Thursday, December 31, 2015

TTCL YATOA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA VITUO VYA YATIMA DAR ES SALAAM.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akikabidhi sehemu ya msaada kwa baadhi ya watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi Mlezi wa Watoto na Vijana, Stella Mwambenja wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya watoto wa kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wa chakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016 kwa vituo vitatu vya watoto yatima Dar es Salaam. Kulia ni Mlezi wa Watoto na Vijana wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede, Stella Mwambenja. 
Mmoja wa watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede cha Buguruni Malapa Dar es Salaam akitoa shukrani kwa kampuni ya TTCL baada ya kukabidhiwa msaada huo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Amanda Luhanga (kulia) wakipewa historia fupi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge kwa Ofisa Mfawidhi, Ojuku Mgezi (katikati) kabla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya. 
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Ofisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge, Ojuku Mgezi (wa pili kushoto) msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Wengine ni viongozi na wawakilishi wa jumuiya ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. 
Sehemu ya makazi ya Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge 
Sehemu ya msaada ukishushwa kwenye Kituo cha Makazi ya Wazee Nunge. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas  (kulia) akizungumza na watoto wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Honoratha cha Temeke jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada Mlezi wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Honoratha cha Temeke jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. TTCL imetoa msaada wa mifuko ya Unga, Sukari, Mchele, Maharage na Mafuta ya Kupikia kwa vituo vitatu tofauti vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (katikati) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa Kituo cha Kulelea Watoto Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Temeke cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016. 

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA BARUA PEPE ZA KAWAIDA KATIKA MAWASILIANO YAKE


Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kushoto) akipokelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam. 
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (katikati) akiwasili Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kwa ziara ya kikazi leo jijini Dar es salaam.
Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) akitembelea maeneo mbalimbali ya Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao leo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam. 


Mkurugenzi wa Uratibu wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Benjamin Dotto akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es salaam. 


Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza na Watendaji na baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao leo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala hiyo jijini Dar es salaam. 

Na. Aron Msigwa –MAELEZO. 
Serikali imepiga marufuku matumizi ya Barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA Serikalini. 

“Sasa kuna watumishi 7000 wanaotumia anwani za Barua pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu” Amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye mawasiliano binafsi. 

Amesema kwa kutambua umuhimu wa uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia mitandao mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia Barua Pepe za Serikali. 

Mhe. Kairuki amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za umma zinaunganishwa na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano. 

“Katika hili ninatoa siku 60 muhakikishe kuwa mnakamilisha kwa Taasisi zilizobaki ili kwa wale watakaopuuzia hatua zianze kuchukuliwa” Ameeleza Mhe. Angella. 

Aidha, ametoa wito kwa watendaji wa Wakala hiyo kuweka mpango wa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa kitaaluma watumishi waliopo kazini kwa kujenga utaratibu wa kuwarithisha uzoefu watumishi ili kuendelea kuimarisha ufanisi na utendaji wa Wakala hiyo. 

Mhe. Kairuki amewataka kuwa wabunifu katika kuanzisha mifumo mipya ya TEHAMA ili kuimarisha dhana ya Serikali mtandao ili kupunguza gharama hadi kufikia asilimia 5 ya fedha zinazotumika kuendeshea masuala mbalimbali ambayo yangefanywa kupitia matumizi ya TEHAMA. 

Akizungumzia kuhusu ununuzi wa vifaa vya TEHAMA serikalini ameitaka Wakala hiyo kutoa ushauri ili kudhibiti mianya ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha katika kununulia vifaa hivyo kwa gharama kubwa wakati vinaweza kupatikana kwa bei ya kawaida. 

“katika hili Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika katika upotevu wa mapato muhakikise mnazisaidia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika masuala ya ununuzi wa mifumo na vifaa vya TEHAMA ili mifumo inayonunuliwa iwe na manufaa kwa wananchi na thamani halisi ya fedha” 

Amesema Serikali itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kupitia mtandao ili wananchi waweze kupata huduma hizo mahali walipo kwa gharama nafuu na kutoa wito kwa watumishi wa Wakala ya Serikali mtandao (e-Gov) kuwa wabunifu katika kutengeneza programu mbalimbali na mifumo salama itakayowasaidia wananchi kupata huduma. 

Aidha, katika hatua nyingine ameitaka e-Gov kuendelelea kujenga uwezo katika kudhibiti dharura na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika matumizi ya TEHAMA na kuitaka Wakala hiyo iendelee kulifanyia kazi suala la kuwezesha mifumo ya Serikali kuzungumza kati ya taasisi moja hadi nyingine ili huduma zote ziweze kupatikana katika eneo moja na kuondoa urudufu wa mifumo iliyopo. 

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Gov) Dkt. Jabiri Bakari akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala hiyo amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali toka kuanzishwa kwake Julai 11, 2012 imeendelea kupata ufanisi katika uimarishaji wa Serikali Mtandao. 

Amesema kuwa Wakala hiyo inaendelea kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinawafikia wananchi kupitia mtandao mahali walipo na kuhakikisha kuwa inafanikisha lengo la huduma zote za Serikali kupatikana chini ya dirisha moja. 

Aidha amesema kuwa Wakala ya Serikali Mtandao itaendelea kuhakikisha kuwa usimamizi wa viwango vya matumizi ya TEHAMA katika Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali vinazingatiwa. 

Waziri Mahiga akutana na Mabalozi wa Qatar na Kuwait waliopo nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akifanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Mhe. Abdullah Jassim Almaadadi alipofika Wizarani kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa katika wadhifa wake mpya na pia kumhakikishia ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar. Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 30 Desemba, 2015. 
Balozi Al maadadi naye akizungumza huku Mhe. Mahiga akimsikiliza. 
Mazungumzo yakiendelea 
Waziri Mahiga akiagana na Balozi Al Maadadi mara baada ya kumaliza mazungumzo. 
.......Mkutano na Balozi wa Kuwait nchini 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib, alipokuja kumtembelea Wizarani na kufanya mazungumzo naye kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kuwait na pia kumpongeza. 
Balozi Mahiga akiagana na Balozi wa Kuwait mara baada ya kumaliza mazungumzo naye. 
Picha na Reginald Philip

Wakulima waaswa kwenye matumizi ya mikopo

Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Benki, Bibi Neema Christina John (aliyevaa miwani) wakati wa uhakiki wa fomu zilizojazwa na moja kati ya vikundi vilivyofanikiwa kupata mkopo kutoka Benki hiyo.
Mwanasheria mwandamizi wa TADB, Bibi Salome Masenga (Kulia) akimuelekeza mmoja wa wanakikundi waliopata mikopo kutoka Benki hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (Aliyesimama) akiwapungia wakulima waliojitokeza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa, katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), wakiwapungia wakulima waliojitokeza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa, katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bibi Amina Masenza (Kulia) wakifuatilia kwa makini matukio wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa, katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bw. Kasunga (Kulia).

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla hiyo.












Na Mwandishi wetu, Iringa

Wakulima wote nchini wameaswa kutumia vizuri mikopo wanayopewa ili kuweza kutimiza malengo yao binafsi na ya Serikali katika kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mama Amina Masenza wakati wa wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa iringa, katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Mama Masenza alisema kuwa wakulima wakitumia mikopo waliyopewa kwa malengo husika watafika mbali na kuweza kuchagiza mikakati ya Benki hiyo katika kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kilimo kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

“Naamini, wakati Benki ya Maendeleo ya Kilimo itapoanza kufanya tathmini ya mikopo hii iweze kuona matunda ya uwekezaji wake hasa kwa nyie ambao mmeweza kubahatika kupata fursa ya awali kabili kunufaika na huduma za TADB,” aliwasihi.

Mama Masenza aliwaomba  wakulima hao kuwa Mfano Bora na wanaojitambua vilivyo, hasa nia ya kutoka katika kiwango fulani cha maisha kwenda katika hatua nyingine za juu zaidi kimaisha kwa kuongeza kipato na ubora wa kimaisha kwa ujumla kupitia huduma za TADB. 

“Nawasihi kutotumia pesa hizi kinyume na malengo yaliyokusudiwa, kwani kwa kufanya hivyo, siyo tuu tunaiua Benki yetu bali pia tunajimaliza wenyewe kiuchumi. Wito wangu kwenu ni kujipanga kwa dhati ili kuweza kutimiza malengo makuu ya mikopo hii ambayo ni kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini,” aliongeza.

Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kwamba Benki yake imedhamiria kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini ili kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.

Bw. Samkyi alisema TABD imejizatiti kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mapinduzi ya kilimo kwa kuongeza tija na upatikanaji wa mikopo ya riba nafuu maalum kwa sekta ya kilimo, kama njia ya kuleta Mapinduzi yenye tija kwa wakulima nchini. 

“Benki imejipanga kutoa mikopo yenye riba nafuu katika muda mfupi, wa kati na mrefu kwa Wakulima wadogo wadogo,  wa kati na wakubwa, hususan kuziba pengo la upatikanaji wa fedha za kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani katika tasnia za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu (ufugaji nyuki),” alisema Bw. Samkyi.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba kwa kuanzia walengwa wakuu wa TADB ni wakulima wadogo wadogo, hatahivyo, hata wale wakulima wa kati na wakubwa watahudumiwa.

Bw. Samkyi imejidhatiti katika kufanya tathmini ya kina katika mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi kwa minajili ya kuongeza thamani na ushindani kwenye masoko.

“Sera ya TADB ni kutathmini mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi, na ambayo utatuzi wake utaongeza tija na uwezo wa ushindani kwenye masoko, na hivyo kukuza uchumi wa walio wengi na kupunguza umaskini,” aliongeza.

Katika hafla hiyo, jumla ya vikundi nane (8) vyenye jumla ya wakulima wadogo wadogo 857, vilimiza vigezo na kupewa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja. 

Kwa mujibu wa Bw. Samkyi kabla ya kutoa mikopo hiyo, benki iliwatembelea na kutoa elimu kwa wakulima jinsi ya kuimarisha vikundi vyao, ambapo jumla ya vikundi 89 vyenye jumla ya wanakikundi 21,526 vilifikiwa.

Akizungumzia malengo ya TADB kwa upana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila alisema kuwa Benki inalenga kutelekeza kwa vitendo Maelekezo ya Serikali ya kupunguza changamoto zinazomkabili mkulima.

“Tunalenga kuwafikia wakulima wote nchini kadri siku zinavyoendelea kwenda na kutegemea mtaji unavyoongezeka ama upatikanaji wa fedha toka vyanzo mbali mbali ili kuweza kuwawezesha kumudu shughuli zao za kilimo,” alisema. 

Aliongeza kuwa kwa sasa Benki inalenga kusambaa nchi nzima kwa kuanzisha Ofisi za Kikanda ndani ya miaka mitano ijayo, kuwajengea uwezo na kuanzisha Programu Maalumu ya Vijana wajihusishao na shughuli za Kilimo cha kibiashara na kushirikiana na wadau wengine kuhuisha shughuli za umwagiliaji na miradi ya kisasa ya umwagiliaji.

Malengo mengine ni kutafuta fedha toka vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha Wakulima katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye mazao ya Kilimo na kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na Minne (14) ya Mwanzo na kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia kuwaunganisha Wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ilizinduliwa Rasmi na Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima nchini, mnamo tarehe 8 Agosti 2015 mjini Lindi. Uanzishwaji wa Benki hii ni utekelezaji wa malengo ya muda mrefu ya Serikali, katika kuitikia wito wa wananchi na wadau wengine wa maendeleo ili Tanzania iweze kupiga hatua endelevu za kimaendeleo.

MWALIMU GODFREY GODWIN KIHENGU NA MARIAM BARAKA BINAGI WAUAGA RASMI UKAPER

Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akiwafungisha ndoa Bi.Mariam Baraka Binagi (wa pili kulia) wa Rebu Tarime, Mara pamoja na Mwalimu Godfrey Godwin Kihengu (wa pili kushoto) wa Nyansurura Tarime, Mara ikiwa ni katika ibada iliyofanyika jana Desemba 30,2015 katika Kanisa Anglikana Buhemba Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Picha na BMG (Binagi Media Group)
Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akimkabidhi bwana harusi cheti cha ndoa
Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akimkabidhi bibi harusi cheti cha ndoa
Maharusi wakionyesha vyeti vyao vya ndoa
Bi.Mariam Baraka Binagi (Kushoto) akiwa pamoja na bwana harusi Godfrey Godwin Kihengu.
Bibi harusi akimlisha keki bwana harusi
Maharusi wakinyweshana Shampeni
Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wachungaji
Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake akiwemo mama yake mzazi pembeni ya bibi harusi
Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake
Maharusi wakiwa pamoja na Wakwe zake
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na wadogo zao
Bibi harusi akiingia Ukumbini siku ya Sendoff iliyofanyika juzi Desemba 29,2015
Kushoto ni bi harusi akiwa ukumbini siku ya Sendoff iliyofanyika juzi Desemba 29,2015
Bi.Mariam Baraka Binagi (Kulia) akiwa pamoja na bwana harusi Godfrey Godwin Kihengu (Kushoto)
Kaka wa bibi harusi ambae pia ndie mmiliki wa BMG (Kushoto) akiwa pamoja na Mama Mzazi wa bibi harusi
Kaka wa bibi harusi ambae pia ndie mmiliki wa BMG (Kulia) akiwa pamoja na dada wa bibi harusi
"Tunawatakiwa Maisha Mema na Yenye Fanaka katika ndoa yenu na Mola azidi kuibariki"
Zaidi BONYEZA HAPA