Wednesday, January 30, 2013

BENKI YA KCB TANZANIA IMETOA MSAADA KWA SHULE ZA MSINGI NA HOSPITALI JIJINI DAR

 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa katikati akimkabidhi moja ya msaada wa madawati kati ya 89 Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Makumbusho Bi.Benedicta Lyimo,yaliyotolewa na benki hiyo yenye thamani ya Milioni 17.4,anaeshuhudia kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye.
 ) Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa kushoto na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye wakioneshwa moja ya jengo la wodi ya kujifungulia wakinamama na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza Dare s Salaam mara baada ya kukabidhi rasmi vifaa mbalimbali vikiwepo vitanda vya kujifungulia vine vyote vikiwa na thamani ya Milioni 7.4 kwa ajili ya kituo hicho.   
  Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa  akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye,wakati alipokuwa akikagua moja ya vitanda kati ya vinne vya kujifungulia wakina mama kabla ya kuvikabidhi rasmi kwa uongozi wa Hospitali ya Sinza iliyopo jijini Dar es Salaam vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 7.4 ,kushoto Meneja Masoko wa benki hiyo Emelda Gerald.
 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa  akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makumbusho alipofika shuleni hapo kutoa  msaada wa madawati  89 na vifaa vya kusomea,vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 17.4 kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye.
 Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Bi.Christine Manyenye na Meneja Masoko wa benki hiyo Emelda….wakimsikiliza Muuguzi wa Hospitali ya Sinza jijini Dar es Salaam Rachel Mshana mara walipofika hospitalini hapo kukabidhi msaada wa vitanda vine na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kujifungulia akinamama wajawazito vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 7.4.
 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa kulia akimkabidhi moja ya msaada wa madawati na meza  Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kibamba   yenye watoto wenye ulemavu wa akili Bi.Asia Mpate,yaliyotolewa na benki hiyo yenye thamani ya Milioni 17.4,katikati  ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye.
 Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa  akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza ya jijini Dares Salaam,Benedict Luoga moja ya kitanda kati ya vinne Salaam vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 7.4 vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kujifungulia akinamama wajawazito. 

Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania,Bw.Edmund Mndolwa kulia akimsikiliza jambo Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kibamba   yenye watoto wenye ulemavu wa akili Bi.Asia Mpate,baada ya kumkabidhi rasmi msaada wa madawati 89 yenye thamani ya Milioni 17.4,wapili kulia k Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christine Manyenye,na kushoto ni Mwalimu msaidizi wa shule hiyo Bi.Mwajabu Minja.

 Na Mwandishi wetu
Shule ya Msingi ya Kibamba  katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam inakabiliwa na  uhaaba wa madawati 500,  jambo linalowalazimu wanafunzi  wa shule  hiyo kukaa chini wakati wakifundishwa darasani.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Asia Mpate alibahanisha hayo jana na kusema  kuwa shule yake yenye wanafunzi 1,950,kuliwa na  madawat 320  na madarasa 13 tu.

Mwalimu Mkuu huyo alikuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa misaada na Benki ya  KCB iliyotoa madawati 25, meza  tatu,   viti vya walimu sita, madafyari 235 na peni 200 , vyote vikiwa na thamani ya Sh, Milioni 5 kwa shule hiyo.

Alisema kuwa uhaba  mkubwa wa madawati katika shule yake kumepelekea utoro mkubwa kwa wanafunzi wake  kwani wanafunzi wake hulalamikia  hali mbaya na ugumu wa  kukaa chini sakafuni.

Mpate  amesema kuwa wanafunzi wengi wa shule yake wamechanganyikiwa na hali hiyo  na hivyo huamua kutohudhuria masomo, jambo linaofanya  ufanisi  mdogo wa elimu kwa wanafunzi wake.

" Utoro ni mkubwa katika shule yetu kwa sababu hali halisi ya madarasa ni  ya kutisha, hatuna madarasa ya kutosha wala vitendea kazi . Tunashukuru Benki ya KCB kwa msaada wao ambao tunaamnini kuwa  utatusaidia kuboresha  kiwango cha elimu  katika shule  yetu", alisema mwalimu mkuu huyo..

Kwa upende wake Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi wa benki hiyo,  Dk Edmund  Mndolwa alisema kuwa  msaada huo  ni sehemu ya wajibu wake  wa benki kusaidia jamii na kwamba benki yake imejidhatiti kusaidia kuinua  kiwango cha elimu  nchini  Tanzania.

Aliwashauri wanapokea misaada ya benki hiyo kutumia ipasavyo na inavyotakiwa   misaada  inayotolewa na benki yake.

Kwenye hafla hiyo pia  benki ya KCB ilitoa msaada wa madawati 64 yenye thamani ya Sh. Milioni  tano kwa Shule ya Msingi ya Makumbusho pia ya jijini.
Wakati huo huo  hopsitali ya  Sinza  ya jijini Dar es Salaam imepokea msaada wa  vifaa vya hospitali vyenye thamani ys Sh. Milioni 7.4 kutoka kwa Benki ya KCB katika hafla  iliyofanyika kwenye hopsitali  hiyo jana.

Dokta Mwandamizi wa  hospitali  hiyo, Dk Benedict  Luwoga  alishukuru benki hiyo kwa msaada huo  na kusema kuwa  vifaa hivyo vilikuja kwa wakati na kuvitaja  vifaa hivyo ni  pamoja na vitanda vinne  vya kuzalisha kwa mama  wajawazito.

Alisema kuwa  hospitali yake ilizidiwa uwezo  kwa sababu ilikuwa na   vitanda  viwili tu vya kuzalisha mama wajawazito , kwa hiyo vitanda hivyo vinne zaidi ilikuwa ni ukombozi mkubwa kwa hospitali yake.

"Tunashukurui Benki ya KCB kwa msaada huo, umekuja kwa wakati ambapo hospitali ilikuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi. Amezitaka kampuni zingine ziige mfano wa benki ya KCB", alisema Dk Luwoga.



No comments: