Thursday, November 28, 2013

Kombe la Dunia latikisa jiji la Nairobi nchini Kenya,Kutua jijini Mwanza na Dar es Salaam,Tanzania Kesho

Kampuni ya Coca Cola ambao ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Dunia,wamefanikiwa kulileta Kombe hilo kwa mara nyingine tena Barani Afrika,ambapo leo hii Kombe hili lipo Jijini Nairobi nchini Kenya na kesho Mapema linatarajiwa kuondoka jijini hapa na kulelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae kuelekea jijini Dar es Salaam.hivyo wakazi wa maeneo mbali mbali ya jijini Dar kaeni mkao wa kula kwa ajili ya kuliona na kupiganalo picha Kombe hilo.
 Wakazi wa Jiji la Nairobi nchini Kenya wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa KICC uliopo katikati ya Mji,wakifatilia Burudani mbali mbali za Muziki kutoka kwa wasanii wengi wa nchini humo pamoja na wale wa kimataifa ambao wapo kwenye ziara ya Kutembea na Kombe la Dunia,kupitia Kinywaji cha Coca Cola.Kombe hilo kwa sasa lipo nchini Kenya ambapo kesho litawasini Jijini Mwanza nchini Tanzania na kupokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
 Msanii wa Muziki kutoka nchini Brazil,David Correy akirusha Fulana zake kwa Mashabiki wake lukuki waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa KICC,jijini Nairobi nchini Kenya jioni hii wakati wa tamasha la wazi la Ziara ya Kombe la Dunia linadhaminiwa na Kampuni ya Coca cola,ambalo leo lipo nchini Kenya na kesho asubuhi litaelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
 Msanii huyo wa Muziki kutoka nchini Brazil aitwae David Correy akiendelea kutoa burudani na nyimbo zake mbali mbali.
 David Correy akiwaaga mashabiki wake.
 Mkali wa miondoko ya R&B na Raga kutoka nchini Kenya,Kevin Wyre akifanya yake mbele ya mashabiki wake lukuki waliofurika kwenye Uwanja wa kwenye Uwanja wa KICC,jijini Nairobi nchini Kenya jioni hii wakati wa tamasha la wazi la Ziara ya Kombe la Dunia linadhaminiwa na Kampuni ya Coca cola,ambalo leo lipo nchini Kenya na kesho asubuhi litaelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
Mkali wa miondoko ya R&B na Raga kutoka nchini Kenya,Kevin Wyre akiendelea kufanya yake.
Ni shangwe tupu ndani ya Uwanja huu wa KICC.
Wakali wa Muziki wa Kufokafoka (Rap),P-Unit wa hapahapa nchini Kenya nao wakifanya yao mbele ya mashabiki wake lukuki waliofurika kwenye Uwanja wa kwenye Uwanja wa KICC,jijini Nairobi nchini Kenya jioni hii wakati wa tamasha la wazi la Ziara ya Kombe la Dunia linadhaminiwa na Kampuni ya Coca cola,ambalo leo lipo nchini Kenya na kesho asubuhi litaelekea Jijini Mwanza,nchini Tanzania ambapo litapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na baadae litaelekea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine.
DJ akifanya makeke yake.
Yaani mambo ni Dole tupu tu hapa.


No comments: