufanyika kwa minada miwili (2) ya madini ya vito hususan tanzanite jijini Arusha ambapo Serikali ilipata jumla ya shilingi milioni 793 ikiwa ni mrabaha uliolipwa Serikalini kutokana na minada hiyo.