Wednesday, October 31, 2018

MSAFARA WA WAZIRI LUGOLA WANUSURIKA KUGONGWA NA BASI LILILOKUA MWENDOKASI LIKIOVATEKI KATIKA KONA GAIRO, DEREVA AKAMATWA



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Dereva wa Basi la Hekima za Mungu, Isaac Vian, alipomkimbilia Waziri huyo huku akimuomba msamaha mara baada ya kusimamishwa kutokana na kuendesha kwa mwendo kasi pamoja na kuovateki katika kona katika eneo nje kidogo na mji wa Gairo Mkoani Morogoro. Dereva wa Basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ lililokua linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama Mkoani Shinyanga alielekezwa akaripoti kituo cha polisi mkoani Dodoma ili aweze kufunguliwa mashtaka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiangalia namba za usajili T140 AZZ la Basi la abiria la Hekima za Mungu lililokua linatoka Jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama ambalo Waziri alilisimamisha kutokana na kosa la mwendokasi pamoja na kuovateki katika kona nje kidogo wa Mji wa Gairo Mkoani Morogoro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na abiria wa basi la Hekima za Mungu baada ya Dereva wa Basi hilo, Issac Vian kuendesha kwa mwendokasi na kuovateki katika kona kali ambapo angeweza kusababisha ajali kwa kugongana na gari la Waziri Lugola, uso kwa uso Kijijini, nje kidogo na Mji wa Gairo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akishuka katika Basi la Hekima za Mungu mara baada ya kuzungumza na abiria na kuwataka kukemea mwendokasi pamoja na kuovateki katika kona alivyofanya dereva wa basi hilo, Isaac Vian (kushoto), nje kidogo ya mji wa Gairo, mkoani Morogoro, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimuonya Dereva wa Basi la Hekima za Mungu, Isaac Vian (kushoto), kwa kosa la kuendesha basi hilo kwa mwendokasi pamoja na kuovateki katika kona nje kidogo ya mji wa Gairo, mkoani Morogoro, leo. Hata hivyo Dereva huyo Waziri huyo alielekeza akamatwe kutokana na kosa hilo ambalo lingesababisha ajali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Felix Mwagara, MOHA-Gairo.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amenusirika kupata ajali wilayani Gairo, Mkoani Morogoro baada ya basi la Hekima za Mungu kuovateki katika kona wakati gari la waziri huyo likiwa eneo sahihi.

Tukio hilo lilitokea saa 6:04 mchana wakati Waziri huyo alipokua anatokea Mjini Dodoma kuelekea Jijini Dar es Salaam, katika eneo la nje kidogo ya Mji wa Gairo, basi hilo likiwa mwendokasi likiovateki katika kona, ndipo dereva wa gari la Waziri Lugola alipunguza spidi ili kuiepuka ajali hiyo.

Hata hivyo Basi hilo lilipopita, Waziri huyo aliekeza gari hilo lifuate kwa nyuma mpaka walikamate, hata hivyo Basi hilo lilikamatwa na dereva wa basi hilo kukaguliwa kama alikua na sifa ya kua dereva. Bara baada ya kumkagua dereva huyo, Waziri Lugola alizungumza na abiria wa basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ ambalo lilikua linatoka Dar es Salaam kuelekea Mjini Kahama mkoani Shinyanga.

“Kwanini mnashindwa kukemea hii tabia ya huyu dereva, mnataka awaue?, alitaka kusababisha ajali mbaya sana hapa, nanyi mmekaa kimya, mnafanya makosa kutokuripoti hii tabia mbaya kabisa,” alisema Lugola. Aliongeza kua, yeye ni Waziri ambaye anakemea mwendokasi na kiuwataka madereva nchini waendeshe kwa umakini, lakini dereva huyo anashindwa kufuata sheria za usalama barabarani, hivyo anapaswa kuchukuliwa hatua na iwe fundisho kwa madereva wenye tabia kama hiyo.

Licha ya Dereva wa Basi hilo, Isaac Vian alikiri kosa hilo na kuomba msamaha lakini Waziri Lugola aliekeza akamatwe lakini atakapofika mwisho wa safari.

No comments: