Sunday, August 28, 2011

mkazi wa mbeya ajishindia gari kwenye promosheni ya jivunie ya airtel.


Baadhi ya wakazi wa Tukuyu Mbeya wakishangilia na wengine kulibusu gari jipya aina ya Toyota Corolla lililotolewa zawadi na kampuni ya simu za mkoni ya airtel kwa Bw Albert George Mwasibata aliyeibuka mshindi katika promosheni iliyoisha ya Airtel JIVUNIE katika viwanja vya Tukuyu Mbeya mwishoni mwa wiki hii.
Mshindi wa gari ya promosheni ya Airtel JIVUNIE  wa mkoani mbeya  Bw Albert George Mwasibata akiwapungia mikono wakazi wenzake wa mkoani humo kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa gari yake mpya aina ya Corolla katika viwanja vya Tukuyu mbeya baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya gari hiyo kufanyika mwishoni mwa wiki.
Mshindi wa gari ya promosheni ya Airtel JIVUNIE  Bw, Albert George Mwasibata akiwasha gari lake jipya aina ya Corolla mara baada ya kukabidhiwa katika hafla ya makabidhiano iliyoandaliwa na Airtel  katika viwanja vya Tukuyu Mbeya .
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando kulia akimpongeza mshindi wa Promosheni iliyoisha ya Airtel JIVUNIE Bw. Albert Mwasibata katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya Rungwe Tukuyu Bw Moses Mwidete  ambae alikuwa mgeni rasmi wakati wa makabidhiano hayo katika viwanja vya mpira wa miguu Tukuyu Mbeya.wishoni mwa wiki.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Tukuyu Bw, Moses Mwidete (watatu toka kulia) akikabidhi ufunguo wa gari mpya aina ya Toyota corolla kwa mshindi wa promosheni ya Airtel JIVUNIE bw Albert Mwasibata katikati. Wa kwanza kushoto ni Ofisa Masoko wa airtel  Kanda ya Kusini Bw Jonas Mbaga akishuhudia makabidhiano kwa pamoja na wafanyakazi wenzake kulia katika viwanja vya mpira Tukuyu
Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimuelekeza sehemu ya kuweka sahihi  Bi  (kati) ambae ni mke wa Bw, Albert Gerge Mwasibata, wa kwanza toka kulia  mshindi wa gari ya airtel katika promosheni iliyoisha ya Jivunie  ikiwa ni ishara ya kupokea zawadi ya gari yao mpya aina ya Corolla kutoka Airtel
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na wananchi wa Tukuyu Mbeya wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa minara ya mawasiliano ya Airtel pamoja na kukabidhi zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Corolla mshindi mkazi wa mkoa huo Bw, Albert George Mwasibata aliyeibuka mshindi katika promosheni ya jivunie.
 
=========  ============  ============== 
 
Airtel yavuma nyanda za juu kusini
 
 Na Ripota wetu
Yazindua huduma za mawasilino Tukuyu Mbeya na mbinga Ruvuma,  Yakabidhi gari kwa mshindi wa promosheni ya jivunie Tukuyu
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mwishoni mwa wiki hii imezindua huduma za mawasiliano mjini na vijijini ikiwa ni katika muendelezo wa dhamira yake ya kufikia wanananchi wengi na kuinua shughuli za uchumi nchini.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja wa Kanda wa Airtel bw Fredrick Mwakitwang alisema “Airtel leo tunazindua na kupanua huduma zetu mkoani mbeya –Tukuyu katika vijiji vya Katumba, Watco, Ibililo, Ikuti  na Mkoani Ruvuma katika kijiji cha Litola kilichopo Mbinga.
 
Wakazi wa Mbinga na Tukuyu sasa wataboresha shughuli zao za kilimo na biashara kwa urahisi na kupata taarifa mbalimbali zitakazo wawezasha kufanikisha kazi zao za kila siku kupitia mawasiliano ya Airtel kwa uhakika.
 
Wakati huo huo Airtel ilikabidhi gari mpaya aina ya Corolla kwa mshindi wa promosheni ya Airtel Jivunie Bwana Albert George Mwasibata mkazi wa Tukuyu Mbeya.  Shindano ili liliwashirikisha wateja wote wa Airtel na bwana Mwasibata kuibuka mmojawapo wa mshindi kati ya washindi wengi waliopatikana nchini kote.
 
Akiongea katika halfa maalumu iliyoandaliwa na Airtel mkoani  Mbeya Tukuyu   Meneja mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema,  Airtel  imejidhatiti na kujipanga kuwapatia wateja wake huduma bora na kwa bei nafuu
 
leo hii tumefikisha huduma hii hapa Tukuyu vijijini, hii inaonyesha wazi kuwa tunaendelea kutekelezaji dhamira ya kuchangia maendeleo ya nchi  kupitia sekta ya mawasiliano.  Airtel tunaimani kuwa  kuboresha mawasiliano katika vijiji itaongeza  chachu ya kipeeke katika kuchangia maendeleo ya nchi kwa ujumla.
 
Leo hii Vijiji vya Ibililo, watcoIkuti, na Litola wilaya ya Rungwe Tukuyu mnaweza kutumia mawasiliano ya Aitel ya Robo shilingi kwa sekunde kwa kufanya biashara na watu walioko mikoa mingine na kujipatia faida kubwa itakayosaidia kuboresha maisha yenu” alisema mmbando
 
Aidha Bwana Mmbando alichukua fulsa hiyo kukabidhi gari kwa mshindi wa Mshindi wa promosheni ya Airtel Jivunie Bw, Abert George Mwasibata nakumpongeza kwa kuibuka kuwa mshindi wa promosheni hiyo.
 
“ wakazi wa Tukuyu hii ni bahati kwetu! sasa tushiriki na tuamini  promosheni zinazoendelea kwani kila mteja anaweza kuibuka mshindi kama mwenzetu huyu!
 
Akiongea baada ya kukabidhiwa Zawadi hiyo bwana Mwasibata alisema nashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kunikabidhi gari hili leo, hii ni furaha ya pekee kuona Airtel kwa kupitia promosheni ya jivunie imeweza kunikabidhi rasmi zawadi hii, najisikia Faraja ya pekee.
 
Naye katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Tukuyu by Moses Mwandete akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Tukuyu alisema “Tunaipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kutufikishia mawasiliano na kuwa mtandao pekee na wakwanza kupatikana katika vijiji vya Katumba watco, ibililo / ikuti na itola kanda ya kusini. 
 
Airtel imeweka kielelezo na kutoa changamoto kwa wadau wengine katika sekta hii kufikisha huduma zao mahali ambapo mawasiliano hayapo ili kuweka ushindani wa kibiashara ili kuendelea kutupatia unafuu zaidi. 
 
 Leo hii Katumba Watco, Ibililo, Ikuti  Itola pamoja na vijiji vya jirani watafaidiaka na huduma za mawasiliano za mtandao wa simu ya Airtel. Tunawaahidi kuwapa ushirikiano kutoka serikalini katika kufanikisha shughuli zenu za biashara hapa nchini ambazo ni chachu kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla.
 
Pamoja na hilo nichukue fulsa hii kumpongeza mshindi wa promosheni ambaye ametokea Tukuyu mbeya namsihi aendelee kuwa balozi mzuri wa Airtel.

No comments: