Thursday, January 31, 2013

KAMPUNI YA BE FORWARD YAKABIDHI ZAWADI YA GARI KWA MTEJA WAO ALIYESHINDA ‘PHOTO CONTEST’


Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya magari ya Be Forward Tanzania, Mashariki na Kati Oliver Philbert akizungumzia kuzinduliwa rasmi kwa Kampuni ya Be Forward hapa Tanzania na pia tukio la kampuni hiyo kukabidhi zawadi kubwa ya gari kwa mmoja wa wateja wake kutoka Uganda aliyeibuka mshindi wa shindano la photo contest..
Amesema Be Forward ni kampuni inayojihusisha na uuzaji magari nchini Japan kwa njia ya mtandao wa Internet, na ili kuongeza ufanisi na Imani kwa wateja wetu tumefungua kampuni Tanzania ambayo inajishughulisha na huduma kwa wateja.
Be forward Tanzania itatengeneza ajira zaidi ya 1,000 kwa watanzania hivyo kuipunguzia mzigo serikali na kuongeza kipato kwa watanzania.
Kampuni hiyo iliendesha ‘Photo Contest’ ambapo wateja wake walitakiwa kutuma picha za magari walionunua kutoka katika kampuni hiyo, na kisha ziliwekwa katika mtandao wa Be Forward na katika ‘Kurasa yao ya Facebook na watu kuzi’like’.
Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akizungumza machache ambapo amewataka watanzania kujisikia huru kufika na kufanya kazi na kampuni hiyo, pia amempongeza mteja wao kutoka Uganda aliyeibuka kuwa mshindi wa zawadi ya gari na kuahidi kuwa wanafanya maandalizi ya kuendesha kitu kingine tena kwa ajili ya wateja wao.
Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akimkabidhi mfano wa funguo ya gari Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan (kushoto).
Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan akitoa shukrani kwa washiriki wote wa nchi mbalimbali walioshiriki na hatimaye yeye kuwa mshindi na pia kampuni ya Be Forward kwa kubuni shindano la “photo Contest’ na kuwataka wananchi wa Afrika Mashariki hasa Tanzania ambapo kampuni ndio imefunguliwa wasisite kujitokeza na kufika kwenye ofisi zao kujipatia huduma.
Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa ( wa pili kulia) na baadhi ya wageni waalikwa wakimsikiliza mshindi wa shindano hilo Bw. Kakuru Adnan (hayupo pichani) wakati wakati akitoa shukrani zake kwa kampuni hiyo.
Pichani Juu na Chini ni Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akikabidhi zawadi kwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa (wa pili kushoto waliochuchuma) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ofisi ya Tanzania na wageni waalikwa.
Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa akimkabidhi rasmi mshindi wa shindano la picha ambaye pia ni mteja wa kampuni hiyo gari aina ya Toyota CorollaBw. Kakuru Adnan kutoka nchini Uganda.
Mshindi wa shindano la gari lililoendeshwa na kampuni ya Be Forward Bw. Kakuru Adnan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni hiyo pamoja na baadhi ya wakuu wa vitengo na idara mbalimbali za kampuni hiyo kutoka nchini Japan.
Rais wa kampuni ya Be Forward kutoka Japan Bw. Hironori Yamakawa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ofisi za Tanzania na wa makao makuu nchini Japan.
Bw. Kakuru Adnan akitoa tabasamu bashasha baada ya kuliwasha gari hilo.
Bw. Kakuru Adnan akiondoka na gari lake alilojishindia tayari kuanza safari ya kurudi nchini Uganda. Hafla hiyo imeandaliwa na kampuni ya EndePa event planners waliopo Mikocheni B, Mlandege Street.

Wednesday, January 30, 2013

Dkt. Migiro afanya ziara wilaya mpya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao wako kando kando ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya Burundi.Dkt. Migiro pia amewaasa wananchi wa maeneo hayo kuwa na umoja,mshikamano na upendo ili kuweza kuhimarisha mambo mbali mbali ya Wilaya.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha waliokuja kumpokea.
Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimuaga Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwapungia watoto wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa Kijiji hicho jana.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi (kulia) akikabidhi Taarifa ya Utekelezani wa Ilani ya Uchaguzi kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea ripoti ya Chama Wilaya ya Buhigwe,kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Buhigwe,Bi. Bennosa Mjema.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo,Ndg. Elisha Bagwanya
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Buhigwe wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha sambamba na Bibi Buchiro Edmas Kapina wakati wa Ziara ya kutembelea wilaya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akilakiwa kwa shangwe na kinamama wa Kijiji cha Kilelema.
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Kilelema,Everist Samson akisoma taarifa ya kijiji kuhusiana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kijiji hizo zikiwemo zile za kuvamiwa na majambazi wanaotoka nchi jirani ya Burundi.Kijiji hiki kipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi kwa kijiji cha Buhema Mkoani Lutana,nchini Burundi.

Wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilelema,Benedict Samson Mahuta (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya eneo la Soko kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati),alietembelea eneo litakalojengwa soko la Kimataifa katika Kijiji hicho cha Kilelema.
Picha ya Pamoja na Watendaji wa Kijiji cha Kilelema.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (pili kulia) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi Charles (kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi unaotenganishwa na sehemu ya Mto Maragarasi.

BENKI YA KCB TANZANIA IMETOA MSAADA KWA SHULE ZA MSINGI NA HOSPITALI JIJINI DAR

 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa katikati akimkabidhi moja ya msaada wa madawati kati ya 89 Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Makumbusho Bi.Benedicta Lyimo,yaliyotolewa na benki hiyo yenye thamani ya Milioni 17.4,anaeshuhudia kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye.
 ) Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa kushoto na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye wakioneshwa moja ya jengo la wodi ya kujifungulia wakinamama na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza Dare s Salaam mara baada ya kukabidhi rasmi vifaa mbalimbali vikiwepo vitanda vya kujifungulia vine vyote vikiwa na thamani ya Milioni 7.4 kwa ajili ya kituo hicho.   
  Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa  akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye,wakati alipokuwa akikagua moja ya vitanda kati ya vinne vya kujifungulia wakina mama kabla ya kuvikabidhi rasmi kwa uongozi wa Hospitali ya Sinza iliyopo jijini Dar es Salaam vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 7.4 ,kushoto Meneja Masoko wa benki hiyo Emelda Gerald.
 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa  akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makumbusho alipofika shuleni hapo kutoa  msaada wa madawati  89 na vifaa vya kusomea,vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 17.4 kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye.
 Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Bi.Christine Manyenye na Meneja Masoko wa benki hiyo Emelda….wakimsikiliza Muuguzi wa Hospitali ya Sinza jijini Dar es Salaam Rachel Mshana mara walipofika hospitalini hapo kukabidhi msaada wa vitanda vine na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kujifungulia akinamama wajawazito vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 7.4.
 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa kulia akimkabidhi moja ya msaada wa madawati na meza  Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kibamba   yenye watoto wenye ulemavu wa akili Bi.Asia Mpate,yaliyotolewa na benki hiyo yenye thamani ya Milioni 17.4,katikati  ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye.
 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa  akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza ya jijini Dares Salaam,Benedict Luoga moja ya kitanda kati ya vinne Salaam vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 7.4 vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kujifungulia akinamama wajawazito. 

Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa kulia akimsikiliza jambo Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kibamba   yenye watoto wenye ulemavu wa akili Bi.Asia Mpate,baada ya kumkabidhi rasmi msaada wa madawati 89 yenye thamani ya Milioni 17.4,wapili kulia k Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye,na kushoto ni Mwalimu msaidizi wa shule hiyo Bi.Mwajabu Minja.

 Na Mwandishi wetu
Shule ya Msingi ya Kibamba  katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam inakabiliwa na  uhaaba wa madawati 500,  jambo linalowalazimu wanafunzi  wa shule  hiyo kukaa chini wakati wakifundishwa darasani.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Asia Mpate alibahanisha hayo jana na kusema  kuwa shule yake yenye wanafunzi 1,950,kuliwa na  madawat 320  na madarasa 13 tu.

Mwalimu Mkuu huyo alikuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa misaada na Benki ya  KCB iliyotoa madawati 25, meza  tatu,   viti vya walimu sita, madafyari 235 na peni 200 , vyote vikiwa na thamani ya Sh, Milioni 5 kwa shule hiyo.

Alisema kuwa uhaba  mkubwa wa madawati katika shule yake kumepelekea utoro mkubwa kwa wanafunzi wake  kwani wanafunzi wake hulalamikia  hali mbaya na ugumu wa  kukaa chini sakafuni.

Mpate  amesema kuwa wanafunzi wengi wa shule yake wamechanganyikiwa na hali hiyo  na hivyo huamua kutohudhuria masomo, jambo linaofanya  ufanisi  mdogo wa elimu kwa wanafunzi wake.

" Utoro ni mkubwa katika shule yetu kwa sababu hali halisi ya madarasa ni  ya kutisha, hatuna madarasa ya kutosha wala vitendea kazi . Tunashukuru Benki ya KCB kwa msaada wao ambao tunaamnini kuwa  utatusaidia kuboresha  kiwango cha elimu  katika shule  yetu", alisema mwalimu mkuu huyo..

Kwa upende wake Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi wa benki hiyo,  Dk Edmund  Mndolwa alisema kuwa  msaada huo  ni sehemu ya wajibu wake  wa benki kusaidia jamii na kwamba benki yake imejidhatiti kusaidia kuinua  kiwango cha elimu  nchini  Tanzania.

Aliwashauri wanapokea misaada ya benki hiyo kutumia ipasavyo na inavyotakiwa   misaada  inayotolewa na benki yake.

Kwenye hafla hiyo pia  benki ya KCB ilitoa msaada wa madawati 64 yenye thamani ya Sh. Milioni  tano kwa Shule ya Msingi ya Makumbusho pia ya jijini.
Wakati huo huo  hopsitali ya  Sinza  ya jijini Dar es Salaam imepokea msaada wa  vifaa vya hospitali vyenye thamani ys Sh. Milioni 7.4 kutoka kwa Benki ya KCB katika hafla  iliyofanyika kwenye hopsitali  hiyo jana.

Dokta Mwandamizi wa  hospitali  hiyo, Dk Benedict  Luwoga  alishukuru benki hiyo kwa msaada huo  na kusema kuwa  vifaa hivyo vilikuja kwa wakati na kuvitaja  vifaa hivyo ni  pamoja na vitanda vinne  vya kuzalisha kwa mama  wajawazito.

Alisema kuwa  hospitali yake ilizidiwa uwezo  kwa sababu ilikuwa na   vitanda  viwili tu vya kuzalisha mama wajawazito , kwa hiyo vitanda hivyo vinne zaidi ilikuwa ni ukombozi mkubwa kwa hospitali yake.

"Tunashukurui Benki ya KCB kwa msaada huo, umekuja kwa wakati ambapo hospitali ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi. Amezitaka kampuni zingine ziige mfano wa benki ya KCB", alisema Dk Luwoga.Monday, January 28, 2013

UN YAENDESHA MAFUNZO KUHUSU SHUGHULI ZA UNDAP NA HAKI ZA BINADAMU KWA WAANDISHI WA HABARI VISIWANI ZANZIBAR


Afisa habari ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akieleza nia ya Umoja wa Mataifa Tanzania kuendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar juu ya Haki za binadamu na jinsi Mpango wa msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP) unavyoshirikiana na Serikali ya Zanzibar katika maeneo matatu muhimu ambayo ni Uchumi, Kupunguza umaskini na Utawala na uwajibikaji. Semina hiyo imefanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View visiwani Zanzibar.
Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan akitoa hotuba ya makaribisho katika mkutano na waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar ambapo amesema wanatarajia kupata mawazo mengi zaidi ya kujenga kutoka kwa waandishi ambapo yatasaidia Umoja wa Mataifa pamoja na Serikali kuihudumia nchi kwa upeo wa juu zaidi.
Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga akizungumza na waandishi wa habari wa visiwani Zanzibar kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wao kama UN katika kutekeleza hoja za mipango wa maendeleo (UNDAP) kutokana na kuchelewa kupewa majibu na uchelewashaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo ambapo ameelezea Mpango Mkakati wa UNDAP visiwani Zanzibar ikiwemo kutoka ufafanuzi wa mafanikio pamoja na changamoto zinazoukabili mpango huo.Amesema mpango huu ni wa pamoja kwa ajili ya Tanzania unaendena na mafanikio ya malengo ya maendeleo ya kimataifa ambapo unachukua nafasi ya program za pamoja na miradi mingi inayodhaminiwa na UN chini ya Model ya misaada ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kwa mpango wa kazi moja ulioshikamana kwa ajili ya mifuko ya fedha, program na wakala zote za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ya siku moja wakimsikiliza Afisa Mawasilano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.
Katibu wa Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Hamisa Mmanga Makame akitoa somo katika mafunzo hayo ambapo amezungumzia masuala ya Haki za Binadamu, umuhimu wa kuzingatia jinsia na wajibu wa vyombo vya habari katika kuleta usawa.
Afisa Mipango mwandamizi wa shirika la kazi duniani (ILO) Anthony Rutabanzibwa ambapo amevipongeza vyombo vya habari vya Afrika Mashariki kwa kutoa kipaumbele katika habari zinazohusu haki za binadamu na kuwataka waandishi kuzingatia zaidi habari za kiuchunguzi ili kuwa na uhakika zaidi na yale wanayoaandika ikwemo kujua chanzo cha habari unayoitoa.
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin akielezea mada ya umuhimu wa mawasiliano kwa maendeleo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya habari na serikali kwa ujumla kubadilisha sera zinazosimamia vyombo hiyo ili ziweze kutoa fursa kwa waandishi kuwa huru katika uandishi na kuripoti habari bila kubanwa.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar Hassan Khatibu, Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan, Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga, Mwezeshaji wa mafunzo hayo mwandishi mkongwe Salim Said Salim na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin.
Rais wa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Kenneth Simbaya akitoa maoni yake kuhusiana na nini kifanyike katika kuboresha tasnia ya habari ambapo ameshauri mafunzo kuendelea kutolewa si tu kwa waandishi pia kwa wamiliki wa vyombo vya habari.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya waandishi ws habari wa visiwani Zanzibar wakichangia mawazo yao wakati wa mafunzo hayo.
Afisa mipango wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku yaliyoendeshwa na Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akijadili jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa mafunzo hayo.