Wednesday, December 7, 2016

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya kazi yadhihirisha Tathimini ya Upimaji wa Ardhi Nchini


Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani  Bw. Justo Lyamuya akitoa tathimini ya upimaji  Ardhi nchini kwa  waandishi wa Habari ( hawaonekani pichani) kulia  kwake ni Mkurugenzi Msaidizi upimaji na Ramani Bw. Simon Katambi na kushoto  kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini Wizarani hapo Bi.  Mboza Lwandiko.
------------------------------------
Viwanja 32,303 na mashamba 76 yamepimwa nchini toka robo ya kwanza ya mwaka / Julai  - Septemba 2016, kwa maazimio ya upimaji wa vipande 400,000 vya Ardhi ifikapoJuni, 2017.
Akitoa taarifa kwa Vyombo vya habari; Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw.  Justo Lyamuya ameeleza. Alisema, toka mwaka 1961 hadi 2016 vimepimwa viwanja 1,359,899 na mashamba 24,579. Kwa kipindi cha miaka 6 iliyopita kuanzia 2010 hadi Juni 2016 vimepimwa viwanja 558,403 na mashamba 4,314. 
Bw. Lyamuya alitoa ufafanuzi wa upimaji uliofanyika wa maeneo mbalimbali nchini. 
Alieleza Upimaji wa ardhi chini ya maji (Hydrographic Survey) umefanyika kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa ushirikiano na Jeshi la majini la India, kufuatia makubaliano kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya India tumeweza kupima bandari za Dar es Salaam, Zanzibar na Mkoani Pemba. 
Ramani za Bandari hizo zipo kwenye duka la ramani tayari. Mwaka huu upimaji wa bandari ya Tanga umefanyika na kazi ya uwandani imekamilika na ile ya ofisini inaendelea.

No comments: