Tuesday, October 30, 2018

TTGA WATAMBUA MCHANGO WA WAONGOZA WATALII WALIOOKOA MTOTO WA FARU


Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Utalii Nchini (TTGA) Khalifa Msangi. Picha na Vero Ignatus
Edward Mfaume miongoni ya waliookoa mtoto Faru juzi asiuwawe na simba. Anafanya kampuni ya Kiboslope, akipokea cheti kutoka kwa Mwenuekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela. Picha na Vero Ignatus
Juma Rajabu Sumbi ni miongoni mwa wale waliookoa mtoto wa Faru mwaka jana Moru,Ni Freelencer kwa sasa anawafanya nyingi za Tawisa. simba. Anafanya kampuni ya Kiboslope, akipokea cheti kutoka kwa Mwenuekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela. Picha na Vero Ignatus
Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Utalii Nchini (TTGA) Khalifa Msangi. Haji Mbuguni Mjumbe wa kamati ya Mazingira Na mahusiano (TTGA) pamoja na Juma Rajabu Sumbi ni miongoni mwa wale waliookoa mtoto wa Faru mwaka jana 2017.Picha na Vero Ignatus
Pichani anaonekana Simba akimshambulia mtoto wa Faru,juzi ngorongoro, guides waliweza kumuokoa, TTGA wametambua mchango wao mkubwa wamefanya matukio yote mawili kuwapongeza guides na kuwapa vyeti. Picha kwa hisani ya TTGA.


Pichani anaonekana mtoto wa Faru aliyekuwa amezama kwenye matope serengeti Moru mwaka jana 2017 akaokolewa baada ya kuonwa na guides, wakawaita Rengers. Picha kwa hisani ya TTGANa. Vero Ignatus Arusha

Chama cha Waongoza Watalii Tanzania(TTGA) kimetoa vyeti kwa Madereva 12 waongoza watalii waliofanikiwa kumuokoa mtoto wa Faru asiuwawe na Simba katika Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa Ngoro ngoro na Hifadhi ya Taifa Serengeti.
 

Akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa TTGA Khalifa Msangi amesema kuwa waongoza watalii wa Tanzania wapo vizuri sana kwa kuwa ndio sekta inayoongoza katika kuingiza fedha za kigeni hapa nchini na kuchangia pato la Taifa (GDP).

Msangi amesema Waongoza watalii wana mchango mkubwa wa kuiletea taifa maendeleo kwa kuwa wakifanya kazi kwa Uzalendo,na kujituma basi ni wazi kuwa wanapelekea Idadi ya watalii nchini.

Aidha amesema Chama hicho kimeamua kuwapa Vyeti kama Ishara ya kutambua mchango uliofanywa na Madereva hao kwa kutambua kuwa mnyama faru ni mnyama Adimu na yupo mbioni kutoweka duniani.

“Kwanza tuwapongeze Madereva hawa kwa kazi kubwa ya Kizalendo walioifanya na madereva hawa wanastahili pongezi kwanza kwa kuhataraisha maisha yao na Wageni, ili tu kuweza kuokoa mtoto huyo wa faru ambaye mama yake alishamua kukimbia kutokana na kundi la samba,wamesfanya jambo la kizalendo sana”alisema Msangi.

Msangi amesema Madereva sita waliweza kumnusuru mtoto wa faru katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngoro ngoro na namna bora ya kuwaongezea madereva wengine sita mnamo mwaka 2017 waliweza kumnusuru mtoto wa faru ambaye pia alititi katika tope katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTGA Christopher Nzela amewataka Waongoza watalii nchini watambue kuwa wao ni Mabalozi wa nchi na waendelee kuuza nchi vizuri kwa kuwa kwa kufanya hizo wataweza kusaidia Juhudi za kuongeza Idadi ya watalii nchi kama Serikali inavyotamka kila siku.

Kwa Upande wao baadhi ya madereva waliotunikiwa Vyeti akiwemo Edward Mfaume na Juma Sumbi wameiomba serikali kupitia Mamlaka za Hifadhi zilizopo nchini kutambua kuwa wao sio Maadui zao bali ni wafanyakazi wenzao hivyo kuomba ushirikiano wa dhati kwa kuwa rasilimali zilizopo zipo kwa Ajili ya kunufaisha Taifa.

Hata hivyo wameongeza kuwa Madereva wa Utalii wamekuwa wakifika kila mahali tofauti na Wafanyakazi wa hifadhi kwa kuwa wapo wachache na Waongoza watalii kuwa wengi hivyo kufika kila mahali ndio maana matukio hayo huwakuta Waongoza watalii na sio Askari wa Wanyamapori (Rangers).

No comments: