Wednesday, August 10, 2011

Jaji Mkuu aapisha mawakili wapya 288 jijini Dar es salaam leo

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akimtunuku cheti mmoja kati ya mawakili wapya 288 wa Kujitegemea walioapishwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu Mh. Mohamed Chande Othman akimtunukui hati y Uwakili  Bw. Lowassa
Sehemu ya watunukiwa
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (wa saba kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Frederick Werema (wa tatu kulia) wakiwa pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawakili wapya walioapishwa. Picha na Mary Gwera,Mahakama ya Rufani.
 Wakisubiri zamu ya kuchukua vyeti vyao
 Sehemu ya mawakili walioapishwa
 Firing squad...
Muda wa Taswira...
Kundi la pili
Familia zikifurahia 


Siku ya furaha kwa familia hizi
Kina mama wana kila haki ya kujidai baada ya binti zao kufanikiwa kuwa mawakili
Sehemu ya wadau
Familia yenye furaha
Mrakibu wa Polisi James Kasusura akipewa heko na mai waifu wake
WWakili mkuu wa serikali Mh. Werema akiwa meza kuu ya viongozi wengine wa TLS na Mahakama. Kulia ni Msajili wa mahakama ya Rufaa Mh. Francis Mutungi
Mdau akienda kukaa baada ya kutunukiwa uwakili
Kinadada nao wako mstari wa mbele kwenye taswira
Magwiji wa Sheria wastaafu
Mama Longway alikuwepo

wadau wakishuhudia vijana wakiukwaa uwakili
Wadau wakisubiria mdogo wao apate uwakili

libeneke la upatikanaji wese katika baadhi ya vituo jijini dar leo

 Wakazi wa Tabata Segerea na maeneo ya jirani na hapo wakisogeza vidumu katika foleni ya kupata huduma ya mafuta kwenye kituo cha Lake Oil kilichopo maeneo ya Tabata Sanene mapema mara baada ya Serikali kutoa tamko la kuvitaka vituo vyote vya mafuta vianze kutoa huduma hiyo haraka iwezekanavyo japo bado kuna baadhi ya vituo vinaendelea kukaidi amri hiyo ya Serikali.
 Mtoa huduka katika kituo cha Mafuta cha Lake Oil kilichopo Tabata Sanene akiendelea kutoa huduma hiyo mara baada ya kupokea amri kutoka kwa bosi wake kwamba aanze kupiga bei wese lililopo kwenye stoku.
 Jamaa keshapata na sasa anashukuru mungu.
 Hawa wa Boda Boda wamechelewa kufika na hapa wanawaza kwenda kuanza kupanga foleni.
 "Eehh... sasa Mafuta tumepata,ila tutaondokaje hapa na wakati tairi halipo??" hivi ndivyo walivyokuwa wakizungumza hawa jamaa ambao walisotea kupata mafuta huku tairi la gari lao likiwa kwa fundi pancha.
 "Daaahh.... hapa ahueni kidogo sasa,maana tokea huko mpaka huku!!
 Foleni ilienda taratibu,hapa katika kituo ya Lake Oil cha Tabata Sanene.
 Kimbembe kingine kilianzia hapa Sinza Afrika Sana,ambapo kituo cha Mafuta cha Camel kimeanza kuuza mafuta tena chini ya usimamizi wa askari Polisi.yaani hapa ni vurugu mtindo mmoja,maana kila mtu anahitaji mafuta kwa wakati mmoja.
 Wese likishushwa kwenye kituo cha Camel Sinza Afrika sana.
 Hapa ni tafrani mpaka msaada wa Askari Polisi huyu aliamua kuingilia kati na kuwataka watu wote kufuata taratibu iliyokuwa imepangwa kituoni hapo.
 Foleni ya Magari na watu wote wakihitaji mafuta.
 Hivi ndivyo mambo yalivyo hivi sasa.
 Ukifanikiwa kupata mafuta na pumzi inashuka vyema,maana hali ni mbaya sana.
 Wadau wakisaidiana kuweza mafuta kwenye gari lao mara baada ya kufanikiwa kuyapata.
 Kituo cha Camel Oil Sinza leo.
 Kituo cha Oil Com pale Sayansi nako mambo yako namna hii.
 Afande akiwa katulia pembeni baada ya kuona jamaa hawataki kutoa huduma ya Mafuta katika kituo cha OilCom pale Sayansi, Kijitonyama.

NBC yazindua Akaunti mbili zinazofuata kanuni za KIISLAMU za CORPORATE ISLAMIC CURRENT ACCOUNT pamoja na BUSINESS ISLAMIC CURRENT ACCOUNT

 Dada wa mapokezi katika uzinduzi wa Akaunti za KIISLAMU  za CORPORATE ISLAMIC CURRENT ACCOUNT pamoja na BUSINESS ISLAMIC CURRENT ACCOUNT za Benki ya Taifa ya Biashara Jumanne agosti 9, 2011 hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam.
 
 Wadau Peter Mgongo (shoto) na Masanja katika hafla hiyo
 Wageni waalikwa wakipakua futari
 Wageni waalikwa wakifuturu
 Futuru ikiendelea
 Futari
 Muda wa futari kwa wahudhuriaji
 Rais Mstaafu akizindua akaunti hizo
 Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa benki ya NBC Dkt. akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBC Bw. Lawrence Mafuru na Mkurugenzi wa Islamic Banking wa NBC Bw. William Kallaghe wakiagana na wageni
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa benki ya NBC Dkt. akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBC Bw. Lawrence Mafuru na Mkurugenzi wa Islamic Banking wa NBC Bw. William Kallaghe wakiagana na wageni
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa benki ya NBC Dkt. akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBC Bw. Lawrence Mafuru na Mkurugenzi wa Islamic Banking wa NBC Bw. William Kallaghe wakiagana na wageni
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa benki ya NBC Dkt. akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBC Bw. Lawrence Mafuru na Mkurugenzi wa Islamic Banking wa NBC Bw. William Kallaghe wakiagana na wageni
 Wadau wa NBC wakiwa na furaha kwa uzinduzi huo
 Mkurugenzi Mkuu wa NBC Bw. Lawrence Mafuru akitoa maelezo ya akaunti hizo za Islamic Banking huku mgeni rasmi, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili shoto) Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya NBC, Mkurugenzi wa Islamic Banking wa NBC Bw. William Kallaghe na Bw. Abbas Mwinyi
sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hii

Tuesday, August 9, 2011

TAMKO LA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU UPATIKANAJI WA MAFUTA NCHINI


Waziri wa Nishati na Madini,Mh. William Mganga Ngeleja





Mheshimiwa Spika,
  1. Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kulishukuru Bunge lako tukufu kwa kunipa fursa hii ya kutoa taarifa kuhusu hali ya biashara ya mafuta ya petroli hapa nchini.
  1. Kama tunavyofahamu, mafuta ya petroli ni muhimu sana  kwa uchumi wa nchi yetu kwani viwanda, vyombo vya usafiri, na huduma nyinginezo nyingi hutegemea mafuta na bidhaa zake. Bei ya mafuta inapopanda, bei zingine nyingi hupanda kwa mfano bei za usafiri zinapanda, bei za vyakula zinapanda, bei za bidhaa za viwandani zinapanda; nakadhalika.
  1. Mheshimiwa Spika, tarehe 22 Juni 2011 Serikali, kupitia kwa Waziri wa Fedha wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, alitoa maagizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia kupunguza bei za mafuta. Hatua ambazo ziliagizwa kuchukuliwa ni pamoja na:
  1. Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);
  1. Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
  2. kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;
  3. kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financiang Charges); na
  4. Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).

HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI 
  1. Serikali kupitia EWURA ilianza mara moja mchakato wa kurekebisha Kanuni ya ukokotoaji wa bei za mafuta hapa nchini kwa lengo la kuleta unafuu wa bei kwa mlaji. Hatua ya kwanza ilikuwa kuandaa hoja (discussion paper) ambayo ilitoa mapendekezo ya maeneo mbalimbali yanayofaa kurekebishwa ili kupata maoni ya wadau wa sekta ya mafuta. Mapendekezo hayo yalizingatia maagizo ya Serikali pamoja wa ushauri  mbalimbali wa wadau katika sekta ya mafuta hapa nchini.

USHIRIKISHAJI WADAU
  1. Mchakato wa kupata maoni ya wadau (taftishi) ulianza tarehe 4 Julai 2011 na kukamilika tarehe 26 Julai 2011. Kwa kawaida, mchakato huo ungechukua siku 81 lakini kutokana na unyeti wa suala hili, Mamlaka ililazimika kuufupisha hadi  siku 23.
  1. Mkutano wadau uliitishwa tarehe 22 Julai 2011 ili kupitia rasimu ya kanuni pamoja na jedwali la uchambuzi wa maoni ya wadau lililoandaliwa na EWURA.  Wadau walioshirikishwa katika taftishi hiyo ni pamoja na makampuni ya mafuta, Baraza la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (Consumer Consultative Council), Baraza la Ushauri la Serikali, Taasisi za Umma kama vile TRA, TBS, WMA, TPDC, TPA, SUMATRA, na TIPER. Maoni mbalimbali ya wadau yalipokelewa na kuchambuliwa na EWURA ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara ya Nishati na Madini,  Wizara ya Fedha na Uchumi, Shirika la Maendeleo ya Mfuta Tanzania (TPDC), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, EWURA na Makampuni ya Mafuta. 
  1. Tarehe 23 Julai 2011, EWURA iliitisha kikao cha wawakilishi wa wadau wakubwa ambao ni pamoja na CCC, TPDC, TPA, Wizara ya Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu na baadhi ya makampuni ya mafuta kupitia mapendekezo yaliyokuwepo na kutoa maoni ya mwisho kabla ya kuwasilishwa kwenye Bodi kwa maamuzi.

MAAMUZI YA EWURA
  1. Tarehe 26 Julai 2011, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA ilikaa na kupitia mapendekezo ya marekebisho ya vipengele mbalimbali vya kanuni ya kukokotoa bei ya mafuta. Maamuzi hayo ya Bodi yamepelekea punguzo la bei za mafuta kwa viwango vifuatavyo: Petroli TZS 202.37; Dizeli TZS 173.49; na Mafuta ya Taa TZS 181.37. Mabadiliko haya ya bei ni sawa na punguzo la asilimia 9.17; 8.31; na 8.70 kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa sawia. Kanuni hii ya kukokotoa bei za mafuta imeanza kutekelezwa kuanzia tarehe 03 Agosti 2011.
  1. Tarehe 3 na 4 Agosti 2011 makampuni ya mafuta yaliwasilisha kutoridhishwa na maamuzi yaliyofanywa na EWURA hususan kuhusu kupunguzwa kwa wigo wa asilimia 7.5; margins za makampuni ya mafuta, na gharama za kuchelewesha meli bandarini (demmurage charges).
  1. Kufuatia vikao hivyo vya Serikali, makampuni pamoja na EWURA siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti 2011, Mamlaka ya EWURA ilifanya marekebisho mengine katika vipengele vifuatavyo:
  1. Gharama za ucheleweshaji meli bandarini (demmurage charges) ziliongezwa kutoka wastani wa TZS 1.85 kwa lita hadi TZS 8.76 kwa lita.
  1. Viwango vya faida kwa kampuni za mafuta (OMCs margins) ziliongezwa kutoka TZS 108.69 kwa lita hadi TZS 110.57.

HALI YA UPATIKANAJI NA USAMBAZAJI MAFUTA BAADA YA KUANZA KUTUMIKA KWA KANUNI MPYA 
  1. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bishara ya mafuta hapa nchini. Ufuatiliaji uliofanywa kwenye maghala ya kuhifadhia mafuta umedhihirisha kuwa kuna mafuta ya kutosha hapa nchini na pia kuna meli kadhaa ambazo zipo nje ya gati zikisubiri kupakua mafuta. Aidha, makampuni ya mafuta yameuza mafuta kwa wingi siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti 2011.
  1. Hadi Ijumaa tarehe 05.08.2011, kiasi cha mafuta yaliyokuwepo katika maghala ya baadhi ya makampuni ya mafuta yaliyokaguliwa ni  lita milioni 191.813 ambayo inakidhi matumizi ya nchi kwa kati ya siku 8 hadi 67 kulingana na aina ya mafuta kama inavyoonekana kwenye jedwali Na. 1 hapa chini:

Jedwali 1: Mafuta yaliyoko Nchini tarehe 05 Agosti 2011

MaelezoMafuta ya PetroliMafuta ya DizeliMafuta ya TaaMafuta ya NdegeMafuta Mazito
Akiba iliyopo(lita)41,934,13992,650,30041,227,8704,384,29710,805,070
Wastani wa Matumizi kwa siku875,0003,100,000615,240560,5001,087,695
Makadirio ya siku za kutumika483067810
                   
  
MAUZO YA MAFUTA KWENYE MAGHALA (JUMLA)
  1. Takwimu zilizowasilishwa EWURA na mkandarasi anayeweka vinasaba katika mafuta yauzwayo hapa nchini (GFI) na kuhakikiwa na wakaguzi wa EWURA zinaonesha kuwa kwa siku ya Ijumaa tarehe 5 Agosti 2011 mauzo ya mafuta kutoka kwenye maghala (depots) yalikuwa ni malori 329 kwa aina mbalimbali za mafuta, kwa ajili ya soko la ndani.
  1. Tarehe 3 Agosti walipakia malori 40 wakati tarehe 4 Agosti 2011 yalipakiwa malori 185. Kwa kawaida, wastani wa mauzo kwa siku ni takriban malori 250 hadi 300. Takwimu hizi zinadhihirisha kuwa kuanzia tarehe 5 Agosti 2011, mauzo ya mafuta yameongezeka na kufikia kiwango cha kawaida.
  1. Katika hali ya kawaida, makampuni mengi ya mafuta hayafanyi kazi katika siku za mapumziko. Kwa hiyo, siku ya Jumamosi tarehe 6 Agosti 2011, jumla ya malori 115 yalipakia mafuta.
MAUZO YA MAFUTA KWENYE VITUO (REJAREJA)
  1. Ukaguzi uliofanywa na EWURA kwenye vituo vya mafuta jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa unaonesha kuwa vituo vingi vilianza kuuza mafuta kama kawaida. Ukaguzi huo pia umehusisha kupata takwimu za mafuta yaliyopo kwenye vituo ili kuhakikisha kuwa hakuna kituo kinachohodhi mafuta na kuacha kuuza. Kuna baadhi ya vituo vilikuwa vikisubiri kupata mafuta kwa vile walikuwa wameishiwa, hasa kwa sababu makampuni ya mafuta hayakuuza mafuta kwa kiwango cha kawaida siku ya tarehe 3 na 4 Agosti 2011.
  1. Makampuni mengi yaliendelea kupakia malori ya mafuta mpaka usiku 5 Agosti 2011 hivyo ilitarajiwa kwamba kungekuwa na usambazaji mwingi zaidi kwenye vituo kuanzia Jumamosi tarehe 6 Agosti 2011.
VIWANGO VYA BEI
  1. Ukaguzi uliofanywa na EWURA unaonesha kuwa bei za mafuta kwenye vituo vinavyouza mafuta zimezingatia bei kikomo zilizotolewa na Mamlaka ya EWURA tarehe 3 Agosti 2011. Ukaguzi huo umefanyika katika miji ya Arusha, Moshi, Dar es Salaam na Dodoma.  Aidha, hakuna taarifa zilizopokewa na EWURA kutoka mji wowote kuhusu kukiukwa kwa bei kikomo iliyopo sasa.
HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI 
  1. Mheshimiwa Spika, bidhaa za mafuta ya petroli inatoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi katika nchi zote duniani.  Upatikanaji wa uhakika wa mafuta na kwa bei stahili vitafanya uchumi wa nchi yetu kukua kwa kasi zaidi na kuwa endelevu.
  1. Serikali inachukua hatua zifuatazo ili kuhakikisha kuwa mafuta ya kutosha yanapatikana sehemu zote nchini.
      1. Serikali kupitia EWURA inafuatilia mwenendo wa usambazaji wa mafuta kutoka katika maghala ya makampuni ya mafuta kwenda kwenye vituo vya mafuta;
      1. Serikali kupitia EWURA itachukua hatua za kisheria kwa kampuni zilizokiuka masharti ya leseni na kusababisha uhaba wa mafuta kwenye vituo vya kuuza mafuta nchini;
      2. Leo Serikali kupitia EWURA imeipa leseni COPEC kampuni tanzu ya Serikali kupitia TPDC kuanza kufanya biashara ya mafuta mara moja; na
      1. Serikali kwa kupitia EWURA imekamilisha taratibu za uagizaji wa mafuta kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa mafuta yanapatika na kwa gharama nafuu zaidi wakati wote.
  1. Mheshimiwa Spika, kufuatia hali iliyojitokeza, EWURA imetoa Compliance Order kwa makampuni manne ambayo ni BP, Engen, Oilcom na Camel Oil, ambapo wanatakiwa watekeleze hatua zifuatazo:
      1. Mara moja wanatakiwa kuanza kutoa huduma katika maghala yao ikiwa ni pamoja na kuanza kuuza mafuta katika vituo vya rejareja ikiwemo vituo vilivyo chini ya miliki zao;
      2. Waache mara moja kitendo chochote kitakachosababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania; na
      3. katika kipindi cha masaa 24 wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria dhidi yao kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta pamoja na Sheria ya EWURA.
  1. Mheshimiwa Spika, baada ya kuisha kwa muda uliotolewa na EWURA, adhabu stahiki zitatolewa kwa wahusika ikiwa ni pamoja na kusitisha ama kufuta leseni.
  1. Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida na kwa mujibu wa Sheria, mtu asiporidhika na maamuzi ya EWURA anapaswa kukata rufani katika Baraza la Ushindani(Fair Competition Tribunal). Hatua hii haijafuatwa hadi sasa na Serikali ingeshauri kwamba masuala kama haya ni vema yakafuata taratibu za kisheria.
  1. Mheshimiwa Spika; naomba kuwasilisha.

MAONYESHO YA KILIMO NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAFANA SANA

Waziri wa Maendeleo ya Mifungo, Dk. Mathayo David Mathayo akifunga maonyesho ya kilimo nyanda za juu Kusini jijini Mbeya kwenye kiwanja John Mwakangale.
Waziri David Mathayo akipokea maandamano ya wakulima wa nyanda za juu kusini wakati wa kufunga maonyesho ya nanenane jijini Mbeya.wa kwanza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh. John Mwakipesile.
Waziri akipata maelezo toka kwa mkuu wa wilaya Mbeya Evance Balama alipotembelea banda la halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Baadhi ya watumishi wa wakishurahia na kupokea vyeti vyao vya ushindi katika mabanda Bora katika maonesho hayo ya Nane Nane
Kama kawaida wachina hawakukosa eneo hili kuchemkia biashara ya maua
Maandamano yakiwa yanaingia viwanja vya nane nane
Baadhi ya wateja wakipata maelezo katika banda la Vodacom
Mzee kyando wa kikundi cha huzuni cha baba wa taifa alikuwepo
Umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria maonyesho ya kilimo nane nane nyanda za juu kusini Mbeya.Picha na Mbeya Yetu Blog.