Pichani
kulia ni Muendesha boda boda Magembe Daniel akiwa na Mama yake Mzazi
Mama Magembe,wakiwa wameshika mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi
milioni 140 baada ya kuibuka mshindi wa mchezo wa kubahatisha TatuMzuka
hivi karibuni
Magembe
ambaye ni Mkazi wa Kibiti-Rufiji anamshukuru Mama yake Mzazi kwa kumlea
vizuri,kama vile haitoshi anamshukuru zaidi kwa kumnunulia Piki piki na
kuifanyia biashara,anasema na ndi maana mara baada ya kupata taarifa
kuwa nimeshinda mchezo wa TatuMzuka,Mtu kwanza kabisa kumtaarifu alikuwa
ni mama yake mzazi, kuwa ameshinda mchezo wa kubahatisha wa
TatuMzuka,anasema mama yake hakuamini lakini alimtia moyo yakuwa na
subira zaidi ili kubaini kama ni kweli ama la.
"Vijana
wenzangu ninaofanya nao kazi wamenisihi nitulie,kwa sababu mara nyingi
baada ya kuipata fedha nyingi, vijana hukengeuka,nilijiwekea nadhiri
kuwa nikipata fedha nyingi ntafanya biashara zangu,lakini ndoto yangu
kubwa ni kujenga nyumba kubwa ambayo ntaishi na familia yangu,ingawaje
bado sijaoa",aliongeza kusema Magembe.
Pichani
kulia ni Afisa Mkuu wa Masoko-Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha kijana
mwendesha boda boda,Mageme Daniel aliyejinyakulia kitita cha shilingi
milioni 140 za TatuMzuka hivi karibuni jijini Dar
Maganga
alisema kuwa mpaka sasa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka umevunja
historia kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 20 za Kitanzania,ambazo
zimekwenda kwa Washindi mbalimbali wa Mzuka Jackpot,Washindi wa Mzuka
Daily na washindi mbalimbali,ambapo washindi milioni 58 wamejitokeza
kujishindia mamilioni ya TatuMzuka.
"Tatumzuka
imeendelea kuwa fahari ya wachezaji wa mchezo wa kubahatisha kwa sababu
ina uwezo wa kutoa washindi wengi,hivyo nawaomba Watanzania waendelee
kucheza mchezo huu,na kwamba hamasa kubwa ni kuendelea kuwafikia
washiriki wengi zaidi kila kona ya nchi yetu,kuhakikisha mchezo huu
unakuwa fahari ya Watanzania,wenye kuwaletea tija ya kimaendeleo katika
nyanja mbalimbali",alisema Maganga.
Pichani kushoto ni Afisa Mkuu wa Masoko-Tatu Mzuka Sebastian Maganga akiwa pamoja na kijana
mwendesha boda boda,Magembe Daniel aliyejinyakulia kitita cha shilingi
milioni 140 za TatuMzuka hivi karibuni jijini Dar.
No comments:
Post a Comment