Balozi wa
Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cook Leo amemtembelea ofisini kwake Kamishna
Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na
Kupambana na dawa za kulevya Bw.
Rodgers William Siyanga na kufanya mazungumzo ya namna serikali za Uingereza
na Tanzania zitakakavyoweza kushirikiana katika kudhibiti tatizo la dawa
za kulevya . Katika ziara hiyo Balozi Cook aliambatana na maafisa kutoka ubalozi
wa Uingereza nchini Tanzania Bw.
Christopher Kiddle na Bw. Andrew Stephens.
Balozi
wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cook (wapili kutoka kushoto)
alipomtembelea Kamishna Jenerali wa
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na
dawa za kulevya Bw. Rodgers William
Siyanga (wa kwanza kulia) ofisini kwake leo asubui Jijini Dar es salaam. Balozi
Cook aliambatana na maafisa kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw.
Christopher Kiddle (wa kwanza kushoto) na Bw. Andrew Stephens (wa tatu
kushoto), kutoka kulia (wapili) Makamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya
No comments:
Post a Comment