Msanii Richard Maviko, (katikati) akiwa na wasanii wenzake wakitoa salamu maalum ya kumuunga mkono mgombea wa udiwani katika Kata ya Kilungule Said Fella, ambaye amezindua rasmi kampeni katika kata hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lameck Ditto akiongea kwa niaba ya wasanii wenzake ambao walikuwepo katika uzinduzi wa mgombea wa udiwani kata ya Kilungule iliyopo.
Asha Kigundula
WASANII mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya juzi walimuunga mkono Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yamoto Band na meneja wa Wanaume Family Said Fella, katika uzinduzi wa kampeni za kuwania Udiwani katika kata ya Kilungule, iliyopo Mbagala Dar es Salaam.
Katika mkutano huo ambao ulifurika vilivyo kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wakazi wa kata hioyo kujitokeza kwa wiki kumsikiliza mgombea huyo, ambaye alifanyika uzinduzi wake kwenye uwanja wa njia panda ya Chasimba Majimatitu B.
Baadhi wasanii hao ni Siti Almas, Amin Mwinyimkuu, Lameck Ditto, Rich Mavoko, Queen Darleen na meneja wa msanii Nassib Abdul Hamis Taletale 'Babu Tale'.
Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake Ditto aliwataka wakazi wa Maji matitu kutofanya makosa kwa kumpa mpinzani, wampe Said Fella ili awe diwani wao.
Alisema kila mtu atambue kuwa ukimchagua mtu wa CCM utakuwa umefanya jambo la muhimu kwa sababu ndiyo anayeweza kutelekeza ilani ya chama hicho.
Ditto alisema atamfahamu Fella ni mchapakazi hivyo kumpa kwake kata hiyo lazima iwe na mafanikio makubwa.
Alisema sehemu yoyote anayokuwepo Fella lazima iwe na mafanikio hivyo hata kama hiyo itakuwa moja ya kata zenye mafanikio makubwa.
"Naomba msifanye makosa kuchagua upinzani mchagueni Fella kuwa diwani wenu na mchagueni Issa Makungu kuwa mbunge wenu wa Mbagala na John Magufuli kuwa Rais wa Tanzania"alisema Ditto.
Akizungumza kwa upande wake Fella alisema anaitambua Kata hiyo ina matatizo mengi, hivyo akipata nafasi atahakikisha anaziofanyia kazi.
Fella alisema yeye ni mkazi wa eneo hilo ana amini kupata kwake nafasi kutatua mambo mengi kwa kuwa yupo karibu na viongozi wakubwa ambao atakuwa akikutana nao.
"Nitaweza kukutana na viongozi wakubwa na kutatua matatizo yetu ya huku Kilungule ambayo ninayofahamu vizuri kwa sababu nami ndiyo mkazi wa eneo hilo"alisema Fella.
No comments:
Post a Comment