Programu
ya Football for Friendship (F4F) 2018 inabadilisha ndoto ya kombe la
Dunia la FIFA kuwa kweli kwa Zipora Mollel pamoja na Laigwanani Lomayani
Mollel, vijana hao kutoka kabila la Maasai wamechaguliwa kwenda Russia
kuiwakilisha Tanzania huku gharama zote zikibebwa na F4F.
F4F
ni programu ya kimataifa ya watoto ya kila mwaka inayoratibiwa na
kampuni ya kimataifa Gazprom ambayo inaunga mkono miradi ya kijamii
ulimwenguni na kuweka viwango vipya kuhusiana na sera za kijamii.
Inatarajiwa
kufanyika Moscow, Russia kuanzia Juni 8-15, kuelekea michuano ya Kombe
la Dunia, lengo la programu hii ni kutangaza maadili yanayohusiana na
mpira wa miguu kwa vijana wadogo ikiwa ni pamoja na kuheshimu mila,
utaifa na usawa.
Laigwanani
Mollel ataiwakilisha Tanzania akiwa mchezaji anayechipukia wakati
Ziporah Mollel yeye atashiriki kama mwanahabari chipukizi, watakuwa
wawakilishi wa nchi kwenye kombe la Dunia licha kwamba timu ya taifa
imeshindwa kufuzu katika mashindano hayo. Wataungana na wachezaji wenye
umri wa miaka 12 pamoja na waandishi kutoka mataifa 210 na kujumuika
kushiriki programu ya siku nane (8).
Mwaka
2018 mataifa mapya 147 na kanda zitashiriki programu ya F4F
inayohusisha watu 3,700 wenye umri kati ya miaka 12 na 16 walioshiriki
program hiyo kwa zaidi ya miaka mitano.
Laigwanani
Mollel na Ziporah (miaka 12) wataambana na meneja wa uendeshaji kutoka
Lengo Football Academy, Bw. Amani Mzava, kocha Bw. Alvin Girelisu. Lengo
Football Academy inajivunia kushirikiana na Clouds FM na Clouds TV.
Mwanahabari mashuhuri wa michezo Shaffih Dauda kutoka Clouds FM/TV
ataongozana na msafara wa watanzania kwenda Russia kuiwakilisha
Tanzania.
Jumla
ya timu 32 za kirafiki za kimataifa zitashindana katika mechi za
kirafiki kucheza mpira wa miguu 'Friendship World Championship' Juni 12,
2018. Kuelekea mashindano hayo kila mchezaji atafundishwa makocha
watoto ambao ambao ni wachezaji wenye umri kati ya miaka 14 na 16 kutoka
mataifa tofauti.
Zaidi
ya vyombo vya habari 5,000 kutoka sehemu mbalimbali Duniani vitaripoti
progamu hiyo kitu ambacho kinatazamiwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni
elimu ya kipekee. Vyombo vya habari vitashirikisha waandishi wa habari
watoto wa F4F wenye umri wa miaka 12 kutoka nchi 211 wataripoti habari
zao za F4F ambazo zitasambaa ulimwengu mzima.
Fursa
hii ni matokeo ya F4F (RUS) programu inayoendelea kwa kushirikiana na
Lengo Football Academy (TZ) ambayo imeidhinishwa na TFF. Lengo Football
Academy ni shirika la Tanzania na Australia linalosaidia vijana wa
Arusha, Tanzania kwa kutumia nguvu ya mpira wa miguu kutengeneza njia
kwa vijana kufikia ndoto zao kwenye maisha ndani na nje ya uwanja. Lengo
Football Academy inashirikiana na Football for Friendship (F4F)
kusaidia nchi 12 kuhudhuria programu ikijumuisha Tanzania, Australia,
New Zealand pamoja na nchi 9 za visiwa vya Pasific.
Emanuel
Saakai, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lengo Football Academy
amesema, "tunafurahi kushirikiana na Football for Friendship na kupata
fursa ya kutoa vijana wawili kutoka kwenye Academy yetu ya Arusha kwenda
kupata uzoefu. Tumepata upendeleo kuandaa programu hii kwa nchi nyingi
Duniani kote, hakika tutaiweka Tanzania kwenye ramani ya Russia 2018.
No comments:
Post a Comment