Friday, August 31, 2018

MAWAKILI WA SERIKALI KUWA NA CHAMA CHAO – AG

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akitoa mada kuhusu Nafasi na Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wakati wa mkutano unaoendelea wa Mawakili wa Serikali waliokatika utumishi wa umma. Pamoja na mambo mengine Dk. Kilangi amesema Mawakili wa Seriakali walio katika utumishi wa umma watakuwa na chama chao.
Sehemu ya mawakili wa serikali kutoka wizara mbalimbali, Idara na Taasisi zinazojitegema, Wakala na Serikali za Mitaa ambao wapo Jijini Dodoma kwa mkutano wao wa siku mbili.

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi amesema, anakusudia kuanzisha Chama cha Wanasheria walio katika utumishi wa Umma. Dk. Kilangi ameyaeleza hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu Nafasi na Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa Mawakili wa Serikali walio katika utumishi wa umma wanaokutana katika mkutano wao wa siku mbili unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Mawakili hao wa Serikali wapatao mia tisa ( 900) wanatoka Wizara mbalimbali, Idara za Serikali, Taasisi na Mashirika yanayojitegemea, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mkutano huo ambao ni wa pili kufanyikia ulifunguliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amebainisha kwamba, kuanzishwa kwa Chama hicho ni kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Muswaada wa Sheria ya Marekebisho Mbalimbali ( Na.2) 2018 inayoeleza kuwa , “ Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaweza kuanzisha Chama cha Wanasheri katika Utumishi wa Umma”.

Amewaeleza Mawakili wa Serikali kwamba Chama hicho kitakuwa kinakutana mara moja kwa mwaka kwaajili ya kujadili masuala mbalimbali ya kisheria ikiwamo maendeleo ya taaluma hiyo. Dk. Kilangi amesema, pamoja na wanachama wa chama hicho kukutana mara moja kwa mwaka, Waziri mwenye dhamana na mambo ya sheria anaweza kuitisha mikutano ya wanasheria waliokatika utumishi wa umma kila anapoona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Amefafanua zaidi kwa kusema, ripoti ya mikutano ya chama hicho itawasilishwa kwa Waziri wa Katiba na Sheria na kwamba, Waziri atatunga Kanuni kuhusu usimamizi, uongozi, muundo na uendeshaji wa shughuli za chama. Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuanzishwa kwa chama cha Mawakili wa Serikali walio katika utumishi wa Umma hakutawanyima fursa mawakili hao ya kujiunga au kuwa wanachama wa vyama vingine vya kitaaluma kikiwamo Tanganyika law Society ( TLS).

Akizungumzia kuhusu kuanzishwa kwa daftari la mawakili wa serikali, Mwanasheria Mkuu amesema, daftari hili litaanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Muswaada wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali ( Na. 2) 2018 unaotamka kwamba, “ Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataanzisha Daftari la Mawakili wa Serikali ( Roll of State Attorneys)”.

Amesema daftari hilo likuwa na majina ya mawakili wa serikali kwa kuzingatia ukuu ( seniority ) miongoni mwao na kusisitiza kwamba, hatua hiyo haitaathiri sifa au hadhi ambayo mtu alikuwa nayo kabla ya kuazishwa kwa daftari hilo.

Kuhusu mawakili hao sasa kutambulika kama wanasheria wa Serikali ( State Attonerys ) Mwanasheria Mkuu wa Serikali amelitolea ufafanuzi kwa kusema Kila Afisa Sheria aliyeteuliwa au kuajiriwa katika Wizara, Idara inayojitegemea, wakala au serikali za mitaa sasa anakuwa wakili wa serikali na kwa sababu hiyo yuko chini ya usimamizi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali isipokuwa kwa Wanasheria wa Serikali ambao wapo chini ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

“Hivyo Afisa huyo anachukuliwa kuwa anafanya kazi na kutekeleza majukumu na mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Wizara zao , Idara zinazojitegemea, wakala wa serikali na Serikali za mitaa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataweweza kutoa maelekezo ya jumla au maelekezo mahsusi kwa mawakili wa serikali walio katika utumishi wa umma kuhusu utekelezaji wa majukumu yao ya kisheria.

Akawahimiza wanasheria hao kila mmoja wao kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa bidii, maarifa na ujuzi wake huku akitanguliza maslahi ya taifa lake katika kila jambo analokishughulikia. Akahadharisha kwamba, hatasita kuchukua hatua dhidi ya mtumishi yeyote atakaye kiuka maadili ya Mawakili katika utumishi wake.

Awali akifungua Mkutano huo Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, amewataka Mawakili wa Serikali kutumia njia mbadala ya usuluhi katika baadhi kesi za madai pale inapobidi na kufikia usuluhishi nje ya Mahakama. Jaji Mkuu amesema , ikiwa njia ya usuluhishi nje ya mahakama utafanyika, basi utapunguza muda wa undeshaji kwa kesi hizo ambazo nyingine huchukua hadi miaka kumi bila kufikia muafaka.

“Niwaombe wanasheria wa Serikali katika kesi nyingine za madai pale inapobidi wajaribu sana kulenga kufikia usuluhishi wa nje ya mahakama badala ya kuendesha kesi kwa miaka hata kumi, kuanzia kesi inapoanza ngazi ya chini hadi kufikia Mahakama ya Rufani” amesema Jaji Mkuu na Akasisitiza kwamba, “ Kuna wakati wanasheria wa Serikali wanakiri kwa pembeni, kuwa kesi wanayoendesha haina nafasi ya kushinda au hata wakishinda gharama hadi kupata ushindi huyo ni kubwa. Wanapambana tu kwa sababu Mkuu wa Idara au Kitengo amesema hivyo”.

Akasisitiza kwa kusema. “Hapa ndipo ipo haja ya kujenga Imani ya Mawakili hawa ( wa Serikali) na kuwaruhusu wapate usuluhisho wa mashauri nje ya mahakama”.

Akitoa takwimu za Kituo cha Usuluhishi ( Mediation Centre) cha Mahakama Kuu Dar es Salaam kwa mwaka jana ( 2017) kinaonyesha kuwa jumla ya mashauri 41 yalisuluhishwa na kituo bila ya kufikishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa na kati ya hizo, ni 10 tu zilikuwa za taasisi ya Umma.

16 WANAODAIWA KUKWAPUA FEDHA ZA USHIRIKA WILAYANI HAI ,WAWEKWA NDANI KWA AMRI YA DC SABAYANa Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,
Kanda ya Kaskazini.


-WADAIWA KUFANYA UBADHILIFU WA ZAIDI YA MIL 200.
-WENGINE WAUZA VIPURI VYA MASHINE.
WATU 16 wakiwemo viongozi wa Bodi ya Ushirika wa Umoja wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni (UWAMI) wanashikiliwa na Jeshi la  Polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya  wakituhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa fedha za mradi zaidi ya Sh Mil 200.
Mbali na Viongozi wa Bodi ya ushirika huo wakiongozwa na Mwenyekiti wake ,Nuru Ndoma pia wamo baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji, Viongozi wa kamati ya mpito ya kusimamia mradi huo ikiongozwa na Alex Mkwizu.
Kukamatwa kwa Viongozi hao kunatokana na taarifa ya uchunguzi uliofanywa na kamati iliyoundwa na  Mkuu huyo wa wilaya kuchunguza madai ya ubadhilifu wa fedha baada ya kukataa taarifa yaawali ya  kamati kama hiyo iliyoundwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Gelasius Byakanwa.
Tuhuma zinazowakabili watu hao zimetajwa kuwa ni pamoja na kuuzwa kinyemela kwa Mashine ya kulimia (Power tiller ) aina ya Kubota iliyotolewa na Wizara ya Kilimo kwa kijiji cha Mijongweni ambayo inatajwa kuuzwa kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Yusuph Losindilo.
Baadhi ya viongozi hao pia wanatajwa kutakatisha fedha za malipo ya ukodishwaji wa mashine ya kuvunia Mpunga kwa kuziingiza katika akaunti ya kijiji na kasha kuzitoa wakati huo huo na kuzipangia matumizi yasiyokuwa na maelezo ya kutoshereza.
Aidha watu hao pia wanadaiwa kuuza baadhi ya vipuri vya Mashine hizo na baadae kuonesha kuwa wamenunua vipuri kwa ajili ya matengenezo ya mashine hizo huku ikionyesha vipuri vinavyodaiwa kununuliwa ni vile vilivyoletwa pamoja na mashine.
Katika taarifa yake ,Mwenyekiti wa kamati hiyo maalumu ya uchunguzi ,Valeria Banda alisema wizara ya Kilimo ,chakula na Ushirika kupitia Halmashauri ya wilaya ya Hai ilipeleka mashine tano za kuvuna na moja ya kupura mpinga kwa lengo la kupunguza adha ya wananchi kuvuna na kupura mpunga kwa kutumia mikono.
“Lengo jingine la kutolewa kwa mashine hizi ilikuwa ni kuongeza chanzo cha mapato kwa wananchi wa kijiji cha Mijongweni ,mashine tatu zenye thamani ya Sh Mil 222.5 zilikuwa ni Combine Harvester aina ya Kubota , mbili aina ya Daedong na moja ya Kupura mpunga (Paddy thresher) zenye thamani ya Sh Mil 152.8”alisema Valeria.
Alisema katika kuendeleza ubadhilifu watu hao wanadaiwa kushindwa kusimamia matumizi ya mashine hizo  ambapo inadaiwa wajumbe wa bodi walipangiana zamu ya kusimamia mashine izo wakati wa zoezi la uvunaji kwa maslahi yao binafsi huku wengine wakivuna nyakati za usiku bila kuwasilisha hesabu za mavuno hayo kwa uongozi.
 “Mfano Mayunga Mathayo anatuhumiwa kuvuna nyakati za usiku na kutowasilisha hesabu za fedha alizokuwa anapata ,hali iliyosababisha afukuzwe kuwa mjumbe wa bodi.Mayunga pia aliuza Hydrolic pump (Orignal) aina ya Kubota yenye thamani ya sht Mil 5 ya mashine namba tisa ya kuvuna mpunga na kufunga pump isiyo na ubora kwenye mashine hiyo ambayo kwa sasa imeharibika.”alisema Valeria.
Valeria alisema fedha zilizokuwa zinapatikana shambani zaidi ya asilimia 50 zilifanyiwa matumizi shambani na wakati mwingine fedha zote zilitumika huko huko shambani bila kufikishwa ofisini na hata zilizofikishwa bado zilipangiwa tena matumizi.
“Baada ya fedha kufanyiwa matumizi zilizobaki zilipelekwa SACCOS ya jitegemee na kutolew wakati huo huo kwa matumizi mengine yasiyo na kibali wala vithibitisho vyovyote ,mfano Oktoba 18 ,2016 kiasi cha sh 810,000 ziliingizwa kwenye akaunti na tarehe hiyo hiyo Sh 800,000 zikatolewa ,katibu wa Bodi Severa Kimati aliyehusika kuziweka na kuzitoa hakuwa na maelezo ya kutosha zaidi ya kusema alitumwa na mwenyekiti wa Bodi Nuru Ndoma”alisema Valeria.
Alisema fedha ambazo zingetakiwa kuwekwa katika akaunti ya kijiji toka Machi,2016 wakati mashine hizo zikianza kufanya kazi hadi kufikia Juni ,2018 kipindi ambachowalifanya kazi wajumbe wawili kutoka kwenye jamii zilipaswa kuwa Sh Mil 285.6 lakini kiasi kilichopo ni Sh Mil 10.9 ambazo zilipatikana baada ya afisa mtendaji na afisa ugani kuamua kusimamia mashine moja katika kipindi cha mwezi mmoja.
Akizungumza baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ,Mkuu wa wilaya ya Hai,Lenga Ole Sabaya alimuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Hai,Lwelwe Mpina kumkamata aliyekuwa Mkuu wa idara ya Ushirika wa wilaya hiyo , Raphael Mbwambo ambaye alitajwa pia kuhusika katikaubadhirfu huo.
Alisema viongozi wa Bodi, ya Ushirika huo hawakuwa na uhalali kutokana na kwamba hakuna wanahisa wala wanachama waliokaa  na kuwachagua  na kwamba waliteuana kwa maslahi yao binafsi huku akitaka fedha zote zilizopotea kurejeshwa.
“HAwa viongozi wa Bodi kwa kushirikiana na wajumbe wa serikali ya kijiji warudishe fedha walizoiba za wananchi wanyonge wa kijiji cha Mijongweni ,Nimeelekeza wasiingie kwenye ofisi yoyote ya umma,hawa ni waharifu kama waharifu wengine hadi itakapothibitika vinginevyo.”alisema Ole Sabaya.
Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo ,Nuru Ndomba  na Katibu wake wake  Severa Kimati  pamoja na wajumbe wengine, Salama Amani,Sadiki Msangi, Abuu Musa na D eogratius Bruno,.
Wengine ni Alex Mkwizu, Mashati Amani, Bakari Malola, Adamu Mdaki,Mayunga Mathayo ,Abdalah Dhamiri,Richard Msele,Ramadhan Miraji ,Miraji Araba na Koswai Mrisho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza wakati wa mkutano wa utoaji wa taarifa ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa na mkuu huyo kuchunguza ubadhilifu wa fedha za Ushirika wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwahoji baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Mijongweni kuhusiana na ubadhilifu uliofanyika katika Ushirika huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya ,akizungumza juu ya maamuzi yaliyochukuliwa mara baada ya kamati aliyoiunda kuwasilisha taarifa yake.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini juu ya maamuzi yaliyochukuliwa na Mkuu huyo wa wilaya .
Baadhi ya wananchi wakionesha mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wera akizungumza katika mkutano huo.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mijongweni ,Omary Mohamed akizungumza kwa niaba ya wananchi wengine katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akitizama baadhi ya mashine zilizotolewa kwa Ushirika huo ambazo zinatajwa kutumika huku mapato yake hayajulikani yalipo.
Moja ya Mashine hizo ikiwa tayari imeharibika baada ya kuondolewa Roller inayotumika kwa ajili ya kutembelea.
Mashine mpya ya Ushirika huo ambayo haijaanza kutumika bado.
Baadhi ya watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha za Mradi wa Ushirika huo wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada ya kukamatwa wakiwa eneo la mkutano.

Thursday, August 30, 2018

WAZIRI LUGOLA MGENI RASMI MKUTANO MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, JIJINI DODOMA.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, wakati Waziri huyo alipokua anawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo kwa akili ya kufungua kikao kazi cha Makamanda wa Jeshi hilo. Wakati Makamanda hao wanajitambulisha, Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda hao kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno na Uokoaji. Hata hivyo, makamanda hao baadaye waliruhusiwa kuingia ukumbini kuendelea na kikao. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, (CGF) Thobias Andengenye, na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,  Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akizungumza na Makamanda wa Jeshi lake katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao hicho ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia). Katika kikao hicho, Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda waliohudhuria kikao hicho kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno Uokoaji, hata hivyo baadaye aliwaruhusu kuendelea na kikao hicho.
.

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akizungumza na Makamanda wa Jeshi lake katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao hicho ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia). Katika kikao hicho, Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda waliohudhuria kikao hicho kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno na Uokoaji, hata baadaye aliwaruhusu kuendelea na kikao hicho
 Sehemu ya Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliofukuzwa kikaoni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), katika Kikao Kazi cha Jeshi hilo kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo. Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda hao waliohudhuria kikao hicho kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno na Uokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Kikao Kazi chao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo. Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda waliohudhuria kikao hicho kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno na Uokoaji.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Kikao Kazi chao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo
 Sehemu ya makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Kikao Kazi chao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo
  Sehemu ya makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Kikao Kazi chao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo.
.

 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola (Mb), mara baada ya kufungua rasmi Kikao cha Makamanda wa Jeshi hilo katika ukumbi wa Bwaro la FFU, Jijini Dodoma.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kushoto-waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima (wapili kulia), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (watatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na makamanda wa Jeshi hilo, baada ya Waziri Lugola kufungua kikao kazi chao, kilichofanyika katika ukumbi wa polisi, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Patrobas Katambi (watatu kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (wapili kulia), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wapili kushoto), Makamishna na Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mara baada kufungua rasmi Kikao cha Makamanda wa Jeshi hilo katika ukumbi wa Bwaro la FFU, Jijini Dodoma
(Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

Tuesday, August 28, 2018

SHILOLE (SHISHI BBY) NA FUTE WAZINDUA RASMI RIWAYA YAO YA BROKEN HEART ,NDANI YA DUKA LA VITABU LA MAK BOOKS AND BRAINS MLIMANI CITY DAR.

Kuhusu BROKEN HEART: Hakuamini mahusiano yake na mtu aliyempenda yaishe kwa yeye kudumbukizwa kwenye dimbwi la msongo wa mawazo, aliyempenda aligeuka kuwa adui.
'Mapenzi ni kitu ambacho kinaweza kukufanya chizi, sihitaji tena mwanaume maishani mwangu.' Alizungumza.
Lakini maisha ni safari, na akiwa katika safari ya maisha alijikuta akizama kimapenzi kwa mwanaume mwingine, mwanaume aliyedhani ni tofauti na waliopita.
Shilole A.K.A Shishi Baby Kulia akiwa pamoja na Jackson  Fute kuzindua rasmi riwaya waliyo andilka pamoja inayokwenda kwa jina la Broken Heart, uzinduzi huo ulifanywa ndani ya Duka la vitabu la Mak Books and Brains Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Bwana Jackson Fute (Kushoto) akiongea na waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua riwaya waliyo andika na Shilole.
Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Bongo Movie na sasa Mtunzi wa vitabu Bi. Zena Yusuf Mohamed Maarufu kwa jina la Shishi Baby, akielezea kwa ufupi namna alivyopata wazo la kuandika Riwaya ya Broken Heart kuwa inalenga historia yake ya kweli kabisa na kuongeza kuwa amefurahi kumshirikisha mwandishi chipukizi Bw. Jackson Fute na kazi imeenda vizuri. pia aliwaomba watanzania wamuunge mkono kwani kitabu kinauzwa kwa Tsh 15,000 tu na Online Ebook ni Tsh 3,000 kinapatikana kote Duniani.
Mhariri wa Riwaya ya Broken Heart Bi Zuhura Seng'enge maarufu kwa jina la The African Lioness ambaye pia ni Mshairi, Mtunzi, Mwandishi na Mfasiri akielezea namna alivyo ipokea kazi ya kuhariri Riwaya hiyo na kukili kwamba ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya kazi hiyo. "Moja ya changamoto nilizozipata wakati nahariri Riwaya hii ilikuwa ni utamu wa simulizi zilizokuwemo ndani mpaka nikachelewa kumaliza kazi hiyo kwa muda kutokana na kunogewa na visa mkasa"
alisema Zuhura.
 Waandishi wa Habari wakiendela kufanya mahojiano na Shishi Baby pamoja na Jackson Fute wakati wa uzinduzi wa Riwaya hiyo.
 Mhariri wa Riwaya hii  Bi. Zuhura Seng'enge akipokea Riwaya yake kutoka kw Shishi Bby
 Mmoja wa wadau Bw. Hassan A.K.A Double D wa Uswahilini Matola  nae akipokea Riwaya yake
 Bw. David Kisamfu  Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
 Mtaalam wa picha za mnato Bw. Zajilu Zaid nae akionesha Riwaya yake ya Broken Heart baada ya kuinunua
 Anaitwa Silver (kushoto) Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
Bw. Francis nae Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
 Ukiingia tuu katika Duka la vitabu la Makbooks Brains Mlimani City  utakutana na Riwaya ya Broken Heart
 Mmoja wa wanunuzi akiwa anasoma Dibaji
 Kulia ni mmoja wa wafanyakazi katika Duka la vitabu la Mak Books and BrainsBi. Fina akimpa mfuko wenye Riwaya ndani Shishi Baby ili amkabidhi mnunuzi.
Hili hapa ndio duka la vitabu la Mak Books and Brains lililopo Mlimani City hapa ndipo utapata Riwaya ya Broken Heart. Picha zote na Fredy Njeje