Friday, January 31, 2014

Washindi wa Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ warejea kutoka Old Trafford

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) akifurahia jambo pamoja na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya safari yao iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel ya Mimi ni Bingwa walioondoka nchini Jumapili wiki hii kwa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Baadhi ya washindi wa tiketi kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakishuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza.Wa kwanza kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando ambaye aliambatana na washindi hao.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiwa pamoja na mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa Bw na Bibi Dickson Lyatuu muda mfupi baada ya kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City nchini Uingereza hivi karibuni.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester united Denis Irwin ( wapili kushoto) akiwa katika picha na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (anayefatia) pamoja na mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa kabla ya kuangalia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza.

WASHINDI wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa jana waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Old Trafford ambapo walikwenda kushuhudia mechi ya moja kwa moja ‘live’ kati ya klabu ya Manchester United na Cardiff City.

Watanzania hao wamekuwa sehemu ya washabiki wa soka waliokuwa na furaha kushuhudia klabu ya Manchester United ikishinda 2-0 dhidi ya Cardiff City, wakati mchezaji Juan Mata akiichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Old Trafford, hawakuweza kuficha furaha yao ya kuwa moja ya tukio hilo la kihistoria.   

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege, moja kati ya washindi wa tiketi ya Airtel Mimi ni Bingwa, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, ambaye alisafiri na mke wake, alisema safari hiyo imekuwa ya manufaa sana katika maisha yao na kampuni hiyo ya simu imeweza kutekeleza yale yote waliyowaahidi washindi wa tiketi katika promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa. 

“Ninafuraha ya kipekee kuweza kurejea nyumbani salama baada ya safari yenye mafanikio makubwa ya kwenda Old Trafford. Suala nililojifunza nikiwa Manchester ni kwamba bado Tanzania inahitaji kufanyakazi kubwa ili kuziwezesha timu zetu kuendelea katika ulimwengu wa soka. Nawashukuru Airtel kwa kunipa mimi na mke wangu nafasi ya kuwa sehemu ya historia hii na kuweza kuyatekeleza yote waliyotuahidi,” alisema.

Meneja Uhusiano wa Aitel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando alisema wakati wa ziara ya kutembelea Old Trafford, timu ya washindi kutoka Tanzania ilionyeshwa ni jinsi gani Manchester United inawajali wachezaji wake waliostaafu, suala linalosaidia kuongeza hari katika timu na kutumia uzoefu kuiboresha timu.

“Huu ni mfano ambao wadau wetu wa michezo wanahitaji kuuiga. Tunatakiwa kuwathamini wachezaji wetu wa zamani na kutumia uzoefu wao ili kuzibadilisha timu zetu kuwa bora kimchezo kitaifa na kimataifa,” alisema.

Kwa upande wake, Andrew Muta Temwa, mshindi wa tiketi kutokea Bukoba alisema fursa ya kukutana na kocha Sir Alex Ferguson ilikuwa ni kama ndoto kwake. 

“Sikutarajia kama siku moja nitakutana na Sir Alex Ferguson moja kwa moja ‘Live’. Kupitia safari hii, Airtel imeweza kuzifanya ndoto yangu kuwa kweli. Nataka kuwahakikishia washiriki wengine wa Mimi ni Bingwa waendelee kucheza ili nao wapate fursa ya kushinda pesa taslim kupitia promosheni hii ya Airtel,” alisema.

Awamu ya kwanza ilijumuisha, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Andrew Muta Temwa mkazi wa Bukoba, Ashraf Mohamed Adam kutoka Tanga na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam na wenza wao.

Airtel ilitangaza kuwa mbali na tiketi, zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 sasa iko tayari kushindaniwa mwishoni mwa droo, ambayo kila mshiriki wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa ana nafasi ya kujishindia kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo.     


Washindi wa safari ya Old Trafford toka promosheni ilipoanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ni pamoja na  Msemwa George Makuzi kutoka Dar es salaam, Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini  Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.

No comments: