Saturday, December 15, 2018

WAZIRI UMMY ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA MAWAZIRI WA AFYA KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI INDIA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa 4 wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto (Partnership for Maternal, Newborn and Child Health Forum 2018) uliofanyika New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba, 2018.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Afya uliofanyika katika jiji la New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba, 2018.
Picha ya pamoja ya Mawaziri wa Afya pamoja na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo
Picha ya pamoja ya Mhe.Waziri Ummy Mwalimu na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano Maalum wa Afya ya Mama na Mtoto jijini New Delhi, India. Wa pili kukia ni Mhe. Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini India

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto} wakati wa Mkutano Maalum wa 4 wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto

Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA, Marekani, Bibi Natalia Kanem wakati wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto uliofanyika New Delhi, India


WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA MAWAZIRI WA AFYA KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO ULIOFANYIKA JIJINI NEW DELHI, INDIA KUANZIA TAREHE 12-14 DISEMBA, 2018.

Tanzania imeshiriki katika Mkutano Maalum unaojadili Afya ya Mama na Mtoto unaojulikana kama "4th Partnership for Maternal,Newborn and Child Health 2018" uliofanyika katika jiji la New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba,2018.

Katika Mkutano huu,Tanzania imewakilishwa na Mhe.Ummy Mwalimu,Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Mkutano huu ulifunguliwa na Mhe.Shri Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India tarehe 12 Desemba, 2018. Mkutano huu unawakutanisha pamoja Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kujadili changamoto zilizopo katika eneo la Afya ya Mama na Mtoto na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua changamoto hizo ili kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mkuu wa India alieleza mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza vifo vya mama mjamzito na watoto wachanga kufuatia mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali ya India na kuzitaka nchi washiriki kuweka mipango thabiti itakayotekelezeka katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Kwa upande wake, Mhe.Ummy Mwalimu alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kupunguza vifo vya mama na motto nchini Tanzania ikiwemo kuboresha utoaji wa huduma za afya katika ngazi za chini kwa kuboresha vituo vya Afya na kuajiri watumishi wapya kwenye maeneo yenye upungufu. Pia, ameeleza hatua nyingine zinazochuliwa na serikali ni kumlinda mwanamke kutokana na unyanyasaji wa jinsia ambapo madawati ya jinsia yamezinduliwa katika majeshi ya polisi na magereza ili kuhakikisha mwanamke analindwa wakati wote.

Kadhalika, Mhe.Ummy ameueleza mkutano huo mikatikati iliyopo nchini ya kuhakikisha uboreshaji na utoaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto unakuwa endelevu, ambapo aliweka bayana mipango hiyo ni pamoja na Kuongeza bajeti ya fedha katika sekta ya Afya, kuimarisha huduma za afya ya Mama na Mtoto kuanzia ngazi ya jamii.

Mipango mingine ni kuimarisha huduma kwa kuboresha vituo vya afya na kuajiri watumishi wanaohitajika, kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa walengwa pamoja na kutoa huduma stahiki ili kupunguza na kumlinda motto kutokana na maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Suala jingine la msingi zaidi ni kuilinda jamii kwa kutoa elimu ya kutosha kuhusu magonjwa ya saratani hususani saratani ya mlango wa kizazi ambayo sasa ni tatizo kubwa kwa akina mama duniani kote.

No comments: