Na Mark B. Childress, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mwaka mmoja uliopita wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, niliandika makala kuhusu jitihada za kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI nchini Tanzania. Toka wakati huo, kwa pamoja tumepiga hatua muhimu kuelekea katika kufikia azma hiyo, tukielekeza rasilimali na shughuli zetu kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi nchini kote. Hata hivyo, bado tunahitajika kuongeza nguvu na kufanya zaidi. Bila ya kuongeza kasi yetu katika mwelekeo huu, maambukizi mapya yataongezeka, jambo litakaloongeza idadi ya Watanzania watakaokuwa wakiishi na VVU hivyo kuathiri maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Kipindi cha miaka mitano ijayo ni kipindi muhimu sana katika kufikia lengo la kutokomeza kabisa UKIMWI duniani ifikapo mwaka 2030. Rais Obama ameweka malengo makubwa kwa Mpango wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR), akitangaza kuwa hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, PEPFAR itakuwa inawasaidia watu milioni 12.9 kupata matibabu yanayookoa maisha ya kufubaza VVU na kuwawezesha wanaume milioni 13 duniani kote kupata tohara. Aidha, kwa kushirikiana na wadau wa kiserikali, asasi za kiraia na sekta binafsi, PEPFAR itajielekeza katika kupunguza maambukizi ya VVU kwa asilimia 40 miongoni mwa wanawake vijana na wasichana katika nchi zilizoathiriwa zaidi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
No comments:
Post a Comment