Sunday, November 30, 2014

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Za EAC Wakamilika Nairobi

 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta (kulia) na Naibu Waiziri wa TAMISEMI (Elimu) Mh. Kassim Majaliwa wakizungumza nje ya Ukumbi wa Mkutano wa Kenyatta kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Miundombinu Nov 29, 2014,Nairobi
 Mkurugenzi wa Miundombinu na Sekta za Kijamii wa Wizara Bw. George Lauwo (kushoto) akifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu Nov 29, 2014 Nairobi, Kenya.
 Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Petro Lyatuu akifuatilia Mkutano wa Miundombinu wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya Nov 29, 2014 Nairobi,
 Mfanyakazi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Edna Chuku akifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya kuhusu Miundombinu Nov 29, 2014 Nairobi, Kenya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) akifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya.

 Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt Abdullah Juma Saadalla (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utawala Bora (katikati) Mh. George Mkuchika na Naibu Waziri wa TAMISEMI (Elimu) Bw. Kassim Majaliwa wakifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya
 Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt Abdullah Juma Saadalla (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utawala Bora (katikati) Mh. George Mkuchika na Naibu Waziri wa TAMISEMI (Elimu) Bw. Kassim Majaliwa wakifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya
 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) akifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki Bw. Amantius Msole (kulia) na Naibu Mwanasheria Mkuu Mh. George Masaju walifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya

Makamu wa Rais wa Kenya Bw. William Ruto akizungumza kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya

TANZANIA 50 PLUS CAMPAIGN WATEMBELEA WAGOJWA WA SARATANI WALIOLAZWA HOSPITAL YA OCEAN ROAD

Mgeni rasma ambaye ni DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akikata utepe kuashilia kugawa zawadi mbalimbali kwa wagojwa wa saratani waliolazwa katika hospital ya ocean road wengine kushoto ni Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki na wa tatu kulia ni Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi
DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima kulia akimkabizi zawadi mgojwa wa saratani Idd Muhode ambaye amelazwa katika hospitali ya ocean road
Baadhi ya wadau mbalimbali wa kujitolea kutoka Tanzania 50 plus campaign wakiwa katika picvha ya pamoja baada ya kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa wa saratani katika hospital ya Ocean Road.

DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akipokea zawadi za wagojwa zilizoenda kugawiwa katika hospitali ta Ocean Road kutoka kwa
Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi mwingine ni
Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa
vitu mbalimbalio vikipakiwa kwenye mfuko kwa ajili ya kugawa kwa wagojwa
vifurushi vikiwa tayali kwa kugawiwa kwa wagojwa wa saratani katika hospitali ya ocean road

Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi kulia akimkabizi zawadi mgojwa Said Kassam aliyelazwa katika hospital ya Ocean Road

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi  wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati  wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana Novemba 29, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi 
wengine walioshiriki katika mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kifurahia jambo na Makamu wa Rais wa  Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Novemba 29, 2014 aliiwakilisha Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo, kwa mujibu wa utaratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unafanyika kila baada ya miaka miwili na lengo lake kuu ni kufanya tathmini juu ya miradi ya miundombinu inayoshirikisha nchi washirika, sambamba na kutazama fursa ya kutanua miundombinu mipya katika nchi hizi kwa lengo la kukuza uchumi wa pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki.
Tathmini hii ya Miundombinu inafanyika kwa kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora katika nchi hizi ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, sambamba na kutanua mtengamano wa nchi hizi na hivyo kuwafanya wananchi wanaoishi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuzidi kuwa wamoja.
Mkutano wa jana uliongozwa na Kaimu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Waziri Mkuu wa Rwanda pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda. Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Mheshimiwa Balozi Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri wa Wizara hiyo kutoka Tanzania, Mheshimkiwa Samwel Sitta, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Donald Kaberuka, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika, Bwana Makhtar Diop, Katibu Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi na Baalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Balozi Filiberto Sebregondi. Pia mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za China, Marekani, Japan na nyinginezo ambazo ni wadau wakubwa wa ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Rais wa Kenya, William Ruto alifafanua juu ya umuhimu wa kuhakikisha Afrika Mashariki inaunganishwa kwa miundombinu imara ili kukuza uchumi na akapongeza jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kufanikisha azma hiyo huku pia akiomba nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuendelea kuungana katika kutekeleza miradi ya miundombinu na kujitahidi kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Mkutano huu pia uliambatana na kupokea ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Wakuu wa Nchi za EAC kuhusu Miundombinu kutoka kwa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya.  Wakuu wa Nchi katika Mkutano huu walipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo waliyoyatoa katika mkutano wa pili uliofanyika mwezi Novemba, 2012 na kuidhinisha miradi 72 ya miundombinu ya kipaumbele ya Barabara, Reli, Nishati na Bandari.
Kwa upande wa utekelezaji; miradi 16 imekamilika, 39 inaendelea kutekelezwa na 17 ipo katika hatua za awali za kutafutiwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake.
Kwa upande wa Tanzania miradi minne imekamilika ambayo ni Umeme katika mji wa Kibondo, mradi wa barabara ya Mbezi-Shule-Tangibovu-Makutano ya Nelson Mandela na barabara ya Tabata. Barabara nyingine iliyokamilika ni Nyangunge – Musoma – Sirari na sehemu ya Simiyu - Musoma inayounganisha Kenya na Tanzania huko ujenzi unaendelea.
Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais amezitaka nchi wanachama kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Miundombinu ili kusaidia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria. “Tusiishie kubakiza mipango hii katika karatasi, tusiishie kuzungumza tu bali huu ni wakati wa kuhakikisha tunarahisisha ufanyaji biashara katika nchi zetu na kupunguza vikwazo visivyo vya lazima,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia aliambatana na Mheshimiwa Dkt. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake tayari wamerejea nyumbani Tanzania ambapo kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, maadhimisho yanayofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Novemba 30, 2014

Saturday, November 29, 2014

MAHAFALI YA 5 YA CHUO KIKUU CHA DODOMA YAFANYIKA LEO MJINI DODOMA

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin W. Mkapa akiongoza mahafali ya tano ya Chuo Kikuu hicho yaliyofanyika leo katika eneo la Chimwaga,ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma leo.

Sehemu ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwa kwenye mahafali hayo mara baada ya kutunukiwa Shahada zao mbali mbali leo.wa pili kushoto ni Mtoto wa Ankal bi. Zahra Muhidin Michuzi.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin W. Mkapa akiwatunuku Shahada ya Uzamivu wahitimu mbali mbali katika Chuo Kikuu hicho cha Dodoma leo.
Wahitimu wa Shahada mbali mbali katika Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwa kwenye mahafali hayo.
shangwe kwa wahitimu hao.
Brass Band ya Jeshi la JKT ikiongoza Mahafali hayo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin W. Mkapa akifunga mahafali ya 5 ya Chuo Kikuu cha Dodoma leo katika