Friday, January 31, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI MBEYA

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na waendesha Bodaboda wa mjini Mbeya, ambapo wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la polisi na polisi jamii katika kulinda usalama wa wananchi, wao wenyewe na mali kwa ujumla, Chanagamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na utulivu. 1AKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambao wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mtenda Soweto jijini Mbeya. 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Blogger wa Mbeya yetu Blog Bwana Joseph Mwaisango.
3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika meza kuu kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo.
4Waendesha Bodabona wakimshagilia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiongea nao leo. 5
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukitoka uwanja wa ndege wa Songwe kuelekea mjini Mbeya leo mara baada ya kuwasili mkoani humo. 6
Shangwe za waendesha bodaboda zikiendelea. 7
Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi. 8
Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi. 9Waendesha Bodaboda wakifuatilia hotuba za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo. 10
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza wakati wa mkutano huo leo. 11
Hapa ni Shangwe tu 12
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea risala ya waendesha Bodaboda kutoka kwa Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda. 13
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibebwa juujuu na waendesha bodaboda mara baada ya kuwahutubia kwenye ukumbi wa Mkenda leo. 14 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na uongozi wa waendesha Bodaboda kushoto ni mwenyekiti Vicent Mwashoma na kulia ni Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA)

Ubalozi wa China watoa msaada kwa waathirika wa mafuriko mkaoni Morogoro

Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youping akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Leteni Jenerali Sylivester Rioba. msaada huo ambao unathamani ya Shilingi milioni 32 umetolewa kwa ajili ya watu walioathirika na mafuriko mkoani Morogoro.
Balozi wa China (katikati) akishikana mikono na Luteni Generali Rioba na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Athony Mtaka wakati wa hafla ya kukabidhi msaada iliyofanyika katika Ubalozi wa China. nyuma yao lori aina ya fuso likiwa limejazwa baadhi ya bidhaa za msaada huo.
Balozi wa China akikabidhi stakabadhi za vifaa vya msaada kwa Leteni Jenerali Rioba huku Mkuu wa Wilaya ya Mvomero akishuhudia.
Wanahabari nao hawakuwa mbali kushuhudia hafla ya makabidhiano.
Balozi wa China, Mhe. Lu Youping akitoa hotuba fupi.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu akitoa hotuba ya kushukuru msaada uliotolewa na Balozi wa China.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mberwa Kairuki akisalimiana na Luteni Jenerali Rioba mara baada ya hafla ya kukabidhi misaada kukamilika. Picha na Reginald Philip Kisaka.

SHULE YA MSINGI KABALE BUKOBA VIJIJINI YAPOKEA UGENI WA MRADI WA "OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION" TOKA MAREKANI

Mwanafunzi wa Shuke hiyo ya Kabale iliyopo Bukoba Vijijini akimkabidhi Bw. J. Joe Ricketts maua ikiwa ni ishara ya kumkaribisha mgeni huyo kutoka USA kupitia Mradi wa (Opportunity Education Foundation) kwenye shule hiyo leo hii.
Bw. J. Joe Ricketts  kutoka USA kupitia Mradi wa (Opportunity Education Foundation)  akiingia kwenye eneo la Shule hiyo kwenye shule hiyo ya Kabale, Baada ya kupokelewa na Walimu wa Shule hiyo. Kutoka kushoto wa Pili ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Kalafaelia Madiloba na kulia ni Dada Sandra aliyeambatana nae Mgeni huyo Bw. Joe Ricketts kutoka USA.
Wanafunzi wa Shule Kabale wakimkaribisha Mgeni huyo kwenye Shule yao leo.
Bw. J. Joe Ricketts  kutoka USA kupitia Mradi wa (Opportunity Education Foundation)  akiingia kwenye eneo la Shule hiyo na hapa alikuwa akiteta jambo na  Dada Sadra
Bw. J. Joe Ricketts  kutoka USA kupitia Mradi wa (Opportunity Education Foundation)  akisikiliza wimbo alioandaliwa na Wanafunzi wa Shule hiyo. Mradi huu wa Opportunity Education Foundation umewafadhili  Shule hiyo Vifaa vya kufundishia, na pamoja na swala la Chakula na Uji kuanzia Darasa la kwanza mpaka la Saba.Wanafunzi wa Shule Kabale wakimwimbia  Mgeni huyo Bw. J. Joe Ricketts wimbo uliokuwa na Ujumbe
Baadhi ya Walimu wa Shule hiyo wa pili kutoka kushoto ni Bw. Mohamed Dauda Mkuu wa Shule Msaidizi.
Mkuu wa Shule ya Kabale iliyopo Bukoba Vijijini Bi. Kalafaelia Madiloba
Mkuu wa Shule ya Kabale iliyopo Bukoba Vijijini Bi. Kalafaelia Madiloba (kushoto) akisoma Ujumbe mbele ya Bw. J. Joe Ricketts  kutoka USA kupitia Mradi wa (Opportunity Education Foundation)
Bw. J. Joe Ricketts  kutoka USA kupitia Mradi wa (Opportunity Education Foundation) Kulia akiwa kwenye maongezi na Bw. Mbaki Mutahaba (kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa Opportunity Education Foundation. (O.E.F)
Mkuu wa Shule ya Kabale(kulia) akifurahia jambo kutoka kwa Bw. J. Joe Ricketts  wakati anamtembeza kwenye maeneo ya Shule hiyo ya Kabale.
Bw. J. Joe Ricketts - Benefactor
Bw. J. Joe Ricketts amejionea swala zima la ugawaji uji kwa Wanafunzi wa Shule hiyo ya Kabale na yeye akashiriki zoezi hilo la ugawaji Uji kwa Wanafunzi.
Baadhi ya Wanafunzi wakifurahia hapa baada ya kupata Ugeni huo kutoka USA
Bwana J. Joe Ricketts akikabidhiwa zawadi na Mwalimu wa Shule hiyo ya Kabale leo
Picha ya Pamoja ya Walimu wa Shule ya Msingi Kabale iliyopo Bukoba Vijijini. Picha zote na Faustine Ruta

Washindi wa Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ warejea kutoka Old Trafford

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) akifurahia jambo pamoja na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya safari yao iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel ya Mimi ni Bingwa walioondoka nchini Jumapili wiki hii kwa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Baadhi ya washindi wa tiketi kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakishuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza.Wa kwanza kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando ambaye aliambatana na washindi hao.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiwa pamoja na mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa Bw na Bibi Dickson Lyatuu muda mfupi baada ya kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City nchini Uingereza hivi karibuni.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester united Denis Irwin ( wapili kushoto) akiwa katika picha na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (anayefatia) pamoja na mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa kabla ya kuangalia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza.

WASHINDI wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa jana waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Old Trafford ambapo walikwenda kushuhudia mechi ya moja kwa moja ‘live’ kati ya klabu ya Manchester United na Cardiff City.

Watanzania hao wamekuwa sehemu ya washabiki wa soka waliokuwa na furaha kushuhudia klabu ya Manchester United ikishinda 2-0 dhidi ya Cardiff City, wakati mchezaji Juan Mata akiichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Old Trafford, hawakuweza kuficha furaha yao ya kuwa moja ya tukio hilo la kihistoria.   

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege, moja kati ya washindi wa tiketi ya Airtel Mimi ni Bingwa, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, ambaye alisafiri na mke wake, alisema safari hiyo imekuwa ya manufaa sana katika maisha yao na kampuni hiyo ya simu imeweza kutekeleza yale yote waliyowaahidi washindi wa tiketi katika promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa. 

“Ninafuraha ya kipekee kuweza kurejea nyumbani salama baada ya safari yenye mafanikio makubwa ya kwenda Old Trafford. Suala nililojifunza nikiwa Manchester ni kwamba bado Tanzania inahitaji kufanyakazi kubwa ili kuziwezesha timu zetu kuendelea katika ulimwengu wa soka. Nawashukuru Airtel kwa kunipa mimi na mke wangu nafasi ya kuwa sehemu ya historia hii na kuweza kuyatekeleza yote waliyotuahidi,” alisema.

Meneja Uhusiano wa Aitel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando alisema wakati wa ziara ya kutembelea Old Trafford, timu ya washindi kutoka Tanzania ilionyeshwa ni jinsi gani Manchester United inawajali wachezaji wake waliostaafu, suala linalosaidia kuongeza hari katika timu na kutumia uzoefu kuiboresha timu.

“Huu ni mfano ambao wadau wetu wa michezo wanahitaji kuuiga. Tunatakiwa kuwathamini wachezaji wetu wa zamani na kutumia uzoefu wao ili kuzibadilisha timu zetu kuwa bora kimchezo kitaifa na kimataifa,” alisema.

Kwa upande wake, Andrew Muta Temwa, mshindi wa tiketi kutokea Bukoba alisema fursa ya kukutana na kocha Sir Alex Ferguson ilikuwa ni kama ndoto kwake. 

“Sikutarajia kama siku moja nitakutana na Sir Alex Ferguson moja kwa moja ‘Live’. Kupitia safari hii, Airtel imeweza kuzifanya ndoto yangu kuwa kweli. Nataka kuwahakikishia washiriki wengine wa Mimi ni Bingwa waendelee kucheza ili nao wapate fursa ya kushinda pesa taslim kupitia promosheni hii ya Airtel,” alisema.

Awamu ya kwanza ilijumuisha, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Andrew Muta Temwa mkazi wa Bukoba, Ashraf Mohamed Adam kutoka Tanga na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam na wenza wao.

Airtel ilitangaza kuwa mbali na tiketi, zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 sasa iko tayari kushindaniwa mwishoni mwa droo, ambayo kila mshiriki wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa ana nafasi ya kujishindia kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo.     


Washindi wa safari ya Old Trafford toka promosheni ilipoanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ni pamoja na  Msemwa George Makuzi kutoka Dar es salaam, Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini  Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.

MH. PINDA AZINDUA RASMI MAPITIO YA MFUMO WA UWEKEZAJI TANZANIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) akikata utepe kuzindua ripoti ya hali ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine ripoti hiyo imegusia sera na na maendeleo ya uwekezaji nchini pamoja na changamoto zinazokwamisha ustawi wa uwekezaji Tanzania.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akionyesha vitabu vya ripoti ya Uwekezaji Tanzania kwa wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ripoti kuhusu hali ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi kitabu cha Ripoti ya hali Uwekezaji nchini Tanzania Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi (kulia) leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na wadau wa uwekezaji mara baada ya kuzindua ripoti kuhusu hali ya uwekezaji nchini Tanzania.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi (kulia) akizungumza jambo na Bi. Marry Hobbs Mwakilishi wa masuala ya Kilimo na Maliasili wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani nchini Tanzania leo wakati wa Uzinduzi wa ripoti ya hali ya Uwekezaji nchini.
Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ripoti ya Uwekezaji nchini Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu changamoto na hali ya uwekezaji katika sekta ya Mifugo na uvuvi nchini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika katika masuala ya uwekezaji nchini endapo itatekeleza kikamilifu Mapitio ya Mfumo wa Uwekezaji yaliyowasilishwa na Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD).

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Januari 31, 2014), wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kitabu cha  Mapitio ya Mfumo wa Uwekezaji kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu Pinda  alisema kuwa malengo ya mapitio ya  mfumo huo ni kuboresha hali ya uwekezaji na biashara nchini ambayo matokeo yake yatasaidia kuongeza wawekezaji katika maeneo mengi.

“Kuna maeneo ya uwekezaji yanayopata uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi (Foreign Direct Investment -FDI) ambayo ni umeme, mafuta, gesi, madini, viwanda, ujenzi na huduma za jamii.”

Amesema kuwa matokeo ya jitihada hizi ni makubwa na yameonekana ndani ya miaka miwili tu. Akitoa mfano, alisema: “Kilimo kimeweza kukua kutoka dola za marekani  milioni 304.5 mwaka 2010 hadi dola za marekani milioni 355.4 katika mwaka 2011. Vilevile kwenye sekta ya Umeme na Gesi imekua kutoka dola za kimarekani  milioni 328.6 hadi dola za kimarekani  539.8 mwaka 2011.”

Kutokana na matokeo hayo, Waziri Mkuu ameeleza kuwa Tanzania ina fursa nyingi zikiwemo rasilimali, nafasi yake kijiografia na historia ya siasa safi ambazo zinaifanya iwe kivutio kikubwa cha uwekezaji. Hali hiyo Waziri Mkuu alisema, imesaidia Pato la Taifa kuendelea kukua kwa asilimia sita kwa miaka 10 mfululizo na mwaka jana ilikua kwa asilimia saba na sasa inatarajiwa kufika asilimia 7.2 kwa mwaka huu.

Miongoni mwa maeneo yanayohusishwa na mfumo huu wa mapitio ya Uwekezaji ni yale yaliyoainishwa katika Matokeo makubwa sasa ambayo ni Kilimo, Maji, Uchukuzi, Elimu na Nishati.

“Ili kufanikisha maeneo hayo ni muhimu tukajenga mazingira bora ya uwekezaji, hivyo Serikali inawataka wadau wote kwa kushirikiana na Sekta binafsi kuchambua kwa makini mapendekezo ya mapitio ya mfumo huo ambayo yanatumika pia kuharakisha mafanikio ya Matokeo makubwa sasa”, alisisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alisema Serikali ya Tanzania inashukuru sana Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) kwa kuweka sura maalum kwenye kitabu hicho  inayozungumzia changamoto za uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo.

“Ninatumaini kuwa utekelezaji wa mapendekezo haya utaongeza ufanisi wa mchakato huu na kuhakikisha kuwa tunazitumia fursa zilizopo na nyingine zaidi katika kuboresha uwekezaji katika kilimo nchini. Na kwenye kilimo ninamaanisha kilimo mazao, mifugo, uvuvi na nyuki,” aliongeza.

Mapema, Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya OECD, Bw.  Rintaro Tamaki, alisema mazingira ya uwekezaji nchini yanabadilika kila mara kutokana na kuvumbuliwa kwa rasilimali mpya kama vile gesi, makaa ya mawe ambazo zinasababisha watu wavutive kuwekeza nchini.

”Kutokana na kugunduliwa na sekta hizo, Serikali isizipuuzie sekta za zamani hususan Sekta ya kilimo, cha msingi ni kuboresha sekta hii kwa kuanzisha viwanda ili kuongeza thamani ya mazao yenu”.