Wednesday, November 30, 2016

BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YANGAMIZI ZAIDI YA TANI 62 ZA BIDHAA ZILIZOHARIBIKA

  Wafanyakazi wa gari ya mizigo wakishusha bidhaa zilizoharibika katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja tayari kwa kuangamizwa katika zoezi ililosimamiwa na Bodi ya Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) wakiwa katika maandalizi ya kuharibu chakula na dawa zilizoharibika na kupitwa na wakati katika dampo la Kibele.
 Magari ya mizigo yakishusha shehena za bidhaa mbovu zilizokamatwa na maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi katika maghala na maduka Zanzibar.
 Mkuu wa operesheni wa uangamizaji wa bidhaa mbovu wa ZFDB ndugu Abdulaziz Shaib Mohd akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuangamiza bidhaa hizo katika dampo la Kibele
Kijiko cha Manisapaa ya Zanzibar kikiharibu bidhaa mbovu na zilizomaliza muda wake wa matumizi katika dampo la Kibele Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar                   
Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeangamiza zaidi ya tani 62 za vyakula vibovu na vilivyopitwa na wakati katika zoezi lililofanyika Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Mkuu wa Idara ya Biashara na Uendeshaji wa ZFDB Ndugu Abdulaziz Shaib  Mohd amesema bidhaa hizo mbovu zinatokana na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kujenga matumaini ya kuingiza faida kwa  bidhaa wanazouza bila kuangalia usalama wa bidhaa hizo kwa afya za watumiaji.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamiza bidhaa hizo, Ndugu Abdulaziz ambae pia ni Mkuu wa operesheni wa uangamizaji amesema bidhaa hizo zimegundulika kufuatia operesheni iliyofanywa na Bodi katika maghala na maduka mbali mbali ya Unguja.
Amesema ZFDB ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi kwa matumizi ya wananchi, itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala yanayowekwa bidhaa na kwenye maduka ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa.
Amewataka wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa wananchi wenzao na kujuwa kwamba biashara mbovu ama zilizopitwa na wakati ni sumu na zinaweza kudhofisha afya zao.
Mkuu wa Idara ya Chakula wa ZFDB bibi Aisha Suleiman amesema  mchango mkubwa wa raia wema ndio uliofanikisha kugundulika  bidhaa mbovu na zilizopitwa na wakati katika maduka na maghala mbali mbali.
Hata hivyo amewataka wananchi kujenga tabia ya kuchunguza tarehe ya kumaliza muda bidhaa wanazonunua na wanapogundua bidhaa imepitwa na wakati watoe taarifa katika Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi  ili hatua  za haraka ziweze kuchukuliwa.
Wakati huo huo Afisa Mkuu wa Idara ya Dawa na Vipodozi wa ZFDB Ndugu Mwadini Ahmada Mwadini amesema vipodozi haramu vilivyokamatwa baadhi yake vinakemikali zenye sumu na hazifai kwa afya ya binadamu.
Amewashauri wafanyabiashara wanaotaka kuanzisha biashara ya dawa na vipodozi kushirikiana na Bodi hiyo kwa lengo la kulinda afya za wananchi.
Dawa zilizoangamizwa katika operesheni hiyo ni mafuta ya kula lita 10,105, sukari tani 2.15, mchele tani 26, tende tani 10, bidhaa  mchanganyiko za mboga mboga tani 13, dawa na vipodozi tania tatu.
                                                         

MENEJA WA TANROADS MKOA WA SHINYANGA AELEZEA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOANI KWAKE

   Meneja wa Mkoa wa TANROADS  Shinyanga (katikati) akipewa maelezo juu ya ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi – Maswa (km 50.30) na Mhandisi Mshauri  wa Kampuni ya Kikandarasi ya KYONGDONG Engineering Co. Ltd  ndugu Kim Hyung Gyu
  Ndugu Kim Hyung Gyu – Mhandisi Mshauri  akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mradi wa maendeleo ya kitaifa wa Mwigumbi – Maswa (km 50.30) kwa Meneja wa Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Augustino Wittonde Phillipo.
  Meneja wa Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Augustino Wittonde Phillipo akikagua culvert la dharura yanayo tumika wakati barabara inapokatika kutokana  mafuriko kulia ni Afisa Habari Mkuu wa TANROADS Bi. Aisha Malima
  Kazi za ujenzi katika barabara ya Mwigumbi – Maswa (km 50.30) zikiendelea

Meneja wa TANROADS mkoa wa Shinyanga Mhandisi Wittonde Philipo ameelezea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara mkoani mwake na kueleza kwamba maendeleo ya miradi mkoani   mwake ni mazuri.
Akiongea na Afisa habari wa TANROADS Bi. Aisha Malima, Mhandisi Phillipo alisema kuwa miradi miwili ipo katika hatua za kati na mwisho katika utekelezaji wake.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na Afisa Habari huyo  na ujumbe wake ni barabara ya Mwigumbi – Maswa yenye kilometa  50.30 inayounganisha mkoa wa Shinyanga na Simiyu.Kwa upande wa mkoa wa Shinyanga ni kilometa 16 na kilometa 34 mkoa wa Simiyu. 

Mradi huu umeanza mwaka jana mwezi wa sita na matarajio ni kumaliza Aprili  mwaka ujao. Utekelezaji wa mradi huu ambapo kwa sasa ni asilimia 65 unasimamiwa na Kampuni ya Mkandarasi ya CHICO kutoka China pamoja na  Wahandisi Washauri wa Kampuni ya  KYONDONG Engineering Co. Ltd kutoka Korea ya Kusini, JV CORE  Consulting PLC ya Ethopia, LUPTA Consults Ltd ya Tanzania na ACE Consultants kwa gharama ya shilling billioni 61.461 na inafadhiliwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Tanzania.

Mhandisi Wittonde Phillipo alielezea changamoto kadha zilizojitokeza wakati wa ujenzi wa barabara hizo kuwa ni ukosefu wa maji kwa ajili ya kazi ya ujenzi. Aidha wakati wa masika mkandarasi aliweka jitihada ya kuchimba mabwawa kuhakikisha kazi haisimami kutokana na ukosefu wa maji.
Changamoto nyingine ilikuwa eneo la kujenga barabara ambapo  alitumia fursa kuwashukuru wananchi walio toa ushirikiano wa kutosha na walio vunja nyumba zao bila ya matatizo yeyote.

Mhandisi Phillipo alieleza kwamba barabara hii inaendelea vizuri na kwa sasa mkoa wa Shinyanga una miradi mingi  ambayo imekamilika kwa kiwango cha lami .

Ujumbe huo ulimaliza ziara yake kwa kutembelea mradi wa barabara ya mkoa ya Uhuru ambayo iko eneo la Lubaga inayojengwa kwa fedha za Serikali kwa asilimia mia moja. Barabara hii ya katikati ya mji itakuwa  na upana wa mita 6.5  na sehemu ya watembea kwa miguu na waendesha pikipiki ya miguu miwili na mitatu.

Barabara hii inajengwa na Mkandarasi mzawa JOTAN Engineering ikiwa ni mkakati mojawapo iliyowekwa kuhakikisha nao wakandarasi wazawa wanapewa nafasi katika miradi ya ujenzi wa barabara.

Afisa Habari huyo wa TANROADS alitoa wito kwa wananchi watunze barabara ambazo zinajengewa kwa pesa ya kodi za wananchi na kuomba madereva wahakikishe hawazidishi uzito katika magari kwa lengo la kulinda barabara ziweze kudumu kwa muda uliopangwa.

Alimaliza kwa kusema kwamba alama za barabarani pia zina umuhimu mkubwa na zinaitajika pia kulindwa ili kunusuru maisha ya watu na mali zao kwani zikikosekana zinaweza kusababisha ajali.

Afisa Habari huyo alimtembelea Mhandisi wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga katika ziara ya kikazi iliyolenga kupata habari za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara mkoani humo.

Airtel yazindua huduma za mawasiliano Lindi Vijijini

Huduma hizi mpya za mawasiliano zitawafikia wakazia wa vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo kwa kuwahakikishia wakazi wote wa Lindi vijijini huduma za mawasiliano za uhakika, huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na hatimae kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga alisema “ tunayofuraha kupata huduma za mawasilino hapa cheleweni na vijiji vya jirani.  Airtel kwa kuzindua mnara huu, serikali tunaungano jitiada hizi za kuboresha mawasiliano huku vijiji kwa sasa wakazi wa vijiji hivi mtaweza kutumia huduma ya mawasiliano kwa kufany a biashara zenu za nazi kwa kujitafutia masoko sehemu nyingine lakini pia itasaidia kuondoa tatizo lakutembe na fedha nyingi pale mnapofanya biashara kwa kuwa mtatumia huduma za kifedha za Airtel Money kujichukulia fedha zenu wakati wowote

Mkuu wa wilaya aliongeza kwa kusema “Mawasiliano haya yatasaidia sana wilaya yangu katika kukuza elimu kwa kuwa nitaweza kuwawasiliana na watendaji wangu wote wakati wowote. Sasa nitoe tamko kwamba nimeongea na Airtel ili kutuma ujumbe wa meseji kwa wazazi wote kwa kuwa ndio mtandao unaotumika na wengi hapa katika vijiji vyetu vya ng’apa ng’apa  kuhusu kuandikisha watoto wote waliomaliza shule za msingi waende sekondari,  Airtel wamenikubalia sasa ikiwa  mzazi atakaidi kuitikia wito nitamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfunga”.

Nataka kuona  huduma hii ya Mtandao wa Airtel tunayoizindua leo inaleta tija katika shughuli za uchumi kama vile uzalishaji wa korosho, kusaidia biashara ndogo za kati na kubadilisha maisha ya jamii kwa ujumla.  Napenda kuchukua fursa hii  kuwahasa wakazi pia kuilinda miundombinu ya mawasiliano haya ili yaduma. Alimalizia kusema Mh, Ndemanga

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Airtel, Saleh Saphy “Tunayofuraha kutoa huduma za uhakika na gharama nafuu nchi nzima, kwa wakazi wa Lindi , tunawahakikishia ofa kabambe za msimu huu wa sikukuu kupitia ofa yetu maalumu ya “Wadatishe” ambayo mnaweza kupata simu orijino kwa gharama nafuu hadi ya shilingi 79,000 tu.-. vilevile wateja wanaweza kupata vifurushi vya intaneti vya 1G kwa shilingi 1000 wakati huu wa msimu wa sikukuu .

Kupitia huduma ya mawasiliano wateja wataunganishwa na huduma za intaneti, huduma za kifedha za Airtel Money kutuma na kupokea pesa, kupiga simu wakati wowote, kusajili simu zao na pia kupata nafasi ya kusoma masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu zao. Hizi ni baadhi tu za huduma zetu hivyo natoa wito kwa wakazi wa cheleweni, Ng’apa na Michee kujiunga na timu ya  Airtel SIBANDUKI na kufurahis huduma zetu.” Alisisitiza Saphy
Kulia ni mkuu wa wilaya Lindi bw,  Shaibu Ndemanga akikata utepe na akishangiliwa na  wananchi wakati wa uzinduzi wa mnara wa Airtel utakaotoa mawasiiano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. anaefuata ni diwani wa viti maalum Lindi Bi, Somoe Pamui, Afisa tawala wilaya Lindi Mh, Thomasi Safari na Meneja Mauzo wa Airtel Bw, Saleh Safy. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi  kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii
Mkuu wa Wilaya Lindi bw,  Shaibu Ndemanga akiongea  na  wananchi wakati wa uzinduzi wa mnara wa Airtel utakaotoa mawasiiano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. anaefuata ni diwani wa viti maalum Lindi Bi, Somoe Pamui na Meneja Mauzo wa Airtek Bw, saleh Safy. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi  kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii
 Kushoto Meneja Uhusiano wa Airtel bw Jackson Mmbando akielezea huduma zitakazotolewa na mnara wa Airtel uliojengwa kijiji cha Cheleweni kwa  Mkuu wa wilaya Lindi bw,  Shaibu Ndemanga (wapili kulia) mara baada ya kuzindua mnara huo huku wananchi wakisikiliza.  katikati ni Meneja wa Airtel Lindi by Saleh safy. Airtel imejenga mnara huo kutoa mawasiliano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo Safy. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi  kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii,.Katika juhudu za kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia maeneo ya pembezoni mwa nchi, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wake wa mawalisiliano na kuanzisha hduma za simu kwa mara ya kwanza katika kijiji cha cheleweni mkoa wa Lindi.

PLAN INTERNATIONAL YAZINDUA MRADI WA KUWAWEZESHA VIJANA NA WATOTO KUPITIA MICHEZO

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Shirika la Plan International limezindua Mradi wa Kuwawezesha Vijana na Watoto kwa Njia ya Michezo ili kuwajengea uwezo wa kuwa mawakala hai wa mabadiliko chanya katika jamii zinazowazunguka.

Mradi huo umezinduliwa leo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo, Wanchoko Chinchibera ambaye ametoa wito kwa watendaji wa Serikali, wazazi pamoja na jamii kwa ujumla kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha mradi huo unatekelezeka.

Chinchibera amesema mradi huo umekuja wakati muafaka kwani watoto na vijana wanakabiliwa na changamoto ya ulinzi, usawa wa kijinsia pamoja na ushirikishwaji mdogo katika michezo hivyo kupitia mradi huo watapata maendeleo mazuri ya kielimu na kimakuzi pamoja na fursa ya kutatua changamoto zao. 

“Kupitia michezo tunajenga afya, akili, malezi na makuzi ya mtoto lakini pia michezo ni sehemu ambayo watoto wanaweza kupaza sauti zao na kujadili kuhusu haki zao za msingi kwa njia ya nyimbo na mashairi hivyo tunaamini kuwa tukianza kuwashirikisha watoto katika suala zima la michezo tutatengeneza kizazi chenye maendeleo,”alisema Chinchibera.

Ameongeza kuwa kupitia michezo, vipaji vingi vitaibuliwa ambavyo vitasaidia katika kutengeneza ajira mbalimbali zitakazowawezesha vijana kujikomboa kiuchumi na kuchangia katika pato la taifa hivyo amewahakikishia wananchi kuwa mradi huo utazaa matunda mazuri.

Kwa upande wake Meneja Miradi wa Shirika hilo, Grace Semwaiko amesema mradi huo ni sehemu ya mpango mkakati wa tatu wa shirika hilo ambao kwa ujumla unalenga kufikia jumla ya watoto 3,075 na vijana 3,109 katika kuwahakikishia ulinzi na usawa wa kijinsia.

“Ni matumaini yetu kuwa mradi huu utatekelezwa vizuri na hatimaye kufikia malengo tuliyojipangia yakiwemo ya kukua kwa uelewa kwa jamii na wadau wote kuhusu usawa wa kijinsia, kuhakikisha vijana na watoto waliowezeshwa wanaleta mabadiliko katika jamii pamoja na kuimarika kwa ulinzi wa watoto katika ngazi ya jamii hadi taifa,” alisema Bi Grace.

Alifafanua kuwa mradi huo unawalenga wanafunzi wa Shule za Msingi kuanzia darasa la 4 hadi la 7, wanafunzi wa Shule 6 za Sekondari, walimu, wazazi, viongozi wa jamii na watendaji wa Vijiji, Kata pamoja na Watoto na Vijana ambao hawasomi.

Mradi huo utaratibiwa na shirika la Plan International pamoja na shirika la Right to Play na utatekelezwa katika Kata mbili za Kiluvya na Malumbo zilizopo wilayani humo ambapo jumla ya vijiji 10 vitanufaika. 

Aidha Bi.Grace aliongeza kuwa Mradi huo unatarajiwa kuwa wa miaka miwili na utagharimu jumla ya shilingi 641,468,700 ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2018.

Shirika la Plan International la nchini Ujerumani ni miongoni mwa mashirika ya Kimataifa yasiyo ya kiserikali ambayo yameonyesha juhudi kubwa za kuibua miradi mbali mbali katika jamii na kuifadhili katika sekta za Afya,Maendeleo ya jamii,Wanawake,Watoto na Michezo.
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani, Wanchoko Chinchibera akiongea na wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kuwawezesha Vijana na Watoto kwa Njia ya Michezo uliozinduliwa leo wilayani humo.Mradi huo unaratibiwa na Shirika la Plan International.
 Meneja Miradi wa Shirika la Plan International, Grace Semwaiko akielezea kuhusu malengo ya mradi wa Kuwawezesha Vijana na Watoto kwa Njia ya Michezo uliozinduliwa leo wilayani Kisarawe.Mradi huo unaratibiwa na Shirika la Plan International.


Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani, Wanchoko Chinchibera akikagua timu ya mpira ya watoto wakati wa mradi wa Kuwawezesha Vijana na Watoto kwa Njia ya Michezo uliozinduliwa leo wilayani humo.Mradi huo unaratibiwa na Shirika la Plan International.

MUUZA MITUMBA SOKO LA KARUME JIJINI DAR ES SALAAM AFUTIWA LESENI YA BIASHARA KWA KUMDHALILISHA MTEJA WAKE WA KIKE


 Diwani wa kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Shirika la Eguality for Growth (EfG), Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele na kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchikichini, Charles Kapongo.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye (kulia),  akitoa taarifa fupi kuhusu kampeni hiyo  mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele, Diwani wa kata hiyo, Joseph Ngowa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchikichini, Charles Kapongo.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye (kushoto), akipeana mkono na mgeni rasmi baada ya kumkabidhi risala.
 Mjumbe wa Soko la Mchikichini, Victor Kalokola akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Msaidizi  wa kisheria masokoni, Irene Daniel akitoa ushuhuda wa hatua zilizochukuliwa kwa baadhi ya watu waliobainika kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Soko la Tabata Muslimu.


Mwenyekiti wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko hilo, Betty Mtewele (kushoto), akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo.
 Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.
 Wadau wa EfG wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wadau wa EfG wakiwa wakiwa katika picha ya pamoja mgeni rasmi wa Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (kushoto)
Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (kushoto), akigawa vipeperushi vya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara wa soko la Mchikichini.

 Wasanii wa kundi la machozi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wasanii wa Kikundi cha Machozi wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) uliofanyika Soko la Ilala Mchikichini Dar es Salaam leo.
Uzinduzi ukiendelea
 Wasaidizi  wa kisheria masokoni, Aisha Juma (kushoto) na Irene Daniel wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Usikivu kwenye uzinduzi huo. Katikati ni Msaidizi wa kisheria masokoni Batuli Mkumbukwa.
 Picha ya pamoja na mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa.

Na Dotto Mwaibale
DIWANI wa Kata ya Mchikichini Joseph John Ngowa (Chadema), amemfutia leseni ya biashara, Alex Richard muuza mitumba katika Soko la Karume Ilala jijini Dar es Salaam baada ya kumbamba akimfanyia udhalilishaji mteja wake wa kike.
Tukio hilo limetokea Dar es Salaam leo mchana wakati Diwani huyo alipokuwa akienda kugawa vipeperushi vya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wafanyabaiashara wa soko hilo baada ya kuzindua kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoanzishwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) ndipo alipoingia kwenye kibanda cha mfanyabiashara huyo na kumkuta mteja wa kike akiwa ametoa nguo zake akipimishwa nguo za mitumba kitendo ambacho ni ukiukaji wa sheria ndani ya soko hilo.
"Kuanzia leo hii naagiza ufutiwe leseni yako ya biashara kutokana na tukio ili la aibu na kidhalilishaji ili iwe fundisho na kwa wengine" aliagiza Ngowa.
Ngowa alitishia kuwafuti leseni za biashara wafanyabiashara watakaobainika kuwadhalilisha wateja wao hasa wanawake na kuwa wanamsaka kijana moja maarufu kwa jina la Kipracheche ambaye ni kinara wa ubakaji na kudhalilisha wanawake katika soko hilo ikiwa ni pamoja na kulisambaratisha kundi la kihalifu sokoni hapo linalojulikana kwa jina la Masabanga.
Mfanyabiashara huyo Alex Richard alipohojiwa na wanahabari kuhusu vitendo hivyo aliomba samahani na kuwataka wenzake waache kufanya vitendo hivyo vya udhalilishaji kwa wanawake.

Mwenyekiti wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko hilo, Betty Mtewele alisema mfanyabiashara yeyote atakaye bainika kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hata unewa huruma atachukuliwa hatua kazi za kisheria.
Akizungumza katika uzinduzi huo Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye alisema katika vitendo vya kupinga ukatili wa kijinsia shirika hilo linaendesha mradi unaoitwa "Mpe Riziki si Matusi" katika Wilaya ya Ilala na Temeke katika masoko sita ambayo ni Mchikichini, Kisutu, Tabata Muslimu, Ferry, Gezaulole na Temeke Sterio lengo likiwa ni kuona wanawake wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala na Temeke wanafanyabiashara zao katika mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kimwili, matusi na kisiasa, vilevile kuona wanawake wakipewa heshima kama binadamu wengine ili waweze kujipatia kipato chao bila vikwazo.
(Imeandaliwa na mtandao wa 
www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)PRESIDENT KENYATTA ADDRESSES EALA …Senate Speaker delivers speech, lauds Assembly for contribution to integration process


East African Legislative Assembly, Nairobi, Kenya: 30th November 2016President Uhuru Kenyatta is challenging the East African Legislative Assembly to concert its efforts in ensuring the integration process is not only on course, but geared towards meeting the aspirations and high expectations of the people. The President is emphatic that the people of the region want nothing else but a Community that works for all and that is effective. 
In this regard, the President is calling on the Assembly to up the stakes on thesensitisation process and on its  consultations with legislative processes including engagement with the Partner States National Assemblies as envisioned under Article 65 of the Treaty of the Establishment of the EAC. 
The President’s remarks were delivered on his behalf by the Speaker of the Senate, Rt Hon Ekwe Ethuro at the Special sitting of the 3rd Meeting of the 5th  Session held at the Parliament Chambers (Senate) yesterday. In attendance were EALA Members, former Members led by Speaker Emeritus, Rt Hon Abdirahin Abdi and representatives of the Private Sector.The President noted the various achievements realised by the Communityto date. 
“I note with appreciation the progress that the Community has made to date.  Eleven (11) years ago, we established the EAC Customs Union. It has generated positive results. This is clearly demonstrated by the trend in intra-EAC trade over the period.  For instance, the value of the total intra-EAC trade rose from US Dollars 1.8 billion in 2004 to US Dollars 5.1 billion US Dollars in 2015 representing a significant growth of 190 percent”, he said. 
The President hailed the business community whom he termed keen partners and drivers of the integration proces. “I laud and commend them for their efforts in boosting our investment profile and partnership in creating jobs for our people. We are therefore duty-bound to support them in addressing the challenges they face in conducting and expanding their businesses in the region”, he added.  
The speech noted the various challenges the region continues to face.“There still exists a considerable number of trade restricting measures that are a hindrance to actualizing free trade in the EAC.  Among the obstacles, include long clearing procedures; road blocks and changes in applicable regulations, which together, contribute to impact trade negatively”, it said in part. 
The Head of State reiterated Kenya’s commitment to the integration process and cited the infrastructure projects as keen in the integration process. 
“We have every reason to take pride in what we have achieved in here in Kenya. We have commenced work on the Standard Gauge Railway (SGR) and we expect it to be operational by the middle of 2017. On-going development works on the Port of Mombasa and regional roads confirms Kenya’s commitment to building and achieving sound infrastructure for the greater benefit of the region”, he said. 
The President noted that EAC needed a strong oversight body and hailed the EALA for rising up to the occasion.

“For example, among the notable achievements of this Assembly include the passage of over 20 Bills cutting across various areas of integration. The Assembly’s legislative priority and performance in the last four years has indeed exhibited clear appreciation and understanding of matters that are of great relevance and urgency in deepening and widening the EAC integration”, the President remarked. 
In his remarks, the Speaker of EALA, Rt Hon Daniel F. Kidega, maintained that citizens of the region were keen to see the process of integration fortified. 
“I can confirm the Assembly is often inundated by citizens’ concerns to see the Common Market agenda become a reality.  Essentially, it is important that we open our East African markets to African people and beyond to


create jobs and opportunities. Likewise, we must avoid situations where we export jobs and allow cheap goods from outside the EAC to permeate the local markets”, Speaker Kidega noted. 

The Speaker noted the fight against Corruption needs to be taken a notch higher in the Partner States. “At the regional level, EALA is on the verge of enacting a Bill on Whistleblowers and on Anti-Corruption, thereby, putting in place a legal framework to report instances of corruption to authorities – given the fact that the vice knows no borders”, he added. 
The Speaker termed matters of peace and security as of paramount importance to the development in the region and further called for the fight against terrorism to be sustained. 
He termed the approximation of the national laws in order to create uniformity within the Partner States as necessary and called on the Partner States to move with haste in the matter.
An EALA Report adopted at the Sitting shows that Republics of Rwanda and Uganda have each approximated ten pieces of laws each, Republic of Kenya (6 laws), United Republic of Tanzania (6 laws) and Republic of Burundi (3 laws). Approximation of National Laws is vital in line with the Article 126 (2b) of the Treaty for the EAC is fundamental. 
The Siting came to an end with the next plenary expected to be held in January in 2017.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU XAVERY MIZENGO PINDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kushiriki katika kuaga mwili wa Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu Marehemu, Xavery Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Zuzu, Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Zuzu, Manispaa ya Dodoma ambako walishiriki katika kuaga mwili wa baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Xavery Mizengo Pinda Novemba 30, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.


Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda akipewa pole na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa wakati awa kuaga mwili wa Baba yake mzazi wa Waziri Mkuu mstaafu, marehemu, Xavery Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akizungumza wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee, Xavery Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Xavery Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu baba yake, Xavery Mizengo Pinda kijijini kwake Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Christina Mndeme na viongozi wengine wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.

Waziri Mkuu, KassimMajaliwa akizungumza na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda baada ya kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda baada ya kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wapili kulia ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).