Wednesday, November 2, 2016

WILAYA YA IGUNGA YATOA TAARIFA YA AUONGO YA UKAMILISHAJI WA MADAWATI KWA RAIS


Na,Jumbe Ismailly,Igunga Nov,02,2016 Taarifa 

BARAZA la kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora limeikataa taarifa ya utengenezaji wa madawati ya Halmashauri hiyo,kwa masharti ya kumtaka aliyetoa taarifa ya kumdanganya Rais,Dk.John Pombe Magufuli aende kwenye vyombo vya habari kukanusha taarifa hizo.

Mapema julai,30,mwaka huu wakati wa ziara yake wilayani Igunga,Mkoani Tabora,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli julai,alikabidhiwa taarifa ya wilaya hiyo inayosema wilaya ya Igunga haina upungufu wa madawati na kibaya zaidi kwa mujibu wa taarifa hiyo ilikuwa na ziada ya madawati mia mbili.

Maamuzi ya Madiwani hao yanafuatia taarifa ya utengenezaji wa madawati iliyotolewa na afisa elimu wa wilaya hiyo, Mwisungi Kigosi kwenye mkutano wa kawaida wa baraza hilo kuonyesha mabadiliko ya takwimu zilizotolewa kwa Rais na walizosomewa madiwani hao.

Wakichangia kwa nyakati tofauti hoja hiyo baadhi ya madiwani,diwani wa viti maalumu CHADEMA,Anna Nyarobi,Charles Bomani wa kata ya Igunga,Gedi Nkuba wa kata ya Nguvumoja na Henry Saidi wa kata ya Mwamala walisema kuwa kuokana na taarifa hiyo kukinzana,kuwa na mkanganyiko na taarifa iliyotolewa kwa Rais na kutokuwa vizuri,hawatakuwa tayari kuipokea taarifa hiyo na kuirudisha kwenye kamati ya madawati wakaipitie tena upya na kisha kuipeleka kwenye baraza maalumu la madiwani.

Anna Nyarobi ni diwani wa viti maalumu kupitia CHADEMA akichangia hoja hiyo alipendekeza kwamba watu waliotoa taarifa za uongo waende kwenye vyombo vya habari na kukanusha taarifa hiyo kwa kusema kuwa taarifa waliyotoa ilikuwa ni ya uongo,ili waweze kurudisha imani za wananchi kwa madiwani wao.

Hata hivyo diwani,Gedi Nkuba alibainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa upungufu wa madawati,alishauri Mkaguzi wa ndani afuatilie taarifa ya madawati hayo pamoja na tathimini ya fedha zote zilizokusanywa kwa ajili ya utengenezaji wa madawati hayo iweze kubainika.

Naye diwani wa kata ya Mwamala,aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa Tume ya kufuatilia utengenezaji wa madawati,Henry Saidi kwa upande wake alibainisha kwamba,baada ya kubaini kuwepo kwa mianya ya ufujaji wa fedha za madawati ya Halmashauri ya Igunga,walishindwa kuendelea na mchakato huo wa utengenezaji wa madawati.

Afisa elimu wa shule za msingi wilaya ya Igunga,Mwisungi Kigosi katika taarifa yake aliyotoa kwa madiwani hao inaonyesha kwamba hadi kufikia sept,21,mwaka huu wilaya hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 2,232 na baada ya kukarabati madawati 725,upungufu halisi uliopo kwa sasa ni madawati 1,507.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Revocatus Kuul alisema alipotembelea katika shule ya msingi Ganyawa alikuta wanafunzi wakiwa wanaendelea na masomo huku wakiwa wamekaa chini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Peter Onesmo aliwashauri madiwani hao kutofanyika kwa baraza maalumu na lakini kutokana na mvutano wa maamuzzi ya madiwani hao,ndipo walilazimika kupiga kura na baada ya kupiga kura, madiwani wote walikubaliana kufanyika kwa baraza maalumu kwa ajili ya kutatua tatizo la taarifa ya upungufu wa madawati hayo.

“Wanaosema tuite baraza maalumu au tuunde kamati ndogo itakayoshirikiana na kamati ya fedha,wanaosema tupeleke kwenye kamati ya fedha wainue mikono,wanaosema kuwe na baraza maalumu wainue mikono,wanaosema liitwe baraza maalumu wameshinda”alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Halmashauri huku akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo.
Ni Mweka hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Bwana Gordon Dinda.(wa pili kutoka kulia) akisikiliza taarifa mbali mbali za kamati za kudumu huku akilazimika kutolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoulizwa na madiwani hao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Bwana Revocatus Kuul(wa kwanza kutoka kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Bwana Peter Onesmo wakati wa mkutanao wa kawaida wa baraza la madiwani walipokuwa wakisomewa taarifa ya utengenezaji wa madawati,taarifa ambayo waliikataa baada ya kubaini kuwa taarifa iliyotolewa julai,30,mwaka huu kwa Rais,wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli ilikuwa ya uongo.
Ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Bwana John Mwaipopo akifungua mkutano wa kawaida wa barazaa la madiwani wa Halmashauri yaa wilaya ya Igunga.
Ni Afisa elimu shule za msingi,Bwana Mwisungi Kigosi akitoa taarifa ya utengenezaji wa madawati kwa madiwani wa Halmashauri hiyo,ambayo hata hivyo ilikataliwa baada ya kubainika haikuwa ikisema kweli.
Ni Diwani wa viti maalumu (CHADEMA),Bi Anna Nyarobi(wa kwanza kutoka kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa ya utengenezaji wa madawati iliyotolewa na afisa elimu wa shule za msimhi katika wilaya ya Igunga,Bwana Mwisungi kigosi(hayupo pichani) ambayo hata hivyo madiwani hwa kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao waliikataa na kuagiza kiandaliwe kikao maalumu cha baraza hilo kwa ajili ya aliyetoa taarifa za uongo kwa rais kwamba wilaya hiyo haina upungufu wa madawati wakati bado yanahitajika zaidi ya madawati 1,500 akatangaze kwa waandishi wa Habari kuwa alisema uongo kwa mkuu wa nchi..
baaddhi ya madawati yaliyotengenezwa na Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora kwa ajili ya kusambaza katika shule za msingi na sekondari zilizopo kaatika wilaya hiyo..

No comments: