Tuesday, August 30, 2011

Notting Hill Carnival 2011

 mdau akiwa na vazi rasmi
 Msafara ukizunguka Notting hill.


Salam,

URBAN PULSE CREATIVE wakishirikiana na Miss Jestina Blog wanakuletea matukio katika picha ya Notting hill Carnival iliyofanyika Jumapili tarehe 28 agosti 2011. Hii  ilikuwa siku ya kwanza  Carnival ya watoto ambayo hufanyika kila mwaka tangu mwaka 1964 ikifuatiwa kesho yake siku ya jumatatu ikiwa siku ya watu wazima. 

 Maelfu ya watu zaidi walijitokeza katika mitaa ya Notting hill wakati wa Carnival ya jana ambayo ni tofauti na miaka yote pia nyongezo ya polisi 1000 wa ziada na kufanya Jumla ya polisi 6500 kwa ajili ya usalama na kufanikisha shuguli nzima ya wanachi walio hudhuria. Hii inatoka na maasi yaliyo tokea hivi karibuni katika kitongoji cha Tottenham na sehemu nyingine  nchini Uingereza. 

 Jumla ya watu 53 wanashikiliwa na polisi kutokana kutaka kufanya fujo jana katika carnival.

Hii ni Carnival kubwa kuliko zote za mabara ya ulaya na ni ya pili kwa dunia

Msanii Kutoka Urban Pulse alifanya makamuzi katika Carnival hii iliyohudhuriwa na watu wengi, mmojawapo wa wadau waliojitokeza kumuunga mkono ni msanii Page kutoka Xfactor.

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE NA MISS JESTINA BLOG 

 nguo za rangi zilirembesha carnival.
 parade imeanza.
 baba na mwana wakifuatilia carnival tokea kibarazani.
 hata wazee hawakupitwa na kitu.
 kila mtu alikuwa bize kuwa sehemu ya carnival.
 Mish Akila Pozi na jestina Kabla ya kupiga show.
 Wadau wakipata menu na nguo zao za urembo.
 wadau wakila pozi na Jestina.
 Msanii pekee Mish aliye perfom kutoka Urban Pulse Akifanya makamuzi.
 Page Kutoka x factor aliekuja kutoa supoti kwa Mish wakati wa show.
 Page kutoka x factor na wadau .
 palikuwa hapatoshi watu wa kumwaga.
 kila corner na mitaa Notting Hill ilikuwa imefurika watu.
malori yakipita mitaa huku yakipiga mziki mzito.

Monday, August 29, 2011

FUTARI YA READING EASTERN AFRICAN COMMUNITY(REACO) JUMAMOSI

 picha ya pamoja na wanajumuia
 Baadhi ya Viongozi wa REACO katika Picha ya pamoja
 Mh Chabaka akifurahia jambo wakati Afisa wa UBalozi Kiondo akiteta na Ustaadhi Sungura
 Mh Naibu Balozi Chabaka akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa REACO
 Baadhi ya viongozi wa REACO wakipata Futar

 wanajumuia pamoja na wageni wakipata Futari kwa pamoja
 watoto wakipata futari
Mh Naibu Balozi akipata futari 
 Futari ilienda sambamba na kubadilishana mawazo
 mtoto mwanajumia nae akila futari
 Futari Ikiendela

wanajumuia wakijiandaa kwa kabla ya kupata futar

Sunday, August 28, 2011

mkazi wa mbeya ajishindia gari kwenye promosheni ya jivunie ya airtel.


Baadhi ya wakazi wa Tukuyu Mbeya wakishangilia na wengine kulibusu gari jipya aina ya Toyota Corolla lililotolewa zawadi na kampuni ya simu za mkoni ya airtel kwa Bw Albert George Mwasibata aliyeibuka mshindi katika promosheni iliyoisha ya Airtel JIVUNIE katika viwanja vya Tukuyu Mbeya mwishoni mwa wiki hii.
Mshindi wa gari ya promosheni ya Airtel JIVUNIE  wa mkoani mbeya  Bw Albert George Mwasibata akiwapungia mikono wakazi wenzake wa mkoani humo kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa gari yake mpya aina ya Corolla katika viwanja vya Tukuyu mbeya baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya gari hiyo kufanyika mwishoni mwa wiki.
Mshindi wa gari ya promosheni ya Airtel JIVUNIE  Bw, Albert George Mwasibata akiwasha gari lake jipya aina ya Corolla mara baada ya kukabidhiwa katika hafla ya makabidhiano iliyoandaliwa na Airtel  katika viwanja vya Tukuyu Mbeya .
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando kulia akimpongeza mshindi wa Promosheni iliyoisha ya Airtel JIVUNIE Bw. Albert Mwasibata katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya Rungwe Tukuyu Bw Moses Mwidete  ambae alikuwa mgeni rasmi wakati wa makabidhiano hayo katika viwanja vya mpira wa miguu Tukuyu Mbeya.wishoni mwa wiki.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Tukuyu Bw, Moses Mwidete (watatu toka kulia) akikabidhi ufunguo wa gari mpya aina ya Toyota corolla kwa mshindi wa promosheni ya Airtel JIVUNIE bw Albert Mwasibata katikati. Wa kwanza kushoto ni Ofisa Masoko wa airtel  Kanda ya Kusini Bw Jonas Mbaga akishuhudia makabidhiano kwa pamoja na wafanyakazi wenzake kulia katika viwanja vya mpira Tukuyu
Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimuelekeza sehemu ya kuweka sahihi  Bi  (kati) ambae ni mke wa Bw, Albert Gerge Mwasibata, wa kwanza toka kulia  mshindi wa gari ya airtel katika promosheni iliyoisha ya Jivunie  ikiwa ni ishara ya kupokea zawadi ya gari yao mpya aina ya Corolla kutoka Airtel
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na wananchi wa Tukuyu Mbeya wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa minara ya mawasiliano ya Airtel pamoja na kukabidhi zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Corolla mshindi mkazi wa mkoa huo Bw, Albert George Mwasibata aliyeibuka mshindi katika promosheni ya jivunie.
 
=========  ============  ============== 
 
Airtel yavuma nyanda za juu kusini
 
 Na Ripota wetu
Yazindua huduma za mawasilino Tukuyu Mbeya na mbinga Ruvuma,  Yakabidhi gari kwa mshindi wa promosheni ya jivunie Tukuyu
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mwishoni mwa wiki hii imezindua huduma za mawasiliano mjini na vijijini ikiwa ni katika muendelezo wa dhamira yake ya kufikia wanananchi wengi na kuinua shughuli za uchumi nchini.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja wa Kanda wa Airtel bw Fredrick Mwakitwang alisema “Airtel leo tunazindua na kupanua huduma zetu mkoani mbeya –Tukuyu katika vijiji vya Katumba, Watco, Ibililo, Ikuti  na Mkoani Ruvuma katika kijiji cha Litola kilichopo Mbinga.
 
Wakazi wa Mbinga na Tukuyu sasa wataboresha shughuli zao za kilimo na biashara kwa urahisi na kupata taarifa mbalimbali zitakazo wawezasha kufanikisha kazi zao za kila siku kupitia mawasiliano ya Airtel kwa uhakika.
 
Wakati huo huo Airtel ilikabidhi gari mpaya aina ya Corolla kwa mshindi wa promosheni ya Airtel Jivunie Bwana Albert George Mwasibata mkazi wa Tukuyu Mbeya.  Shindano ili liliwashirikisha wateja wote wa Airtel na bwana Mwasibata kuibuka mmojawapo wa mshindi kati ya washindi wengi waliopatikana nchini kote.
 
Akiongea katika halfa maalumu iliyoandaliwa na Airtel mkoani  Mbeya Tukuyu   Meneja mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema,  Airtel  imejidhatiti na kujipanga kuwapatia wateja wake huduma bora na kwa bei nafuu
 
leo hii tumefikisha huduma hii hapa Tukuyu vijijini, hii inaonyesha wazi kuwa tunaendelea kutekelezaji dhamira ya kuchangia maendeleo ya nchi  kupitia sekta ya mawasiliano.  Airtel tunaimani kuwa  kuboresha mawasiliano katika vijiji itaongeza  chachu ya kipeeke katika kuchangia maendeleo ya nchi kwa ujumla.
 
Leo hii Vijiji vya Ibililo, watcoIkuti, na Litola wilaya ya Rungwe Tukuyu mnaweza kutumia mawasiliano ya Aitel ya Robo shilingi kwa sekunde kwa kufanya biashara na watu walioko mikoa mingine na kujipatia faida kubwa itakayosaidia kuboresha maisha yenu” alisema mmbando
 
Aidha Bwana Mmbando alichukua fulsa hiyo kukabidhi gari kwa mshindi wa Mshindi wa promosheni ya Airtel Jivunie Bw, Abert George Mwasibata nakumpongeza kwa kuibuka kuwa mshindi wa promosheni hiyo.
 
“ wakazi wa Tukuyu hii ni bahati kwetu! sasa tushiriki na tuamini  promosheni zinazoendelea kwani kila mteja anaweza kuibuka mshindi kama mwenzetu huyu!
 
Akiongea baada ya kukabidhiwa Zawadi hiyo bwana Mwasibata alisema nashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kunikabidhi gari hili leo, hii ni furaha ya pekee kuona Airtel kwa kupitia promosheni ya jivunie imeweza kunikabidhi rasmi zawadi hii, najisikia Faraja ya pekee.
 
Naye katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Tukuyu by Moses Mwandete akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Tukuyu alisema “Tunaipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kutufikishia mawasiliano na kuwa mtandao pekee na wakwanza kupatikana katika vijiji vya Katumba watco, ibililo / ikuti na itola kanda ya kusini. 
 
Airtel imeweka kielelezo na kutoa changamoto kwa wadau wengine katika sekta hii kufikisha huduma zao mahali ambapo mawasiliano hayapo ili kuweka ushindani wa kibiashara ili kuendelea kutupatia unafuu zaidi. 
 
 Leo hii Katumba Watco, Ibililo, Ikuti  Itola pamoja na vijiji vya jirani watafaidiaka na huduma za mawasiliano za mtandao wa simu ya Airtel. Tunawaahidi kuwapa ushirikiano kutoka serikalini katika kufanikisha shughuli zenu za biashara hapa nchini ambazo ni chachu kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla.
 
Pamoja na hilo nichukue fulsa hii kumpongeza mshindi wa promosheni ambaye ametokea Tukuyu mbeya namsihi aendelee kuwa balozi mzuri wa Airtel.

Monday, August 22, 2011

matukio ya ajali ya Mbunge Mussa Khamis Silima Dodoma na Dar es salaam


 Baadhi ya waheshimiwa wabunge wanawake wakiwa hospitali ya mkoa ya Dodoma wakati wa kuckuliwa mwili wa marehemu mke wa Mbunge Mussa Khamis Silima
 Wabunge wanawake wakiwa hospitali ya mkoa wa Dodoma
 Mdau Said Yakub akiwa na wanahabari hospitali ya mkoa wa Dodoma
 Mwili wa marehemu ukishushwa kutoka garini baada ya kuwasili msikirti mkuu wa Ijumaa Dodoma 
 Wabunge na waombolezaji wengine wakiuingiza mwili wa marehemu msikitini 
 Mwili wa marehemu ukiingizwa msikitini
 Mwili ukiingizwa msikitini
 Mwili wa marehemu ukiswaliwa
 Ndani ya msikiti mkuu wa Ijumaa wa Dodoma 
 Waombolezaji wakiwa uwanja wa ndege wa Dodoma
 Mwili wa marehemu kiingizwa kwenye ndege tayari kwa safari ya Zanzibar

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mh. Anne Makinda akiongoza waombolezaji kwenye kusindikiza mwili wa marehemu uwanja wa Ndege wa Dodoma
 Waombolezaji uwanja wa ndege wa Dodoma
 Ndege ikiondoka 
Buriani...
Mzee Samwel Sitta (shoto), waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Mh. william Lukuvi (kulia) wakiwa na kaimu Katibu wa Bunge wakiongea haya na yale katika shughuli hiyo