Wednesday, May 31, 2017

DKT. NCHIMBI AAGIZA HALMASHAURI KUANZISHA BENKI ZA WANA MICHEZI NA KUTENGA VIWANJA VVYA MICHEZO MKOANI SINGIDA.

Halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida zimeagizwa kutenga maeneo yenye hadhi ya kuwa viwanja vya michezo pamoja na kuhakikisha zinakuwa na benki ya wanamichezo katika halmashauri zao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa maagizo hayo leo asubuhi kabla ya kuzindua mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA) kwa ngazi ya mkoa ambapo wanamichezo hao wataunda timu za Mkoa kwa ajili ya mashindano ya kitaifa yatakayofanyika jijini Mwanza mwezi ujao.

Dkt. Nchimbi amesema halmashauri zimekuwa zikiwatelekeza wanamichezo mahiri hivyo wakianzisha benki ya wanamichezo kwa maana ya kuhifadhi kumbukumbu za wana michezo mahiri pamoja na kuwaendeleza hawatapata shida kipindi cha mashindano yoyote. 

Ameongeza kuwa halmashauri zimekuwa zikijisahau katika kuandaa maeneno ya michezo hadi inapofika kipindi cha UMISETA hali inayopelekea kukosekana kwa viwanja vya kufanyia mazoezi ili kuwa na timu bora.

Dkt. Nchimbi amewaasa wana michezo kuwa na nidhamu, utii, bidii na kuitumia michezo kuutangaza Mkoa wa Singida wenye fursa nyingi za uwekezaji pamoja na kujitangaza uwezo wao ili waweze kupata nafasi katika timu mbalimbali za kitaifa.

Aidha amewasisitiza waamuzi wa michezo kutenda haki kwakuwa matendo yao ni darasa la nidhamu na maadili kwa wanafunzi wao na kuwatahadharisha wanafunzi wasio tii kuwa hawatapata nafasi katika timu ya Mkoa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi amewapongeza wakurugenzi wa halmashauri kwa kufanikisha upatikanaji na ushiriki wa timu za michezo za kila halmashauri.

Dkt. Lutambi ameishukuru pia kampuni ya Coca cola kwa udhamini wa UMISSETA kwa kutoa vifaa kwa shule 118 ambavyo ni tisheti 3,776, mipira ya miguu 118 na mipira ya basketball 118 pamoja na ahadi ya kuendelea kugawa vifaa katika shule 45 zilizobaki.

Ameongeza kwa kuwasihi wana michezo wote kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa kuzingatia sheria na kanuni za michezo ili kutengeneza timu ya ushindi ya mkoa.

Akisoma taarifa ya Michezo ya Umiseta Afisa Michezo wa Mkoa Henry Kapella amesema jumla ya wana michezo 576 wameshiriki katika michezo hiyo ambapo wataunda timu ya mkoa ya michezo ya bao, riadha, mpira wa miguu na mpira wa pete. 

Kapella ameongeza kuwa kauli mbiu ya michezo ya Umisseta kwa mwaka 2017 ni ‘Wekeza katika michezo kwa ustawi wa elimu na Viwanda’. 

Kwa upande wao wanafunzi walioshiriki mashindano ya umisseta wamesema michezo inawajenga kiafya na kiakili kwa kuwa wanafunzi wanaoshiriki katika michezo huwa na ufaulu mzuri wa masomo yao.

Wameongeza kuwa michezo inawaongezea nidhamu na kuwajenga kimaadili hivyo kufaulu inakuwa ni rahisi, aidha wamesema michezo ina faida nyingi ikiwemo kuwatengenezea ajira mara baada ya kumaliza masomo yao.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (aliyenyanua ubao) akipiga ubao wa kuashiria uzinduzi wa michezo ya UMISSETA mkoa wa Singida, mbele yake ni wanariadha wakianza mashindano.
 Wanamichezo kutoka Shule za Sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa, kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi na Kulia Kwake ni Afisa Elimu Mkoa wa Singida Florian Kimolo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia kabla ya kuzindua mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa wa Singida.
 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA Mkoa wa Singida.
Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida Henry Kapella akisoma taarifa ya michezo ya Umisseta wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ngazi ya Mkoa.

WATATU WALIOSHITAKIWA KWA KESI YA MADAWA YA KULEVYA WAACHIWA HURU


Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia kesi washtakiwa watatu waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya milioni 25 na kuamuru wasikamatwe.

Amesema washtakiwa hao wasikamatwe na kushtakiwa kwa kufunguliwa shtaka linalofanana na hilo labda kwa maelekezo ya Mahakama Kuu.

Hatua hiyo ua kufuta kesi hiyo imekuja baada ya washtakiwa kuwa rumande kwa zaidi ya miaka mitatu bila ya upelelezi kukamilika na jalada ya polisi kutokuwepo mahakamani mara kadhaa. Washtakiwa walioachiwa huru ni, Salma Juma , Amos Sosoma na Rashid Mtitu.

Kesi hiyo iliyokuwa na namba 21 ya mwaka jana imefutwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage baada ya kukaa mahakamani hapo kwa miaka mine bila ya upelelezi kukamilika.

Amesema Machi 6, mwaka huu, mahakama iliamuru upande wa mashtaka ifikapo Machi 23, itoe taarifa juu ya hatua ya upelelezi lakini ilipofika siku hiyo upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika na jalada la polisi halipo.

Akiendelea kusoma uamuzi huo Hakimu Mwijage alisema kesi iiahirishwa hadi Aprili 5, mwaka huu lakini upande wa mashtaka ulibaki na jibu lile lile kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba wapangiwe tarehe nyingine.

Hata hivyo baada ya kauli hizo kuebndelea kutawala mahakamani hapo mara kadhaa, washtakiwa walilalamika kuwa walifikishwa mahakamani Agosti 26, 2013.Walidai kuwa, kesi yao ilipita katika mahakama mbalimbali mbapo Juni 14, 2016 waliachiwa huru lakini walikamatwa tena na kupandishwa mahakamani hapo na kuendelea kusota rumande.

Katika kesi hiyo ambayo waliachiwa huru kabla ya kukamatwa tena walikuwa wakidaiwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilo 920, zenye thamani ya milioni 138.

Katika uamuzi wake, Hakimu Mwijage amesema upande wa mashtaka Juni 14, 2016 uliwafungulia kesi nyingine mbele yake wakidaiwa kukutwa na gramu 169,500 za dawa za kulevya aina ya Bangi zenye thamani ya Sh 25, 425,000.

Hakimu Mwijage alisema tangu Juni 14, mwaka jana hadi Aprili 5,mwaka huu, upelelezi haujakamilika na wala Upande wa mashtaka hawana jalada la [polisi.

“Tunawezaje kupiga vita dawa za kulevya kama upelelezi hauwezi kukamilika kwa zaidi ya miaka mitatu, magerezani kuna mrundikano wa mahabusu na kuna kesi za Meno ya Tembo na dawa za kulevya ambazo upelelezi wake unacheleweshwa bila ya kuwepo sababu za msingi.”Amesema Mwijage.

Ameongeza mahakama ipo kwa ajili ya kutenda lakini wanachokifanya upande wa mashtaka siyo kuendesha kesi bali ni kuwanyanyasa washtakiwa.“Kwa maoni yangu kesi ya jinai siyo ya kuchezea, shauri hili lilipaswa kusikilizwa Mahakama Kuu kutokana na hoja na malalamiko ya washtakiwa, mahakama hii inayo mamlaka ya kuchukua hatua na kutoa maamuzi.” Amesema Hakimu Mwijage.

Alibainisha kuwa anafahamu kwa mujibu wa sheria hakuna muda wa upelelezi wa kesi kama ya aina hiyo, ila amezingatia mazingira ya kesi , malalamiko ya washtakiwa, na taarifa upelelezi haujakamilika kwa siku 1335.

Amesema kitendo cha kucheleweshwa kukamilika kwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo imeonesha hakuna ushahidi dhidi ya washtakiwa kwa nia ya kutenda haki na kuepuka kwenda kinyume na sheria mahakama imeifuta kesi hiyo na kuamuru washtakiwa hao wasikamatwe na kushtakiwa kwa kufunguliwa shtaka linalofanana na hilo labda kwa maelekezo ya Mahakama Kuu.

BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA VUAI ALI VUAI.

NA IS-HAKA OMAR,  ZANZIBAR.

MAMIA ya Wananchi wameudhuria mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar.Vuai Ali Vuai, Marehemu Bi.Mwanaisha Hassan Vuai huko Kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.

Mazishi hayo yameongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, aliyeambatana na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  pamoja na  jamhuri ya muungano Tanzania.

Bi. Mwanaisha amefariki jana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tasakhtaa  iliyopo  Vuga  Mjini  Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya mazishi hayo, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai alisema kifo cha Mama yake mzazi kimeacha pengo kubwa katika  familia hiyo  kwani marehemu huyo alikuwa akitegemewa na jamii kutokana na busara zake.

Aidha  Vuai amewashukru wananchi mbali mbali waliojitokeza kumuunga mkono katika mazishi hayo na kuwasihi waendelee kuwa na umoja wa kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kijamii.

“  Mama yetu tulimpenda sana lakini ndio hivcyo amefariki sasa kilichobaki kwetu sisi tuliobaki ni kumuombea dua yeye pamoja na wazee wetu wengine waliofariki kabla yake.”, alisema  Naibu Katibu Mkuu huyo. 

Mbali na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Idd pia  Mazishi hayo yameudhuriwa na Viongozi  mbali mbali  wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM   Abdulrahman Omar Kinana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar   Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi”,Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Shaka Hamdu Shaka,  Mkuu wa Mkoa kusini Unguja    Dk.Idrissa  Muslim Hija, Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari  Jabu.

Viongozi wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Idrissa  Kitwana  Mustafa, Mnadhimu wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  wa CCM, Ali Salum Haji pamoja na baadhi ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri  na Makatibu wakuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Bi.Mwanaisha Hassan Vuai amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 ameacha watoto tisa (9) pamoja na wajukuu kadhaa.

Mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema peponi-Amin.
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif  Ali Idd akipokelewa na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali mara baada ya kuwasili katika mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai, huko kijijini kwao Bwejuu.
 Viongozi  mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea Dua  Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
 Viongozi  mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea wakiwa msikitini kabla ya kuanza kuiswalia Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan.
 Baadhi ya Viongozi na wananchi kwa upande wa wanawake wakiomba dua katika mazishi ya Marehemu Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
 Matukio tofauti ya kubebwa kwa maiti inapotolewa msikiti hadi sehemu ya kaburi ilipofanyiwa mazishi.
Viongozi mbali mbali wa Chama na serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Nd. Abdulrahman Omar Kinana wakimfariji Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM  Zanzibar  katika mazishi ya Mama yake mzazi yaliyofanyika huko kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.( PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR).

BODI YA KWANZA YA CHUO CHA TAALUMA YA UREKEBISHAJI TANZANIA YAZINDULIWA

 Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba ya ufunguzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017.
 Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza – SACP. Gideon Nkana akitoa historia fupi ya Chuo.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Dkt. James Jesse akitoa neno la shukrani baada ya hotuba ya Mgeni rasmi.
 Wajumbe wa Sekretarieti ya Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania wakitekeleza majukumu yao katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kulia) akiteta jambo na baadhi ya Wajumbe wa Bodi kabla ya uzinduzi rasmi uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017.
 Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania wakiongozwa na mwenyeji wao Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, SACP. Gideon Nkana(wa kwanza kulia) kutembelea mazingira ya chuo hicho.
 Muonekano wa mbele wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania.
 Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania. Walioketi kutoka kulia ni SACP. Gideon Nkana, Godfrey Semango na Dkt. Zena Mabeho. Kutoka kushoto ni DCP. Ally Lugendo, Bi. Catherine Jorome na Dkt. James Jesse. Waliosimama(kushoto) ni SACP. Dkt. Kato Rugainunura(katikati) ACP. Charles Novart na wa kwanza kulia ni SACP. Uwesu Ngarama(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza)

MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA.


Na Tiganya Vincent, RS- Tabora

31 Mei, 2017

Jumla ya shilingi milioni 180 zimekusanywa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora katika kipindi cha Mwezi huo kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na waindeshaji wa vyombo vya moto.

Takwimu hizo zilitolewa jana mjini Tabora na Kamanda wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali wanazozifanya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani humo.

Alisema makusanyo hayo yametokana tozo kwa madreva wa magari, pikipiki na bajaji na waendesha baiskeli walivunjia Sheria za Usalama barabarani katika kipindi hicho.

Kamanda alitaja baadhi ya makosa ni madereva wa Bodaboda kutovaa kofia ngumu wao na abiria wao , madereva wa magari kuendesha bila kuwa na leseni, mwendokasi, kutozingatia alama za barabara na kupakia abiria zaidi ya uwezo wa chombo cha usafiri.

Kamanda Mtafungwa alitoa wito kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto Mkoani Tabora kuepuka kuvunja Sheria za Usalama Barabarani ili waokoe fedha wanazozipata zitumike kusaidia familia zao katika  matumizi mengine ya maendeleo badala kulipa faini.

“Naomba waendeshaji wa vyombo vya moto kuzingatia Sheria za Usalama barabarani ili wasipigwe faini ambazo zinawafanya watoe fedha ambazo zingewesaidia wao na familia katika shughuli mbalimbali” alisema Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora.

Aidha , alitoa wito kwa vijana wote wanaoendesha Bodaboda na baiskeli maarufu kama daladala kujisajili katika vituo(vijiwe) na kukaa katika maeneo yao waliopagwa na viongozi wao ili kuwasaidie kuwafichua baadhi ya Wahalifu kujificha katika usafiri huo.

Kamanda Mtafungwa alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwabaini baadhi ya wahalifu ambao wanapenda kujificha katika kazi hiyo kwa kutokubali kukaa eneo moja kwa hofu ya kubainika uovu wao.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu sita wakiwemo madereva wa bodaboda wawili kwa tuhuma za kuvunja nyumba usiku na kuiba na wengine kununua mali inayodhaniwa ni ya wizi.

Kamanda Mtafungwa alisema kati ya watuhumiwa hao wanne walikiri kuhusika na uvunjaji nyumba na kuiba mali na wengine wawili walikutwa na mali zinazodhaniwa kuwa za wizi.

Aliwataja waliokamatwa kwa tuhuma za kuvunja nyumba ni Issa Maganga(27), Salum Maganga(19), Hamis Malale(24) na Amri Salum (20) wote wakazi wa Ipuli katika Manispaa ya Tabora .Kamanda Mtafungwa aliongeza kuwa walikutwa na mali zinazodhaniwa kuwa za wizi ni kuwa nia Maganga Salum(28) na Hussein Salum (28) wote wakazi wa Kiloleni Manispa ya Tabora.

Alivitaja vitu vilivyokamatwa ni pamoja na tairi za baiskeli 21, mzani mmoja na mawe yake, mikasi saba ya baiskeli , minyororo nane ya baiskeli, televisheni mbili inchi 32 , solar inchi 24 na kandambili jozi saba.

Vingine ni sigara pakiti 20 , Betri za radio jozi 18 , dawa za meno aina ya Whitedent na mafuta ya kujipaka.Alisema kuwa watuhumiwa hao walishindwa kudhibitisha uhalali wa mali hizo na hivyo nao wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakajibu makosa yanayowakabili.

Kamanda huyo alitoa wito kwa vijana mkoani Tabora kuacha kujiingiza katika vitendo vitakavyosababisha kukamatwa na hatimaye kupelekwa Mahakamani na kuongeza kuwa ni vema wakashiriki katika shughuli mbalimbali kama vile kilimo cha bustani ili kujipatia kipato halali badala ya kufikia kuvunja nyumba na maduka ya watu wengine.

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 38, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 31, 2017

 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akisoma dua ya kuliombea Bunge katika  kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dk.Medard Kalemani akiwasilisha Randama za Makadirio na Matumizi ya Wizara yake  kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe.George Masaju akifuatilia jambo kutoka kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk.Suzan Kolimba  katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akimskiliza Mbunge wa Mtama(CCM) Mhe.Nape Nnauye katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.Dk Charles Tizeba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
  Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Ritta Kabati akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki(CHADEMA) Mhe.Joshua Nassari akifurahi jambo na Mbunge wa Momba(CHADEMA) Mhe.David Silinde katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe.Catherine Ruge akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017. 
Mbunge wa Iramba Mashariki(CCM) Mhe.Allan Kiula akiuliza swali katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017. 

Picha zote na Daudi Manongi, MAELEZO, DODOMA.

Free Bitdefender Tool to Pinpoint Weaknesses in Your Smart Home Compromised smart device could lead thieves to your Banking information, private photos and e-mails

Bitdefender Antivirus, the innovative security solutions provider, has released a free tool that will scan your entire Office/home network to pinpoint weaknesses that could let thieves take your private info and photos and allow hackers and snoops to take control of your Internet-connected devices.

Once installed on your PC, Bitdefender Home Scanner scans your Office/home Wi-Fi network to identify the devices you have connected to your local network. Then it identifies risks on any connected device, like weak usernames and passwords, unsafe communication and different vulnerabilities in the device’s firmware and delivers a thorough report. This includes tips on how to address and secure the network, based on the vulnerability identified. Click below link to get free Bitdefender Office/home scanner tool:     

Bitdefender Office/Home Scanner’s effectiveness is enhanced by Bitdefender’s experience engineering the Bitdefender BOX, the first-of-its-kind piece of hardware that protects everything connected to your network.

A successful hack into even the least significant of your devices could lead to a network takeover that could give thieves your banking information, private photos and e-mails, allow them to control your Office/home security setup, let them eavesdrop via your smart TV and other audio-equipped devices, and know when you are at home or away on holiday.
       
. “Bitdefender’s mission is to bring your entire home/Medium Office network defense strategy up to the highest levels of security in the industry. Bitdefender Office Home Scanner is the first, and most essential, step in a modern security plan: know your weaknesses.”
                                                                                 
BITDEFENDER BOX DEVICEFor other Bitdefender Antivirus Products contact Computer/IT reseller shops
For Business Consumers

Bitdefender Antivirus Plus 2017   (2 or 4 users)
Bitdefender Internet Security 2017    (2 or 4 users)
Bitdefender Total Security Multi-Device 2017

For Corporate Consumers (available for any number of users)

Bitdefender GravityZone Business Security
Bitdefender GravityZone Advanced Business Security

INTERCOM SYSTEM (T) LTD
Bitdefender Cyber Security Country Partner
Morogoro Road, Old Kisutu Bus Stand
P.O.Box 8898, Dar Es Salaam, Tanzania
Telephone +255 22 2121140
Mobile +255 673 221 933

OLE NASHA AHIMIZA MATUMIZI YA MBEGU BORA KWA WAKULIMA

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha (kushoto) akitambulishwa wafanyakazi wa kampuni ya Monsanto Tanzania baada ya ofisi yao kufunguliwa hapa nchini eneo la Njiro mkoani Arusha, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Monsanto Afrika, Dk Shukla Gyanendra. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha (kushoto) akikagua ghala la mbegu bora zenye uwezo wa kumpa mkulima mazao bora.Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha akizungumza jambo baada ya kukagua ghala la mbegu bora za kampuni ya Monsanto zenye uwezo wa kumpa mkulima mazao boraMeneja Kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsato Tanzania, Frank Wenga akieleza mipango kamambe ya kuwafikishia mbegu bora wakulima kote nchini.
Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ofisi ya Monsanto Tanzania.Meneja Kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsato Tanzania, Frank Wenga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari . Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Monsato na mawakala wa mbegu nchini waliohudhuria uzinduzi wa kampuni wa ofisi ya kampuni hiyo jijini Arusha.

KAMPUNI YA ALLIANCE ONE YAANDAA UTARATIBU WA KUPANDA MITI KWA KILA MSIMU WA KILIMO WILAYANI KASULU.

TUMBAKU ni zao ambalo husababisha uharibifu wa Misitu katika uzalishaji wa tumbaku ya Mvuke, kwa kukabiliana na Changamoto hiyo Kampuni ya kuuza na Kununua tumbaku ya Alliance one Wilayani Kasulu imeandaa utaratibu wa kupanda Miti kwa kuwashirikisha Wakulima kutoa Ardhi yao na halmashauri kwa kupanda hekta 288 kwa kila msimu wa kilimo lengo ikiwa ni kuhakikisha kuni zinazotumika katika uchomaji wa tumbaku zinatoka katika chanzo endelevu cha miti wanayoipanda. 

Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya Mashamba ya Miti hekta 144 jana yalitooteshwa kwa kipindi cha mwaka 2014 - 2015 katika Kijiji cha Mganza na Chogo kata ya Heru juu baina ya halmashauri na kampuni hiyo Meneja uzalishaji jani katika Kampuni hiyo, David Mayunga, alisema kampuni hiyo inajihusisha na uendelezaji wa nishati mbadara ya kuchomea tumbaku, kuborsha mabani ya kuchomea iliyaweze kutumia kuni chache.

Mayunga alisema uzalishaji wa tumbaku ya Mvuke unategemea kiasi kikubwa cha kuni hapa Tanzania na Nchi nyingine pia na husababisha uteketezaji wa misitu, kampuni hiyo wamedhamilia kuwa ifikapo mwaka 2020 uzalishaji wa tumbaku utatumia kuni kutoka katika vyanzo endelevu ambapo Wakulima na serikali watatoa maeneo yao waweze kupandiwa miti lengo ikiwa ni kuinua uzalishaji wa tumbaku pamoja na Wakulima.

Alisema tumbaku ni zao la pili kwa Tanzania linalo ingiza fedha za kigeni, kampuni hiyo inafanya zoezi hilo katika maeneo ambayo yanalima tumbaku ilikuweza kiwasaidia Wakulima kutunza mazingira na kufanya biashara ya tumbaku bila kiathiri mazingira, kwa kipindi kilicho pita zao la tumbaku limeshuka sana kutokana na Wakulima wengi kushindwa kulima kutokana na gharama ya zao hilo.

"Pamoja na malengo tuliyonayo ya kuinua zoezi la upandaji miti tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Ardhi hili linatokana na baadhi ya Wananchi kuzuia mashamba yao yasipandwe miti kwa kuhofia kwamba watazulumiwa, kukosekana kwa ushirikiano baina ya Viongonzi na kampuni hili linasababisha kampuni kushindwa kupanda miti kwa malengo yaliyo pangwa", alisema Mayunga.

Alisema zoezi hilo kwa misimu ilyopita walifanikiwa kwa asilimia 85% na siku ya jana walikabidhi kiasi cha hekta 68.7 kwa kijiji cha Chogo na hekta 76.4 zitakabidhiwa Kwa wananchi walioyoa mashamba yao katika kijiji cha Mganza, hata hivyo aliwaomba Wananchi kuendelea kujitolea mashamba yao waweze kupandiwa miti hiyo kwakuwa faida ya miti hiyo wataipata wao na sio kampuni na gharama zote za upandaji na usimamizi zitafanywa na Kampuni.

Kwa upande wake Katibu tawala wa Wilaya ya Kasulu Titus Mguha aliishukuru kwampuni hiyo kwaniaba ya serikali kwa hatua ya kuanza kupanda miti katika Vijiji hivyo hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira na kurudisha misitu kwa maeneo ambayo yalikuwa yameharibiwa na Wakulima na wafugaji na kwasasa watatumia misitu yao binafsi.

Alisema Wananchi wanatakiwa kutoa ardhi kwa Kampuni hiyo kwakua kampuni hiyo inalengo zuri la kuhakikisha Wakulima Watumbaku hawaangaiki kutumia misitu ya asili na badala yake watatumia miyi ambayo wanaipanda katika Misitu hao na kuweza kufanya kilimo cha tumbaku bila kuathiri misitu ya asili.

Nae Mwenyekiti Wa halmashauri ya Mji wa Kasulu , Twallib Mangu alisema Wao kama halmashauri watajitahidi kuingiza suala hilo la upandaji miti katika vikao vyao na Madiwani waweze kuwahamasisha Wananchi wao kitoa ardhi zao kwaajili ya kupandiwa miti ilikuhakikisha na wao wananufaika na mradi huo na kuweza kupata mafanikio ya uhifadhi wa misitu.

Aidha aliiiomba kampuni hiyo kuandaa mikataba itakayo waonyesha ni jinsi  gani Mwananchi atanufaika na mradi huo na kampuni itanufaika na nini ilikuwaondoa Wananchi wasiwasi wa kuhofia kuibiwa , na aliwaomba Wananchi kuwatumia Wanansheria wa Halmashauri kabla ya kusainishwa mikataba hiyo na kuweza kujitokeza kwa wingi waweze kupandiwa miti hiyo.

Baadhi ya Wananchi Lisa Ramadhani na Hatibu Juma waliipongeza sana kampuni hiyo na kuishukuru kwa kuwapandia moti na kwamba miti huiyo itawasaidia kupata kuni na kupata mbao za kujengea na manufaa mengi hivyo wakotayari kujitolea mashamba yao iliwaweze kupandiwa miti hiyo.

Wenceraus Mbuyeko alisema yeye kwa upande wake atatoa hekari 16 waweze kumpandia miti katika shamba lake kwakuwa faida anaziona na baadhi ya Wananchi waliopandiwa miti wanaendelea kunufaika na miti hiyo, kampuni hiyo inamipango mizuri ya kuweza kuinua kilimo cha wakulima wa tumbaku.
 Meneja wa uzalishaji jani wa kampuni ya Alliance one David Mayunga  akisain hati ya makabidhiano ya mashamba ya  miti kwa Halmashauri ya Wilaya ya kasulu.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kasulu Twallib Mangu, akisaini baadhi ya mikataba ya makabidhiano baina ya kampuni ya Alliance one na halmashauri.

RC Rukwa atoa tahadhari ya Ebola kwa wananchi wa Kirando

Katika kuhakikisha Mkoa wa Rukwa Upo salama kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yatakayoweza kujitokeza, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amefanya ziara ya siku tatu katika mwambao wa ziwa Tanyangika kwenye Kata ya Kirando, Kabwe na Kasanga vijiji ambavyo vipo jirani na nchi  ya DRC ili kujionea namna Halmashauri ya Nkasi na Kalambo zilivyojipanga kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hautii mguu katika Mkoa na nchi kwa ujumla.

Ziara hiyo aliianza siku ya Ijumaa tarehe 26 hadi 28. 05. 2017 mara baada ya kumaliza kumalizika kwa mafunzo ya siku tatu yaliyohusu utumaji wa taarifa za magonjwa kwa kieletroniki (e-idsr) yenye kusisitiza tahadhari ya ugonjwa wa ebola uliopo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yaliyotolewa kwa wahudumu wa afya wa Serikali na Sekta binafsi kwa Halmashauri mbili za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga vijijini.

Mafunzo ya awamu ya pili yanatarajiwa kumalizika tarehe 31. 05. 2017 kwa Halmashauri za Kalambo na Nkasi ikiwa ni muendelezo wa awamu ya kwanza kwa Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini na Manispaa ya Sumbawanga yaliyoisha tarehe 26. Mwezi wa tano.

Ili kujiridhisha na maandalizi ya Halmashauri zinazopakana na nchi za jirani yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na Zambia Mkuu wa Mkoa alipita katika bandari maarufu za pwani ya ziwa Tanganyika na kuongea na vyombo vya usalama ikiwemo uhamiaji, Sumatra, TRA, jeshi la polisi, jeshi la wananchi, maafisa forodha pamoja na maafisa afya kutoka Wilayani.

Pia Mh. Zelote aliongea na viongozi wa serikali za vijiji na kata wakiwemo madiwani, watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji, maafisa ugani wa kata na vijiji, maafisa afya wa kata na vijiji na kufanya mikutano ya hadhara ili kuwapa wananchi ujumbe aliokwenda nao katika kuhakikisha ugonjwa huo haunusi katika mkoa wa Rukwa na nchi ya Tanzania.
Pamoja nae Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu, Mratibu wa Chanjo Mkoa Gwakisa Pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Afya wa usimamizi na ufuatiliaji Solomon Mushi, Mkuu wa Wilaya, makatibu tawala wa wilaya pamoja na kamati za ulinzi na usalama za Wilaya.

Katika kila Wilaya aliyopita Mh. Zelote alihakikisha anapewa taarifa za maandalizi ya Wilaya na kisha kwenda kwenye mipaka ili kujionea kwa macho yake maandalizi hayo na pia kuongea na wananchi wanoishi karibu na mipaka hiyo.

Wakati akiwa kwenye ziara hiyo Mh. Zelote alikuwa akisisitiza utayari pamoja na kujihadhari kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata na pia kwa vyombo vya usalama vya maeneo hayo ya mipakani.

Katika suala la utayari Mh. Zelote Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya athari ya ugonjwa huo na namna ya kujikinga nao ikiwa ni pamoja na kuelezwa dalili za ugonjwa na njia za maambukizi ya ugonjwa huo na kuwasisitiza wananchi kwenda zahanati pindi wanapojiskia kuumwa na sio kukimbilia kwenye maduka ya dawa na kuagiza vidonge bila ya kujua ugonjwa anaoutibu.

Pia katika kusisitiza hilo Mh. Zelote aliwasihi wananchi kutokimbilia kwa waganga wa kienyeji pindi wanapoumwa na badala yake wakimbilie kwa wataalamu wa afya kwenye zahanati ama vituo vya afya. Na kuwaonya kuwa kupitia hizi taarifa za ugonjwa wa ebola kunaweza kukajitokeza matapeli ambao watajitangaza kuutibu ugonjwa huo jambo ambalo si kweli, hivyo aliweka msisitizo kuwa ugonjwa wa Ebola hauna Tiba.

“Mtu yeyote atakayejiskia vibaya basi haraka akimbilie kwenye zahanati ama kituo cha afya na sio kwa mganga wa kienyeji, na mjiepushe mbali  sana na matapeli wanaotibu watu vichochoroni ama wanaosema dawa ya Ebola ipo,…. Hakuna,” Mh. Zelote alieleza.

Pamoja na hayo Mh. Zelote alionya kuwa katika kusimamia jambo hilo hatakuwa na utani, dhihaka ama masihara kwayeyote atakaekiuka taratibu zilizowekwa ili kujihadhari na ugonjwa huo kuingia katika mkoa wa Rukwa.

“Mimi nafahamu kwamba watu wanaoishi humu kwenye mipaka wameoa ama kuolewa katika nchi za jirani, na kwamba watanzania utamaduni wetu ni ukarimu kwa wageni lakini katika hili tupunguze ukarimu mpaka jambo hili liishe, na yeyote atakayegundulika anamhifadhi mgeni kinyume na taratibu, huyo ni mhalifu,” Mkuu w Mkoa alisema.

Katika kuonesha athari kubwa inayoweza kupatikana endapo uginjwa huo utapenya katika nchi yetu Mh. Zelote alieleza kuwa gharama za kumshughulikia mgonjwa mmoja ni kubwa sana na kuongeza kuwa endapo ugonjwa huo unathibitishwa kwenye nchi Fulani basi tatizo hilo si la nchi hiyo tu ni la dunia nzima.

“Nguo inayotumika kumshughulikia mtu mmoja inauzwa milioni 10 na kwa wenzetu huko afrika ya magharibi Ivory Coast ambako walikumbana nao watu 11,000 walifariki, wakiwemo madaktari ambao walikuwa wakiwauguza wagonjwa, mtu mmoja tu akiupata basi kijiji kizima kinafungwa hakuna mtu kuingia katika kijiji hicho wala kutoka,” Mh. Zelote alisisitiza.

Lakini pia aliwatoa hofu wananchi na kuwaambia kuwa mpaka sasa Tanzania hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola.

Nae Daktari wa Mkoa Dkt. Kasululu alisema kuwa tangu ugonjwa huo kutolewa taarifa na Wizara ya Afya tarehe 12. 05. 2017 watu watatu wlikuwa wamefariki na wengine 12 walikuwa wako chini ya uangalizi lakini hadi kufuikia tarehe 25. 05. 2017 idadi ya wagonjwa iliongezeka hadi kufikia wagonjwa 45 na kuongeza kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kadiri siku zinavyokwenda mbele.

“Idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeak kila kukicha hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunajiandaa na kujihadhari kweli, maana wagonjwa hawa wapo kwenye misitu ambapo usafiri wa kawaida haufiki isipokuwa Helkopta na pikipiki, hivyo wagonjwa wanaweza kuwa wengi na bado hawajajulikana,” Dkt Kasululu alisisiza.

Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Dk. Makundi Maige alielezea mikakakti ya Halmashauri ya Nkasi namna ilivyojipaga kuhakikisha wanakaa mbali na ugonjwa hatari wa Ebola.

“ Wilaya imeainisha kata tatu za Kirando, Kabwe na Wampembe ambazo zimetengwa kwaajili ya kupokea wageni kutoka nchi za jirani, tukifahamu kuwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyia kuna Kata 10 ambazo ugonjwa huu unaweza kuingia kwa urahisi, ambazo ni Kabwe, Kirando, Wampembe, Itete, Kipili, Mkinga, Korongwe, Ninde, Kizumbi na Kala,” Dk. Makundi aliainisha.

Katika kubainisha upokezi wa wageni hao Dk. Makundi alisema kuwa kituo cha Wampembe kitapokea wageni wanoelekea kijiji cha Kilambo hadi Msamba, Kituo cha Kirando kitapokea wageni wanaoelekea kijiji cha Ninde hadi Kazovu na kituo cha Kabwe kitapokea wageni wanaoelekea kijiji cha Utinta hadi Kalila.

Na kuongeza kuwa wageni wote kutoka nchi za jirani watalazimika kupitia katika vituo hivyo na sio kuingia kiholela kama ilivyozoeleka na kabla ya kuendelea na safari zao watakuwa wakichunguzwa afya zao.

Kwa kuzingatia namna ugonjwa huo unavyoenea Wilaya imetenga eneo maalum kwaajili ya matibabu ili kuepuka kuchanganya wagonjwa watakaobainika kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.

Pamoja na hayo Wilaya imejipaga kuzizungukia kata zote 10 na kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa dini, wazee maarufu, vijana, waalimu na wanafunzi juu ya ugonjwa huo hatari.

Nao upande wa Wilaya ya Kalambo  walieleza mipango yao juu ya udhubiti wa ugonjwa huu, ambapo mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Alcado mwamba aliweza uainisha tahadhari mbalimbali ambazo Wilaya imezichukua kuhakikisha wanaudhibiti ugonjwa huo kutokuingia katika Wilaya hiyo.

Miongoni mwa tahadhari walizochukua ikiwa ni kuwasambazia wananchi vipeperushi vyenye kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola lakini pia kuihamasisha jamii kutoa taarifa haraka kwa uongozi wa serikali pindi tu wakibaini kuna mgeni aliyeingia kinyume na taratibu zilizowekwa.