Tuesday, October 30, 2018

HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akimkabidhi muongozo wa utendaji kazi Mwenyekiti wa Bodi ya sukari Tanzania Bi Mwamini Juma Malemi kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.


Na Mathias Canal-WK, Dodoma


Serikali imeipa changamoto Bodi ya sukari nchini kutekeleza majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kusisitiza kuhuisha uzalishaji wa sukari kwa wingi ili kuondokana na uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.

KaMpuni mbalimbali za uzalishaji wa sukari nchini zimeitikia wito wa Serikali wa kuongeza uzalishaji wa sukari ili nchi iweze kujitegemea kwa bidhaa hiyo pendwa kwa matumizi ya nyumbani na viwandani na ziada jambo litalopelekea Bodi ya sukari kusimamia majukumu yake ipasavyo ili kuondokana na uagizaji wa sukari nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jumatatu tarehe 29 Octoba 2018 na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma.

Waziri Tizeba amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari nchini Bi Mwamini Juma Malemi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi Kudhibiti sukari inayoingia nchini pasina utaratibu huku akiwataka kusimamia kwa weledi ufanisi katika uongezaji wa uzalishaji wa sukari nchini.

Aidha, Dkt Tizeba alisema kuwa ufungashaji wa sukari kwenye ujazo wowote ule kwa kutumia vifungashio vya aina yoyote kama vile mifuko yenye nembo ya SUPER FINE lazima uzingatie Sheria ya Sukari Namba 26 ya Mwaka 2001 ambayo inazuia ufungashaji wa sukari bila kupata idhini ya Bodi ya Sukari Tanzania.Alisema kuwa kwa mujibu wa Sheria hiyo ni marufuku kufungasha au kuuza sukari nyeupe kwa kuwa sukari hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani kama malighafi na sio kwa ajili ya matumizi ya kawaida majumbani.

Alisisitiza kuwa Mtu yeyote atakayebainika kuvunja Sheria hiyo ya Sukari, atawajibika kulipa faini ya kiasi cha fedha kisichopungua Shilingi Milioni Kumi (10,000,000) au kifungo cha miaka mitatu (3) jela au vyote kwa pamoja.“Kuna watu wanaolipa kodi ili wazalishe sukari lakini inapoingia sukari ambayo imepenya kinyemela hata ulinganifu wa soko madukani unakuwa mdogo kwa kuwa wanaoingiza bila utaratibu wanauza kwa kiasi cha chini kwa kuwa hawana uchungu wa kulipa kodi”

“Na hili sio jambo la hiara Bodi ni lazima isimame kidete kubaini mianya yote ya wafanyabiashara wanaoingiza sukari bila utaratibu” Alikaririwa Dkt Tizeba.Kuhusu sukari ya viwandani (Industial Sugar) Dkt Tizeba alisema kuwa, wafanyabiashara wamekuwa wakiomba kiwango kikubwa cha kibali cha uagizaji wa sukari lakini serikali ikihakiki kupitia kodi waliyolipa inakuwa haifanani na kiasi kilichoagizwa.

TTGA WATAMBUA MCHANGO WA WAONGOZA WATALII WALIOOKOA MTOTO WA FARU


Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Utalii Nchini (TTGA) Khalifa Msangi. Picha na Vero Ignatus
Edward Mfaume miongoni ya waliookoa mtoto Faru juzi asiuwawe na simba. Anafanya kampuni ya Kiboslope, akipokea cheti kutoka kwa Mwenuekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela. Picha na Vero Ignatus
Juma Rajabu Sumbi ni miongoni mwa wale waliookoa mtoto wa Faru mwaka jana Moru,Ni Freelencer kwa sasa anawafanya nyingi za Tawisa. simba. Anafanya kampuni ya Kiboslope, akipokea cheti kutoka kwa Mwenuekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela. Picha na Vero Ignatus
Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Utalii Nchini (TTGA) Khalifa Msangi. Haji Mbuguni Mjumbe wa kamati ya Mazingira Na mahusiano (TTGA) pamoja na Juma Rajabu Sumbi ni miongoni mwa wale waliookoa mtoto wa Faru mwaka jana 2017.Picha na Vero Ignatus
Pichani anaonekana Simba akimshambulia mtoto wa Faru,juzi ngorongoro, guides waliweza kumuokoa, TTGA wametambua mchango wao mkubwa wamefanya matukio yote mawili kuwapongeza guides na kuwapa vyeti. Picha kwa hisani ya TTGA.


Pichani anaonekana mtoto wa Faru aliyekuwa amezama kwenye matope serengeti Moru mwaka jana 2017 akaokolewa baada ya kuonwa na guides, wakawaita Rengers. Picha kwa hisani ya TTGA



Na. Vero Ignatus Arusha





Chama cha Waongoza Watalii Tanzania(TTGA) kimetoa vyeti kwa Madereva 12 waongoza watalii waliofanikiwa kumuokoa mtoto wa Faru asiuwawe na Simba katika Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa Ngoro ngoro na Hifadhi ya Taifa Serengeti.
 

Akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa TTGA Khalifa Msangi amesema kuwa waongoza watalii wa Tanzania wapo vizuri sana kwa kuwa ndio sekta inayoongoza katika kuingiza fedha za kigeni hapa nchini na kuchangia pato la Taifa (GDP).

Msangi amesema Waongoza watalii wana mchango mkubwa wa kuiletea taifa maendeleo kwa kuwa wakifanya kazi kwa Uzalendo,na kujituma basi ni wazi kuwa wanapelekea Idadi ya watalii nchini.

Aidha amesema Chama hicho kimeamua kuwapa Vyeti kama Ishara ya kutambua mchango uliofanywa na Madereva hao kwa kutambua kuwa mnyama faru ni mnyama Adimu na yupo mbioni kutoweka duniani.

“Kwanza tuwapongeze Madereva hawa kwa kazi kubwa ya Kizalendo walioifanya na madereva hawa wanastahili pongezi kwanza kwa kuhataraisha maisha yao na Wageni, ili tu kuweza kuokoa mtoto huyo wa faru ambaye mama yake alishamua kukimbia kutokana na kundi la samba,wamesfanya jambo la kizalendo sana”alisema Msangi.

Msangi amesema Madereva sita waliweza kumnusuru mtoto wa faru katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngoro ngoro na namna bora ya kuwaongezea madereva wengine sita mnamo mwaka 2017 waliweza kumnusuru mtoto wa faru ambaye pia alititi katika tope katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela amewataka Waongoza watalii nchini watambue kuwa wao ni Mabalozi wa nchi na waendelee kuuza nchi vizuri kwa kuwa kwa kufanya hizo wataweza kusaidia Juhudi za kuongeza Idadi ya watalii nchi kama Serikali inavyotamka kila siku.

Kwa Upande wao baadhi ya madereva waliotunikiwa Vyeti akiwemo Edward Mfaume na Juma Sumbi wameiomba serikali kupitia Mamlaka za Hifadhi zilizopo nchini kutambua kuwa wao sio Maadui zao bali ni wafanyakazi wenzao hivyo kuomba ushirikiano wa dhati kwa kuwa rasilimali zilizopo zipo kwa Ajili ya kunufaisha Taifa.

Hata hivyo wameongeza kuwa Madereva wa Utalii wamekuwa wakifika kila mahali tofauti na Wafanyakazi wa hifadhi kwa kuwa wapo wachache na Waongoza watalii kuwa wengi hivyo kufika kila mahali ndio maana matukio hayo huwakuta Waongoza watalii na sio Askari wa Wanyamapori (Rangers).

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 30,2018

















Monday, October 29, 2018

DDkt.Kigwangalla awashukuru viongozi wa dini,Wazee wa mila NZEGA:

Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mkewe Dkt. Bayoum Kigwnagalla wakisindikizwa na Wazee wa mila wa Lusu wakati alipowasili kutoa shukrani na dua kwa wananchi wa jimbo lake hilo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mbunge wa jimbo la Manonga, Seif Gulamali wakifuatilia kwa makini wakati wa tukio la kutoa shukrani na dua maalum iliyoandaliwa kwa wananchi wa jimbo lake hilo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifanyiwa tambiko la kichifu na Watemi wakiongoza na Chifu Ng’wana Ng’washi wa Wasukuma wakati wa kutoa dua na shukrani.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokewa na Wananchi wa Jimbo hilo wakati alipowasili kwenye Kata ya Lusu wakati wa kutoa dua na shukrani.
…………………………..
Dkt. Kigwangalla: “Sasa naanza safari mpya”

WAZIRI wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewashukuru viongozi mbalimbali wa dini Nchini kwa dua na maombi yao kwa kipindi chote alichopata ajali hadi sasa kupona na kurejea tena na majukumu yake.

Akizungumza katika mkutano wake wa pili uliofanyika katika Kata ya Lusu Tarafa ya Nyasa iliyopo kwenye jimbo lake hilo la Nzega Vijijini, jana Oktoba 28, 2018,  Dkt. Kigwangalla amewashukuru viongozi hao wa dini pamoja na Wazee wa Mila kwani wao wamekuwa chachu kwenye kupona kwake tokea alipolazwa Hospitali kwa zaidi ya miezi miwili kwa kuuguza majeraha ya mwili wake kutokana na ajali ya gari aliyopata Agosti 4, mwaka huu.
Amesema viongozi wa hao wa dini pamoja na  Wananchi kila mmoja kwa nafasi yake walikuwa ni wa kipekee na dua zao zimeweza kusaidia  na kwa sasa amerejea kutoa shukrani na kupokea dua zao hizo kwani kwa sasa ameanza kufanya kazi.

“Kwa sasa nimeanza kurudi kwenye majukumu yangu kama kawaida. Kwa hivyo nikaona kabla ya kuanza kuonekana nikiruka huku na kule kwenye majukumu ya kiwizara, nikasema hapana nirudi kwanza nyumbani nipate dua za wazazi wangu, dua za wazee na viongozi wa dini.
Kwa tukio lile kwa sisi tunaoamini,  ni mkono wa Mungu ulikuwa mahala pale” amesema Dkt. Kigwangalla.

Aidha, Dkt. Kigwangalla amewatoa hofu wananchi wa jimbo lake juu ya watu waliokuwa wakipitapita jimboni kwa lengo la kulinyemelea na kutoa maneno ya kumkatisha tamaa.“Kwa waliokuwa wanatembea na wakikesha usiku kucha wakisubiri nife wameanguka. Mungu amesimama  mbele yangu, mimi ni mzima naendelea kutekeleza majukumu yangu mdogomdogo mpaka nitakapokuwa imara kabisa. Sasa naanza upya” amesema Dkt. Kigwangalla.
Pia amewahakikishia wananchi hao kuwa kazi za maendeleo ya jimbo hilo zinaendelea na wasaidizi wake wa ofisi ya Mbunge inaendelea kuratibu kwa ukaribu kabisa na  milango ipo wazi.

Katika hatua nyingine Wazee wa Mila na Watemi wakiongoza na Chifu Ng’wana Ng’washi wa Wasukuma walifanya tambiko la kichifu la kumtambikia ili akawe tayari kwa kazi za kulitumikia Taifa katika majukumu ya Kibunge na Uwaziri.

 Dkt. Kigwangalla yupo katika ziara ya kutoa shukrani na dua maalum kwa Wananchi wa jimbon lake hii ni tokea kurejea kutoka kuuguza majeraha ya mwili wake tokea kupata ajali Agosti 4, mwaka huu wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi Mkoani Manyara.
NA ANDREW CHALE, NZEGA

SACOSS NCHINI ZAASWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WANACHAMA


Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma. 
Meza Kuu wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Mjumbe wa Mkutano Mkuu akitoa hoja ya kuthibitisha notisi kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Mlezi wa Magereza Saccoss ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa. 
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini Bw. Philemon Chilewa akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kwenye Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha. 
Mlezi wa Magereza Saccoss ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiagana na Mgeni rasmi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa baada ya ufunguzi wa Mkutano huo. 
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(waliosimama). Walioketi(wa tano toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos, SACP. Mbaraka Semwanza(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tano unaofanyika kwa siku moja Mkoani Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS nchini akisalimiana na Wajumbe mbalimbali ambao ni Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipowasili kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 29 – 30, 2018 jijini Dodoma. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza(kulia) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia ukumbini tayari kwa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga. Picha zote na Jeshi la Magereza





Na Lucas Mboje, Dodoma

VYAMA vya ushirika nchini vimetakiwa kuendelea kutoa elimu ya ushirika mara kwa mara kwa wanachama wake ili kujenga uelewa wakutosha kuhusu sheria, kanuni na masharti mbalimbali ya ushirika.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa sita wa mwaka wa Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza nchini, Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa ametoa rai hiyo kwa vyama vya ushirika nchini kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwani ni muhimu katika uendeshaji wa shughuli za chama.

Amesema kuwa elimu ya ushirika isitolewe tu kwa watendaji na viongozi wa chama bali itolewe kwa wanachama wa ushirika ili wajue uendeshaji wake na kunufaika na huduma zitolewazo na chama. “Vyama vingi vya ushirika hapa nchini vimekufa kwa kukosa elimu ya ushirika, niwaombe sana wasimamizi wa ushirika muendelee kutoa elimu kwa wanachama”. Amesisitiza Kaimu Mrajis Chilewa.

Aidha, Kaimu Mrajis Chilewa amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria ya ushirika pamoja na kuheshimu na kusikiliza maoni ya wanachama kwani wao ndo wenye mali.

Ameongeza kuwa kwakuwa Mkutano huo utahusisha uchaguzi wa mjumbe mmoja wa Bodi, Bw. Philemon Chilewa pia amewaasa wajumbe wa Mkutano huo kuwa makini katika uchaguzi huo kwa kuchagua mtu mwenye weledi na mwenye mapenzi ya dhati na ushiriki wao ili aweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.

Awali, akimkaribisha Mgeni rasmi katika Mkutano huo, Mlezi wa Magereza Saccos, ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini – CGP Phaustine Kasike amesema kuwa idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa zaidi ya bilioni 20 hivi sasa.

Pia, Mlezi wa Magereza Saccos, CGP Kasike ameongeza kuwa pamoja na changamoto za mabadiliko ya kiuchumi, kumekuwa na ushindani mkubwa wa Taasisi za kifedha katika kutoa huduma za mikopo kwa wanachama.

Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza nchini kilianzishwa mwaka 2005 kwa lengo la kupunguza umasikini na kuinua hali ya maisha ya watanzania hususani watumishi wa Jeshi la Magereza.

Italia yaiahidi Afrika Ushirikiano wa kiuchumi


Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia na Afrika wameazimia kukuza na kuimarisha Ushirikiano katika nyanja mbalimbali, hususan biashara na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kweli barani Afrika.

Mawaziri hao walifikia azimio hilo wakati wa mkutano wa pili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia na Afrika uliofanyika Farnesina, Italia tarehe 25 Oktoba 2018 na kuhudhuriwa na Mawaziri wa zaidi ya nchi 40 akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). 

Mawaziri hao walikutana kwa madhumuni ya kujadili kwa pamoja changamoto zinazohusu usalama, uhuru, amani, demokrasia na namna wadau wa Italia (wenye viwanda, Wafanyabiashara, wanazuoni na taasisi zisizo za kiserikali) watakavyoweza kushiriki katika kukuza uchumi barani Afrika hasa katika sekta ya uwekezaji na biashara. 

Katika hotuba yake kwenye mkutano huo ambao ulifunguliwa na Rais wa Italia, Mhe. Sergio Mattarella, Mhe Waziri Mahiga alisisitiza suala la amani kuwa ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi barani Afrika. Aidha, alieleza umuhimu wa Jumuiya za Kikanda katika kusuluhisha migogoro mbalimbali inayotokea kwenye Bara la Afrika. Katika hilo, alijulisha jitihada zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kusuluhisha mgogoro nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Sanjari na mkutano huo, Waziri Mahiga alipata fursa ya kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Mhe Enzo Moavero na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Gilbert F. Houngbo.

Kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Viongozi hao walikubaliana kuwa, kuandaliwe Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Tanzania na Italia ya kufanya majadiliano ya mara kwa mara yenye lengo ya kukuza ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, utalii, elimu na utamaduni.

Kuhusu mazungumzo na Rais wa IFAD, wawili hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Mfuko huo kwenye maeneo makuu mannne ambayo ni Huduma za kifedha kwa wakulima wadogo, kuwajengea uwezeo vijana ili waweze kufanya kilimo kama sehemu ya ajira, kuboresha sekta ya mifugo pamoja na masuala ya lishe bora. 

Aidha, Rais wa IFAD alimuahidi Mhe Waziri kuwa mfuko huo utaendelea kushirikiana vizuri na serikali ya Tanzania hata kwenye miradi inayoendelea ikiwemo Programu ya Miundombinu ya masoko, uongezaji wa thamani na kuwawezesha wakulima wadogo wa vijijini kifedha (Marketing Infrastructure, Value Addition and Rural Finance-MIVRAF). Madhumuni ya programu hiyo ni kupunguza umasikini na kuharakisha ukuaji wa uchumi vijijini ili kuboresha kipato na usalama wa chakula kwa jamii ya watu wa vijijini.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam, Tanzania
29 Oktoba 2018 

NAIBU WAZIRI HASUNGA AFUNGA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MTANZANIA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akizungumza na  Athumani Issa wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akiwasaidia akina Mama wa kabila la Wamwela  kutwanga nafaka  wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akipewa kibuyu chenye  pombe na Halima Abdallah ambacho kimekuwa kikitumiwa na kabila hilo kunywea pombe  wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akiangalia baadhi ya mabaki ya samaki aina ya nguva aliyekutwa amekufa kando kando mwa bahari ya Hindi mkoani Lindi wakati alipotembelea mabanda  kabla ya   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga (katikati) akiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakiwa wameongozana na   Wakurugenzi pamoja na Wazee wa kabila la Wamwela wakati kutembelea nyumba ya kabila la Mwela katika kijiji cha Makumbusho  kabla ya kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es salaam 
Baadhi ya vikundi vya ngoma vikitumbuiza wakati wa  kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika kijiji cha Makumbusho    jijini Dar es salaam 


                              ( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)   

SWEDEN YASAINI MAKUBALIANO MAPYA NA SHIRIKA LA FEMINA, YATOA BILIONI 4.5 KUENDELEZA MPANGO MKAKATI 2018/20

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

UBALOZI  wa Sweden nchini umesaini makubaliano na shirika la Femina Hip ikiwa ni msaada wa kutekeleza mpango mkakati wa Femina Hip kwa mwaka 2018/2020. Katika makubaliano hayo  jumla ya shilingi bilioni 4.5 zimetolewa kwa shirika hilo ili kuendelea kukuza elimu ya afya ya uzazi, haki, uwezeshaji kiuchumi na uraia kwa vijana nchini. 

Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Ulf Kallstig na mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang katika ofisi za ubalozi wa Sweden leo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa makubaliano hayo Ulf Kallstig amesema kuwa mchango wa Sweden utaboresha mipango ya Femina Hip inayolenga kuwawezesha vijana kutoka kona zote nchini hasa katika kuwajengea juhudi za kuwawezesha, kuboresha maisha ya vijana nchini na kuwajengea tabia ya uwajibikaji.

Aidha amesema kuwa, "Vijana wana jukumu muhimu katika kuiendesha Tanzania kuelekea taifa la uchumi wa kati wa viwanda na ni muhimu kwetu kuzishirikisha sauti za vijana katika mijadala ya kimaendeleo inayolenga kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanafanikiwa pamoja na ari ya ushirikishwaji na ustawi wa Tanzania" ameeleza Ulf.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang amesema kuwa, " Femina Hip inashukuru kwa ushirikiano na ubalozi wa Sweden, tutaendelea kuchangia kazi zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba katika kizazi hiki cha vijana hususani wasichana wanalindwa na kusaidiwa kuwa raia wema wenye kuwajibika ipasavyo" ameeleza Dkt. Minou.

Dkt. Minou amesema kuwa, asasi za kiraia ni chombo muhimu na zina nafasi ya kipekee katika kuwapa sauti wananchi na kwa Femina kwa miaka mingi imekuwa chombo kinachoaminiwa kwa kuimarisha kitengo cha uhamasishaji na ushirikiano kwenye mitandao ya shule za sekondari na mashirika ya ndani katika kufikisha ujuzi muhimu vijana kila kona nchini.

Mkurugenzi wa habari wa Femina Amabilis Batamula amesema kuwa, wakielekea miaka 20 ya Femina wanaishukuru sana serikali ya Tanzania na Sweden kwa kuwaunga mkono na  hadi sasa wanawafikia watu Milioni 15 kwa mwaka na kuna  zaidi ya klabu 2340 za Fema kwa  katika shule za sekondari kote nchini.

Aidha Batamula ameishukuru serikali kwa kuruhusu na kutambua mchango wa asasi za kiraia  ikiwepo Femina katika kuwajenga vijana katika ujenzi wa taifa.

Pia amesema kuwa katika wiki ya vijana iliyohitimishwa kitaifa Mkoani Tanga, mgeni rasmi Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipendekeza uwepo wa Klabu za Fema katika shule zote za serikali na binafsi nchini na wao wanasubiri mwitiko kutoka kwa vijana katika shule mbalimbali nchini.

Mwisho ameushukuru ubalozi wa Sweden kwa kuwa marafiki wazuri kwa Serikali na Femina na kwa msaada walioupata leo utawasaidia sana vijana.
Mkurugenzi mtendaji wa Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam ambapo ametoa shukurani kwa ubalozi wa  Sweden kwa  kuonyesha ushirikiano ambao utaiwezesha shirika la Femina kuendekeza juhudi za kuwawezesha kuboresha Maisha ya  vijana wa Tanzania na kuwajengea tabia ya uwajibikaji.
  Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden Ulf Kallstig pamoja na Mkurugenzi mtendaji  wa Femina Hip Dkt.Minou Fuglesang leo Jijini Dar es Salaam katika ubalozi wa  Sweden wakisaini mkataba wa makubaliano Mapya ya shilingi bilioni 4.5 za Kitanzania na shirika la Femina Kwa kipindi cha mwaka 2018-2020 ili kuboresha  mipango ya shirika hilo.
Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden Ulf Kallstig wakikabidhiana mkataba huo na Mkurugenzi mtendaji wa Femina  Dkt Minou Fuglesang pamoja na  Mkurugenzi  wa  habari wa shirika hilo Amabili  Batamula baada ya zoezi la utiaji saini kumalizika leo Jijini Dar es Salaam katika ubalozi wa Sweden.