Wednesday, December 7, 2016

GOLF JWTZ LUGALO WATAKIWA KUTOBWETEKA NA MFULULIZO WA USHINDI WANAOUPATA

Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ.

Wachezaji wa Golf wa klabu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wametakiwa kutobweteka na mfululizo wa ushindi waliopata katika mashindano mbalimbali badala yake wemewatakiwa kujiweka tayari na mashindano ya Kimataifa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa klabu  hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo mara baada ya kurejea kwa Timu  hiyo iliyokuwa ikishiriki Mashindano ya Chairman Troph yaliyofanyika kwa siku Mbili Moshi Mkoani Kilimanjaro ambako ilinyakua vikombe Vinne.

“Najua sie ni Klabu bora ya Golf nchini na yenye wachezaji wazuri kitaifa lakini sasa ni wakati wa kujiandaa Kimataifa ambako tutaitangaza nchi vyema katika mchezo huo na kuliletea Sifa jeshi letu.” Alisema Brigedia Jenerali  Luwongo.

Aliongeza kuwa licha ya kuweka maandalizi ya ushiriki wa kimataifa kwa mwaka 2017 lakini ni fursa kwa wanaotaka kujifunza golf wakati huu wa likizo za mwisho wa mwaka kujitokeza klwani shughuli zote za golf katika uwanja wa Lugalo zitaendelea  kama kawaida.

Kwa Upande wake  mkuu wa Utawala wa Klabu ya Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule alisema katika mashindano hayo ya siku mbili yaliyofanyika Desemba Tatu na Nne Mwaka huu huku  yakitumia mtindo wa Stroke Play Net ambapo Timu ya Lugalo iliwakilishwa na wachezaji 10.

Kapteni  Mandengule Alisema  walifanikiwa kunyakua vikombe vitano ambavyo vimedhihirisha kuwa umahiri wa klabu unazidi kuongezeka kwani ni mashindano manne mfululizo Timu ya Lugalo inafanya vyema.

Alisema kutoka  Klabu ya Lugalo mshindi wa Kwanza ambaye alifanikiwa kuleta ushindi wa Jumla  kwa klabu ya Lugalo ni  Seif Mcharo Divisheni  A  Mshindi ni Richard Mtweve, Divisheni  C ilichukuliwa na Enock Magile na Wanawake mshindi wa kwanza ni Vicky Elias na Mshindi wa pili ni Sara Denis.

Kwa Upande wake   Mshindi wa Jumla kutoka Lugalo Seif Mcharo alisema Ushindio huo ulitokana na maandlizi mazuri yaliyofanyika wakati wa kuelekea katika mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakiandaliwa.

Kwa  upande wake mshindi wa Divisheni A Richard Mtweve alisema licha ya Kuibuka na ushindi lakini ushindani ulikuwa mkubwa kutokana na matokeo mazuri yaliyotokea kwa wachezaji wote kupata alama nzuri kulinganisha na Alama zilizopatikana katika mashindano mengine.

Katika mashindano hayo Klabu Tano zilishiriki katika mashindano hayo ambazo ni Lugalo, Gymkhana Dar es Salaam , TPC, KILI, MOSHI.

No comments: