Tuesday, May 31, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli ametoa wito kwa watanzania kuwekeza katika sekta ya viwanda ili kuwezesha nchi kuwa na uwezo mkubwa wa ajira na kuchochea maendeleo;https://youtu.be/vRnPp2cjNi0

SIMU.TV: Jopo kuu la upelelezi la polisi visiwani Zanzibar limefanya mahojiano maalumu na aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais visiwani humo Maalim Seif Shariff Hamad;https://youtu.be/c6ebk0olzIQ

SIMU.TV: Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa amesema wizara yake itaweka mkazo katika diplomasia ya viwanda ili kuwezesha uwekezaji mkubwa katika sketa hiyo; https://youtu.be/RFCLfs9eTrc

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameitaka jamii ya watanzania kwa kushirikiana na serikali kulinda urithi wa taifa ili ziweze kutuletea maendeleo;https://youtu.be/DmgV5qCJ-6M

SIMU.TV: Waandishi wa habari wamekumbushwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ili kuepusha migogoro inayoweza kusababishwa na matumizi mabaya ya kalamu zao;https://youtu.be/AIpBJtpBrkA

SIMU.TV: Benki yan maendeleo ya Afrika ADB imezitaka nchi za Afrika kuwekeza katika sekta ya umeme ktika maeneo ya vijijini; https://youtu.be/clhAoZnv0vc

SIMU.TV: Matumizi ya huduma za kifedha za simu kwa wakulima wadogo nchini ni madogo kwa sababu wakulima wengi hawajui kutumia huduma hizo;https://youtu.be/X5S03DGJ7GI

SIMU.TV: Kampuni ya vifaa vya plastiki Jambo Plastiki imesema maeneo mengi yenye mikusanyiko ya watu ni machafu kwa sababu hakuna vifaa bora vya kukusanyia taka;https://youtu.be/sN5BJ9_BCvY

SIMU.TV: Kampuni ya uvumbuzi ya Regency Innovation na benki ya UBA wazindua kadi inayokuwezesha kutoa fedha popote maarufu kama Visa Card; https://youtu.be/vaeL-V53ybA

SIMU.TV: Serikali imemfungia miaka mitano rais wa ngumi za kulipwa PST Emmanuel Mrundwa na shirikisho hilo kwa muda wa miaka mitano bila kujihusisha masuala ya michezo;  https://youtu.be/xjO-yxpQuC4   

SIMU.TV: Baraza la michezo la taifa BMT laongeza siku tano zoezi la uchukuaji fomu kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga; https://youtu.be/r4xk5sbZYF8
SIMU.TV: Timu ya taifa ya Misri inatarajia kuwasili kesho nchini tayari kwa mchezo wao dhidi ya taifa stars siku ya Jumamosi; https://youtu.be/qmuWTEkRx0I

SIMU.TV: Tamasha la majimaji serebuka limeingia siku ya nne hii leo huku bingwa wa ngoma za asili akiwa tayari keshapatikana; https://youtu.be/cZ4cvhI-97o

SIMU.TV: Watu nane wakazi wa kata ya Mzizima mkoa wa Tanga wameuwa kikatili kwa kukatwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji haramu.https://youtu.be/pTMpNrf95_E  

SIMU.TV: Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ameahidi kumfuta kazi mara moja mtendaji yeyote atakaye bainika kukwamisha juhudi za kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda. https://youtu.be/klkkg9MCeok
SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kulinda maeneo yenye vivutio vya utalii na kuyaendeleza kwa faida ya taifa. https://youtu.be/Spxp0paAOx0

SIMU.TV: Tatizo la udumavu wa akili kwa watoto wadogo linalotokana na ukosefu wa lishe bora limeonekana kuwa kubwa na kuhitaji juhudi za wadau kulikabili.https://youtu.be/SvlZL9dtR6Q

SIMU.TV: Mahakama ya rufaa ya Tanzania leo imesikiliza rufaa iliokatwa na mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP dhidi ya kufutwa kwa kosa la utakatishaji wa fedha lililokuwa likiwakabili aliyekua mkurugenzi wa TRA Hary Kitilya na wenzake shose Sinare na Sioi Sumari. https://youtu.be/ASAlx0lJOI0

SIMU.TV: Halmashauri ya wilaya ya Lindi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria ambapo wamegawa vyandarua kwa familia za halmashauri hiyo. https://youtu.be/x-FZT-bKqyM

SIMU.TV: Mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini TANTRADE imeaswa kutoa mafunzo kwa wafanyabiashra wa nyama kuhusu umuhimu wa ngozi na namna ya kutoa ngozi ilio bora na yakununulika kwa urahisi. https://youtu.be/2iVTb5LWf-A

SIMU.TV: Kampuni ya Dar Brew imewahakikishia wakulima wa zao la mtama nchini kuwa watapata soko la uhakika kutoka katika kiwanda hicho kinachotengeneza bia ya asili ya Kibuku. https://youtu.be/OROFDpZNPlc

SIMU.TV: Baadhi ya abiria wanaosafiri na ndege za kampuni ya Fast jest wamelalamikia kupata usumbufu hasa katika kusafirsha mzigo kwa kuambiwa walipie mara mbili.https://youtu.be/HsM1qNwjpRw

SIMU.TV: Timu ya taifa ya Misri inatarajia kuwasili nchini hapo kesho kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Taifa stars siku ya jumamosi. https://youtu.be/XwbzBBGNSQ4

SIMU.TV: Nyota wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu amejiunga na wenzake leo kambini kwa ajili ya  maandalizi ya mcheo wa jumamosi dhidi ya Misri.https://youtu.be/xB8RlqjnoHE

SIMU.TV: Baraza la michezo nchini limesogeza mbele zoezi la uchukuaji wa fomu za kuomba kugombea nafasi mbalimbali katika klabu ya Yanga.https://youtu.be/i5R7_ByAUv4

SIMU.TV: Baadhi ya wadau wa klabu ya yanga wameendelea kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba kugombea nafasi mbalimbali katika klabu hiyo.https://youtu.be/zIqDspXWtFQ

SIMU.TV: Timu ya Golikipas ya jijini Dar es Salaam imecheza na Vingunguti Kombaini katika mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kutafuta vipaji. https://youtu.be/WuMELZbKAxk

SIMU.TV: Wasanii kutoka vikundi mbalimbaliza vya ngoma wamepamba katika shindano la majimaji serebuka lililokuwa likiendelea katika manispaa ya Songea.https://youtu.be/yPB_JChj8xQ

SIMU.TV: Mshambuliaji chipukizi wa Manchester united Rushford ameongeza mkataba utakaomfanya aendelee kusalia katika klabu hiyo msimu ujao.https://youtu.be/437o_ahBVKU

MATUKIO KWENYE KIKAO CHA 33 CHA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


 Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.


Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi akichangia kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga leo mjini Dodoma.


Baadhi ya Mawaziri wakifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa leo mjini Dodoma.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga(kushoto) na Madiwani wa jimbo la Iringa Mjini waliolitembelea Bunge.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.


Wabunge kutoka mkoa wa Iringa Mhe. Augustine Mahiga, Mhe. William Lukuvi na Mhe. Peter Msigwa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madiwani wa Iringa mjini waliolitembelea Bunge leo mjini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson akiwasikiliza waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliofika Ofisini kwake kuwasilisha Taarifa ya Umoja huo kuhusu Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015.

Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani) ofisini kwake Dodoma.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Roeland Van De Geer (kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Taarifa  ya kuhusu Uchaguzi Mkuu mjini Dodoma uliofanyika nchini Tanzania Oktoba 25, 2015.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya Mhe. Judith Sargentini (kushoto) na Balozi wa Umoja huo  Mhe. Roeland Van De Geer (katikati) waliofika Ofisini kwake Dodoma leo.
 Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya Mhe. Judith Sargentini akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Taarifa ya Uchaguzi ya Waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU) kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25, 2015. Hafla hiyo imefanyika leo mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waangalizi wa Uchaguzi  kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliomtembelea Ofisini kwake leo mjini Dodoma. PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum.