Saturday, February 28, 2015

TUZO ZA WASANII BORA WA MUZIKI WA ZANZIBAR MWAKA 2015

Mkurugenzi wa Biashara Zanzibar Nd. Mohamed Baucha wa kulia akimkabidhi Tunzo ya Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya Nassir Hassan (Vanila) mara baada ya kuibuka mshindi, tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation LTD katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Hall  Bwawani Mjini Zanzibar.
 Mwanamitindo marufu wa Zanzibar Farouk Abdillahi akimkabidhi Tunzo ya Video bora mwaka ya Taraab Bi. Saada Nassor
 Mwanamuziki bora wa mwaka wa Afro poo Saidi Kitwana (Mabawa) kushoto akipokea tunzo kwa Katibu Mtendaji Bodi ya Sensa Zanzibar Nd. Suleiman Mbarouk.
 Meneja wa Zenji Entertainment Seif Moh'd (kushoto) akimkabidhi tunzo Mwanamuziki Bora wa kiume wa tarabu asili Cholo Ganun.
 Mwakilishi kutoka Baraza la Sanaa Zanzibar Maulid Madam akimkabidhi tunzo ya Mwanamuziki bora wa kike wa Tarab asili Bi. Rukia Ramadhan katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar.
 Meneja wa Fedha Z.M.C.L Bi. Saide Moh'd akimkabidhi tunzo Mwanamuziki bora wa mwaka wa kizazi kipya Riko Singo katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar.
 Mwanamuziki bora wa mwaka wa kike wa kizazi kipya Baby J akipokea tunzo kwa Meneja wa Z.M.C.L Tawi la Dar es Salam mara baada ya kuipuka kidedea tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Midia Corporation LTD iliopo Zanzibar.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wadau mbali mbali wakishuhudia wasanii wa Zanzibar wakipewa tunzo katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar.
 Wasanii wa kikundi cha Smart Comed Zanzibar wakitoa Burudani.
 Msani Mr Blue akitumbuiza katika Tamasha la Wasanii wa Zanzibar.
 Mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikiulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akimkabidhi tunzo ya muandaaji bora wa Tamasha Zanzibar Music Award mwaka 2015 Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa Redio ya Zenji FM Mohamed Seif Khatib katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwani Mjini Zanzibar. 
 Mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikiulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Zanzibar Midia Corporation LTD. Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

No comments: