Wakazi wa Tabata Segerea na maeneo ya jirani na hapo wakisogeza vidumu katika foleni ya kupata huduma ya mafuta kwenye kituo cha Lake Oil kilichopo maeneo ya Tabata Sanene mapema mara baada ya Serikali kutoa tamko la kuvitaka vituo vyote vya mafuta vianze kutoa huduma hiyo haraka iwezekanavyo japo bado kuna baadhi ya vituo vinaendelea kukaidi amri hiyo ya Serikali.
Mtoa huduka katika kituo cha Mafuta cha Lake Oil kilichopo Tabata Sanene akiendelea kutoa huduma hiyo mara baada ya kupokea amri kutoka kwa bosi wake kwamba aanze kupiga bei wese lililopo kwenye stoku.
Jamaa keshapata na sasa anashukuru mungu.
Hawa wa Boda Boda wamechelewa kufika na hapa wanawaza kwenda kuanza kupanga foleni.
"Eehh... sasa Mafuta tumepata,ila tutaondokaje hapa na wakati tairi halipo??" hivi ndivyo walivyokuwa wakizungumza hawa jamaa ambao walisotea kupata mafuta huku tairi la gari lao likiwa kwa fundi pancha.
"Daaahh.... hapa ahueni kidogo sasa,maana tokea huko mpaka huku!!
Foleni ilienda taratibu,hapa katika kituo ya Lake Oil cha Tabata Sanene.
Kimbembe kingine kilianzia hapa Sinza Afrika Sana,ambapo kituo cha Mafuta cha Camel kimeanza kuuza mafuta tena chini ya usimamizi wa askari Polisi.yaani hapa ni vurugu mtindo mmoja,maana kila mtu anahitaji mafuta kwa wakati mmoja.
Wese likishushwa kwenye kituo cha Camel Sinza Afrika sana.
Hapa ni tafrani mpaka msaada wa Askari Polisi huyu aliamua kuingilia kati na kuwataka watu wote kufuata taratibu iliyokuwa imepangwa kituoni hapo.
Foleni ya Magari na watu wote wakihitaji mafuta.
Hivi ndivyo mambo yalivyo hivi sasa.
Ukifanikiwa kupata mafuta na pumzi inashuka vyema,maana hali ni mbaya sana.
Wadau wakisaidiana kuweza mafuta kwenye gari lao mara baada ya kufanikiwa kuyapata.
Kituo cha Camel Oil Sinza leo.
Kituo cha Oil Com pale Sayansi nako mambo yako namna hii.
Afande akiwa katulia pembeni baada ya kuona jamaa hawataki kutoa huduma ya Mafuta katika kituo cha OilCom pale Sayansi, Kijitonyama.
1 comment:
Serikali ina uwezo wa kuwashughulikia hawa wamiliki wa makampuni yanayoagiza na pia wasambazaji wa mafuta. Je ni nini kinachoifanya serikali hadi leo kushindwa kutekeleza? masaa 24 yamekwisha !????!!mgao wa umeme, uchakachuaji mafuta na sasa uhaba wa mafuta!!!!???!! au inalipa fadhili kutokana na matumizi ya hela za makampuni hayo?
Post a Comment