Kaimu
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bathow Mmuni, akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, wakati wa Semina ya Waajiri kuhusu Sheria
Mpya ya Hifadhi ya Jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa
na NSSF.
Meneja
Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke,
James Oigo, akisisitiza jambo wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria
mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na
kuandaliwa na NSSF. Kulia ni Kaimu Meneja Kiongozi NSSF Mkoa wa Ilala,
Christine Kamuzora na Kaimu Meneja Bima ya Afya NSSF, Zakia Mohamed.
Kaimu
Meneja Bima ya Afya NSSF, Zakia Mohamed, akizungumza wakati wa semina
ya waajiri kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini
Dar es Salaam na kuandaliwa na NSSF.
Kaimu
Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Salim Kimaro, akizungumza wakati wa semina ya waajiri
kuhusu sheria mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam
juzi na kuandaliwa na NSSF.
Meneja
Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke,
James Oigo, akitoa mada wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria mpya
ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi na kuandaliwa
na NSSF.
Baadhi ya Waajiri wakiwa katika semina.
Meneja
Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke,
James Oigo, akijibu maswali wakati wa semina ya waajiri kuhusu sheria
mpya ya hifadhi ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi na
kuandaliwa na NSSF. Kushoto ni Meneja Kiongozi NSSF Mkoa wa
Kinondoni,Marko Mgheke na Kaimu Meneja wa Uendeshaji NSSF, Omary Mzia.
Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendesha semina kwa waajiri wa
Mkoa wa Temeke katika jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na waajiri
takrabani 200 waliopo katika mkoa wa Temeke kwa mgawanyo wa mipaka ya
NSSF.
Akifungua
Semina hiyo juzi, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bathow Mmuni,
aliwaambia waajiri kwamba sheria mpya ya hifadhi ya jamii imeshasainiwa
na Rais na sasa zimebakia taratibu za kiuendeshaji.
‘Semina
hizo ambazo zimepangwa kuendelea nchi nzima zikiwa na lango la
kuwahimiza waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati ili
kuliwezesha Shirika kulipa mafao ya wanachama kwa ufanisi, kuzijua
changamoto zinazowakumba waajiri na kujibu hoja nyingi walizokuwa nazo
waajiri kuhusu uelekeo mpya baada ya Mifuko ya Hifadhi ya jamii
kuunganishwa na kubaki miwili yaani NSSF na PSSSF’, alisema Mmuni.
Naye
Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, James Oigo, akiwasilisha mada
kwa waajiri hao alisema, Sheria mpya imefafanua kuwa Mfuko mpya wa
waajiriwa wa sekta ya Umma (PSSSF) utakuwa unahudumia waajiriwa wote
waliopo katika sekta ya umma wakati NSSF itahudumia waajiriwa wote wa
sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Akifafanua
kuhusu Sheria hiyo Oigo alisema kuwa, NSSF ni mfuko pekee utakaokuwa
unahudumia wanachama Waajiriwa wote wa sekta binafsi, Waajiriwa wote wa
Kigeni walioajiriwa Tanzania Bara, Waaajiriwa wote waliajiriwa katika
taasisi za kimataifa zinazofanya kazi Tanzania Bara, Watu wote
waliojiajiri wenyewe na wale wa sekta isiyo rasmi.
Aidha
amefafanua kuwa,waajiriwa wote ambao wataajiriwa baada ya sheria hii
kuanza ndio watakuwa katika mfuko ama wa PSSSF endapo wanaajiriwa katika
sekta ya umma na NSSF endapo wanaajiriwa katika sekta binafsi, Aidha
kwa wale ambao walishaajiriwa wakati sheria hii inaanza ambapo walikuwa
katika mifuko iliyounganishwa watakuwa wanachama wa mfuko wa PSSSF bila
kujali wapo setka binafsi au ya umma na wale ambao walikuwa wanachama wa
NSSF watabakia kuwa wanachama wa NSSF bila kujali sekta wanayotoka.
Alizidi kufafanua kuwa kanuni ya ulipaji mafao na idadi ya mafao
yatakuwa ya aina moja kwa mifuko yote miwili.
Wakati
huo huo, Meneja wa NSSF Mkoa wa Kinondoni, Marco Magheke, alisema,
Shirika limejipanga kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama wake
na kuwahakikishia waajiri kuwa NSSF itamaliza changamoto ndogondogo
ambazo waajiri walizitaja wakati wa semina hiyo.
No comments:
Post a Comment