Wednesday, November 2, 2016

Dc Momba abaini utaratibu mbovu wa utoaji huduma katika kituo cha Afya Tunduma


Na Saimeni Mgalula,Songwe

MKUU wa wilaya ya momba Mkoani hapa,Juma Irando ametoa onyo kali kwa mganga mtawala wa kituo cha afya cha Tunduma Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha na kurekebisha mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya Sereikali ya awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Hayo aliyasema baada ya kwenda kutembelea kituo hicho cha afya jana na kubaini utaratibu mbovu wa utoaji huduma zakiafya baada ya kukaa katika kituo hicho kwa muda wa nusu saa bila ya kumuona hata muudumu mmoja akiwa mapokezi

''Viongozi niliongozana nao walilazimika kuwatafuta watoa huduma kwa dakika zaidi ya 45 baada ya kuwasuburi mapokezi kwa kipindi cha dakika 30 bila kupewa huduma pamoja na kuwepo kwa wagonjwa waliokuwa wakisuburi kusikilizwa eneo la mapokezi kwa kipindi kirefu''alisema.

Hali iliyomlazimu Dc Irando kuwasiliana na Mganga mkuu wa Wilaya ya Momba aliyefahamika kwa jina moja Dr Felister na kumtaka ampe jina la mganga mtawala wa kituo na mganga wa zamu, ambao walipatikana baada ya dakika 30 kinyume na utaratibu.alisema

Dc Irando pia aligundua kutokujazwa kwa taarifa za wagonjwa katika vitabu vya kuchukulia taarifa za wagonjwa kituoni hapo wakati akimuhoji mganga mtawala wa kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Dr Kaogo ofisini kwake, ambapo vitabu vya wagonjwa vilivyokutwa kituoni hapo vilionyesha kuhudumiwa wagonjwa 15 kwa siku na vingine kuonyeshwa kutokujazwa tangu tarehe 11 mwezi huu.

''Nikiwa kama mkuu wa wilaya siwezi kukubaliana nasuala la uzembe kazini ambaye alisema uhalali wa kituo hicho kuhudumia wagonjwa 15 tu kwa siku licha ya kuwa ndio kituo pekee kinachotoa huduma chenye hadhi ya wilaya'',alisema baada ya kubaini kinaudumia wagonjwa kumi na tano.
Dc Irando alipowahoji wagonjwa hao walikiri kutokusikilizwa kwa muda huo hali iliyomlazimu mkuu wa wilaya kuwafata wahudumu wodini, kuonesha kuwa hawakuwa wakijuwa uwepo wa Mkuu wa wilaya kituoni hapo, wauguzi waliokutwa wodini hawakuonesha kushtuka wala kuuliza shida waliyonayo hadi pale Dc Irando alipojitambulisha, huu ni ushahidi wa utaratibu mbovu walionao watumishi wa kituo hicho kwa wagonjwa wanaofika kuhudumiwa katika kituo chao.

Dc alimtaka Mganga mkuu wa wilaya kumpa maelezo juu ya utaratibu mbovu wa utoaji huduma kwa wananchi unaofanywa na watumishi wa kituo hicho pamoja na kukaa na watumishi wa kituo hicho na kuwataka kubadilika mara moja akiahidi kurejea hapo kesho yake.

Aliagiza kuwepo kwa watoa huduma muda wote wa kazi na kutoa ovyo kali kwa mganga mtawala wa kituo hicho Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha na kurekebisha mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya Sereikali ya awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

.Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tunduma Ally Mwafongo (chadema) alimwambia mkuu wa wilaya kuwa kituo hicho kina utaratibu mbovu na watumishi wa kituo hicho wanafanya kazi kwa mazoea hivyo kumtaka mkuu wa wilaya kuingilia kati ili wananchi wasiendelee kunyanyasika.

Akiongozea juu ya huduma mbovu za watumishi wa kituo hicho Mwafongo alisema kuwa alifika kituoni hapo siku kadhaa zilizopita mida ya saa mbili usiku hakukuta wahudumu wala waganga wanaotakiwa kuwepo licha kukuta uwepo wa wagonjwa waliokuwa wanasubiri kusikilizwa kwa muda mrefu na kumshukuru mkuu wa wilaya kujionea yeye mwenyewe isijekuonekana kuwa wanawachongea

No comments: