Thursday, November 28, 2013

Kilimanjaro stars wafungana 1-1 NA Zambia

 Timu ya Taifa, kilimanjaro Stars Leo imecheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup  na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos, ambao uko takriban kilometa 60 kutoka Nairobi. Timu hizo zimefungana 1-1. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua sana, Katika mechi iliyotangulia ambayo iliwakutanisha Burundi NA Somalia, Burundi iliwafunga Somalia goli 2. Yafuatayo ni matukio katika picha
 Hapa vijana wetu wakiwa katika Picha ya Pamoja Kabla ya kwanza kwa kipindi cha kwanza
 Bwana shiyo Pamoja na Gavana wa Machakos wakiwasalimia wachezaji.
 Mtanange ukiendelea uwanja wa Machakos
 Kilimanjaro Stars wakipata dua kabla ya mchezo 
 Kocha wa Zambia akihojiwa na wanahabari
 Mashabiki wa Kilimanjaro Stars wakishangilia timu yao
 Wachezaji wetu wakitoka nje ya uwanja baada ya mchezo huo
 Makocha wa timu zote mbili wakihojiwa baada ya mchezo
Bwana Innocent Shiyo wa tatu  kutoka kushoto wakati wa wimbo Wa Taifa wa Tanzania ukipigwa. kulia kwa Bwana Shiyo ni Balozi  wa Zambia nchini kenya Mh Josephine Mumbi Phiri. Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya

Kombe la Dunia latikisa jiji la Nairobi nchini Kenya,Kutua jijini Mwanza na Dar es Salaam,Tanzania Kesho

Kampuni ya Coca Cola ambao ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Dunia,wamefanikiwa kulileta Kombe hilo kwa mara nyingine tena Barani Afrika,ambapo leo hii Kombe hili lipo Jijini Nairobi nchini Kenya na kesho Mapema linatarajiwa kuondoka jijini hapa na kulelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae kuelekea jijini Dar es Salaam.hivyo wakazi wa maeneo mbali mbali ya jijini Dar kaeni mkao wa kula kwa ajili ya kuliona na kupiganalo picha Kombe hilo.
 Wakazi wa Jiji la Nairobi nchini Kenya wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa KICC uliopo katikati ya Mji,wakifatilia Burudani mbali mbali za Muziki kutoka kwa wasanii wengi wa nchini humo pamoja na wale wa kimataifa ambao wapo kwenye ziara ya Kutembea na Kombe la Dunia,kupitia Kinywaji cha Coca Cola.Kombe hilo kwa sasa lipo nchini Kenya ambapo kesho litawasini Jijini Mwanza nchini Tanzania na kupokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
 Msanii wa Muziki kutoka nchini Brazil,David Correy akirusha Fulana zake kwa Mashabiki wake lukuki waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa KICC,jijini Nairobi nchini Kenya jioni hii wakati wa tamasha la wazi la Ziara ya Kombe la Dunia linadhaminiwa na Kampuni ya Coca cola,ambalo leo lipo nchini Kenya na kesho asubuhi litaelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
 Msanii huyo wa Muziki kutoka nchini Brazil aitwae David Correy akiendelea kutoa burudani na nyimbo zake mbali mbali.
 David Correy akiwaaga mashabiki wake.
 Mkali wa miondoko ya R&B na Raga kutoka nchini Kenya,Kevin Wyre akifanya yake mbele ya mashabiki wake lukuki waliofurika kwenye Uwanja wa kwenye Uwanja wa KICC,jijini Nairobi nchini Kenya jioni hii wakati wa tamasha la wazi la Ziara ya Kombe la Dunia linadhaminiwa na Kampuni ya Coca cola,ambalo leo lipo nchini Kenya na kesho asubuhi litaelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
Mkali wa miondoko ya R&B na Raga kutoka nchini Kenya,Kevin Wyre akiendelea kufanya yake.
Ni shangwe tupu ndani ya Uwanja huu wa KICC.
Wakali wa Muziki wa Kufokafoka (Rap),P-Unit wa hapahapa nchini Kenya nao wakifanya yao mbele ya mashabiki wake lukuki waliofurika kwenye Uwanja wa kwenye Uwanja wa KICC,jijini Nairobi nchini Kenya jioni hii wakati wa tamasha la wazi la Ziara ya Kombe la Dunia linadhaminiwa na Kampuni ya Coca cola,ambalo leo lipo nchini Kenya na kesho asubuhi litaelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
DJ akifanya makeke yake.
Yaani mambo ni Dole tupu tu hapa.


MAMISS WAANZA KUJINOA TAYARI KWA MISS TANZANIA USA PAGEANT JUMAMOSI NOV 30

Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant akiwaasa Mamiss Tanzania USA Pageant leo Jumamtano Novemba kwenye hotel ya Marriott
Pamela Egbe Messy mratibu wa Miss Africa USA Pageant akiwaelimisha walimbwende
MaWinny Casey Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na mratibu wa Miss Tanzania USA Pageant, Asha Nyang'anyi (kulia)
Mamiss Tanzania USA Pageant wakimsikiliza Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant alipokuwa
Lady Kate, Pamela, Ma Winny na Asha katika picha ya pamoja na Mamiss Tanzania USA.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

PINDA ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU JOHN SIMALENGA MJINI NJOMBE LEO

 Waziri Mkuu, Mizengo pinda akisalimiana na Maaskofu wa kanisa la Anglican nchini wakati alipowasili kwenye kanisa kuu la Anglican la Njombe kuhudhuria mazishi ya Askofu wa Dayosisi  ya South West Tanganyika, , John  Andrew Simalenga 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pindaakitoa heshima za mwisho kwa Askofu John Andrew Simalenga katika mazishi ya Askofu huyo wa Dayosisi ya South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican lyaliyofanyika Njombe  Novemba 28, 2013.  Kushoto ni Askofu Mkuu wa kanisa la Anglican nchini, Dr. Jacob  Chimeledya
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda wakishiriki katika Ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya South West Tanganyika yaliyofanyika Njombe 
 Mwili wa Askofu wa Kanisa la Anlican Dayosisi  ya Southa  west, John Andrew Simalenga ukitelemshwa kaburini kwenye mazishi yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la  Dayosisi hiyo mjini Njombe 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka mchanga katika kaburi la Askofu wa Dayosisi ya  South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican, John Andrew Simalenga yaliyofanyika  mjini Njombe
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu wa Dayosisi ya South West Tanganyika , John Andrew Simalenga  katika mazishi yaliyofanyika leo Njombe 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa  la Anglican Dayosisi ya South West Tanganyika , John Andrew Simalenga yaliyofanyika leo Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA), DAR ES SALAAM.

 - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hituba yake ya uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam
  Wadau wakisikiliza hotuba ya ufunguzi
 Wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa akisoma hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi
  
 Waalikwa katika hafla hiyo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma, wakati alipotembelea katika chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi Chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) Sunday Richard, wakati alipotembelea chumba hicho baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa (wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma (kulia) na Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa, nje ya Jengo la Mawasiliano baada ya kutembelea Chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika picha ya pamoja na wadau wa mawasiliano na viongozi wa TCRA baada ya  uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam. Picha na OMKR

Same waadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

 Wakazi wa wilaya ya Same na maeneo ya jirani wakiwa katika maandamano ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
 Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika jana wilayani Same.
 Maandamano yakiendelea
 Washiriki wakiwa katika eneo la tukio
 Meneja mipango wa shirika la NAFGEM linalojihusisha na kupinga vitendo vya ukeketaji Honoratha Nasuwe akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika wilayani Same.
 Afisa wa kitengo cha elimu ya haki za binadamu na jinsia wa shirika la KWIECO ,Elizabeth Mushi akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika wilayani Same.
 Wadau wakifuatilia hafla hiyo

 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika jana wilayani Same,kamanda wa polisi wa wilaya ya Same ,OCD Asterio Maiga akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kituo kikuu cha mabasi cha wilaya ya Same.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi. 
Picha na habari na  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Moshi.