Wednesday, October 31, 2018

SERIKALI YAANDAA MPANGO MKAKATI KUWANOA WASAIDIZI WA KISHERIA NCHINI

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo Maalum ya Wawezeshaji watakaotoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria ili waweze kupata usajiri rasmi na wa kisheria wa kutoa huduma za kisheria kwa wananchi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Law School of Tanzania (LST) na kufadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF) yaliofanyika Dodoma jana.


SERIKALI imeandaa mpango mkakati wa kutoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za msaada wa kisheria kwa watanzania maskini wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya kisheria nchini.

Mpango wa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria nchini unatarajiwa kuanza mapema Novemba mwaka huu na walengwa wakuu ni wasaidizi wote wa kisheria ambao wanaotoa huduma za msaada wa
kisheria katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Katika sehemu ya maandalizi ya mafunzo hayo, Serikali kupitia ofisi ya Msajili wa Watoa Huduma za Kisheria –Wizara ya Katika na Sheria, imeendesha mafunzo yaliyolenga kupika wataalum (wawezeshaji) wapatao 40 kutoka mashirika mbalimbali ya huduma za kisheria) watakaoendesha mafunzo hayo maalamu kwa wasaidizi wa kisheria.

Mafunzo ya kupika wawezeshaji yamefanyika Dodoma na yaliandaliwa na Law School of Tanzania (LST) kwa kushirikiana na Tanzania Law Society (TLS) na kufadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF)—taasisi inayofadhiliwa miradi/shughuli mbalimbali ya wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumzia mafunzo hayo Mratibu wa Mafunzo ya Wawezeshaji Suleiman Pingoni amesema mafunzo hayo yanalenga kupika wataalam mahiri wakaoendesha mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria, yanayotajiriwa kuanza rasmi mapema Mwezi Novemba, na kumalizika kabla ya Disemba 31, Mwaka huu.

Mafunzo kwa wawezeshaji, kwa mujibu wa Bw.Pingoni, yalilenga kuwawezesha kupata ufahamu wa kutosha kuhusu maswala ya msingi kuhusu sheria ya Msaada wa Sheria (Legal Aid Act ) ya Mwaka 2017 na Kanuni zake, matakwa ya sheria kuhusu usajiri na usaili wa wasaidizi wa kisheria. Sheria ya Msaada wa Kisheria inawataka wasaidizi wa kisheria kupata mafunzo maalum ili waweze kusajiliwa na kupewa leseni za kutoa huduma za kisheria kwa wahitaji.

“Kimsingi, sheria ya Msaada wa Kisheria imewatambua wasaidizi wa kisheria na kazi wanazofanya hivi sasa. Hata hiyo, sheria hiyo hiyo, inawataka wasaidizi hawa wa kisheria kupata mafunzo maalum ili waweze  kupatiwa liseni/vitambulisho ili waruhusiwa kutoa huduma za kisheria,” amesisitiza Bw. Pingoni.Kwa mantiki hiyo, Ofisi ya Msajili wa Watoa Huduma za Kisheria ameandaa mafunzo kwa wawezeshaji

watakaotoa mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria, ili waweze kukidhi matakwa ya sheria.Ameeleza wasaidizi wa kisheria watakapata mafunzo hayo maalum watapatiwa vyeti, ambavyo vinawazesha kutuma maomba ya kusajiliwa na kutambuliwa kama wasaidizi wa kisheria kwa mujibu wa Sheria, na baada kupatiwa vitambulisho maalum.

“Lengo kuu la michakato hii yote ni kupata wasaidizi wa kisheria mahiri na wenye uwezo, ambao wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, wakaoweza kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wananchi, amesema Bw.Pingoni.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi-LSF Scholastica Jullu ameelezea mafunzo maalum kwa wasaidizi wa kisheria kama “hatua kubwa katika jitiada za serikali na wadau wa huduma za kisheria zinazolenga kupanua wigo wa huduma za msaada wa kisheria na kuwezesha watu maskini, wanaodhulimiwa na kunyanyaswa kupigania na kupata haki zao.”No comments: