Saturday, July 22, 2017

SH. BILIONI 1.669 KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI ILEJE-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 1.669 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya ya Ileje mkoani Songwe.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai 22, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Itumba.

Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo sh. bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika miji miwili ya Isongole na Itumba wilayani Ileje.“Kiasi kingine cha sh. milioni 669 kimetengwa kwa ajili ya maji katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ileje katika mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Hata hivyo, amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa Kampeni ya Rais Dkt. Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kusogeza huduma ya maji kwa urahisi.Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400.

Wakati huo huo Waziri Mkuu ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Songwe kuhakikisha inaimarisha ulinzi katika maeneo ya mipaka.Amesema kamati hiyo inatakiwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mipaka ili kuizua wageni kuingia bila ya kufuata taratibu zilizowekwa kisheria.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Bw. Joseph Mkude alisema katika kipindi cha Julai 2016 hadi Juni 2017 jumla ya wahamiaji haramu 38 walikamatwa kwenye wilaya hiyo.Alisema kati ya wahamiaji hao haramu 36 ni raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wawili walikua raia wa Malawi na wote walirudishwa makwao.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JULAI 22, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Ileje baada ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa wilaya hiyo  akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 22, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge Janet Mbene wa Ileje (kulia) na Juliana Shonza wa Viti Maalum baada ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa wilaya ya Ileje kuanza ziara wialyani humo Februari 22, 2017. (Picha na ofisi ya Wziri Mkuu). 
 Baadhi ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na taasisi binafsi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao mjini Ileje Julai 22, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma, viongozi wa dini na viongozi wa taasisi binafsi mjini Ileje Julai 22, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa jengo la hospitali ya wilaya ya Ileje akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe, Julai 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kushoto) wakitazama mbegu za mahindi zinazozalishwa na Kikundi cha SAM cha Ileje wakati alipotembelea banda la kikundi hicho kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje Julai 22, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vifaranga wa samaki wakati alipotembelea banda la Kikundi cha wanawake cha Tukazane cha Ileje  kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje Julai 22, 2017.

VYUO NA VYUO VIKUU-UVCCM WAMKINGIA KIFUA RAIS.DK MAGUFULI

Na Nassir Bakari

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kupitia Idara yake ya Vyuo na Vyuo vya Elimu ya Juu, umemkingia kifua Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli ukisema kwamba hafanyi uteuzi kwa njia za kibaguzi bali anafanya hivyo kwa kuzingatia weledi na uwezo wa anayemteua.

UVCCM imesema, hayo leo jijini Dar es Salaam, na kupinga vikali kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, kwamba Rais Dk. Magufuli amekuwa akifanya uteuzi kwa kuzingatia ubaguzi wa ukanda, ukabila, dini na jinisa.

Akifungua Kikao cha kazi cha Viongozi wa Vyuo na Vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu- UVCCM, Daniel Zenda alisema, UVCCM kupitia Idaya yake, inapinga na kulaani vikali kauli hizo za Tundu Lissu kwa sababu ni kauli za hatarai kwa kuwa zina lengo la uchochezi, kudhalilisha na kugawa Wananchi kwa misingi ya kibaguzi.

"Ndugu Watanzania kauli hii ya Tundu Lissu ni yenye lengo la kuchonganisha, kudhalilisha na kuwagawa wananchi, Sisi Vjana wa Vyuo na vyuo Vikuu, tunalaani kwa nguvu zetu zetu kauli hii. Kwa mfano ukitazama uteuzi wa Mkuu wa Majeshi nchini anatoka Bara, lakini hupo chini ya Waziri wa Ulinzi Dk. HusseinMwinyi ambaye anatoka Zanzibar", sasa hapo ubaguzi unakujaje", alisema na kuhoji.

Alisema, kimsingi katika kufanya uteuzi, Rais anazingatia haki yake ya kikatiba ambayo inampa mamlaka ya kuteua na kutengua kwa kadri anavyoona inafaa. "ibara ya 36 kifungu cha pili ambayo kinasema Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara za taasisi za Serikali na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara hizo", alifafanua.

"Mnajua siasa ni kama dawa, dawa huwa inaisha muda wake, sasa huyu Tundu Lissu naye amekwisha muda wake kisiasa, ndiyo maana inafika wakati anazungumza maneno ya kipuuzi katika jamii, nawaomba ndugu Watanzania wenzangu tuyapuuze maneno yake, hayana maana, Ndugu Wananchi wa Singida Mashariki tunawaomba 2020 msifanye makosa tena tuleteeni anayefaa kuliko huyu Tundu Lissu", alisema Zenda.

Alisema, kuisha kisiasa kwa Tundu Lisu na upinzani kwa jumla, kunatokana na uchapakazi ulioonyeshwa na uongozi wa awamu ya tano, chini ya Rais Dk. Magufuli. " Hawa kina Tundu Lisu kwa sasa hawana hoja, ndiyo maana sasa wanatapatapa kujaribu kutafuta pa kushika.

"Sisi kama vijana wasomi tunaiunga mkono Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. Magufuli kwa mambo yote inayoyafanya, Watanzania wenyewe tumekuwa ni mashahidi wazuri wa hayo mambo, tunaomba Mungu ampe afya njema ili aendelee kututumikia Watanzania" alisema Zenda.

Kaimu Katibu Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu-UVCCM Daniel Zenda akizungumza wakati wa kikao cha kazi na viongozi wa Vyuo na Vyuo Vikuu mkoa wa Dar es Salaam, leo .Kaimu Katibu Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu-UVCCM Daniel Zenda (kulia) akiongoza kikao cha Kazi cha Viongozi wa Vyuo na Vyuo Vikuu-UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, leo katika ukumbi wa jengo la Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar s Salaam. PICHA NA BASHIR NKOROMO

WAZIRI UMMY AZINDUA ZAHANATI NGUVUMALI JIJINI TANGA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katika akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Zahanati ya Kata ta Nguvumali leo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa na wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Said. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katika akisisitiza jambo kwa Muuguzi wa Afya wa Zahanati ya Nguvumali baada ya kuizindua kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo,Dkt Ally Bughe 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa na kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nguvumali na wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF)Alhaj Mussa Mbaruku 
Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF)Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza katika halfa hiyo 
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nguvumali akizungumza katika hadhara hiyo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa Mbaruku 
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji akizungumza katika halfa hiyo 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na madiwani wa Jiji la Tanga mara baada ya kuwasili katika zahanati hiyo kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapa Selebosi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kushoto katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kuzindua zahanati hiyo leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akipanda mti kwenye zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa na Waziri Ummy. 
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia uzinduzi huo
Waheshimiwa madiwani kutoka Kata mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia uzinduzi huo
Wananchi wakifuatilia uzinduzi huo 
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia uzinduzi huo
Msanii wa maigizo mkoani Tanga ,Dkt Njau akionyesha umahiri wake katika uzinduzi huo

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Serikali Yapongezwa kwa Kuwaleta Pamoja wadau wa Mazingira na Wazalishaji Mifuko ya PlastikiWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifungua Kikao cha Wazi cha kupokea maoni ya wadau kuhusu dhamira ya Serikali kupiga marufuku uzalishaji,uuzaji,usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustine Kamuzora akiongea wakati wa ufunguzi wa Kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.

Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akiongea wakati wa Kikao hicho mapema leo.

Mwenyekiti wa Umoja wa wazalishaji wa mifuko isiyo na athari kwa mazingira Bw. Jumanne Mgude akionesha mfuko unaozalishwa hapa nchini usio na athari kwa mazingira wakati wa Kongamano hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Wande Printing and Packaging (T) Ltd Bw. Joseph Wasonga akitoa maoni ya wamiliki wa Viwanda vya Kuzalisha mifuko ya plastiki hapa nchini wakati wa kikao hicho.

Katibu wa Umoja wa wazalishaji wa mifuko isiyo na athari kwa mazingira Bw. Sadick Mgonge akitoa maoni ya umoja huo wakati wa Kikao hicho leo.

Sehemu ya wadau walioshiriki kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mjadala na maoni ya washiriki .(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)


Frank Mvungi-Maelezo

Wadau wa Mazingira na Wazalishaji wa Mifuko ya Plastiki hapa nchini wameipongeza Serikali kwa kuwakutanisha pamoja ili kujadili kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki na kutoa maoni yao kwa Serikali juu ya kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.

Akizungumza wakati akifungua kikao cha wazi cha kupokea maoni ya wadau kuhusu dhamira ya Serikali kupiga marufuku uzalishaji, uuzaji, usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema dhamira ya Serikali ni kupata maoni ya wadau na wazalishaji wa mifuko hiyo ili Serikali ifanye tathmini kabla ya kuchukua hatua na kuweka mazingira yatakayowezesha utekelezaji wa Sheria ya Mazingira kwa kila mdau.

“Changamoto imekuwa kubwa katika matumizi ya mifuko ya plastiki katika swala la mazingira kwani tumeshuhudia miundo mbinu yetu ikiathirika, mifugo na hata viumbe vya baharini na kwa mujibu wa tafiti kuna hatari baadae mifuko hii ikawa mingi zaidi baharini kuliko samaki” Alisisitiza Makamba.

Akifafanua Makamba amesema kuwa Serikali imeona ni vyema ikakutana na wadau ili ipate maoni yao kwa kuzingatia kifungu cha 178 cha Sheria ya Mazingira kinachotaka wananchi na wadau kushirikishwa na kupata taarifa kuhusu maswala ya mazingira.

Aliongeza kuwa kuanzia sasa Ofisi yake itakuwa ikishirikiana na wadau katika mambo yote yanayohusu mazingira ili kuongeza tija na kutoa fursa kwa wadau hao kutoa maoni yatakayosaidia katika usimamizi wa Sheria na Kanuni.Naamini kutakuwa na kuvumiliana wakati wa kutoa maoni ili Serikali ipate maoni ya wadau wote kwa ufasaha na hii itasaidia Serikali katika kuchukua hatua ikiwemo kuhakikisha kuwa kuna usimamizi dhabiti wa Sheria ya Mazingira.

Pia Waziri Makamba alilitaka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kusimamia Sheria ya Mazingira kikamilifu ili kulinda rasilimali za Taifa.Kwa upande wake Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Plastiki Tanzania Bw. Ahmed Abdallah amepongeza utaratibu huo wa Serikali kukutana na wadau.

Kumekuwa na maoni mbalimbali kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki huku baadhi ya wadau wakidai imekuwa na athari kubwa katika mazingira zikiwemo magonjwa, uharibifu wa miundo mbinu na kuleta mabadiliko ya tabia nchi .

ONYO KALI KWA WAUZA PEMBEJEO FEKI, HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WATAKAOBAINIKA.Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Beatus Chowaji akisoma bango mara baaa ya kuzindua mradi wa Faida Mali unaoshirikiana na shirika la AMDT katika kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida.

Mkurugenzi wa Shirika la AMDT Michael Kayombo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Faida Mali wenye lengo la kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida kulima kibiashara.

Baadhi ya wadau waliohudhuruia uzinduzi wa mradi wa Faida Mali wenye lengo la kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida kulima kibiashara.

Mkurugenzi wa mradi wa Faida Mali mkoa wa Singida Tom Silayo akisoma taarifa ya mradi huo kwa wajumbe waliohudhuria uzinduzi wa mradi utakaowasaidia wakulima kulima alizeti kibiashara.

Mtendaji Mkuu wa Chama cha wasindikaji wa Mbegu za alizeti Tanzania Daud Musa Mwasantaja akiwahakikishia wakulima wa alizeti upatikanaji wa soko katika uzinduzi wa Mradi wa Faida Mali.

……………………………………………………………………….

Wauzaji wa pembejeo ambao sio waaminifu wamepewa onyo kali na endapo atabainika yeyote anayewalaghai wakulima na kuwauzia pembejeo ambazo sio hali hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Beatus Chowaji ametoa onyo hilo wakati akizindua mradi wa Faida Mali unaoshirikiana na shirika la AMDT katika kuwasaidia wakulima wa alizeti Mkoani Singida ili kulima zao hilo kibiashara zaidi.

Chowaji amesema kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya wakulima ambao hukumbana na wauzaji wa pembejeo ambao sio waaminifu na kuwalaghai kwakuwa wakulima hao hawana elimu na uelewa hasa wa viuatilifu au mbegu ambazo ni halisi.

Ameongeza kuwa mkono wa serikali ni merfu na utawabaini popote walipo hivyo waache mara moja kwani kwa kufanya hivyo wanakirudisha nyuma kilimo cha alizeti ambacho ni tegemeo kwa ajili ya uchumi wa viwanda Mkoani Singida.

“Singida tuna Viwanda vya kuamua mafuta ya alizeti vikubwa viwili, vya kati vitatu na vidogo 115 na kufanya jumla ya viwanda vya alizeti kuwa 120, vyote hivyo vinategemea alizeti ya mkulima, lakini pia mkulima anakuwa na matarajioa makubwa, hao wauzaji pembejeo wasio waaminifu hatutawavumilia, tena waache mara moja”, amesisitiza Chowaji.


Aidha amelipongeza shirika la AMDT kupitia mradi wa Faida mali kwa kuuchagua Mkoa wa Singida ili kuboresha kilimo cha alizeti hasa kwa ajili ya mkulima mdogo.

Chowaji amesema viwanda vya alizeti Mkoani Singida hufanya kazi kwa miezi minane kwa mwaka badala ya mwaka mzima kutokana na kuwa alizeti inayozalisha bado haitosheleshi viwanda hivyo kufanya kazi mwaka mzima.

Amesema matumaini makubwa ya serikali mkoani hapa ni kuwa mradi huo utasaidia kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kuifanya Singida ya Viwanda kuwa bora zaidi pamoja na kuliboresha zao lenyewe la alizeti kwa kutumia pembejeo za kisasa zaidi.

Chowaji amewataka wakulima wote wa alizeti kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga katika vikundi ili waweze kufikiwa kwa urahisi na kunufaika, pia waache kilimo cha mazoea kwakuwa alizeti ni biashara kubwa ambayo itawakomboa kiuchumi na kukupa pato la mkoa wa Singida.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la AMDT Michael Kayombo amesema shirika hilo kupitia Mradi wa Faida mali utahakikisha unasaidia upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo wa alizeti Mkoani singida.


Kayombo ameongeza kuwa mradi utaboresha huduma za ugani kwa kutoa taarifa sahihi na mapema juu ya kilimo cha alizeti kwa wakulima na taarifa hizo zitatolewa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno hivyo kuwafikia mapema.

Amreongeza kuwa watahakikisha wakulima wanapata soko la uhakika la zao hilo ndani na nje ya mkoa wa singida pamoja na kuhakikisha bei ya zao hilo ni yenye kumnufaisha mkulima na sio kumdidimiza zaidi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Chama cha wasindikaji wa Mbegu za alizeti Tanzania Daud Musa Mwasantaja amesema viwanda vya alizeti bado vina uhitaji mkubwa wa alizeti kwa kuwa viwanda vyao vimekuwa vikiendeshwa chini ya malengo kutokana na mbegu hizo kuwa chache.

Mwasantaja amesema wana imani kuwa mraadi wa Faida Mali utasaidia kuongeza uzalishaji wa alizeti hivyo kuwasaidia kuongeza pia uzalishaji katika viwanda vyao.

Ameongeza kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha na hivyo wakulima wasiwe na wasiwasi walime zao hilo kwa wingi watapata wateja na kwa bei ambayo ni nzuri.

Nao wakulima walioshiriki uzinduzi wa maradi huo wamesema mradi huo umekuja muda muafaka kwakuwa na wao wanatamani kupata faida kutokana na kilimo hicho kwakuwa baadhi bado wanalima kwa mazoea na kwa kutumia mbegu ambazo hazizalishi kwa wingi.

ZSSF Yatiliana Saini na Banki Tpb Bank Utowaji wa Mikopo Kwa Wanachama wa ZSSF Zanzibar.

MKURUGENZI Mkuu wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi kushoto na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Jamii Zanzibar (ZSSF) Makame Mwadini wakitiliana saini makubaliano ya kutowa mikopo ya Kielimu na Kuazia Maisha kwa Wanachama wa (ZSSF)hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ZSSF kilimani Zanzibar, wakishuhudia Mwanasheria wa ZSSF Mohammed Fakih na Afisa Mawasiliano wa Tpb Bank Chichi Banda
Mkurgenzi Mkuu wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi kushoto akibadilishana mikataba wa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF kupata mikopo kupitia Banki ya Tpb Bank, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Mwadini Makame,  kuwawezesha kupata Mkopo wa Elimu ya Juu na kuaza maisha kwa Wanachama wa ZSSF, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Kilimani Zanzibar.wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa pande hizo mbili.
Maofisa wa Tpb Bank wakifuatilia mkutano huo wa utilianaji saini ya kutowa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF Zanzibar kupitia benki hiyo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za ZSSF Kilimani Zanzibar.
Maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wakifuatila mkutano huo wa utilianaji wa saini.
Afisa Mawasiliano wa Tpb Bank Chichi Banda akitowa nafasi kwa waandishi wa habari kuuliza maswali wakati wa hafla hiyo.
Mkurgenzi Mkuu wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini kuelezea madhumuri ya hafla hiyo kuwanufaisha Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar kupata mikopo kupitia Banki yake Tpb Bank. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Mwadini Makame
akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makubaliani ya kupata mikopo kwa Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, kupitia Banki ya Tpb Bank.
Maofisa wa Tpb Bank wakifuatilia hafla hiyo ya utilianaji wa saini na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF. 
Mwandishi wa habari akiulisa swali wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya ZSSF na Tpb Bank, kutowa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF kupata Elimu ya Juu na Mkopo wa kuazia maisha. 
Mwandishi wa habari akiuliza swali wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mikopo wa Banki ya Tpb Bank Ndg. Henry Bwogi akifafanua na kujibu maswali yalioulizwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya pande hizo mbili. 
Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Bi Raya Hamad Khamis akitowa shukrani kwa washiriki wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini uliofanyika katika Ofisi za Jengo la ZSSF Kilimani Zanzibar. 
Viongozi wa Tpb Bank na ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa hafla hiyo. 
Mkurugenzi wa Banki ya Tpb Bank Sabasaba Moshingi akiwa na Maofisa wa ZSSF wakibalishana mawazo baada ya kumaliza hafla ya utilianaji wa saini na ZSSF, katikati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZSSF Ndg.Mwadini na Afisa wa ZSSF Miradi Ndg. Muumin.
Mkurugenzi wa Banki ya Tpb Bank Sabasaba Moshingi akisalimiana na Afisa wa ZSSF Ndg Filifili. 

Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com
Zanzinews.com.