Viwanja 32,303
na mashamba 76 yamepimwa nchini toka robo ya kwanza ya mwaka / Julai - Septemba 2016, kwa maazimio ya upimaji wa
vipande 400,000 vya Ardhi ifikapoJuni, 2017.
Akitoa taarifa kwa Vyombo vya habari; Mkurugenzi
wa Upimaji na Ramani, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Justo
Lyamuya ameeleza. Alisema, toka mwaka 1961 hadi 2016 vimepimwa viwanja
1,359,899 na mashamba 24,579. Kwa kipindi cha miaka 6 iliyopita kuanzia 2010
hadi Juni 2016 vimepimwa viwanja 558,403 na mashamba 4,314.
Bw. Lyamuya alitoa ufafanuzi wa
upimaji uliofanyika wa maeneo mbalimbali nchini. Alieleza Upimaji wa ardhi
chini ya maji (Hydrographic Survey)
umefanyika kwa kipindi cha miaka
mitatu mfululizo kwa ushirikiano na Jeshi la majini la India, kufuatia
makubaliano kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya
India tumeweza kupima bandari za Dar es Salaam, Zanzibar na Mkoani Pemba.
Ramani za Bandari hizo zipo kwenye duka la ramani tayari. Mwaka huu upimaji wa
bandari ya Tanga umefanyika na kazi ya uwandani imekamilika na ile ya ofisini
inaendelea.
Katika eneo la Upimaji Mipaka ya
Vijiji; Alisema kuwa vijiji 10,667 kati ya vijiji 12,000 vimepimwa. Chini ya
Mradi wa Land Tenure Support Programme
umepima
vijiji 52 kwenye wilaya 3 za Morogoro (Kilombero, Malinyi na Ulanga).
Katika Upimaji wa usimikaji alama za
Msingi za Upimaji, alieleza kuwa; Alama za msingi za upimaji zimesimikwa nchi
nzima zikiwa katika viwango tofauti. Zero order zipo 16, First Order zipo 72 na
second order 525. Baadhi ya maeneo alama hizi zimesambazwa katika umbali
utakaoruhusu upimaji kufanyika kwa urahisi. Sambamba na usambazaji huo wa alama
za upimaji; umbo la dunia (Tanzania Geoid)
limekokotolewa kurahisisha upatikanaji wa vipimo vya miinuko.
Vile vile, katika eneo la Upimaji
Mipaka ya Kimataifa, Bwn. Lyamuya alisema; “Kwa mipaka ya kimataifa mipaka yote
ya baharini na majirani zetu imeandaliwa Mikataba ya makubaliano na kuridhiwa.
Kwa upande wa Maziwa makubaliano ya uwekaji mpaka ndani ya Ziwa Tanganyika Kati
ya Tanzania, DRC, Zambia na Burundi, yamefikiwa. Utekelezaji utaendelea baada
ya fedha kupatikana”.
Bwn. Lyamuya alikiri uwepo wa
changamoto mbalimbali zilizopo katika taaluma ya upimaji na kutaja baadhi ya
maazimio yaliyoazimiwa katika Kongamano la wapima lililofanyika tarehe 2 na 3
Novemba 2016. Baadhi ya maazimio hayo ni pamoja na kila Kampuni inayotambulika
na kusajiliwa kushiriki kikamilifu katika kuchangia lengo la kutoa hati laki 4
kwa mwaka 2016/17 kwa kuwasilisha taarifa ya kiasi cha vipande vya ardhi
iliyopima na kila kampuni kwenye mkutano ujao na kuandaa mapendekezo ya ada ya
kitaaluma na gharama za upimaji wa ardhi zitakazotozwa ambazo zitasambazwa na
kutumika nchini kote
Aidha, azimio jingine
lililoazimiwa na wanataaluma hao ni pamoja na
kumtambua Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi; Mh. William
Lukuvi, kupewa uanachama wa heshima wa IST/ Institute
of Surveyers Tanzania, kutokana na jitihada zake kubwa katika kushughulikia
matatizo ya ardhi nchini, na mchango wake katika kuwatambua wapima ardhi kuwa
ndio suluhisho la kuwawezesha wananchi kumilikishwa ardhi.
Habari na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
–
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
No comments:
Post a Comment