Saturday, September 30, 2017

DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Septemba 30,2017 ameweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.

Mbali ya kuweka jiwe la msingi pia ameendesha harambee kwa ajili ya kupata shilingi milioni 200 kwa ajili kukamilisha ujenzi huo,ambapo wazazi na walezi wameshiriki katika harambee hiyo. 

Akizungumza katika shule hiyo,Matiro aliwapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi kwa kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule hiyo ambayo imejizolea sifa lukuki kwa utoaji wa elimu bora. 

“Shule hii imejizolea sifa nzuri,hii ni miongoni mwa shule bora kabisa nchini,kila mzazi anapenda mtoto wake asome kwenye shule nzuri,ukifika Shinyanga ukauliza shule gani nzuri,utatajiwa shule hii,nimeambiwa siri ya mafanikio haya inatokana na maono na utayari wa wazazi na marafiki kuisaidia shule hii”,alifafanua Matiro. 

“Sisi kama serikali tunaunga mkono sekta binafsi,kutokana na shule hii kufanya vizuri,ni ukweli usiopingika kuwa imeleta ushindani mkubwa kwa shule zetu za serikali,nasi kwa upande wa shule zetu za serikali hatuna budi kuiga, tuje kujifunza nini wanafanya hapa Little Treasures”,aliongeza Matiro. 



Aliwaasa wazazi na walezi mkoani Shinyanga kupeleka watoto shule kwani urithi pekee kwa watoto ni elimu na wala siyo mali ambazo hupotea kirahisi sana. 

Katika hatua nyingine alizitaka shule za taasisi binafsi kutoza ada zinazoendana na hali ya uchumi wa wazazi huku akiwasihi wazazi kutoa ushirikiano katika shule akitolea mfano wa shule ya Little Treasures ambayo imekuwa karibu zaidi na wazazi na walezi wa wanafunzi. Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic alisema ili kukamilika kwa jengo la bwalo la chakula jumla ya shilingi milioni 200 zinahitajika na tayari uongozi wa shule umetenga shilingi milioni 50 hivyo bado zinahitajika shilingi milioni 150. 

Naye Meneja wa shule hiyo,Wilfred Mwita alisema pindi jengo hilo litakapokamilika litatumika kama sehemu ya wanafunzi na wafanyakazi wa shule hiyo kula chakula lakini pia kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo michezo na mikutano. 

Akisoma risala,Mkuu wa shule hiyo,Paul Kiondo alisema shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ina wanafunzi wa bweni na kutwa ilianza na wanafunzi wanne pekee na sasa ina jumla ya wanafunzi 662 kati yao,wavulana ni 304 na wasichana 318 na imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali. 



Jumla ya shilingi milioni 15 zimepatikana katika harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula,ambapo wazazi na walezi pamoja na marafiki wa shule hiyo wamechangia huku Mkuu wa wilaya Shinyanga Josephine akitoa shilingi Milioni 2 pamoja na mifuko 30 ya saruji. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa pili kulia) akiwasili katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisoma maandishi baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures. 
Maandishi yakisomeka kwa lugha ya Kiingereza yakiwa na maana ya 'Jiwe la Msingi limewekwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro leo Septemba 30,2017'. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimwagilia maji mti alioupanda katika shule ya Little Treasures. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiondoka katika eneo panapojengwa jengo la Bwalo la chakula katika shule ya msingi Little Treasures.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Tilulindwa Sulusi. 
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakimwongoza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika maaandamano kuelekea eneo la mkutano kwa ajili ya harambee kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula katika shule hiyo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika maandamano hayo.Wa kwanza kushoto mbele ni Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic,kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Tilulindwa Sulusi. 
Meza kuu: Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Kulia ni Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic,kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Tilulindwa Sulusi. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika shule ya msingi Little Treasures ambapo aliipongeza shule kuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia wanafunzi. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika shule ya msingi Little Treasures ambapo alisema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuinua kiwango cha elimu. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwasisitiza wazazi kupeleka watoto shule kwani ndiyo urithi unaofaa kwa watoto. 
Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita akizungumza wakati wa harambee hiyo ambapo aliwaomba wazazi na walezi wa wanafunzi pamoja na marafiki kuendelea kushirikiana na shule hiyo. 
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akizungumza wakati wa harambee hiyo ambapo aliishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana shule hiyo ili kuboresha kiwango cha elimu mkoani Shinyanga na nchi kwa ujumla. 
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Little Treasures,Tilulindwa Sulusi akitoa neno. 
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akisoma risala. 
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza ngoma ya Kijaluo mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 
Wanafunzi wakicheza muziki. 
Wazazi na walezi waliohudhuria mkutano huo wa harambee kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula. 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Said Pamui naye alikuwepo katika harambee hiyo ambapo alichangia shilingi 500,000/- kusaidia ujenzi wa bwalo la chakula katika shule hiyo. 
Wazazi wakipiga makofi. 
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza ngoma ya Kikurya. 
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiimba ngonjera. 
Wazazi na walezi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea. 
MC Mama Sabuni akifanya yake. 
Wazazi wakiwa katika eneo la tukio. 
Tunafuatilia kinachoendelea... 
Walimu wa shule ya msingi Little Treasures wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri. 
Wazazi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea. 
Waandishi wa habari wa magazeti ya Daily News na Habarileo,Suleiman Shagata na Kareny Masasy wakiwa katika eneo la tukio. 
Waandishi wa habari John Mponeja wa Channel Ten na Getruda Mallya wa Radio Faraja wakifurahia jambo. 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Said Pamui (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi Little Treasures Tilulindwa Sulusi wakiondoka katika shule hiyo baada mkutano wa harambee. 
Picha ya kumbukumbu mbele ya jengo la utawala shule ya msingi Little Treasures.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

SEKTA BINAFSI ZAONGEZA NGUVU KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA SINGIDA.

Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Singida Dkt Mohamed Mbalazi akitoa mada katika mkutano ulijadili uboreshaji wa ushirikiano baina ya serikali na wadau wa sekta binafsi zinazotoa huduma ya Afya Mkoani Singida.
Afisa Lishe Mkoa wa Singia Teda Sinde akifafanua jambo katika mkutano ulijadili uboreshaji wa ushirikiano baina ya serikali na wadau wa sekta binafsi zinazotoa huduma ya Afya Mkoani Singida.
Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Mkoa wa Singida Dkt Evans Mlay (wa kwanza kushoto) akipitia dondoo, kabla ya kuwasilisha mada iliyoonyesha mchango mkubwa wa wadau Sekta ya Afya katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu Singida, Kulia kwake ni Afisa Mradi wa AMREF Mkoa wa Singida Donathapeace Kayoza.
Mwakilishi wa Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Cosmas Sikali akizungumza na wadau wa sekta binafsi zinazotoa huduma katika Mkoa wa Singida.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Salum Manyatta akisikiliza kwa makini maoni na michango mbalimbali ya wadau ambao ni taasisi na mashirika binafsi yanayotoa huduma za Afya Mkoani Singida.
Meneja Mradi wa EGPAF Kanda ya Kati Dkt Joseph Obedi akiandika baadhi ya mapendekezo ya kuboresha ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika uboreshaji wa huduma za Afya Mkoa wa Singida.




Wadau mbalimbali wa sekta binafsi wameweza kuongeza nguvu katika kuboresha sekta ya Afya Mkoani Singida kutokana na ushirikiano mzuri ulipo baina yao na serikali.

Hayo yamebainishwa katika mkutano maalumu wa siku mbili uliohitimishwa jana Mjini Singida, ambapo viongozi wa serikali, taasisi na mashirika 15 yanayotoa huduma za Afya na Ustawi wa jamii Mkoani hapa wamejadiliana namna ya kuboresha ushirikiano baina yao.

Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Singida Dkt Mohamed Mbalazi amesema katika mapambano dhidi ya Ukimwi na Virusi vya Ukimwi (VVU) Mkoani hapa, Sekta binafsi zimekuwa na mchango mkubwa.

Dkt Mbalazi amesema wadau hao wameweza kutoa dawa za kupunguza makali ya VVU, tiba lishe, mafunzo kwa watoa huduma wa afya, ufuatiliaji wa watumia wa dawa za VVU pamoja na kuandaa takwimu jambo ambalo limeboresha mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

“Sisi kama watendaji wa serikali tunathamini na kutambua mchango wa wadau wa sekta afya kwakuwa ni nguzo muhimu sana, mfano wadau wetu shirika la EGPAF, wametenga bilioni 1.6 kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi na maambukizi ya VVU” Mkoani Singida”, amesema na kuongeza kuwa,

“Fedha hizo zitaongea nguvu pale ambapo kuna changamoto au bajeti inakuwa haitoshelezi, lakini pia tunaendelea kutoa wito kwa wadua wengine waendelee kuongea nguvu na wigo wa ushirikiano kwakuwa lengo letu ni moja yaani kumsaidia mwananchi apate huduma bora za afya”, amesisitiza Dkt Mbalazi.

Naye Afisa Lishe Mkoa wa Singida Teda Sinde amesema wadau wamekuwa watekelezaji wazuri wa masuala ya Lishe Mkoani hapa hasa kwa ngazi ya jamii hivyo ushirikiano kati yao umekuwa wa manufaa makubwa.Teda amesema mkutano huo wa wadau umewawezesha watendaji na viongozi wa serikali kuelewa kwa upana zaidi kazi wanazofanya wadau pamoja na changamoto wanazopitia ili waweze kusaidiana katika kuboresha hali ya Lishe Mkoani hapa.

“Mkutano huu umeongeza na kuboresha ushirikiano baina yetu na wadau wetu ambao wengi wao wanatoa chakula lishe na elimu ya lishe kwa akina mama wajawazito, watoto wenye umri wa miezi sita mpaka 59 na akina mama wanaonyonyesha watoto chini ya miezi sita”, ameeleza Teda.

Ameongeza kuwa mkutano huo umeweza kusaidia katika kupanga mikakati ya utoaji huduma ili kuepusha wadau wanaotoa huduma ya aina moja kutoelekeza nguvu katika maeneo yanayofanana au ambayo hayana uhitaji mkubwa kuliko mengine.

Akifungua Mkutano huo Mwakilishi wa Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Cosmas Sikali aliwataka wadau kujadili sera, sheria, kanuni, maeneo ya kipaumbele katika miradi mbalimbali, mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa mipango mikakati inayosisitiza ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na binafsi.

Sikali amesema endapo nguvu hizi kwa pamoja zitaunganishwa na kuratibiwa vizuri kwa kiasi kikubwa changamoto zilizopo katika sekta ya afya na ustawi wa jamii pamoja na maradhi kwa wananchi yataweza kupungua.Ameongeza kuwa serikali peke yake haitaweza kufikia malengo ya kupunguza vifo vya watoto, akina mama wajawazito na kuweza kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, pamoja na kuboresha afya ya mazingira na kupata maji safi na salama bila kushirikiana na Sekta binafsi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Salum Manyatta amesema mkutano huo umeshirikisha wadau wote muhimu wanatoa huduma za afya na ustawi wa jamii mkoa wa Singida.Dkt Manyatta amesema mkutano huo umeweka malengo na maazimio ya pamoja na wadau wa sekta binafsi ili kuimarisha sekta ya afya na ustawi wa jamii Mkoani Singida.

TSN,TBC ZA TWAA TUZO ZA DSE 2017 PIA ZIPO NMB, TBL NA STANDARD CHARTERED BANK

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  ya Chombo bora cha habari mwaka 2017 (Magazeti), Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk. Jim Yonazi (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSEMoremi Marwa. (Picha:Mroki Mroki/TSN Digital).
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  ya Chombo bora cha habari mwaka 2017 (Digital), Kaimu Mkurugenzi wa habari na Matukio wa TBC, Prudence Costantine (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSEMoremi Marwa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani (kulia) baada ya Benki hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSEMoremi Marwa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania,(TBL), Bruno Zambrano (kulia) baada ya Kampuni hiyo kuibuka mshindi katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSEMoremi Marwa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Dorothy  Mwanyika akimkabidhi Tuzo  kwa Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB anaeshughulika na Mikakati na mahusiano ya wawekezaji, Anna Mwasha (kulia) baada ya Benki hiyo kuibuka mshindi wa pili katika tuzo za mwaka huu zinazotolewa na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa wanachama na wadau wake. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSEMoremi Marwa.
 Wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered wakiwa katika picha
 wafanyakazi wa TBL nao wakifurahia tuzo yao.
 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk. Jim Yonazi akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa habari na Matukio wa TBC, Prudence Costantine (kulia) baada ya Vyombo hivyo vya habari vya serikali kushinda tuzo za DSE 2017. 
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wakifurahia tuzo yao.
 Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa TSN na majaji katika tuzo za DSE.
 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk. Jim Yonazi akiwa na
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani (kulia. 
 Picha ya pamoja ya washindi na watumishi katika taasisi zao.
Wageni mbalimbali waliohudhuiria hafla hiyo wakiwa ukumbini wakati wa utoaji tuzo.