Wednesday, November 2, 2016

KIOTA KIPYA CHA MARAHA NA BENDI MPYA YA MJENGONI VYAZINDULIWA RASMI JIJINI ARUSHA


Mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John Mdeme akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi huo
wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa mjengoni kabu pamoja na mjengoni band wakiwa wanaagiza nyama kwa ajili ya kula(habari pich na Woinde Shizza).
Bendi mpya inayojulikana kama Mjengoni bandi ikiwa inatumbuiza wageni waalikwa , washabiki pamoja na wananchi waliouthuria katika uzinduzi huo
mashabiki na wapenzi wa bendi ya mjengoni wakiwa wanasakata rumba hatariii

Msaniii wa bendi ya Fm Academia Kingombe Blaise na aliuthuria katika uzinduzi huu wa bandi ya mjengoni pamoja na klabu mpya matata ya Mjengoni.
Mmiliki wa blog ya libenee la kaskazini Woinde Shizza wa kwanza kulia nyuma yake ni mmiliki wa blog ya Jamii blog Pamela mollel ,wakanza kushoto ni dada Fatuma wa Stax Tv pamoja na Veronica Ignatus wote tulibahatika kuhuthuria na kushuhudia uzinduzi rasmi wa bendi ya mjengoni pamoja na klabu ya mjengoni .
Jiji la Arusha kwa nyama ni penyewe na pia klabu ya mjengoni kwa kuchoma nyama nzuri ndio pamonaongoza wadau wengi walionekana kuvutiwa na nyama ilikuwa imechoma na wataaalam wa klabu hiyo.
Rais wa bendi Robert Mukongya (Digital) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari waliouthuria uzinduzi huo
Burudani ikiendelea kutoka kwa bendi ya mjengoni





mmiliki wa jamii blog Pamela mollel akiwa anafafanua jambo kuhusiana na kiota iki kipya kilichozinduliwa rasmi jijini Arusha ambapo alitumia muda huo kuwa sihi wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na wale wageni ambao wanauthuria katika mkoa huu kutoacha kufika mjengoni klabu kwa ajili ya kujipatia nyama choma safi na freshi pamoja na muziki muzuri kutoka katiak bendi ya mjengoni

Habari picha na Woinde Shizza,wa libeneke la kaskazini blog

Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni Bandi imezinduliwa rasmi mkoani Arusha huku ikiwaaidi mema wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni wanaoingia ndani ya jiji hilo

Akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi rasmi wa bendi hiyo Rais wa bendi Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa wamejipanga kufanya mkoa wa Arusha kuwa na bendi kubwa inayotoa burudani ya nguvu kama zilivyo bandi zingine za jiji la Dar es salaam akatolea mfano FM Academia na malaika bendi.

Alisema kuwa wakazi wa mikoani wamekuwa wakitegemea bendi kutoka jijini dar lakini kwa sasa ivi wamesogezewa burudani karibu kabisa na itakuwa kila siku za wekendi

Aidha alibaiisha kuwa bendi hiyo anayoisimania inawanamziki wengi ambao wanauwezo wa hali ya juu pamoja na uzoefu wakutosha ivyo anaamini wapenzi wa mziki wa dance wataipenda bendi hiyo na kuikubali

Alisema adi sasa bendi na inanyimbo zake na wanajipanga kwa ajili ya kurekodi ili wapenzi ,wadau na wananchi waweze kupata mziki na kuhusikia katika maredio na hata wanapokuwa majumbani.

Alimalizia kwakusema kuwa bendi hiyo ya mjengoni itakuwa inatoa burudani kila wekendi hivyo wakazi wa jiji la Arusha pamoja na wageni wanaoingia wajitokeze kuja kupata burudani ya nguvu inayotoka kwa wanamuziki wa bendi hiyo.Kwa upande wake wa mkurugenzi wa mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John mdeme alisema kuwa ameamua kufungua kiota ichikipya ili wakazi wa jiji la arusha wawez e kupata sehemu ya kistaarabu ya kupata chakula ,nyama choma nzuri pamoja na mziki mzuri wa live bandi

Alisema kuwa kimepita kipindi kirefu wakazi wa jiji la Arusha wamekuwa wanakosa sehemu ya kwenda kupata burudani nzuri ya mziki wa bakurutu pamoja na live bendi inayoeleweka tangu hotel ya sabasaba ifungwe ivyo ameamua kuileta burudani hiyo ili wananchi wa Arusha waweze kupata sehemu ya kustarehe.


Alimewakaribisha wageni kutoka mikoani pindi wanapofika jijini Arusha kutoaacha kuja mjengoni kujipatia burudani ya nguvu kutoka katika bendi ya mjengoni pamoja na nyama choma nzuri na freshi inayotengenezwa na wachoma nyama waliobobea katika sekta hiyo.













watu wakila bata



huyu ndio mpiga kinanda

















Rais wa Bendi ya Mjengoni akiimba kwa hisia
















UN NA EU ZATOA EURO LAKI NANE KUSAIDIA WATOTO WA KIKE

Shirika la Umoja wa Mataifa la UN kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wametoa Euro laki nane kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu na wahanga wa mimba za utotoni waishio kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit .

Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi Anna Muro amesema kuwa msaada huo utasaidia kuwawezesha wanawake Waweze kushiriki kwenye maendeleo ya jamii .

Akizungumza katika kituo hicho kinacholelea watoto 30 wenye watoto ambao walipata mimba katika umri mdogo na kushindwa kuendelea na masomo ambapo wanasaidiwa na kituo hicho kupata elimu ya ufundi wa ushonaji na mapishi ili kupata stadi zitakaowasaidia kujikwamua kimaisha.
Mwasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara akitoa maelezo kwa Maafisa wa UN na EU wakati walipotembelea kituo shirika hilo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama, Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kulia) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia).(Picha na Ferdinand Shayo).

Anna amesema kuwa watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya usafirishaji wa binadamu jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu na haki za watoto hivyo amewataka Jamii na serikali kupiga vita usafirishwaji wa watoto.

Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama amewataka watoto wanaoishi katika kituo hicho kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata kujiendeleza kielimu na kukua kiuchumi ili kutokomeza umasikini na mimba za utotoni kwa watoto wa kike.

Muasisi wa kituo hicho Martina Simon Siara ameshukuru ugeni kutoka UN na EU uliofika kituoni hapo kwa ajili ya kutazama shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho pamoja na kuwaunga mkono ili waweze kuongeza tija katika kuisaidia jamii.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (wa pili kulia) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Muasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara (kulia) walipotembelea shirika hilo lililopo jijini Arusha.
Wawakilishi kutoka EU na UN wakitazama shughuli za mikono zinazofanywa na watoto wanaoishi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipotembelea kituo hicho hivi karibuni kilichopo jijini Arusha.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro wakishirikiana kuingiza shanga ambazo hutumika kushona mavazi ya utamaduni yanayoshonwa na watoto wa kike wanaoshi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit (katikati) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Rosemary Innocent.
Binti mwenye ulemavu wa ngozi, Rosemary Innocent na wenzake wakiendelea na darasa la kutengeneza vitu mbalimbali kituoni hapo.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kushoto) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja na binti aliyeshona vazi la kuvutia la kimasai lililonakshiwa na shanga walipotembelea kituo hicho.
Wawakilishi wa UN na EU wakitazama kitengo cha elimu ya mapishi katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
wanafunzi wanaojifunza ushonaji katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama akitazama mabinti wanaojifunza ushonaji nguo kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa vijana na watoto wanaoishi katika kituo hicho walipokitembelea jijini Arusha.
Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro akizungumza na wale, vijana pamoja na watoto wanaoishi kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Wawakilishi wa UN na EU katika picha ya pamoja na walezi na watoto wanaoishi kwenye kituo hicho.

BENKI YA AFRIKA MASHARIKI YAIKOPESHA NHC BILIONI 65, KUENDELEZA UJENZI WA MRADI WA 711 KAWE



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) Bi Vivienne Yeda mara baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi Bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya 711 Kawe jijini Dar es salaam, Hafla ya kutiliana saini mkataba huo imefanyika katika makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria NHC Bw.Martin Mdoe.(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) Bi. Vivienne Yeda mara baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi Bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya 711 Kawe jijini Dar es salaam kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria NHC Bw.Martin Mdoe.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) Bi Vivienne Yeda wakisaini mkataba wa mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi Bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya 711 Kawe jijini Dar es salaam kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria NHC Bw.Martin Mdoe.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) wenye mkopo wa thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya 711 Kawe jijini Dar es salaam, Katikati ni Michael Mwalukasa Mkurugenzi wa Nyumba Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria NHC Bw.Martin Mdoe.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) wenye mkopo wa thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi Bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya mradi wa 711 Kawe jijini Dar es salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki East Africa Development Bank Bi. Vivienne Yeda na kushoto ni Michael Mwalukasa Mkurugenzi wa Nyumba Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akibadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki East Africa Development Bank Bi. Vivienne Yeda na Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara.
Maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Kutoka kulia ni Tuntufye Mwambusi Meneja Masoko, Chediel Msuya, Hindu Said Afisa Hazina na Richard Ndeona Meneja wa Hazina.
Baadhi ya Maofisa kutoka Benki ya East Africa Development Bank (EFDB) wakiwa katika hafla hiyo.
Wakurugenzi wa Vitengo Shirika la Nyumba la Taifa NHC wakiwa katika hafla hiyo.

RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA BIASHARA,VIWANDA NA MASOKO.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika jana Ikulu Mjini Unguja 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika jana Ikulu Mjini Unguja. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Rashid Ali Salum akitoa maelezo wakati wakujadili vifungu katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016, kilichofanyika jana Ikulu Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) 
Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe,Balozi Ali Abeid Aman Karume akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika kikao cha robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016, kilichofanyika jana Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) (kulia) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee, 
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi akitoa mchango wake katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016, kilichofanyika jana Ikulu Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, 
Wakuu wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016, kilichofanyika jana Ikulu Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani), 
Baadhi ya maafisa wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016, kilichofanyika jana Ikulu Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani), [Picha na Ikulu.]

IMF Staff Holds Review Mission to Tanzania

End-of-Mission press releases include statements of IMF staff teams that convey preliminary findings after a visit to a country. The views expressed in this statement are those of the IMF staff and do not necessarily represent the views of the IMF’s Executive Board. Based on the preliminary findings of this mission, staff will prepare a report that, subject to management approval, will be presented to the IMF's Executive Board for discussion and decision.

IMF team lead by Mauricio Villafuerte, visited Tanzania from Oct 18–28, to conduct 5th PSI review
Projected growth of 7% in 2016 is still within reach Tanzania remains at low risk of external debt distress.

A team from the International Monetary Fund (IMF), led by Mauricio Villafuerte, visited Tanzania from October 18–28, 2016 and held discussions with the authorities on the fifth review under the Policy Support Instrument (PSI) program that was approved on July 16, 2014. [1]

At the end of the mission Mr. Villafuerte issued the following statement:

“Preliminary data for the first half of 2016 indicate that economic growth was strong and that the projected growth rate of around 7 percent for the year as a whole remains within reach. However, there are downside risks to economic growth associated with the current tight stance of macroeconomic policies and the slow pace of implementation of public investment.

“Inflation declined to 4.5 percent in September, below the target of 5 percent. The current account balance has improved significantly due to lower capital goods imports as externally-financed investment has slowed down and exports of gold and manufactured goods increased. The Bank of Tanzania’s foreign exchange reserves have strengthened in recent months.

“Implementation of the PSI-supported program has been satisfactory. Preliminary data indicate that most quantitative assessment criteria for end-June 2016 were met. The pace of implementing structural reforms has been slow, but has picked up recently.

“Notable progress has been made in stepping up revenue collections and, based on data for the first quarter, the ambitious program target for the 2016/17 fiscal year is within reach. However, current spending has been lower than programmed. Together with the customarily slow pace of project implementation at the beginning of the fiscal year, this has led to a fiscal surplus in the first quarter. In addition, liquidity conditions have been tight contributing to upward pressure on borrowing costs in the economy.

“The mission held discussions on how to address these macroeconomic challenges. In particular, it noted the importance of mobilizing external financing to step up the pace of planned capital spending. Tanzania is at low risk of external debt distress and has room to borrow externally on concessional and nonconcessional terms to meet its financing needs. The mission commended the authorities’ efforts to improve the efficiency of spending and noted that it should not compromise the delivery of essential services. It also recommended continued steps to ease liquidity conditions in the economy. These could include liberalizing further the capital account in line with commitments under the East African Monetary Union Protocol; acquiring a sovereign credit rating to expand Tanzania’s opportunities to borrow abroad; and widening the range of monetary policy tools.

“The mission welcomed the adoption of the second Five-Year Development Plan. The mission noted that it was essential to improve the dialogue with the private sector and accelerate reforms to bolster the business environment. The mission also welcomed the steps taken to clear existing domestic arrears and prevent their further incurrence.

“Discussions will continue in the coming weeks to reach final understandings on an economic policy framework that can underpin the completion of the fifth review under the PSI. The IMF Executive Board is tentatively expected to discuss the review in early-2017.

“The mission met with Minister Philip I. Mpango, Governor Benno Ndulu, Permanent Secretary Doto M. James, and other senior officials of the government and the Bank of Tanzania.

“The IMF team is appreciative of the constructive and open policy dialogue and thanks the authorities for their hospitality during the visit.”


[1] The PSI is an instrument of the IMF designed for countries that do not need balance of payments financial support. The PSI helps countries design effective economic programs that, once approved by the IMF's Executive Board, signal to donors, multilateral development banks, and markets the Fund's endorsement of a member's policies (see http://www.imf.org/external/np/exr/facts/psi.htm). Details on Tanzania’s PSI program are available at www.imf.org/tanzania.

WILAYA YA IGUNGA YATOA TAARIFA YA AUONGO YA UKAMILISHAJI WA MADAWATI KWA RAIS


Na,Jumbe Ismailly,Igunga Nov,02,2016 Taarifa 

BARAZA la kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora limeikataa taarifa ya utengenezaji wa madawati ya Halmashauri hiyo,kwa masharti ya kumtaka aliyetoa taarifa ya kumdanganya Rais,Dk.John Pombe Magufuli aende kwenye vyombo vya habari kukanusha taarifa hizo.

Mapema julai,30,mwaka huu wakati wa ziara yake wilayani Igunga,Mkoani Tabora,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli julai,alikabidhiwa taarifa ya wilaya hiyo inayosema wilaya ya Igunga haina upungufu wa madawati na kibaya zaidi kwa mujibu wa taarifa hiyo ilikuwa na ziada ya madawati mia mbili.

Maamuzi ya Madiwani hao yanafuatia taarifa ya utengenezaji wa madawati iliyotolewa na afisa elimu wa wilaya hiyo, Mwisungi Kigosi kwenye mkutano wa kawaida wa baraza hilo kuonyesha mabadiliko ya takwimu zilizotolewa kwa Rais na walizosomewa madiwani hao.

Wakichangia kwa nyakati tofauti hoja hiyo baadhi ya madiwani,diwani wa viti maalumu CHADEMA,Anna Nyarobi,Charles Bomani wa kata ya Igunga,Gedi Nkuba wa kata ya Nguvumoja na Henry Saidi wa kata ya Mwamala walisema kuwa kuokana na taarifa hiyo kukinzana,kuwa na mkanganyiko na taarifa iliyotolewa kwa Rais na kutokuwa vizuri,hawatakuwa tayari kuipokea taarifa hiyo na kuirudisha kwenye kamati ya madawati wakaipitie tena upya na kisha kuipeleka kwenye baraza maalumu la madiwani.

Anna Nyarobi ni diwani wa viti maalumu kupitia CHADEMA akichangia hoja hiyo alipendekeza kwamba watu waliotoa taarifa za uongo waende kwenye vyombo vya habari na kukanusha taarifa hiyo kwa kusema kuwa taarifa waliyotoa ilikuwa ni ya uongo,ili waweze kurudisha imani za wananchi kwa madiwani wao.

Hata hivyo diwani,Gedi Nkuba alibainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa upungufu wa madawati,alishauri Mkaguzi wa ndani afuatilie taarifa ya madawati hayo pamoja na tathimini ya fedha zote zilizokusanywa kwa ajili ya utengenezaji wa madawati hayo iweze kubainika.

Naye diwani wa kata ya Mwamala,aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa Tume ya kufuatilia utengenezaji wa madawati,Henry Saidi kwa upande wake alibainisha kwamba,baada ya kubaini kuwepo kwa mianya ya ufujaji wa fedha za madawati ya Halmashauri ya Igunga,walishindwa kuendelea na mchakato huo wa utengenezaji wa madawati.

Afisa elimu wa shule za msingi wilaya ya Igunga,Mwisungi Kigosi katika taarifa yake aliyotoa kwa madiwani hao inaonyesha kwamba hadi kufikia sept,21,mwaka huu wilaya hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 2,232 na baada ya kukarabati madawati 725,upungufu halisi uliopo kwa sasa ni madawati 1,507.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Revocatus Kuul alisema alipotembelea katika shule ya msingi Ganyawa alikuta wanafunzi wakiwa wanaendelea na masomo huku wakiwa wamekaa chini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Peter Onesmo aliwashauri madiwani hao kutofanyika kwa baraza maalumu na lakini kutokana na mvutano wa maamuzzi ya madiwani hao,ndipo walilazimika kupiga kura na baada ya kupiga kura, madiwani wote walikubaliana kufanyika kwa baraza maalumu kwa ajili ya kutatua tatizo la taarifa ya upungufu wa madawati hayo.

“Wanaosema tuite baraza maalumu au tuunde kamati ndogo itakayoshirikiana na kamati ya fedha,wanaosema tupeleke kwenye kamati ya fedha wainue mikono,wanaosema kuwe na baraza maalumu wainue mikono,wanaosema liitwe baraza maalumu wameshinda”alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Halmashauri huku akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo.
Ni Mweka hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Bwana Gordon Dinda.(wa pili kutoka kulia) akisikiliza taarifa mbali mbali za kamati za kudumu huku akilazimika kutolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoulizwa na madiwani hao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Bwana Revocatus Kuul(wa kwanza kutoka kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Bwana Peter Onesmo wakati wa mkutanao wa kawaida wa baraza la madiwani walipokuwa wakisomewa taarifa ya utengenezaji wa madawati,taarifa ambayo waliikataa baada ya kubaini kuwa taarifa iliyotolewa julai,30,mwaka huu kwa Rais,wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli ilikuwa ya uongo.
Ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Bwana John Mwaipopo akifungua mkutano wa kawaida wa barazaa la madiwani wa Halmashauri yaa wilaya ya Igunga.
Ni Afisa elimu shule za msingi,Bwana Mwisungi Kigosi akitoa taarifa ya utengenezaji wa madawati kwa madiwani wa Halmashauri hiyo,ambayo hata hivyo ilikataliwa baada ya kubainika haikuwa ikisema kweli.
Ni Diwani wa viti maalumu (CHADEMA),Bi Anna Nyarobi(wa kwanza kutoka kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa ya utengenezaji wa madawati iliyotolewa na afisa elimu wa shule za msimhi katika wilaya ya Igunga,Bwana Mwisungi kigosi(hayupo pichani) ambayo hata hivyo madiwani hwa kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao waliikataa na kuagiza kiandaliwe kikao maalumu cha baraza hilo kwa ajili ya aliyetoa taarifa za uongo kwa rais kwamba wilaya hiyo haina upungufu wa madawati wakati bado yanahitajika zaidi ya madawati 1,500 akatangaze kwa waandishi wa Habari kuwa alisema uongo kwa mkuu wa nchi..
baaddhi ya madawati yaliyotengenezwa na Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora kwa ajili ya kusambaza katika shule za msingi na sekondari zilizopo kaatika wilaya hiyo..

Security, Privacy and Trust, Major Challenges in ICTs - Eng. Kilaba



By  a Correspondent, TUNISIA

DESPITE fast advancement and multiple benefits of Information Telecommunication Technologies (ICTs), issues of Security, Privacy and Trust remain major concern both at National and Global levels. 
 Addressing the World Telecommunication Standardization Assembly (WTSA-16) in Jasmine Hammamet, Tunisia recently at the Global Standardization Symposium, the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Director General Engineer James Kilaba (pictured right) said  emerging technologies in ICTs play a central role on security (Networks, systems, devices, data and Users), privacy (data and Users) and trust (Networks, systems, devices, data and Users).  
“At any ICTs discussion platforms like this, we normally don’t miss talking about ICTs related Services, Devices,  Growth, subscriptions or Users, Network and Signal coverage and even revenues. Today, we are discussing the impact of emerging technologies on security, privacy and trust in ICTs” the TCRA DG told the WTS Assembly.

Eng. Kilaba said there has been technological shift from an internet dominated by Personal Computers (PCs) with wired connections, to the current mobile devices connected by wireless signals. He further said this has facilitated more access to communications and by extension, through Internet, to the cyber world. He added that the main cause of discussions at the Assembly was about ICTs related Services, Devices, Growth, subscriptions or Users, Network and Signal coverage. 
“Regulators around the world are being challenged by the role/demands of Users (people) and evolutions of Devices irrespective of where they are mounted, fitted, connected or used as far as Security, Privacy or Trust are concerned. So, it is basically the People who also have cultural diversity complemented by time-zone differences”. said the TCRA Chief.
Now, from the perspective of developing countries, Tanzania has done a lot on cyber security. Eng. Kilaba narrated that from the perspective of developing countries, the United Republic of Tanzania has National Cyber Security System in place and stakeholders are involved. 
“We have implemented our National Computer Emergency Response Team (TZ-CERT) and is used for dissemination of cyber security knowledge, information and skills to various stakeholders and Users, to be able to acquire necessary levels of expertize needed to actively tackle serious cybercrime incidents. We have implemented DNSSEC at our Domain Name Registry System. We have a newly established National Data Centre. We have also started to deploy mechanisms so as to prevent misuse of data or information from a stolen mobile device in the country.” He said.      
The TCRA Boss added that at East African Region, Computer Emergency Response Teams (CERTs) has been implemented in four countries and to a large extent, the countries share and exchange information on cyber security incidents and threats. He also said through the regional our Organization EACO, member countries also meet and discuss issues on the cyber-security. He explained that the particular challenges faced in the context of security, privacy and trust in ICTs could be categorized in five basic factors like inadequate harmonization on Standards, Policies, Laws and Strategies.   
“Standards, Laws and Strategies are required to improve a nation's cyber defense posture. As the matter does not end within one country’s borders, the established Standards, Laws and Regulations need to be harmonized within regions and globally. It is believed that there are few world-class cyber experts to adequately handle cyberspace offenses and defense”. He elaborated further. 
The TCRA DG also under-scored the need for National Cyber-security Strategies that would promote dissemination of cyber security knowledge, information and skills to various stakeholders and Users, to be able to acquire necessary levels of expertizes needed to actively tackle serious cybercrime incidents. Eng. Kilaba told the Assembly that there was need for proper Management of Cyber-Security – Beyond National borders.

“Some of our developing countries have no well-established and adequately equipped National Computer Incident Response Teams (CIRTs) or Computer Emergency Response Teams (CERTs). These kinds of facilities when well established provide national approach for coordination, analysis, responses and secure information sharing in regards to cyber security incidents and threats. 

He explained that there was a need therefore, for developing countries to have hand-shaking National-CERTs that would assist on early detection, monitoring and countering attacks, intrusions, new forms of malicious code distribution or any other type of malicious behavior. 
“Effective and collaborative management of cyber security is a critical capability for the defense and preservation of civil society. Cybercrime is one of the world’s largest and fastest-growing categories of crime in cyberspace”. He noted with concern.

On Critical Infrastructures, he sighted that some of the critical infrastructures like Domain Names Registry Systems in respective countries are not well secured, and therefore vulnerable to attacks. Such kind of attacks when successful, they cause economic impact to our countries, adding that it was important that all critical infrastructures like Domain Names Registry Systems in our countries are properly secured and monitored.

He named Numbering Resources Management for Internet of Things (IoTs) and Machine to Machine (M2M) communications as very key, as the area was also emerging as new and therefore, requiring special attention in developing countries. The TCRA Chief said with caution that inadequate education and awareness to citizens was similarly detrimental.

“Education to enable Users to understand issues relating to security, privacy and trust in ICT is lacking. This education if provided will enable users to make informed decisions on the trustworthiness of ICT applications and services including social contacts and selective information sharing. There is unlawful use of ICTs by irresponsible people who use Human Rights and Privacy issues as their defenses”. Said Eng. Kilaba and appealed to Experts coordinated by ITU to play their part, so as to mitigate the challenges paused by Security, Privacy and Trust in ICTs. 
The World Telecommunication Standardization Assembly is held every four years and defines the next period of studies for ITU-T. WTSA-16 is being held in Yasmine Hammamet, Tunisia, from 25 October to 3 November 2016 preceded by the Global Standardization Symposium on 24 October 2016.


​​​​

Mwaka Mmoja wa Magufuli, Huduma Zaimarika Maradufu Muhimbili

Na John Stephen, MNH
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeimarisha nafasi yake ya kutoa huduma za afya kama hospitali ya taifa ili kupunguza rufaa za wagonjwa wanaokwenda nje ya nchi kutibiwa.
Muhimbili imejipanga kutoa huduma katika ubora wa hali ya juu na tayari imepeleka wataalamu wake nje ya nchi ili kujengewa uwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa.
Akizungumza na waandishi wa habari LEO, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Buberwa Aligaesha amesema Muhimbili imepeleka wataalamu 20 nchini India kwa ajili kujifunza upandikizaji figo pamoja na kutoa huduma bora kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.
Aligaesha amesema madaktari na wataalamu wengine wamerejea kutoka India ambako walikwenda kujifunza upandikizaji wa vifaa kwa wagonjwa wenye matatizo ya masikio.
Utekelezaji Maagizo ya Rais John Pombe Magufuli
Amesema baada ya Rais John Pombe Magufuli kuingia Ikulu, alitembelea Muhimbili na kuagiza hospitali hiyo itengeneze mashini ya MRI na  kwamba agizo hilo lilitekelezwa kwa wakati.
“Baada ya mashini hiyo kutengenezwa ilifanya kazi vizuri na katika kipindi cha Disemba 2015 hadi Oktoba 2016 wagonjwa 17,951 walipatiwa vipimo vya MRI ukilinganisha na wagonjwa 1,911 waliopatiwa vipimo Disemba 2014 hadi Oktoba 2015. Hii ni sawa na asilimia 839.35,” amesema Aligaesha.
Aligaesha amesema pia mashini ya CT-Scan ilitengenezwa na kufanya kazi vizuri na katika kipindi cha Disemba 2015 hadi Oktoba 2016, wagonjwa 10,259 walipatiwa huduma ukilinganisha na wagonjwa 3,319 waliopimwa Disemba 2014 hadi Oktoba 2015. Amesema ongezeko hilo ni sawa  asilimia 209.09.
 “Kasi ya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeongezeka maradufu kutokana na wafanyakazi kulipwa  stahili zao kwa wakati na kusababisha kuongezeka kwa vipimo vya radiolojia kwa asilimia 129.57,” amesema.
Huduma za Upasuaji
Aligaesha amesema leo kwamba kasi ya kufanya upasuaji imeongezeka na kwamba wagonjwa kati ya 40 hadi 50 kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa wanafanyiwa upasuaji.
“Katika kuongeza wigo wa wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa upasuaji, hospitali inaongeza vyumba vya upasuaji saba kutoka 13 hadi 20. Katika upande wa ICU, vitanda vimeongezeka kutoka 21 vilivyopo sasa hadi kufikia 101 sawa na ongezeko la vitanda 80. Hii ni sawa na asilimia 67.3 ambalo ni takwa la Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO),” amesema Aligaesha.
Aligaesha amesema  hospitali imeboresha huduma za afya na kwamba katika kipindi cha Disemba 2015 hadi Oktoba 2016, wagonjwa 55,073 walipatiwa huduma za vipimo vya radilolojia ukilinganisha na wagonjwa 23,989 waliopimwa Disemba 2014 hadi Oktoba 2015.
Muhimbili Yalipa Malimbikizo
Amesema uongozi wa hospitali umeongeza kasi ya kupunguza kero za wafanyakazi na kwamba wamekuwa wakilipa malimbikizo ya madai ya wafayakazi ambayo walikuwa wakidai kwa kipindi kirefu.
 Aligaesha amesema kutokana na utekelezaji wa kutoa huduma bora kwa wagonjwa, hivi sasa wagonjwa wanapata dawa kwa zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa ya hospitali hiyo.
 “Tumeboresha mfumo wa Tehama katika utoaji na uagizaji dawa, na wagonjwa wanaokosa katika maduka yetu, Hospitali inanunua haraka ili mgonjwa huyo aweze kupata dawa. Hivi sasa ukosekanaji wa dawa Hospitalini umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na huduma kuimarika ndani ya Muhimbili. Kabla ya hapo upatikanaji wa dawa ulikuwa chini kwa asilimia 35 hadi 35, sasa mambo ni mazuri,” amesema Aligaesha.
Pia, hospitali imeongeza mapato kwa zaidi ya asilimia 100 baada ya kupunguza kero za wafanyakazi.
Katika hatua nyingine, hospitali hiyo imekuwa kwenye mikakati ya kupunguza matumizi kwa kununua dawa na vifaa tiba kutoka viwandani badala ya kununua madukani.
 “Kwa mfano, Hospitali imenunua dawa za figo (immunosuppressant) kutoka nchini India kwa Shilingi milioni 226 wakati hapa nchini zingegharimu Shilingi milioni 500,” amesema Aligaesha.

Dc Momba abaini utaratibu mbovu wa utoaji huduma katika kituo cha Afya Tunduma


Na Saimeni Mgalula,Songwe

MKUU wa wilaya ya momba Mkoani hapa,Juma Irando ametoa onyo kali kwa mganga mtawala wa kituo cha afya cha Tunduma Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha na kurekebisha mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya Sereikali ya awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Hayo aliyasema baada ya kwenda kutembelea kituo hicho cha afya jana na kubaini utaratibu mbovu wa utoaji huduma zakiafya baada ya kukaa katika kituo hicho kwa muda wa nusu saa bila ya kumuona hata muudumu mmoja akiwa mapokezi

''Viongozi niliongozana nao walilazimika kuwatafuta watoa huduma kwa dakika zaidi ya 45 baada ya kuwasuburi mapokezi kwa kipindi cha dakika 30 bila kupewa huduma pamoja na kuwepo kwa wagonjwa waliokuwa wakisuburi kusikilizwa eneo la mapokezi kwa kipindi kirefu''alisema.

Hali iliyomlazimu Dc Irando kuwasiliana na Mganga mkuu wa Wilaya ya Momba aliyefahamika kwa jina moja Dr Felister na kumtaka ampe jina la mganga mtawala wa kituo na mganga wa zamu, ambao walipatikana baada ya dakika 30 kinyume na utaratibu.alisema

Dc Irando pia aligundua kutokujazwa kwa taarifa za wagonjwa katika vitabu vya kuchukulia taarifa za wagonjwa kituoni hapo wakati akimuhoji mganga mtawala wa kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Dr Kaogo ofisini kwake, ambapo vitabu vya wagonjwa vilivyokutwa kituoni hapo vilionyesha kuhudumiwa wagonjwa 15 kwa siku na vingine kuonyeshwa kutokujazwa tangu tarehe 11 mwezi huu.

''Nikiwa kama mkuu wa wilaya siwezi kukubaliana nasuala la uzembe kazini ambaye alisema uhalali wa kituo hicho kuhudumia wagonjwa 15 tu kwa siku licha ya kuwa ndio kituo pekee kinachotoa huduma chenye hadhi ya wilaya'',alisema baada ya kubaini kinaudumia wagonjwa kumi na tano.
Dc Irando alipowahoji wagonjwa hao walikiri kutokusikilizwa kwa muda huo hali iliyomlazimu mkuu wa wilaya kuwafata wahudumu wodini, kuonesha kuwa hawakuwa wakijuwa uwepo wa Mkuu wa wilaya kituoni hapo, wauguzi waliokutwa wodini hawakuonesha kushtuka wala kuuliza shida waliyonayo hadi pale Dc Irando alipojitambulisha, huu ni ushahidi wa utaratibu mbovu walionao watumishi wa kituo hicho kwa wagonjwa wanaofika kuhudumiwa katika kituo chao.

Dc alimtaka Mganga mkuu wa wilaya kumpa maelezo juu ya utaratibu mbovu wa utoaji huduma kwa wananchi unaofanywa na watumishi wa kituo hicho pamoja na kukaa na watumishi wa kituo hicho na kuwataka kubadilika mara moja akiahidi kurejea hapo kesho yake.

Aliagiza kuwepo kwa watoa huduma muda wote wa kazi na kutoa ovyo kali kwa mganga mtawala wa kituo hicho Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha na kurekebisha mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya Sereikali ya awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

.Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tunduma Ally Mwafongo (chadema) alimwambia mkuu wa wilaya kuwa kituo hicho kina utaratibu mbovu na watumishi wa kituo hicho wanafanya kazi kwa mazoea hivyo kumtaka mkuu wa wilaya kuingilia kati ili wananchi wasiendelee kunyanyasika.

Akiongozea juu ya huduma mbovu za watumishi wa kituo hicho Mwafongo alisema kuwa alifika kituoni hapo siku kadhaa zilizopita mida ya saa mbili usiku hakukuta wahudumu wala waganga wanaotakiwa kuwepo licha kukuta uwepo wa wagonjwa waliokuwa wanasubiri kusikilizwa kwa muda mrefu na kumshukuru mkuu wa wilaya kujionea yeye mwenyewe isijekuonekana kuwa wanawachongea

Waziri wa Fedha na Mpango Dkt. Philip Mpango awasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018


Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma

Serikali imeainisha maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2017/2018 kulingana na mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka ujao wa fedha.
 

Waziri wa Fedha na Mpiango Dkt. Philip Mpango amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.

Dkt. Mpango amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na miradi ya kielelezo ya maendeleo ambayo inayolenga kufanikisha utekelezaji wa Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ni pamoja na miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma, Mchuchuma Liganga, ujenzi wa reli ya kati kutoka Dar es salaam, Tabora hadi Kigoma yenye urefu wa km 1,251 kwa “Standard Gauge” pamoja na matawi yake ya Tabora kupitia Isaka hadi Mwanza yenye urefu wa km 379, Isaka hadi Rusumo km 371, Kaliua kupitia Mapanda hadi Karema km 321, Keza hadi Ruvubu km 36 na Uvinza hadi Kelelema kuelekea Musongati yenye urefu wa km 203.

Miradi mingine ya kielelezo ni uboreshaji wa Shirika la Ndege TAanzania (ATC), ujenzi wa mitambo ya kusindika gesi mkoani Lindi, uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumimkoani Tanga, Bagamoyo, Kigoma, Ruvuma, uanzishwaji wa kituo cha biashara cha Kurasini, kusomesha vijana katika stadi za mafuta na gesi, uhandisi na huduma za afya.

Waziri Dkt. Mpango ameyataja maeneo mengine ya kipaumbele kuwa ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa kukuza uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo y uchumi na maendeleo ya watu, mazingira ya wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji, ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na maeneo mengine muhimu kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa taifa.

Dkt. Mpango amesema kuwa shabaha ya uandaaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2017/18 unaongozwa Serikali kusimamia mambo ya uchumi kwa ujumla ikiwemo kuongeza kasi ya ukuaji wa pato halisi la taifa kufikia asilimia 7.5 kwa mwaka 2017, asilimia 7.9 mwaka 2018 na asilimia 8.2 mwaka 2019, kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja kufikia asilimia 5.0 katika kipindi cha muda wakati, kuwa na pato ghafi la taifa la sh. trilioni 123.9 kwa mwaka 2017/18, sh. trilioni 139.7 kwa mwaka 2018/19 na sh. trilioni 165.4 mwaka 2019/20 pamoja na mapato ya kodi kufikia asilimia 14.6 ya pato la taifa mwaka 2017/18, asilimia 15.5 mwaka 2018/19 na asilimia 15.8 mwaka 2019/20.

Aidha, ametaja misingi ya mpango na bajeti kuwa ni amani, usalama, utulivu na utangamano wa ndani ya nchi na nchi jirani ambavyo vitaendelea kudumishwa nchini. Kuhusu mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018, Dkt. Mpango amesema amewaagiza Maafisa Masuuli kuzingatia masuala muhimu wakati wa uandaaji wa mipango na bajeti za mafungu yao ili kutekeleza Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015.

Zaidi ya hayo, Dkt. Mpango amesisitiza uwepo usimamizi na udhibiti wa matumizi, ulipaji na ongezeko la madeni ya Serikali, ukusanyaji wa mapato pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za utekelezaji.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Hawa Ghasia alipokuwa akitoa taarifa ya kamati yake amesema kuwa Kamati yake inardhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kusimamia Sheria ya Bajeti na kanuni zake ambayo inahakikisha usimamizi na uwajibikaji katika hatua zote za mchakato wa bajeti unazingatiwa.

Naye Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Halima Mdee alipokuwa akiwasilisha hotuba yake amesema kuwa Kambi Rasmi inaunga mkono hatua za kisheria zinazochukuliwa na Serikali kwa wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuhujumu uchumi wa nchi.

Mkutano wa Tano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uanatarajiwa kuhitimishwa Novemba 11 mwaka huu huku shughuli mbalimbali za kuishauri Serikali zikiwasilishwa kupitia mijadala ya Wabunge.