Monday, October 29, 2018

SACOSS NCHINI ZAASWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WANACHAMA


Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma. 
Meza Kuu wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Mjumbe wa Mkutano Mkuu akitoa hoja ya kuthibitisha notisi kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Mlezi wa Magereza Saccoss ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa. 
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini Bw. Philemon Chilewa akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kwenye Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. 
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha. 
Mlezi wa Magereza Saccoss ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiagana na Mgeni rasmi Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa baada ya ufunguzi wa Mkutano huo. 
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(waliosimama). Walioketi(wa tano toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos, SACP. Mbaraka Semwanza(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tano unaofanyika kwa siku moja Mkoani Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS nchini akisalimiana na Wajumbe mbalimbali ambao ni Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipowasili kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 29 – 30, 2018 jijini Dodoma. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mbaraka Semwanza(kulia) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia ukumbini tayari kwa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga. Picha zote na Jeshi la Magereza





Na Lucas Mboje, Dodoma

VYAMA vya ushirika nchini vimetakiwa kuendelea kutoa elimu ya ushirika mara kwa mara kwa wanachama wake ili kujenga uelewa wakutosha kuhusu sheria, kanuni na masharti mbalimbali ya ushirika.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa sita wa mwaka wa Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza nchini, Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Philemon Chilewa ametoa rai hiyo kwa vyama vya ushirika nchini kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwani ni muhimu katika uendeshaji wa shughuli za chama.

Amesema kuwa elimu ya ushirika isitolewe tu kwa watendaji na viongozi wa chama bali itolewe kwa wanachama wa ushirika ili wajue uendeshaji wake na kunufaika na huduma zitolewazo na chama. “Vyama vingi vya ushirika hapa nchini vimekufa kwa kukosa elimu ya ushirika, niwaombe sana wasimamizi wa ushirika muendelee kutoa elimu kwa wanachama”. Amesisitiza Kaimu Mrajis Chilewa.

Aidha, Kaimu Mrajis Chilewa amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria ya ushirika pamoja na kuheshimu na kusikiliza maoni ya wanachama kwani wao ndo wenye mali.

Ameongeza kuwa kwakuwa Mkutano huo utahusisha uchaguzi wa mjumbe mmoja wa Bodi, Bw. Philemon Chilewa pia amewaasa wajumbe wa Mkutano huo kuwa makini katika uchaguzi huo kwa kuchagua mtu mwenye weledi na mwenye mapenzi ya dhati na ushiriki wao ili aweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.

Awali, akimkaribisha Mgeni rasmi katika Mkutano huo, Mlezi wa Magereza Saccos, ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini – CGP Phaustine Kasike amesema kuwa idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa zaidi ya bilioni 20 hivi sasa.

Pia, Mlezi wa Magereza Saccos, CGP Kasike ameongeza kuwa pamoja na changamoto za mabadiliko ya kiuchumi, kumekuwa na ushindani mkubwa wa Taasisi za kifedha katika kutoa huduma za mikopo kwa wanachama.

Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza nchini kilianzishwa mwaka 2005 kwa lengo la kupunguza umasikini na kuinua hali ya maisha ya watanzania hususani watumishi wa Jeshi la Magereza.

No comments: