Mwanadada mkali wa soka Iringa na mikoa ya nyanda za juu kusini Speransia Mhondele akionyesha uwezo wake kisoka |
Hapa aklionyesha jinsi ya kutuliza mpira kwa gamba |
Akionyesha mbinu ya kumkabili adui kwa mpira wa angani |
Hapa akijiandaa kuondoka na mpira baada ya kuutuliza kutoka hewani |
Timu ya watuma salam mkoa wa Iringa ambayo binti Speransia ( wa pili kushoto waliosimama) alipata kuonyesha soka la uhakika jana wakati wa mchezo wa kirafikin kati ya watangazaji wa radio Furaha Fm na watuma salam mchezo uliomalizika kwa watangazaji kushinda baada ya kuigagadua timu ya watuma salam mabao 2-0
.......................................................................................
Spransia Evaristo
Mhondele ni binti wa miaka 18 mkazi
wa Kihesa katika manispaa ya Iringa mwenye kipaji
cha hali ya juu katika
mchezo wa mpira wa
miguu mwenye ndoto za kuj kulipa
heshima kubwa Taifa la Tanzania katika soka la
wanawake .
“mimi nilihitimu masomo yangu ya sekondari mwaka 2012 katika shule ya
sekondari Mlamke katika Manispaa ya
Iringa na nimepata kuchaguliwa kujiunga na timu za UMISETA katika mchezo wa soka wanawake “
Nilianza kucheza
mpira mwaka mwaka 2010 nikiwa katika
mashindano ya UMISETA yaliyofanyika
katika Ifunda kwa wilaya ya Iringa ambako nilikwenda
kushiriki mchezo wa Basketi .
Baada ya kufika huku nilikuta kuna ushindani mkubwa katika
mchezo huo ambao nilichaguliwa na hivyo baada ya kuchujwa
wengi nikiwemo mimi katika mchezo huo
ndipo nillipoamua kubadili mchezo na kuanza kucheza mchezo wa mpira wa miguu kwa
kufanya mazoezi .
Nilifanya mazoezi
usiku na mchana na baada ya mashindano mengine ya UMISETA ndipo nilipoamua kuelekeza
nguvu huko na kujiunga kabisa
katika timu ya mpira wa miguu ya
wanawake .
Kujiunga kwangu na
timu ya mpira wa
miguu wanawake kuniliwezesha kupita hatua kwa kuchaguliwa
kuwakilisha mkoa wa Iringa katika mashindano ya kanda ya kusini
kwa kuelekea mkoani Ruvuma kwa mara ya kwanza kufika katika mkoa huo na baada ya kufanya vizuri huko nilichaguliwa
kuwakilisha kanda ya kusini
katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani .
“ Jitihada binafsi
nilizoonyesha na wachezaji wenzangu tuliiwezesha
timu yetu kutoka
kanda ya nyanda za juu kusini
kushika nafasi ya tatu kitaifa “
Mchezaji huyo anadai
kuwa ndoto yake kubwa katika soka kuja kuchezea timu kubwa
za kitaifa ili kuweza
kuonyesha uwezo wake zaidi .
“Kwa sasa nasuburi
ruhusa ya mzazi wangu
ili kuweza kuniruhusu
kujikita zaidi katika michezo ili
kuweza kutafuta fursa ya
kulitumikia Taifa langu
Tanzania katika michezo …..nilishindwa
kujiunga na timu za
wanawake nje ya mkoa kutokana na
wazazi kunizuia kutokana na wakati huo
nilikuwa masomoni “
Spransia anasema kuwa
katika maisha yake wakati
akiwa shule kwa sehemu
kubwa alikuwa akiwaza michezo
zaidi na
hasa kuwa na ndoto ya kuja
kuchezea timu kubwa za mpira wa miguu kwa
wanawake na yawezekana hata
kufeli kwake kulitokana na mawazo ya michezo .
Hata hivyo
anasema kuwa kati ya mambo ambayo katika
maisha anaona bado
kufanikiwa na hana ndoto ya
kukimbilia kuolewa wala katika
mahusiano na wanaume kwa sasa ni
kutokana na kutotimiza azma yake ya
kuchezea timu kubwa ya
soka wanawake nje ya
mkoa wa Iringa .
Kwani amesema katika mashindano ya UMISETA kwa jitihada zake binafsi amepata kuifungia
timu yake magoli matatu na kuwa
kwa sasa baada ya kuhitimu
elimu ya sekondari amepata
kuchezea timu mbali mbali kama Kwa kilosa FC , Sengo FC na timu
ya watuma salam mkoa
wa Iringa wanaume ambapo kwa
upande upande wa Sengo Fc nimepata kufunga magoli mawili .
Pia amesema kuwa anaomba
chama cha mpira wa miguu
wanawake Taifa iwapo
kuna nafasi ya kusajili
wachezaji wapya kuweza
kumtazama hata kumpa nafasi ya
majaribio ili aweze kuonyesha kipaji chake .
Mwandishi wa
makala haya alipata
kushuhudia kandanda safi iliyoonyeshwa na mchezaji huyo
Speransia wakati wa mchezo wa
kirafiki kati ya timu ya watuma
salam mkoa wa Iringa na timu ya
watangazaji wa kituo cha radio Furaha
Fm ambapo mchezaji Speransia
alipata kuchezea timu ya watuma salam na kuwa binti
pekee katika timu hiyo
ya wanaume ila aliweza
kuwahenyesha watangazaji wa
radio Furaha Fm japo ndio iliyoweza kushinda kwa magoli 2-0 dhidi ya watumasalam
Mwandishi wa
makala haya ni milimiki wa mtandao wa www.matukiodaima.com
|
No comments:
Post a Comment