Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini jijini Dar es Salaam leo.
Na Magreth Kinabo
SHERIA mpya ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 zitaanza kutumika rasmi kesho Septemba Mosi mwaka huu, hivyo watumiaji na watoa huduma waaswa kuzingatia sheria hizi ili kuepuka mkondo wa sheria.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
“Sheria hizi ni nzuri zitaanza kutumika Septemba Mosi mwaka huu,kuanzia saa 6.00 usiku . zina maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya Taifa letu,” alisema Profesa Mbarawa.
Aliongeza kuwa sheria hiyo ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 hazihitaji utungaji wa kanuni kwa kuwa iko wazi.
Alisema tayari wizara imeanza kuelimisha watu kuhusu sheria hiyo na itendelea kuwajengea uwezo wadau mbalimbali.
Profesa Mbarawa alisema sheria ya makosa ya mtando ya mwaka 2015 na Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa nayo, bali nchi mbalimbali zina sheria kama hiyo ,ambapo alitolea mfano Uingereza,India,Malaysia, Uganda na Korea ya Kusini.
Akizungumzia kuhusu madai sheria hiyo kuhusika na suala la Uchaguzi Mkuu, alisema si kweli, bali imekamilika katika kipindi hicho ndio maana baadhi ya watu wanadai hivyo.Aliongeza kwamba sheria hiyo imetunga ili kudhibiti matumizi ambayo si mazuri.
“ Mtu akitumiwa ujumbe akiupokea hapaswi kuisambaza kwani atakapousambaza atakuwa na amefanya kosa,”alisisitiza.
Aliyataja baadhi ya makosa kuwa ni usiri, usalama wa upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo kama vilekuingilia mawasiliano ya kompyuta au mifumo ya kompyuta kinyume cha sheria na wizi wa taarifa kimtandao.
Makosa dhidi ya kompyuta ikiwa ni pamoja na,udanganyifu kwa kutumia kompyuta,kugushi kwa kutumia kompyuta wizi wa utambulisho wa mtu binafsi mtandaoni, matumizi ya vifaa kinyume cha sheria.
Makosa yanayohusiana kimaudhui kama vile usambazaji wa ponografia, ponografia za watoto makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki, michezo ya kmari mtanadaoni kiunyume cha sheria, kashfa na habari za uongo na makosa dhidi ya haki na hati miliki.
Pia inatambua muungano wa makosa inajumuisha kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa kutumia mtandao.
Kwa upande wa sheria ya miamala ya kieletroniki ya mwaka 2015, baadhi ya makosa likiwemo la wajibu wa watoa huduma kwa walaji, bidhaa ,huduma au mawasiliano ambayo hayajaombwa na uhalali wa Muamala wa elektroniki.
Aliongeza kuwa kanuni za sheria hiyo zinatayarishwa zikiwa tayari zitangazwa na zitaanza kutumika wakati wowote.
No comments:
Post a Comment