Tuesday, August 22, 2017

DK.KIKWETE SIJAANZA KILIMO/UFUGAJI BAADA YA KUSTAAFU WATAKAOSUBIRI KUANZA UZEENI WAMECHELEWA

 Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete,akionyesha Kilimo cha mahindi ya njano kwa ajili ya kuongeza rutuba kwa ng'ombe .


 Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete,akionyesha eneo analohifadhi majani ya malisho ng'ombe .Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete,akionyesha baadhi ya mifugo yake na kueleza umuhimu wa Ufugaji wa kisasa ili kupata maziwa ya kutosha na ng'ombe kuwa na afya.(Picha na Mwamvua Mwinyi )

Na Mwamvua Mwinyi,Msoga

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete ,amesema ameanza kufanya kilimo na ufugaji tangu mwaka 1988/1989 hivyo anaetegemea kufanya shughuli hizo baada ya ustaafu amechelea .

Aidha ameeleza matarajio yake kwa sasa ni kuongeza mifugo ya ng'ombe majike wa maziwa 500 watakaoweza kutoa maziwa lita 2,000 hadi 4,000 kwa siku .

Katika hatua nyingine dk.Kikwete amesema endapo wafugaji watazingati ufugaji wa kisasa kwa kuwa na maji ya kutosha ,malisho ,kinga ya chanjo na kuogeshwa ni lazima watanufaika kwa kupata soko la uhakika hasa maziwa 

Akizungumza baada ya kutembelewa na baadhi ya waandishi wa habari mkoani Pwani ,shambani kwake Msoga ,Kikwete alisema anaetarajia kufuga na kulima akifika miaka 67 atapata changamoto kwani sio kazi rahisi .

"Ukishazeeka ndio uanze kufuga ama kulima ,ahaahha haahah (alicheka) itakuwa ngumu sana ,kwani pia hata miaka ya kuishi hatujui " alisema dk.Kikwete .

Alifafanua ,endapo atafikia malengo aliyojiwekea ataweza kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza siagi .

Alisema kwasasa anang'ombe zaidi ya 400 mchanganyiko ambapo 46 ndio wanakamuliwa maziwa na kutoa lita 400 kwa siku na hununuliwa yote .

Alieleza maziwa yana soko kama utamtunza ng'ombe hivyo kutokana na ufugaji anaoufanya anauhakika atafikia adhma yake .

Alielezea kuwa,kwa kufuata ufugaji wa kitaalamu amelima hekari 30 za mahindi ya njano kati ya hekari 800 alizonazo ambayo husaidia virutubisho kwa ng'ombe ambapo wameshavuna hekari nne na wanaendelea kuvuna .

Dk.Kikwete alisema ,anatarajia pia kulima majani ya malisho zaidi hekari 200 zaidi ili zitosheleze mahitaji.

"Nilianza kufuga ng'ombe 20 kule Bagamoyo wakati nikiwa waziri baadae nikawahamishia Msoga na wameendelea kuongezeka " alisema dk.Kikwete .

Alibainisha ,miaka miwili iliyopita wafugaji hususan wa Msoga walipata hasara ya mifugo yao kufa kwa wingi kutokana na ukame .

Dk.Kikwete ,alisema yeye alibahatika ,hakuna hata mfugo wake uliokufa kutokana na akiba aliyojiwekea ya malisho na maji .

Kuhusu kilimo cha mananasi alisema alianza mwaka 1989 .

"Mananasi huvunwa baada ya  miezi 18 tangu kupandwa "
Dk.Kikwete alisema ,shamba lake lina ukubwa wa hekari 200 ambapo hekar 64 ndizo zimelimwa .
Alisema wakulima wa mananasi wana changamoto ya maji ya umwagiliaji ,wakipata maji wataweza kuvuna wakati wowote .
Mstaafu huyo alisema ,wanahitaji dola mil.15 katika mradi wa maji ya umwagiliaji kwani maji yapo mbali WAMI.
Alisema ametumia umaarufu wake na kuweka mitego yote lakini bado hajafanikiwa ila ipo siku watafanikiwa kupata mradi huo .
Baadhi ya wakazi waliopata kibarua cha kuvuna mahindi ya njano kwenye shamba la dk.Kikwete wamemshukuru kwa kuwapatia ajira .
Walisema ,wameweza kujiendesha na maisha yao ya nyumbani ikiwemo watafutia watoto wao mahitaji ya kielimu .

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELA MIRADI YA UMEME WA GESI YA KINYEREZI II NA ULE WA UPANUZI KINYEREZI I

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (Mb), wapili kulia, akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, kutembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2018. Kamati hiyo pia ilitembelea kituo cha kupkea gesi asili kilicho jirani na Miradi hiyo.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAMATI ya Bunge ya Bajeti, imetembelea miradi ya kuzalisha umeme wa gesi ya Kinyerezi II, na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I unaoendeshwa na Serikali kupitia Shrika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, pia ilitembelea kituo cha kupokea gesi asili inayotumika kuzalisha umeme kilichoko jirani na miradi hiyo.
Katika ziara hiyo, mwenyeji wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, (Mb), Mhe.Dkt.Medard Kalemani, aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa miradi hiyo inaendelea kama ambavyo Serikali ilitarajia na kwamba Watanzania wategemee ongezeko kubwa la upatikanaji wa umeme pindi miradi hiyo itakapokamilika. “Mhe. Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Kamati, miradi hii kunzia ule wa Kinyerezi I unaopanuliwa ambapo kutakuwa na ongezeko la umeme Megawati 35 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 185 zitakazozalishwa kutoka Kinyerezi I, na huu wa Kinyerezi II utakapokamilika Agosti mwakani (2018) utatupatia Megawati 240 na ukijumlisha na miradi mingine itakayofuatia ya Kinyerezi III na VI, tutakuwa na jumla ya Megawati 1175.” Alifafanua Mhe. Dkt. Kalemani.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephene Manda aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa mradi huo utakuwa na jumla ya mashine 8 ambazo zitafua umeme na tayari ufungaji wa mashine hizo umeanza na unaendelea na kuongeza kuwa kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, TANESCO itaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na kufanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kadri kazi ya ufungaji wa mashine hizo utakavyokuwa unakamilika.
Alisema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

Wajumbe wa Kamati hiyo pian walipata fursa yua kujionea kazi ya utandazaji wa mabomba makubwa ya kupitisha gesi kutoka kituo cha kupkea gesi kuelekea kwenye eneo la miradi hiyo.“Niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na haya ndio matarajio ya wabunge kuona kuwa miradi hii ambayo inagharimu fedha nyingi za walipa kodi inakamilika kwa wakati ili hatimaye serikali iweze kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kama ilivyoahidi wananchi.”Alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia. Baada ya kumaliza ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi hiyo ya umeme wa gesi asilia.


 Dkt. Kalemani (katikati mbele), akiwaongoza wajumbe hao baada ya kutembelea eneo la mradi wa upanuzi Kinyerezi I
 Hili ndio eneo la upanuzi wa mradi wa umeme Kinyerezi II
 Mtandao wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia kutoka kituo cha kupokea gesi hiyo kuelekea eneo la miradi hiyo.
 Mafundi wa TPDC wakiwa wamesimama kwenye eneo la utandazaji wa mabomba hayo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia, (wapili kushoto), akizungumza jambo wakati akiongozana na Naibu Waziri Dkt. Kalemani (kushoto) na wajumbe wa kamati.
 Mhe. Hawa Ghasia akiwa tayari kuanza ziara.
 Dkt. Kalemani akiongea wakati wa ziara hiyo.
Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, wakati wajumbe wa Kamati walipowasili eneo la Miradi.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC), Mhandisi  Kapuulya Musomba(kulia), akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania, (TANSCO), Dkt. Alex Kyaruzi, (katikati), na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Dkt. James M. Nzagi.
  Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James


 Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Generation), Mhandisi Abdallah O. Ikwasa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania, (TANSCO), Dkt. Alex Kyaruzi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (wakwanza kulia) na  Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James wakiwasili eneo la mradi.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwaonyesha kitu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo, (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Jerome Dismas Bwanausi
 Mhe. Hawa Ghasia akizungumza baada ya ziara ya kutembelea kituo cha kupokea gesi asilia kinachosimamiwa na TPDC.
 Wajumbe wa Kamati wakipita pembezoni mwa moja ya mashine kubwa (genereta), kati ya 8 zinazofungwa kwenye mradi wa Kinyerezi II
Mhandisi Manda, (waliyenyoosha mkono), ambaye ni Meneja Mradi wa Kinyerezi II, akwapatia maelezo wajumbe wa Kamati akiwemo Naibu Waziri Dkt. Kalemani.

RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA


Jumatatu Agosti 21, 2017, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (aliyesimama pichani) alifanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zimamoto karibu na soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kusikiliza kero za wananchi. 

Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa,na watumishi mbalimbali wa serikali alisikiliza kisha kujibu kero za wananchi huku pia akitoa nafasi kwa watumishi kutoka idara mbalimbali kujibu hoja na kero za wananchi. 

Miongoni mwa kero zilizoibuka eneo la mkutano huo ni pamoja na ardhi ambapo baadhi ya wananchi walieleza kutoridhishwa namna ardhi inavyotolewa na jinsi migogoro ya ardhi inavyotatuliwa. 

Kero nyingine ni ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari polisi waliodaiwa kutowajali wananchi wanaofika katika kituo cha polisi huku askari polisi wakiendelea kufanya mambo yao ikiwemo kuchat kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuhudumia wananchi wanaofika kituoni.
Mkutano unaendelea,viongozi wakiandika dondoo muhimu/maswali ya wananchi

Suala la vumbi katika barabara ambazo ujenzi wake haukamiliki mjini Shinyanga nalo likiibuka kwamba afya zao ziko hatarini kutokana na vumbi hilo. Pia wananchi wakaomba kuwekewa taa za barabarani pamoja na askari wa usalama barabarani katika eneo la Japanese Corner mjini Shinyanga ambapo panadaiwa kutokea ajali za mara kwa mara. 

Kero ya bei kubwa ya maji nayo haikusahaulika,wananchi walieleza kuwa bei ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA). Hali kadhalika wananchi wakaomba kuwekewa sehemu ya kupumzikia walau wawekewe mwamvuli katika mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule akizungumza


Wananchi pia waliomba kuongezwa kwa waganga katika kituo cha afya Kambarage ambacho kinadaiwa kuzidiwa na idadi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma. Wazee nao wakatoa kilio chao cha kutaka huduma bora ya afya wakiomba kuingizwa kwenye bima ya afya badala ya kupewa tu dawa bure. 

Akijibu hoja mbalimbali za wananchi, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack aliwataka watumishi wa umma kuzingatia maadili yao ya kazi katika kuwatumikia wananchi huku akiwasisitiza kutatua kero za wananchi kwa wakati.
Katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akijibu hoja za wananchi

Telack alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa pale inapotokea mkandarasi anayejenga barabara mjini hajamwaga maji kwenye barabara kwani wamemwagiza kuwa anamwaga maji ili kuepusha vumbi. Aidha baada kusikiliza kero za wananchi, mkuu huyo wa mkoa aliagiza kupewa taarifa ya utekelezaji wa mambo mbalimbali waliyokubaliana wakati wa mkutano huowa hadhara ifikapo Septemba 15,2017 ili kuhakikisha kero za wananchi zinapungua. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiendelea kuzungumza na wananchi.
Viongozi mbalimbali wakiwa eneo la mkutano, kushoto ni Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akifuatiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Simon Haule na mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga.
Mkazi wa Shinyanga mjini Ndyamkama Venant akieleza kero zake kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga. 
Mwananchi akieleza kero zake.
Mkazi wa Shinyanga akieleza kero yake.
Mwananchi akieleza kero yake 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akisikiliza kero za wananchi 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule akijibu kero za wananchi kuhusu jeshi la polisi 
Afisa Ardhi wa manispaa ya Shinyanga,Alex Rutailwa akijibu hoja za wananchi kuhusu migogoro ya ardhi. 
Viongozi mbalimbali wakiwa eneo la mkutano.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akijibu hoja za wananchi kuhusu maji. 
Mkutano unaendelea.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi akijibu hoja za wananchi 
Mkutano unaendelea.
Mwananchi akieleza kero zake 
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mwananchi akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Mkutano unaendelea.
Wananchi wakiwa katika mkutano huo.
Mwananchi akieleza kero yake.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog