Friday, December 14, 2018

Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana

Majid Abdulkarim
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu na Maafisa Mipango wote wa Halmashauri nchini kutumia taaluma zao katika kukuza uchimi wanchi ili kuleta matokeo bora kwa watanzania wanao watumikia.

Hayo yamebainishwa leo wakati  wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 yatakayo fanyika leo na kesho hapa jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli. Dk. Chaula amesema mafunzo hayo ni fursa kwa maafisa hao  kuhakikisha wanapata ujuzi wa kuweza kupata matokeo bora katika kukuza uchumi wanchi hii.
“Ili kufikia matokeo bora ya kukuza uchumi wa nchi hii mnatakiwa kuwa wabunifu kwa kuchukua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa ili kuinua uchumi nchi hii” Alisema Dk. Chaula.

Dk. Chaula ameongeza kuwa kila mtumishi wa Umma anadhamana kubwa kwa taifa hili , na dhamana yenyewe ni kuhakikisha tunawatumikia vyema watanzania wenzetu ili kuleta matokeo bora kwa nchi yetu kama Muhasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyo fanya mpaka leo kupitia matokeo yake tunamkumbuka. Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango OR-TAMISEMI, amesema kuwa kupitia mafunzo hayo maafisa hao watanufaika kwa kupata  uelewa wa kuandaa bajeti iliyobora na kuwa walimu wazuri kwa maafisa wengine katika maeneo yao ya kazi.

Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3), Dk. Emanuel Malangalila amesema kuwa maafisa hao wakatumie hujuzi huo watakao upata katika mafunzo haya ili kuleta matokeo bora katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kukuza uchumi katika halmashauri na mikoa yao. Akihitimisha kwa neno la shukurani kwa niaba ya washiriki wenzake Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Ruvuma Edmundi Godwell Siame amesema yote aloyaelekeza Dk.Chaula watayafanyia kazi ili kuhakikisha taaluma yao inakuza uchumi wanchi hii na kuhakikisha mafunzo hayo yanaleta matokeo bora katika kukuza uchumi wa nchi.
 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli. 
Baadhi ya  Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu na Maafisa Mipango  wa Halmashauri nchini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula (hayupo pichani) leo katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020, leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli.
 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) Dk. Emanuel Malangalila leo wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020, leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli.

No comments: