Monday, April 30, 2018

TCCIA KWA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM WAZINDUA TYMNaibu makamu mkuu wa chuo kikuu Dar es salaam, Pro. Cuthbert Kimambo akiongea na TYM wakati wa kusain makubaliano na TCCIA.

Katika kuhakikisha Taifa letu la Tanzania linakuwa imara kiuchumi na kuwa na nguvu kazi kubwa ya Taifa, Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture ‘TCCIA’ imeingia makubaliano maalumu pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo TCCIA imetiliana saini katika makubaliano hayo ‘Memorundum of Understanding’ .

Makubaliano haya yanatoa nafasi kubwa kwa vijana kupitia TCCIA Youth Members, kitengo maalumu kwa vijana hasa waliopo vyuoni kuweza kutumia rasilmali zilizopo TCCIA kuweza kujijenga zaidi katika kazi zao pindi wanapokuwa bado wapo shule na hata baada ya kumaliza shule.

Akizungumza na TYM Makamu wa Rais wa TCCI Bw. Octavian Mshiu alisema TCCIA imeingia makubaliano haya na chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kuhakikisha inatoa fursa kwa vijana wengi kuweza kupata nafasi za kuonesha kazi zao, kupata nafasi ya kuwa na watu ambao watawawezesha kuweza kutimiza ndoto zao ‘Mentorship’, kutoa nafasi ya wenye makampuni na biashara kuwatumia vijana wa ndani ambao sio tu ni wabunifu bali pia wenye uthubutu wa kuleta mabadiliko chanya kwenye nchi yetu, katika kuongeezea hilo prof. Cuthbert Kimambo lisema, makubaliano haya hayataishia tu kwa chuo cha UDSM bali wataendelea na kwenye vyuo vyote nchini
Makamu WA Rais wa TCCIA Octavian Mshiu, wakibadilishana makubaliano Na naibu makamu Mkuu WA chuo kikuu prof Cuthbert Kimambo baada ya kutia sain kuhusu ushiriki wawezekaji vijana wa Chama hicho TYM.

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti UDSM Dr. Amelia Buriyo katika hotuba yake kwenda kwa wanafunzi baada ya uzinduzi huu alionesha kufurahishwa na jambo hili ambapo alitoa shime kwa vijana kuanza kuamka na kuchangamkia fursa hii adhimu kwao kwani sio kwamba itawakutanisha na watu ambao watawafanya ndoto zao katika miradi wanayoibuni kuwa kweli bali pia kuwezesha kupata nyezo za kufanyia kazi hasa upatikanaji wa mikopo.

Moja ya vijana ambao wamefanikiwa kupitia kujiajiri katika sekta ya ubunifu wa mavazi Bw.Jeff Jersey (Speshoz) alikuwepo kwenye halfa hii ambapo pamoja na mambo mengi aliyoyagusia alisisitiza sana kuhusiana na kuongeza thamani kwenye kila kitu ambacho wanakifanya kwani dunia ya sasa ni dunia ya ushindani na ushindani huhitaji sana ubunifu na kuongeza thamni katika kila kitu ambacho tunakifanya. Bw. Speshoz ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Speshoz aliwahi kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita.
Jeff Jersey "Speshoz" akizungumza na TYM wakati wa kusain makubaliano kati ya TCCIA na UDSM.TCCIA Youth Members ‘TYM’ sasa imefunguliwa rasmi ambapo kila kijana anaweza kwenda kujisajili bila malipo yoyote.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA KATIKA SEHEMU YA IRINGA-MIGORI-FUFU KM 189 ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI